Hoja ya Nape kuwa Samia ameruhusu maandamano na kumrudisha Lissu nchini ni ya kipuuzi. Hivi anaelewa Katiba?

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,656
4,130
Ama kweli ujinga hauondolewi na taji/cheo (the crown does not change the mind). Nape ni mfano wa mtu mwenye cheo lkn mjinga.

Kauli kwamba "Lisu alikimbia nchi halafu Rais Samia kamrudisha",...." rais karuhusu maandamano" ....ni kauli zinzothibitisha jinsi Nape asivyo na uelewa wowote kuhusu katiba.

Kwa kumsaidia tu huyu Nape ni hivi, Katiba ndiyo msingi wa tawala zote duniani. Kilichofanyika awamu ya tano ni uvunjifu wa katiba na ndiyo sababu rais wa awamu ya tano aliitwa dikteta.

Kwahiyo hakuna maana yoyote kumshukuru Samia kwa kuheshimu katiba. Huu ndiyo wajibu wake wa msingi na aliapa kufanya hivyo. Kinachofanywa na Nape ni kiashiria cha hulka iliyopo ndani yake ya kupenda kuendesha mambo kidikteta.

Nape aonywe na akemewe.

#NchiNiYetuSote!

Pia soma
- Nape Nnauye: Nashangaa Watanzania wanaokwenda kusikiliza upuuzi wa Lissu. Tumkemee, tumtenge na tumlaani
 
Labda Nape pia angesema sababu zilizo mfanya huyo Lissu kwenda huko nje? haya mambo wakati mwingine ni kunyamza tu kama busara inavyotaka , lakini hii kujitutumua, inawasaidia wazidi kujianika tu. Mjadala umekuwa mrefu kwa maneno ya Nape, na wao ndio wenye serikali. Sio kila jambo linahitaji kujibiwa, busara wakati mwingine ni kukaa kimya na kupotezea.
 
Nape kaongea ukweli mchungu huyu mama leo hii akitaka msifanye maandamano hamtafanya na hakuna lolote mtafanya kama kipindi cha magufuli. Ni hiyohyo katiba ndio inampa nguvu raisi.

Hivyo huyo Lisu anapaswa kuwa na kiasi sio kwamba kisa wameachiwa uhuru ndio wanajiachia, uhuru unaweza kuchukuliwa kama mwanzo na kusiwe na lakufanya.
 
Back
Top Bottom