Mbunge Condester Sichalwe: Watu wasio waaminifu, walioaminiwa wanajificha kwenye dhamana walizopewa kuumiza watanzania wenzao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE CONDESTER SICHALWE: WATU WASIO WAAMINIFU, WALIOAMINIWA WANAJIFICHA KWENYE DHAMANA WALIZOPEWA KUUMIZA WATANZANIA WENZAO

"Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyofanya kazi vizuri. Anapambana na kuhakikisha hata Wabunge tunaotojea Majimbo ya Vijijini tunapata fedha kwenye miradi ya Maendeleo na kuendelea kuwasaidia wananchi kwenye shughuli mbalimbali. Wananchi wa Momba tulivyokuwa jana sivyo tulivyo leo" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya PAC. Nimegundua kwamba Mheshimiwa Rais anafanya kazi kubwa sana kwa kujitoa, kwa huruma, kwa Weledi na kutamani kuisaidia Jamii yake. Kama Mama amedhamiria kuona ule uchungu wa Kimama kwaajili ya kuwasaidia Watanzania" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Serikali ya CCM haina wapinzani, wapinzani ni baadhi ya Watendaji wa Serikali ambao siyo waaminifu na dhamana walizopewq ndani ya Serikali, wao ndiyo wanaowaumiza Watanzania wenzao kwa nafasi walizopewa lakini wao ndiyo wanamfanya Mheshimiwa Rais apate doa na Watanzania wakati mwingine wamlaumu wakati walipaswa kulaumiwa wao" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Kwenye 10% ya fedha za Halmashauri, Serikali ilidhamiria kuwasaidia wananchi wa kawaida. Vijana, wakina mama na watu wenye ulemavu ambao hawawezi kukopesheka ili waweze kusaidika" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Bilioni 5.6 hazikuweza kupelekwa kwenye mfuko; Bilioni 1.7 hazikupelekwa kwenye mfuko kwenye baadhi ya Halmashauri; Cha kusikitisha Bilioni 88.42 hazikuweza kurejeshwa kwenye mfuko. Kwanini hizi fedha zisingepelekwa kwenye Zahanati? Kuna Vijiji havina Zahanati, hakuna vituo vya afya " - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"TRC, SGR. Dosari zilizobainishwa katika ununuzi wa vichwa na mabehewa ya Treni, TRC ilikataa zabuni mara mbili ya Dollar za Marekani 263,460,514 yasiyo na ushindani ikapelekea kufikia Dollar 478,507,468 naaaa kusababisha ongezeko la gharama Dollar 215,000,046 ambapo ni sawa na Tsh. Bilioni 550" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Shilingi Bilioni 550 ukiipeleka kwenye vituo vya afya ni sawa na vituo vya afya 1,100. Jimbo lote la Momba lingekuwa limepata vituo vya afya, Mkoa wote wa Songwe na Mikoa mingine yote ya Tanzania ingekuwa imepata kwasababu tu kuna mtu hakufuata utaratibu" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Watu wasiokuwa waaminifu waliopewa dhamana walioaminiwa na wanajificha kwenye kichaka cha dhamana walizopewa bila kujua kwamba wanaumiza Watanzania wenzao. CAG anasema kuna mambo tunayapata kwasababu watu kutofuata kanuni na maagizo" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Wapo viongozi wa juu ambao nia yao ni njema ambao wanataka kulisaidia Taifa lakini wachache walioaminiwa ni Wataalam, ni wabobezi wa kufanya kazi badala watumie utaalam wao kulisaidia Taifa wanatumia utaalam wao na dhamana yao vibaya na inawezekana hao watu wamesomeshwa kwa mkopo wa Serikali" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Hao ni wahujumu uchumi kama wahujumu uchumi wengine. Zipo sheria, watu wakikosa makosa kidogo tu wanachukuliwa hatua, kwanini hawa wengine hawachukuliwi hatua? Walikuja kwenye Kamati, taarifa yao iliyoletwa na CAG walikuwa wanaikataa na CAG alikuwa anawashangaa" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Watu wasiendelee kumuangusha Mheshimiwa Rais anapowaamini kwenye Mikataba. Wasifikirie Watanzania ni wajinga sana. Wasiendelee kutuhujumu sana wanalitesa sana Taifa hili. Siyo kwamba Taifa hili halina fedha, hiki kidogo kinachopatikana tukiweza kukitumia vizuri tukakifanyia kazi vizuri tungeweza kufika mbali" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Watu wachache wasikuwa na nia njema na mpenzi ya Taifa hili wanahujumu Taifa hili kujinufaisha pekee yao kwa manufaa yao pekee yao na kuendelea kututosa jambo ambalo si sawa" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba.

WhatsApp Image 2023-11-02 at 20.19.33.jpeg
 
Huyu ni wizi kama wenzi wenzie wa CCM, mikataba inasainiwa na mawaziri ambao ni wanaCCM wenzake, aache kuzunguka aseme kwenye huo wizi yeye hakupata kitu ndiyo maana anapiga kelele hapa
 
Back
Top Bottom