Serikali kuchukua hatua kutatua migogoro baina ya Hifadhi na Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

SERIKALI KUCHUKUA HATUA KUTATUA MIGOGORO BAINA YA HIFADHI NA WANANCHI

"Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto kati ya wananchi na maeneo ya hifadhi za Taifa ikiwemo Jimbo la Momba" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi. Hatua zinazochukuliwa ni pamoja na kufanya tathmini ya aina, chimbuko na namna ya kutatua migogoro husika" - Mhe. Mary Masanja, Naibu Waziri Maliasili na Utalii

"Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inasimamia Misitu minne ya hifadhi katika Wilaya ya Momba ambayo ni Isalalunga, Isalalo, Ivunano na Ivunasawo ambayo kimsingi haina haina mgogoro na wananchi" - Mhe. Mary Masanja

"Katika kuimarisha ulinzi na usimamizi wa hifadhi hizi Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na uharibifu zikiwemo kuweka alama za Kudumu za mipaka, kutoa elimu kwa Jamii, kuondoa wavamizi na kuchukua hatua za kisheria kwa wahalifu" - Mhe. Mary Masanja

"Migogoro ipo kwasababu wananchi wanachukuliwa wanawekwa ndani. Tumeshaleta maombi Wizarani, ni lini maombi yetu yatajibiwa ili kuwapa wananchi kipande cha ardhi ili waendelee kuendesha shughuli zao? - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe

"Kama maombi haya yakitoka yatakuwa ni hapana, Je, Serikali inachukua hatua gani kuendelea kuwasaidia wakulima wapate maeneo ya kulima kwasababu ni watanzania na hawana mahali pa kwenda ili waendelee kulea watoto wao" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe

"Ni kweli Mhe. Condester aliwahi kuleta maombi yake na haya maombi mchakato wake unaendelea. Kwa upande wa matokeo inategemea na maeneo ambayo tunayaona ni ya muhimu hususani maeneo ambayo tunatunza vyanzo vya Maji na maeneo ambayo ni muhimu kwa kuhifadhiwa." - Mhe. Mary Masanja

"Serikali itafanya tathmini na itaangalia umuhimu wa maeneo haya kwa ajili ya kutunzwa na Serikali na yale ambayo tutaona tunaweza kuyaachia basi wananchi wataweza kunufaika na maeneo ambayo tutayaachia" - Mhe. Mary Masanja
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-25 at 11.30.45.mp4
    46.7 MB
Back
Top Bottom