Serikali kuwatumbua wadaiwa bodi ya mikopo

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa onyo kwa wadaiwa sugu ambao hawajajitokeza kuanza kulipa madeni yao, kwamba hatua mbalimbali dhidi yao zinatafuata kokote waliko.

Miongoni mwa hatua hizo, bodi hiyo imetaja kuwa ni kuwatoza wadaiwa hao sugu riba ya asilimia kumi katika deni lao na kutumia taarifa zao kuwazuia kufanya safari za nje ya nchi.

Imeeleza kuwa wadaiwa hao wa tangu mwaka wa masomo wa 1994/95, wataanza kusakwa kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye anawajibika kukagua mali zote za Serikali.

Mbali na CAG, ambaye ana mkono mrefu wa kuwasaka katika ofisi zote za Serikali Kuu, mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa na katika miradi ambayo Serikali ina ubia na sekta binafsi, pia kampuni binafsi za ukaguzi wa hesabu, zenye mkono mrefu katika sekta binafsi, zitatumika kuwasaka katika kampuni binafsi na asasi za kiraia.

“Jukumu la CAG na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wa mahesabu, ni kulazimisha waajiri kuwasilisha taarifa za wafanyakazi wao ambao ni wahitimu wa elimu ya juu na makato ya mkopo waliopewa,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefanya marejeo ya Sheria ya Bodi namba 9 ya 2004 na marekebisho yake, inayomtaka kila mwajiri kutoa maelezo kwa maandishi kwa bodi, kuhusu mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo huo, ndani ya siku 28 tangu mdaiwa alipoajiriwa.

Hatua kali
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mdaiwa yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa kulipa deni lake bila sababu za msingi, kwanza atakuwa akikabiliwa na kesi ya madai chini ya kifungu cha 6 C na H cha Sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004.

Mbali na kukabiliwa na kesi hiyo, pia mkopo wake kwa namna unavyochelewa kuanza kulipwa, utakuwa ukijilimbikizia riba ya asilimia 10. Taarifa hiyo ya bodi imeeleza kuwa mdaiwa huyo taarifa zake zitapelekwa katika taasisi za kumbukumbu ya mikopo zilizo chini ya Benki Kuu (BoT), ambazo zitazuia wadaiwa hao kupata mikopo katika mabenki na asasi zote za fedha.

Mdaiwa huyo pia atazuiwa kupata udhamini wa Serikali katika muendelezo wa masomo yake, lakini pia atazuiwa kujiunga na chuo chochote cha elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa zao pia zitawasilishwa katika Idara ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na katika ofisi zote za kibalozi, ili wakose kibali cha kusafiri nje ya nchi.

Hasara nyingine watakayokabiliwa nayo wadaiwa hao, ni Tozo ya Kulinda Thamani ya Mkopo (VRF) ya asilimia sita kila mwaka, itakayotozwa kwa kila mkopo, ili wadaiwa watakapoanza kulipa mkopo waliochukua, walipe kwa thamani ya sasa.

Tozo hiyo imelenga kuepuka athari ya mfumuko wa bei tangu mdaiwa aliponufaika, lakini pia kuwezesha urejeshwaji wa deni, uwe na thamani ya kumhudumia mwanafunzi mwingine mwenye mahitaji kwa sasa na baadaye.

Ambao hawajaajiriwa
Taarifa hiyo pia imeonya wadaiwa wanaodhani kuwa kutokuajiriwa ni sababu ya kutolipa mkopo huo, kwamba mkopo huo unatakiwa kulipwa baada ya kumalizika kwa mwaka mmoja tangu mdaiwa alipofanikiwa kuhitimu masomo yake, au mwaka mmoja tangu mhusika alipokatisha masomo yake kwa sababu yoyote.

Aidha, taarifa hiyo imeelekeza watakaojitokeza, kama wameajiriwa, asilimia nane ya mshahara wao wa kila mwezi, itatakiwa kukatwa na kuwasilishwa kwenye Bodi ili kulipa deni husika. Lakini pia Bodi hiyo imetengeneza utaratibu kwa ambao hawajaajiriwa, kwamba wanaweza kulipa kiasi cha chini cha Sh laki moja kila mwezi katika akaunti za Bodi zilizopo Benki ya Posta yenye namba CCA0240000032; Benki ya NMB namba 2011100205 na Benki ya CRDB namba 01J1028467503.

Deni lenyewe
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG, hadi Juni 2014, bodi hiyo ilikuwa imewakopesha wanafunzi Sh trilioni 1.8 kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 na kati ya fedha hizo, Sh bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Taarifa hiyo ya HESLB imetolewa siku chache kabla ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ya kusitisha ajira ya Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, George Nyatega kwa tuhuma za udhaifu katika fedha za mikopo zaidi ya Sh bilioni 3.2. Miongoni mwa waliosimamishwa pamoja na Nyatega ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo, Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo, Onesmo Laizer.
 
Kwenye utawala wa serikali ya Awamu ya Tano, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.

Hakuna ubabaishaji na njia za mkato kielimu na kimaisha.

Rais Magufuli anamaanisha anaposema, Mtu asiyefanya kazi asile na kila mtu alipwe kutokana na matendo yake!

Imefikia kiwango neno mkopo kwa wengi linachukuliwa kama kupewa bure.

Mkopo ni deni. Deni lazima lilipwe kama hujafirisika kisheria!

