BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Mfano mvua iliyonyesha jana tarehe 5 Mei, 2023 eti imesababisha tubadilishiwe ruti na nauli ipande, je hii ni sawa?
Mwezi uliopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuja akiwa katika ziara kuzindua mradi wa maji, wakampitisha Njia Nne ambapo kuna lami.
Hivyo hakuona uhalisia wa njia yetu ya huku Goba Mpakani.
Huku daladala ni chache na wakati wa mzua zinabaki chache zaidi au wakati mwingine hazipo kabisa, hivyo tunakuwa tunategemea usafiri wa Bajaj ambapo kutoka Mbezi Mwisho nauli huwa ni shilingi 1,000.
Mtu unatoka na bajeti zako umepanga, unakuta nauli wanakwambia shilingi 1,500 na wakati mwingine hadi shi;ingi 2,000 hii si sawa, kwani hata ukisema utembee ni mbali na si salama.
Shida ni barabara haichongwi mara kwa mara na ina madimbwi mengi sana yanayosababisha mvua kubwa ikinyesha kunakuwa na ugumu wa kupitika kwa sababu yanajaa sana maji.
Pia soma>> Baada ya Mdau wa Jamii Forums kulalamika, Serikali yaanza kuboresho ya Barabara ya Goba - Mpakani