Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 941
Katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Martha Nehemia Gwau aliuliza swali lililojibiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile na kusema kuwa Serikali iko mbioni kujenga uwanja wa ndege wa daraja 2C
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Martha Nehemia Gwau alitaka kufahamu ni lini Serikali itajenga uwanja wa ndege wa Singida. Ambapo Naibu Waziri Kihenzile amemuhakikikishia kwamba eneo lililopo kwa sasa ni hekta 49.1 na tunahitaji kuongeza hekta 97.8.
"Tunaendelea kushirikiana na Kamishina wa ardhi Singida kutwaa ardhi hiyo. Katika Mwaka wa fedha 2024/2025 tutatenga fedha kwa ajili ya uhuishaji wa usanifu wa kina ili kuwa na mahitaji ya kiufundi na mara baada ya hatua hii kukamilika serikali itatenga fedha kuanza utekelezaji wa mradi" Kihenzile
Mhe. David Kihenzile amesema kuwa lengo pia ni kuhakikisha kiwanja hiki kiwe na daraja la 2C ili kuongeza uwezo wa kubeba ndege kubwa pia zenye abiria 50.