Serikali iwe makini na Lissu maana hana cha kupoteza

Yaani sasa tumemgunduwa huyu Lisu ni wa aina gani. Kiukweli kabisa kile anakifanya kwa sasa sio siasa ila kama ni mtaalam wa mambo ya kisiasa tunaweza kusema anatumwa na mabwana zake ktk siasa kuja kuchafua then wanasubiri what next..
Vipi kile alichofanyiwa yeye ni siasa, mbona kijana unajifanya kusahau... je na wewe unatumwa na mabwana zako? Haya mwazo yako ndio yanayotufanya tuitwe Shitholes.
 
Weka wazi mabaya aliyotenda badala ya majungu kwa vile anawakosoa. Kubalini kukosolewa mkijua kuwa ninyi sio Mungu, jibuni hoja kwa hoja. Hivi ndege ya serikali ikikamatwa yapaswa iwe siri?
 
Huwa najiuliza sana, hivi sisi wa Tz tumelogwa nini?. Tundu Lissu yeye anatuonyesha kuwa ile ni nyekundu kwa vielelezo, lakini unashangaa mtu mpumbavu anakuja na hadithi za ajabu ajabu na kusema ile ni nyeupe na si nyekundu kama anavyo sema Lissu bila vielelezo tunabaki tunakenua meno . Lissu kasema ndege imezuiliwa nje ya nchi na wanaotudai n.k, wajinga wajinga na wachumia tumbo wanasema Lissu ni adui wa Taifa na si mzalendo kwa Taifa, hivi nchi hii tunataka viongozi wanaotudanganya tu?. Watanzania wa sasa na hasa vijana hatuta kubali kuona ujinga kama huu ukiendelea maana tunahitaji kujenga future zetu, za watoto wetu na vizazi vijavyo. Ila tukumbuke pia Nchi hii ni yetu sote na si ya kikundi cha watu fulani au chama fulani n.k., Tuna hitaji maslahi ya Taifa letu ya lindwe vinginevyo huko mbeleni hatuta elewana. Mungu ibariki Tanzania na Mungu utulinde ili tuitendee haki nchi yetu bila kuangalia sura ya mtu wa nafasi ya mtu.
 
Njia ya ukimya na kutojibizana na Lisu ndio msumari wa mwisho kwenye maneno ya Lisu ifike mahali ajutie kazi zake bovu na akumbuke shida anawapa familia yake
Tatizo LA serikali yenu, kuna watu wana akili ndogo wanataka waongoze akili kubwa. Hii inawezekana Tanzania tu.
 
Nimekaa na kutafakari sana matendo anayafanya huyu Lisu na nimekuja na mawazo binafsi kwa vyombo vya usalama na mamlaka za juu za kiuongozi.

Ni lazima serikali itambue na kuelewa Tundu Lisu hakuanza leo kuikosoa serikali ila alianza zamani tofauti ya Lisu huyu wa awamu ya tano na Lisu wa awamu zilizopita ni kuwa Lisu wa awamu zilizopita hasa ya tano alipolipuka mahali alizimishwa na vitu tusivyovijua ama alikuwa akifanyia watu fulani kazi ambazo sisi hatuzijuwi lakini huyu wa awamu ya tano ndio sura ya yule yule wa awamu ya nne...

Yaani sasa tumemgunduwa huyu Lisu ni wa aina gani. Kiukweli kabisa kile anakifanya kwa sasa sio siasa ila kama ni mtaalam wa mambo ya kisiasa tunaweza kusema anatumwa na mabwana zake ktk siasa kuja kuchafua then wanasubiri what next..

Kiukweli kabisa kama kweli huyu angekuwa yule Lisu wa awamu ya nne basi huenda nilitegemea angemuunga mkono rais kwa kazi anaifanya ila badala yake sasa amekuwa kuwadi wa nchi za Magharibi akisahau kuna nyumbani na kwa dhambi anaifanya inaweza kuleta majanga makubwa ndani ya familia yake mwenyewe akalia na kukumbuka majuto ni mjukuu. Well hapa nilikuwa namuelezea tu aina ya huyu mtu.

Lisu amekata tamaa na kwa aina ya siasa ameifanya kwa kipindi kifupi ni dhahiri shahiri nafsi inamsuta na kutoamini kwanza kuwa hai na pili jinsi tukio limetokea. Lisu anaweza kutuficha kwa muda mrefu sana ila nina uhakika anajua dhambi yake na ni kwanini haya yote yametokea na ni kwanin amejivika koti la kuhukumu serikali ya Magu ndio ilitaka kumpoteza.

Katika hali kama hii ni bora serikali kujikita katika smartness yaku resolve issue bila kujibizana naye maana huyu bwana anajua kile anakifanya maana yupo katika hali ya kukata tamaa ameshaamua kama mbaya na iwe ila yeye anaharibu.

Mambo yanaendelea yamepangwa kwa ustadi mkubwa hivyo ni muhimu serikali badala ya kumjibu ikatafuta njia za kumfanya asisikie hamu ya kuongea na akaendelea na matibabu yake akiwa bubu na hili linawezekana.

