Serikali iwachukulie hatua hawa Maaskofu wa KKKT kwa kuleta fujo katika Jamii ya waumini

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,336
24,232
Hii sasa ni hatari kwa mustakabali wa amani nchini.

Inavyoonekana kuna kikundi cha Maaskofu ambao wameamua kuleta ufarakano ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Tanzania-KKKT.

Hili kundi yumo Askofu Bagonza wa Karagwe
Askofu Mwaipopo wa Jimbo La Ziwa Tanganyika, Sumbawanga
Na sasa amengia hilo kundi Askofu aliyetimuliwa Dr Mwaikali aliyekuwa Konde
Askofu mstaafu Isaya Mengele wa Kusini Njombe

Serikali ikilifumbia macho suala hili yatatokea yale ya KKKT Meru na Jimbo la Kaskazini miaka ya 90, ambapo watu waliuwawa.

Kuna Maaskofu wamelifanya Kanisa, hasa Dayosisi kuwa mali zao na familia zao, na kuteteana hata kama maovu ya dhahiri yanaonekana.

Serikali isiogope kutumia maguvu yake pale inapoonekana kuwa hali ya amani inataka kutoweka

Mbona kwa vyama vya siasa serikali inachukua hatua haraka?

1648197186153.png


1648197391790.png


1648197575515.png


mengele.jpg
 
Dini ijikite kwenye UTASHI na UBINADAMU tu.

Ijiondoe kwenye TAMADUNI!

hivyo
1.kusiwe na majengo ya Ibada wala Taasisi zake, watu wasali majumbani mwao.

2. Kusiwe na Salamu za kidini bali za ubinadamu

3. Kusiwe na Mavazi ya kidini

4. Kusiwe na majina ya kidini

5. Kusiwe na kutekwa hisia za kupenda nchi za wenye Dini.

Kusiwe na salama mawili kwenye ngozi wala uvaaji wa viashiria vya kidini, mfano unaijua.

6. Kusiwe na mikudanyiko ya kidini bali wahubiriane kwa kusomeana maandiko kwa level za kaya tu.

7. Mahakama, Police, Bunge na Sovereign States wasiulize wala kuapisha watu kwa Dini zao!

Tamaduni za asili katika, kula kuvaa, na Sherehe kuimarishwe ili kuondoa viashiria vya Dini.

Kila Lakheri kwa kila nchi yenye mwenendo huu!
 
Huu mgogoro upoje? kila siku nasoma malalamiko tu humu,mbaya zaidi kila malalamiko ni kipande cha taarifa.Tatizo ni nini?
Kuna Maaskofu wamejigeuza kuwa wao ndio dini, na Katiba zao zinawalinda wakae milele kwenye viti vyao hata kama wamefanya madudu ya kutisha hasa wizi wa fedha za waumini.

FEDHA za Yuda Iskariote wanazopewa ndiyo zinawapa ukuu usiopimika!
 
Kuna Maaskofu wamejigeuza kuwa wao ndio dini, na Katiba zao zinawalinda wakae milele kwenye viti vyao hata kama wamefanya madudu ya kutisha hasa wizi wa fedha za waumini.
FEDHA za Yuda Iskariote wanazopewa ndiyo zinawapa ukuu usiopimika!
Je kuna ushahidi wa dhahiri wa hizo tuhuma? kwanini baadhi yao bado wapo kwenye nafasi? je Mamlaka kuu ya kanisa haioni hayo?

Huyo Dr mwaikali nimesoma ametenguliwa lakini hapa imeandikwa kaingia kwenye kundi hilo,je mtu ambaye katenguliwa mamlaka hayo anayatoa wapi?
 
Je kuna ushahidi wa dhahiri wa hizo tuhuma? kwanini baadhi yao bado wapo kwenye nafasi? je Mamlaka kuu ya kanisa haioni hayo? Huyo Dr mwaikali nimesoma ametenguliwa lakini hapa imeandikwa kaingia kwenye kundi hilo,je mtu ambaye katenguliwa mamlaka hayo anayatoa wapi?
Soma gazeti a Mwananchi leo
 
Mawazo ya kijinga sana, Serikali inapaswa kukaa mbali kabisa na kuingilia mambo ya kidini.
 
Wewe ndiye mjinga zaidi kwa sababu hujui watu kuwekwa ndani tu wakati sio wafungwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Mkuu bora nawe ukawekwa ndani kwa hiari kuwasindikiza hao Maaskofu wanaochochea vurugu.
 
Back
Top Bottom