Kama nchi zingine kama Uingereza wanaweza kuwapata wakopaji na kukusanya mkopo, kwa nini Tanzania tusiweze?

Credit reference agency ni muhimu sana awepo.
 
Tulishawekeza maarifa kichwani no way you can take it,kimsingi Bodi ndio wazembe,unategemea nifanye kazi kijijini mazingira magumu hafu nikajipendekeze bodi eti tafadhari nikate ka mkopo-tunaikaribisha hiyo vita
 
Hivi wanajua kama wenzao walikuwa wanakusanya halafu wanatia ndani hela zote?

Je kwa nini serikali haitaki kuwapatia wananchi wake wote vitambulisho vya utaifa ili iweze kujua nani yuko wapi na anafanya nini kurahisishia serikali yenyewe na mabenki kuwatambua wadai wake?

Hivi serikali inajua kwamba ikifungua kesi ya madai ikishinda italazimika kugharimia kuwafunga hao wadaiwa na kifungo hakizidi miezi sita?

Hivi serikali wakati inakopesha ilitegemea italipwaje? Bank huwa zinakupa kabisa instalments zako, je hii serikali iliwahi kumtaarifu nani personally kuwa inamdai na ikampa instalments zake alipe?

Kipi kilikuwa kigezo cha kudai kuanzia 1994/95?
 
Tulishawekeza maarifa kichwani no way you can take it,kimsingi Bodi ndio wazembe,unategemea nifanye kazi kijijini mazingira magumu hafu nikajipendekeze bodi eti tafadhari nikate ka mkopo-tunaikaribisha hiyo vita
Pumbavu kabisa...halafu unashinda mitandaoni kukosoa serikali kumbe unaikwamisha kwa makusudi.....kulipa deni sio kujopendekeza ni uzalendo ili wengine wanufaike."nyumbu"
 
Na uhakika kabisa hii bodi inajua majina machache sana ya wadaiwa wa hiyo mikopo. Na ndio maana inaogopa kuitoa hio list ya hao wadaiwa.

Eti wanakwambia ukitaka kujua unadaiwa kiasi gani, wasiliana na bodi. Sasa kama hiyo list hipo ni kitu gani kinachowashinda kuiweka kwenye website yao?
 
Wewe ni mpuuzi kabisa maana ya mkopo nini? Lazima ulipe tu. Unaleta maelezo wakati kuna watu wengine wanatakiwa wakopeshwe na wao wasome
 
Kazi zenyewe ziko wapi hadi muanze kudai na kuanza ku block mtu kila sehemu?
Kazi mumewapa wahindi na wageni... Mnategemea watu watalipaje madeni?
Lets say graduate analipwa laki tano kwa mwezi.. Akilipa atabakiwa na nini?
Hapa mtasababisha watu watupe vyeti vyao....watu wataenda kulima.. Sasa huko sijui mtawapataje..
Kulipa deni ni lazima na mkwepa kodi ni mhujumu wa uchumi... Hio ipo wazi
 
Wewe ni mpuuzi kabisa maana ya mkopo nini? Lazima ulipe tu. Unaleta maelezo wakati kuna watu wengine wanatakiwa wakopeshwe na wao wasome
Lazima ulipe?
Sasa kama huna kaZi ya maana?
Usikurupuke hapa. Fursa kwanza zitengenezwe.. Au kama vipi hadi kina Magufuli nao wailipe Serikali .. Si walisoma bure nao?
 
Na uhakika kabisa hii bodi inajua majina machache sana ya wadaiwa wa hiyo mikopo. Na ndio maana inaogopa kuitoa hio list ya hao wadaiwa.

Eti wanakwambia ukitaka kujua unadaiwa kiasi gani, wasiliana na bodi. Sasa kama hiyo list hipo ni kitu gani kinachowashinda kuiweka kwenye website yao?
Mkuu mimi bado najiuliza kuwa kama mtu huna kazi utalipaje?
 
Hapo sasa.

Swali lingine mdau kauliza hivi kipi kigezo kilichotumika kuanza kudai wanufaika kuanzia mwaka 1994/95?
Kwa nini isiwe 1972/73 au 2000/2001 et al?
Ukiangalia kwa makini hawa watunga hizi sheria walisoma kabla ya 1994.... Kwa hio wao hawatagusa wakati walisoma bure kabisa
 
Tulishawekeza maarifa kichwani no way you can take it,kimsingi Bodi ndio wazembe,unategemea nifanye kazi kijijini mazingira magumu hafu nikajipendekeze bodi eti tafadhari nikate ka mkopo-tunaikaribisha hiyo vita
Hujaelimika,huna busara na ni mpumbavu
 
Tulishawekeza maarifa kichwani no way you can take it,kimsingi Bodi ndio wazembe,unategemea nifanye kazi kijijini mazingira magumu hafu nikajipendekeze bodi eti tafadhari nikate ka mkopo-tunaikaribisha hiyo vita
kweli kabisa bodi ni wazembe wanawaza kula tu na hata kazi ndogo ya kukusanya mkopo inawashinda, mimi nimeajiriwa serikalini tangu 2008, na nimeshajaza fomu mara mbili ya kutaka kukatwa mkopo lakini hadi leo naandika sijaanza kukatwa, kuajiri vilaza ni shida sana, utashindwaje kukata deni la mwajiriwa wa serikali? it is unbelivable!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom