Serikali kuwatumbua wadaiwa bodi ya mikopo

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa onyo kwa wadaiwa sugu ambao hawajajitokeza kuanza kulipa madeni yao, kwamba hatua mbalimbali dhidi yao zinatafuata kokote waliko.

Miongoni mwa hatua hizo, bodi hiyo imetaja kuwa ni kuwatoza wadaiwa hao sugu riba ya asilimia kumi katika deni lao na kutumia taarifa zao kuwazuia kufanya safari za nje ya nchi.

Imeeleza kuwa wadaiwa hao wa tangu mwaka wa masomo wa 1994/95, wataanza kusakwa kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye anawajibika kukagua mali zote za Serikali.

Mbali na CAG, ambaye ana mkono mrefu wa kuwasaka katika ofisi zote za Serikali Kuu, mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa na katika miradi ambayo Serikali ina ubia na sekta binafsi, pia kampuni binafsi za ukaguzi wa hesabu, zenye mkono mrefu katika sekta binafsi, zitatumika kuwasaka katika kampuni binafsi na asasi za kiraia.

“Jukumu la CAG na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wa mahesabu, ni kulazimisha waajiri kuwasilisha taarifa za wafanyakazi wao ambao ni wahitimu wa elimu ya juu na makato ya mkopo waliopewa,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefanya marejeo ya Sheria ya Bodi namba 9 ya 2004 na marekebisho yake, inayomtaka kila mwajiri kutoa maelezo kwa maandishi kwa bodi, kuhusu mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo huo, ndani ya siku 28 tangu mdaiwa alipoajiriwa.

Hatua kali
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mdaiwa yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa kulipa deni lake bila sababu za msingi, kwanza atakuwa akikabiliwa na kesi ya madai chini ya kifungu cha 6 C na H cha Sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004.

Mbali na kukabiliwa na kesi hiyo, pia mkopo wake kwa namna unavyochelewa kuanza kulipwa, utakuwa ukijilimbikizia riba ya asilimia 10. Taarifa hiyo ya bodi imeeleza kuwa mdaiwa huyo taarifa zake zitapelekwa katika taasisi za kumbukumbu ya mikopo zilizo chini ya Benki Kuu (BoT), ambazo zitazuia wadaiwa hao kupata mikopo katika mabenki na asasi zote za fedha.

Mdaiwa huyo pia atazuiwa kupata udhamini wa Serikali katika muendelezo wa masomo yake, lakini pia atazuiwa kujiunga na chuo chochote cha elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa zao pia zitawasilishwa katika Idara ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na katika ofisi zote za kibalozi, ili wakose kibali cha kusafiri nje ya nchi.

Hasara nyingine watakayokabiliwa nayo wadaiwa hao, ni Tozo ya Kulinda Thamani ya Mkopo (VRF) ya asilimia sita kila mwaka, itakayotozwa kwa kila mkopo, ili wadaiwa watakapoanza kulipa mkopo waliochukua, walipe kwa thamani ya sasa.

Tozo hiyo imelenga kuepuka athari ya mfumuko wa bei tangu mdaiwa aliponufaika, lakini pia kuwezesha urejeshwaji wa deni, uwe na thamani ya kumhudumia mwanafunzi mwingine mwenye mahitaji kwa sasa na baadaye.

Ambao hawajaajiriwa
Taarifa hiyo pia imeonya wadaiwa wanaodhani kuwa kutokuajiriwa ni sababu ya kutolipa mkopo huo, kwamba mkopo huo unatakiwa kulipwa baada ya kumalizika kwa mwaka mmoja tangu mdaiwa alipofanikiwa kuhitimu masomo yake, au mwaka mmoja tangu mhusika alipokatisha masomo yake kwa sababu yoyote.

Aidha, taarifa hiyo imeelekeza watakaojitokeza, kama wameajiriwa, asilimia nane ya mshahara wao wa kila mwezi, itatakiwa kukatwa na kuwasilishwa kwenye Bodi ili kulipa deni husika. Lakini pia Bodi hiyo imetengeneza utaratibu kwa ambao hawajaajiriwa, kwamba wanaweza kulipa kiasi cha chini cha Sh laki moja kila mwezi katika akaunti za Bodi zilizopo Benki ya Posta yenye namba CCA0240000032; Benki ya NMB namba 2011100205 na Benki ya CRDB namba 01J1028467503.

Deni lenyewe
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG, hadi Juni 2014, bodi hiyo ilikuwa imewakopesha wanafunzi Sh trilioni 1.8 kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 na kati ya fedha hizo, Sh bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Taarifa hiyo ya HESLB imetolewa siku chache kabla ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ya kusitisha ajira ya Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, George Nyatega kwa tuhuma za udhaifu katika fedha za mikopo zaidi ya Sh bilioni 3.2. Miongoni mwa waliosimamishwa pamoja na Nyatega ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo, Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo, Onesmo Laizer.


Bodi imezembea kuwabana waajiri wakate na kurejesha mkopo kwa bodi. Uhalisia ni kwamba bodi haiwapi waajiri taarifa sahihi ili waanze kuwakata waajiriwa ambao ni wanufaika wa loan board.
Kijumla watu wapo tayari kukatwa mishahara kurudisha deni, tatizo njia za urudishaji ndio haziko wazi na utaratibu haupo wazi sana.
 
Mikopo yao ikicheleweshwa utaona post zao hapa utadhani wanaonewa,kumbe ni majipu yasiyotaka kulipa ,
Sasa lipeni tu,shukraan sana kwa Mzee wangu na ukulima wako kunisomesha,simo kwenye wadaiwa mimi
 
Mikopo yao ikicheleweshwa utaona post zao hapa utadhani wanaonewa,kumbe ni majipu yasiyotaka kulipa ,
Sasa lipeni tu,shukraan sana kwa Mzee wangu na ukulima wako kunisomesha,simo kwenye wadaiwa mimi
Bado we utaona watakuja na data kuwa unadaiwa...
 
Kuna uvamizi uliwahi kutokea ofisi zao miaka kadhaa iliyopita inasemekana ziliibiwa computer wakapoteza baadhi ya data
 
Hawa Bodi ya Mikopo bure kabisa. Wanaendesha Taasisi hii Ki-jima. Watu wanamaliza kurejesha mikopo lakini hawatoi hata cheti cha kuthibitisha ukamilishaji wa mkopo kama Benki zinavyofanya. Hii inaonyesha udhaifu wa mifumo tunaojiwekea.
 
Unajua merits za waajiliwa wa bodi needs two lenced eyes. Hvi unaaga nyumbani unaenda kazini huwa wanafanya Kazi gani sasa? Mi ninavyojua lazima muwe na mpango kazi kwamba mwezi January tutawafikia wadaiwa elfu tano au kumi. Mwaka mmoja umewamaliza wote. Wao Kazi yao ni kupulizwa na AC tu pale mwenge. Hawa hawatofautiani sana na wale wa shirika la ndege. Nadhani hawa watumbuliwe wekeni watu na merits zao tena Kazi iwe kwa mikataba malengo yasipotimia humtoi mkataba Mpya.
 
Mikopo yao ikicheleweshwa utaona post zao hapa utadhani wanaonewa,kumbe ni majipu yasiyotaka kulipa ,
Sasa lipeni tu,shukraan sana kwa Mzee wangu na ukulima wako kunisomesha,simo kwenye wadaiwa mimi
Tanzania tunafanya vitu kwa kuiga kuliko kuelewa tunafanya vitu kwa faida gani.

Kutoa elimu nzuri through mikopo unaenda sambamba na kutoa ajira nzuri kwa wasomi hao ili warudishe mikopo ambayo itasaidia wengine kuja kusoma.

Hapa wigo ni mpana sana na inaingiliana kuanzia kwa wasomi, wafanyabiashara mpaka wakulima.
Ni vitu vinategemeana, so serikali inatakiwa ielewe ikiunganisha sector zote hizo zikawa zinazunguka kwa pamoja bodi itatoa mikopo watu wataajiriwa watalipa kodi mikopo itarudishwa serikali itapata fedha, wafanyabiashara watalipa kodi wakulima watanunua pembejeo watazalisha yaani mzunguko utakuwepo ktk kila idara.

Leo hii unamsisitizia mtu asome baba yako anauza mazao mpaka akiba inakata anaamua kuuza ardhi inayozalisha hayo mazao ardhi inaisha inabidi aombe mkopo unasoma umamaliza chuo then unarudi nyumbani kuomba chakula kwa baba kwa sababu huko mjini umezunguka umetafuta ajira mpaka umechoka.
Leo unatakiwa ulipe mkopo ina maana baba yako akate eneo lingine(kama analo) auze akakulipie deni la mkopo wa shule kama hana sijui bodi inachukua hatua gani.

Huu ni mfano hai kwangu, nimeuona live na ni mmoja wapo nimeshiriki ktk hili kwa kununua kiwanja cha Mzee mmoja ili ampeleke mwanae shule, mtoto kamaliza yuko mtaani kahangaika ajira hamna mpaka sasa karudi nyumbani kwa baba yake.
Baba yake ana watoto wengine anawasomesha, hapa sijui nani amsaidie nani?
 
Hapo ndo elimu bure chekechea hadi chuo kikuu tutaikumbuka!wahitimu wote acha tuisome namba.
 
mimi mi mmoja wa walikua wafaidika wa mkopo huo hapo nyuma. miezi kadhaa iliyopita ililetwa list ya kila anayedaiwa na kiasi anachodaiwa. walio wengi nikiwemo mimi deni lilikua mil.11 na vipoint. kiukweli nawiwa na niko tayari kurejesha deni hilo maana nakili mkopo wao ulinisaidia sana. najua kufanya hivo ni kuipa bodi nguvu ya kuweza kuwakopesha wengine wengi ambao bila mkopo hawawezi kumudu ada na gharama za maisha vyuoni. kama unadaiwa na hutaki kwa maksudi kurejesha deni, wewe pia ni jipu na unafaa kutumbuliwa kwa kisu cha moto.
 
lakini MZEE EDO aliahidi kwenye kampen angelisamehe hili Deni
sijui ingekuwaje
 
Bodi kama bodi hawezi kuwafuatilia wafaidika wa mikopo kurejesha mikiopo yao kwasababu ni legelege!

Kuna wakati bodi ilitaka kuipatia tender ya kukusanya madeni yake MAJEMBE AUCTION MART. Lakini kabla ya MAM kuanza kazi wanasiasa wakaingilia kati kwamba wakianza kuwafuatilia hao wadaiwa wa bodi Serikali itakopsa kura za wanafunzi. Hilo zoezi likafa kifo cha mende.

Mimi bado nina support idea ya kuwapatia tender MAM wawafuatilie wadai wote sugu wa bodi ili walipe mikopo yao.

Ninafikiri JPM kwa kupitia Ndarichako wanaweza kufanya hivyo kwani wameonesha wao sio DHAIFU kama mtangulizi wao
 
Back
Top Bottom