Kiukweli mahali amefika sio pazuri na sisi kama serikali ni vyema kujipanga tukijua Tundu sio CHADEMA ila ni zaidi ya tunachokijua wapo washabiki wake mpaka CCM na tujiulize why?

Njia ya ukimya na kutojibizana na Lisu ndio msumari wa mwisho kwenye maneno ya Lisu ifike mahali ajutie kazi zake bovu na akumbuke shida anawapa familia yake..
Frankly speaking sijaona tatizo la Lissu. Lissu ni mtu pekee anayethubutu kutuhabarisha mambo magumu ambayo hakuna mtu anadiriki kuyaongea kwa kuogopa. Mambo yote aliyoongea yamedhihirika kuwa ni kweli. Mfano mikataba mibovu na kuibiwa madini aliongea mwaka 47, leo raisi kagundua ni kweli mikataba ni mibovu na tunaibiwa kweli kweli; ndege kukamatwa ni kweli imekamatwa na mpaka leo hatujaambiwa kama imeachiwa. Ametutahadharisha kuwa tunaweza kukuta yunawalipa acacia hela nyingi sana kwa kukamata makinikia na kuvunja mkataba bila kufuata utaratibu. Hatujapewa mrejesho kuhusu makinikia na hizo pesa ambazo barrick wamesema watatulipa. acacia wamesema hawatambui hayo mapatano na wamesema hawatalipa. Sana sana wanatuhadaa kwa kudai wanapata hasara na wamepunguza wafanyakazi na bla bla nyingi. tatizo la Lissu liko wapi. Ninonavyo acacia wanajenga hoja tu ya kuja kutukamua huko baadae. Labda mkuu unajua wameshatulipa? Kama wamelipa basi watakuwa wamekubali yaishe. Ila wazungu huwa ni washenzi sana wantumia weakness zetu kutukomoa. Tusubiri tuone kama alichoproject Lissu kama kitatokea. Alichosema cha uongo sijakiona kwa kweli. Isitoshe hivi kweli sasa hivi elimu ni bure? hospitali dawa zipo na bei yake ndogo? wanyonge tunapata raha sasa hivi? mafisadi kweli wameisha? Rushwa imeisha? Huduma hospitali za serikali zimebadilika? Kuna mama wa jirani yangu aligongwa na gari na likimbizwa hospitali fulani ya serikali muda wa saa mbili asubuhi mpaka saa nane hakufanyiwa kitu. Hakuna cha first aid wala nini. Wakamrefer muhimbili hiyo saa nane na kufika muhimbili wakawauliza mbona mmetuletea maiti. Wakati mama wa watu alikuwa anaongea ila kule kukosa huduma ya kwanza akafariki. Huduma bado tete. Ila nashauri tusiishie kulalamika tupige kazi tujiongeze wenyewe tusitegemee maisha bora ya mtu.
 
Kuna sehemu umesema sisi kama serikali, oh kumbe na wewe ni kiongoz wa serikali.

Ila mkuu, mbona hata kuandika hujui, hiyo kaz ulipataje? Au ndyo ile kamlete aje? Au umesahaulika kwenye vyet feki wewe? Kwa uandish huo huwez kuwa smart kuliko lisu labda utumie bunduki.

Halafu unasema ulitegeme tl amsifie jpm, kwa hyo hadi kuwaza pia unataka kila mtu awaze kama wewe? Hv wewe uko sawasawa kweli?

Ndo ushangae wako busy na Tundu Lissu alafu huwezi kuja hoja nyepesi ukadhani unaweza mshinda Lissu
 
Me nachokijua Lissu anaweza kua anapendwa na watu wengi kuzidi hata Rais so Waafrika Tupunguze chuki hivi vyama vitufanye tutoane roho
 
Mpaka mda huu naona nyuzi nyingi ni za Lissu sioni mkianzisha nyuzi za kumsifia Rais na bomoabomoa kujenga Reli kwa pesa za Ndani kukuza Uchumi mnaosema unakua kuzidi Nchi zote Afrika mashariki na kati
 
Vipi kile alichofanyiwa yeye ni siasa, mbona kijana unajifanya kusahau... je na wewe unatumwa na mabwana zako? Haya mwazo yako ndio yanayotufanya tuitwe Shitholes.
Alifanyiwa nini kwani. Wamedhulumiana wenyewe huko then mnakuja na mambo yenu ya kinyumbunyumbu hapa
 
Mgonjwa gani yupo kwenye press kila kukicha
Hayo mambo waachie wenyewe kijana. Chukua jembe ukalime, unateseka kwa jambo lisilo na faida kwako.

Kwenye siasa kuna makundi mawili tu.
1 tools
2 enemy
Nauhakika wewe tools tu! (Karai).
 
Weka wazi mabaya aliyotenda badala ya majungu kwa vile anawakosoa. Kubalini kukosolewa mkijua kuwa ninyi sio Mungu, jibuni hoja kwa hoja. Hivi ndege ya serikali ikikamatwa yapaswa iwe siri?
Mnafiki na msaliti kwa nchi yake basi
 
Back
Top Bottom