Serikali kuzisaidia shule binfsi-Luhanjo.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Serikali imewahakikishia wamiliki wote wa shule binafsi nchini, kuwa inathamini sana mchango wao katika kukuza na kuendeleza sekta ya elimu nchini hivyo itatoa kila aina ya ushirikiano kwa shule hizo kwa kadri ya uwezo wa rasilimali zilizopo ili kutimiza jukumu la ukombozi wa elimu ambao utaleta maendeleo ya kweli ya taifa letu.

Hakikisho hilo, limetolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha nne cha shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ghomme iliyopo Kunduchi Ununio, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Bwana Luhanjo ametoa wito kwa watu na taasisi kuwekeza kwenye elimu akisisitiza maendeleo ya kweli, yataletwa na mapinduzi katika sekta ya elimu ambao itakuwa kichocheo cha mapinduzi ya sekta nyingine zote ikiwemo mapinduzi ya viwanda yatakayotoa zana bora kuleta mapinduzi ya kilimo, ndio maana serikali inathamini mchango wa shule binafsi katika sekta ya kilimo.

Akitolea mfano nchi ya Korea, ilipata uhuru mwaka mmoja na Tanzania, mwaka 1961, lakini Korea imepiga maendeleo makubwa kuliko Tanzania kwa sababu walitoa kipaumbele kwenye mapinduzi ya elimu, hivyo serikali inaunga mkono kwa dhati kabisa uwekezaji katika elimu.

Sambamba na serikali kuunga mkono uwekezaji katika elimu, Katibu Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa shule binafsi kutimiza wajibu wao kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wao itakayo kwenda sambamba na kuibua vipaji mbalimbali mvya watoto, na kuwajengea tabia njema na nidhamu ya hali ya juu.

Nae Meneja wa shule hiyo, Dr. Emmanuel Malangalila, aliishukuru serikali kwa juhudi zake za kufungua milango ya uwekezaji katika sekta ya elimu, lakini akasisitiza mchango wa serikali bado ni muhimu zaidi katika kusaidia gharama za uendeshaji haswa vifaa vya maabara na kusimamia mitaala ili elimu inayotolewa ikidhi mahitaji ya jamii husika.

Dr. Malangalila amewashukuru wazazi walioleta watoto wao shuleni hapo na kuwahakikishia kuwa matokeo ya kidato cha nne ndio kipimo sahihi cha kuwathibitishia wao na umma, kuwa legho la Shule ya Ghomme ni kutoa elimu bora katika mazingira mazuri ya kusomea kwa kuwekeza katika elimu, majengo, vifaa na rasilimali watu za waalimu wenye ujuzi na uwezo mkubwa na uzoefu wa muda mrefu kuishi na kuwafunza wototo wa kike.

Dar Malangalila amesema katika kuboresha uhusiano mwema na jamii inayowazungunguka, Shule hiyo imeanzisha tuzo ya Galvinica Memorial Scholaship ambayo kila mwaka, watanchukua mwanafunzi mmoja wa familia za majira, ambao wana vipato vya chini, na kungharimia gharama zote za masomo mpaka kidato cha nne, ili shule hiyo iwe ni sehemu ya mafanikio ya jamii iliyowazunguka. Alitoa wito kwa wafadhili kujitokeza kudhamini watoto toka familia zenye vipato vya chini ili hatimaye kuja kuinua maisha ya familia zao.

Wanafunzi katika risala yao, waliwashukuru wamiliki, walimu na wafanyakazi wa shule hiyo kwa jinsi walivyowahudumia, na kuahidi kuwa watakuwa raia safi huko kwenye jamii wanakoreja, na kusisitiza matumaini yao ya kufanya vizuri hivyo kurejea shuleni hapo kwa kidacho cha tano na sita.

Mmoja wa wazazi, Bi. Betty Mgaya, alitoa ushuhuda wa mabadiliko ya tabia ya binti yake sambamba nay a kitaaluuma aliyoyashuhudia tangu alipojiunga na shule hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.

Mahafali hayo yalitanguliwa na ufunguzi wa jingo la maabara na bweni jipya la wasichana. Shule hiyo iliyoanzishwa miaka 2 iliyopita, ina ya wanafunzi takriban 150. Sherehe za mahafali hayo ziliandamana na tukio la ukataji keki maalum na kupambwa na burudani mbalimbali. Mwisho
 
Back
Top Bottom