Serikali isikubali mtafaruku wa Bandari kuchukua mkondo wa kidini, ni ngumu kuidhibiti

Imetosha, Muafaka chanya upatikane.

Tuzingatie kwenye hili hakuna mshindi, Ila mshindi awe ni taifa. Kuzozana kwetu kuwe kwaajili ya maslahi ya Nchi.

Muungwana akivuliwa nguo huchutama. Kurekebisha ulipokosea sio kujiabisha Bali ni uungwana. Na uungwana ni vitendo.
Hili ndilo la msingi ingawa ni gumu kwa wahusika!!
 
Leo kanisani tumeelezwa maana muungano wa Tanganyika na Zanzibar wengi tulikuwa hatujui chanzo cha huo muungano, Na serikali ilikuwa haijawahi kusema au kuandika mahala popote pale.

Kama gov haijawahi kusema wala kuandika kipi kinayapa hayo maneno ya kanisani uhalali?
 
Nyie vitoto ni wajinga

Wazee kina dr slaa wanaongea uzalendo kulinda bandari nyie mnawalamba makalio watawala
 
Nyie vitoto ni wajinga

Wazee kina dr slaa wanaongea uzalendo kulinda bandari nyie mnawalamba makalio watawala

Kila mmoja anangumzia Uzalendo. Pande zote Mbili. Ni ishu ya mtazamo.
Hapo ishu ni kuweka Mambo Sawa. Hayo marekebisho yafanyike, biashara iendelee. Ugumu unatoka wapi?
 
Umesema vema kiongozi. Ni jukumu sasa la viongozi wetu ususani mhe Rais kuchukua hatua stahiki na kurudisha umoja wa kitaifa ambao tunaona unapotea kwa kasi sana. Tusisubiri Sakata hili limwage damu hata ya mmoja wetu.
 
Najaribu kuwaza yani hivi ni kweli:
TLS-Imekosoa mkataba kisa mwekezaji mwarabu ama waislam na rais muislam
Wapinzani-Wamekosoa mkataba kisa mwarabu ama waislamu na rais muislam
Wabobevu wa Kisheria-Wamekosoa kisa mwarabu ama waislamu na rais muislam
TEC- Wamekosoa kisa mwekezaji mwarabu ama waislam na rais muislam

Unaona kabisa hii agenda ya kuingiza dini ni Upuuzi tu. Ila uko umuhimu wa mkataba kuwekwa sawa, na kusahau mambo ya kidini.
 
Kum 16:19 SUV
Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki.
Kwa nguvu kubwa wanayoitumia hawa watawala kwenye hili suala, lazima kutakuwa na Rushwa /kuhongwa somewhere.
 
Hao TEC walitakiwa kukemewa na waraka ungezuiwa kusomwa kanisani.

Toka day one hili jambo lilikuwa na sura ya Kidini, kwingine ilikuwa ni kujifichia ila Sasa ndio imejitokeza wazi.

Naendelea kusisitiza , Wakatoliki Huwa Hawataki Rais wa.dini nyingine na akitokea lazima wataleta nongwa.

Watatafuta upenyeo kuleta fitina na Sasa wamepata jambo la Bandari,Rais ana nia njema ila Sasa wanataka wamtoe Kwa njia hiyo.

Pascal aliwahi andika Mwanzo kabisa wa Utawala Wa Rais Samia kwamba ataziweza fitina za Watanganyika?
Tuachane na dini zetu mkuu. Vipi we unaona mkataba upo sawa?
 
Kiongozi anapokosa weledi wa kuliongoza taifa, haya ndio matokeo yake. Siku zote tatizo linatakiwa kufanyiwa kazi pale ambapo dalili pekee zinaanza kujionesha juu ya jambo husika, na sio kuamini upepo tu utapita!.

Kiongozi mzuri lazima ajue kutazama reaction ya watu wake, agundue tatizo lilipo, na ajue namna ya kulikabili, kabla halijawa kubwa zaidi na kugeuka gumu kulitatua.

Sasa pale ambapo kiongozi katikati ya tatizo anajitokeza hadharani, anasema ametuzibia masikio, huyu anaonesha vile hajielewi binafsi, hawaelewi wale anaowaongoza, na wala hajui namna ya kutatua matatizo yao.

Matokeo yake sasa, wengi zaidi wanaibuka kuupinga mkataba tofauti na mwanzo, na kadri siku zinavyozidi kwenda mambo yanazidi kuwa magumu, asijue tena ahangaike na kundi lipi, matokeo yake anazidi kupotea.

Frankly speaking, Samia anatakiwa kujiuzulu nafasi yake, amepwaya sana, ameiacha nchi ijiendee tu, yupo yupo tu, sasa haaminiwi na wale anaowaongoza, naamini hata nae hana habari nasi, yeye kwa sasa yupo na baraza lake la mawaziri, na waarabu wa Dubai.
honestly speaking huyu mama hakutakiwa kuwa makamu to begin with, mbona wanawake wa kiislamu wenye uwezo wapo wengi, walishindwa nini kuwachukua hao ........?

next time the power that be wanapochagua kiongozi waangalie na maadili yake, wengine ni corrupt kuanzia maadili, elimu, hata tabia!
 
Back
Top Bottom