Serikali ielekeze jicho kali Wizara ya Ujenzi, TANROAD na TARURA

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Kutokana na miradi ya ujenzi ya barabara na madaraja kuwa na viwango vya chini sana vya ubora, Serikali ielekeze jicho kali Wizara ya Ujenzi, TANROAD na TARURA.

Miradi hiyo inajengwa chini ya viwango kutokana na wale walioaminiwa na serikali (wakaguzi wa miradi hiyo) kula njama kwa kupewa rushwa na wakandarasi wakati wa ukaguzi.

Hii imepelekea wahusika waliaminiwa na serikali kushindana kwa ukwasi wanaopata kwa njia ya rushwa.

Barabara na madaraja zinazojengwa hazidumu au hata kuonyesha ubovu kabla mradi haujaishi kukabidhiwa. Serikali iwafuatilie wahusika wapokea rushwa na wanapobainika waondolewe kazini kabisa na si kuhamishwa.

Nawasilisha.
 
Tuwape tenda wazungu, hizi tenda hazikuubwa kwa ajili yetu. Si kwa kuiba huku.
 
Kutokana na miradi ya ujenzi ya barabara na madaraja kuwa na viwango vya chini sana vya ubora, Serikali ielekeze jicho kali Wizara ya Ujenzi, TANROAD na TARURA.

Miradi hiyo inajengwa chini ya viwango kutokana na wale walioaminiwa na serikali (wakaguzi wa miradi hiyo) kula njama kwa kupewa rushwa na wakandarasi wakati wa ukaguzi.

Hii imepelekea wahusika waliaminiwa na serikali kushindana kwa ukwasi wanaopata kwa njia ya rushwa.

Barabara na madaraja zinazojengwa hazidumu au hata kuonyesha ubovu kabla mradi haujaishi kukabidhiwa. Serikali iwafuatilie wahusika wapokea rushwa na wanapobainika waondolewe kazini kabisa na si kuhamishwa.

Nawasilisha.
Mkuu ungelitoa na mifano kabisa ili mada itendewe haki
 
Ulicho ongea ni kweli Kuna barabara moja ipo wilaya x ilichongwa bila mitaro ya maji sahivi ina week hata mkandarasi hajaikamilisha mvua ishaiaribu na Kuna vipande hakuchonga kabisa na juzi kati naona kapakia vifaa kaanza ondoka site nadhani kashachukuwa chake
 
Mkuu ungelitoa na mifano kabisa ili mada itendewe haki
Ndugu yangu tatizo hili liko sehemu nyingi sana, maafisa wa Wizara ya Ujenzi, TANROAD na TARURA walioaminiwa na serikali kukagua miradi hiyo wanapokea 10% kwa wakandarasi na kuipitisha miradi hiyo bada ya kupata chao. Hawa ndio wanaoigombanisha serikali na wananchi, hawa ni whujumu uchumi walio ndani ya serikali yenyewe. Serikali ilichunguze suala hili na wanaobainika kufanya hivyo waondolewe kabisa kazini na si kuhamishiwa penginge.
 
Fedha nyingi sana inatumika kwenye miradi ya ujenzi wa barabara, madaraja na majengo ya serikali lakini ujenzi huo unakuwa chini ya kiwango. Tukatae suala hili la uvujaji wa fedha za serikali unaofanywa na wachache wasio waaminifu.
 
336679869_747263253594989_8301807931657672152_n.jpg

Ghana wamefanya hivi, Kuna barabara yoyote ya mfano iliyojengwa kwa ustadi nchi hii hadi kuwapa ujiko TANROAD na shavu kwa TARURA? 🤔
 
Ukiwa unajua Jambo moyo unakwambia kuwa kimya usiongee. (Tz is a master of reverse projects)
Inabidi iwe hivi: TARURA/TANROAD welete wazo lipite Wizara ya fedha, arafu liende kugafanyiwa kaza (implementation) Alafu tender itangazwe apatikane Mkandras , MWISHO mwananchi afaidike na kulipa kodi (hiyo ndo circle halis), LEO SASA, mkandras atengeneze demand/deal apeleke TARURA/TANROAD, ALAFU NDO LISOGEZWE MBELE mpaka mkandras apate kazi aliyoianzisha yeye. Alafu unadai ubora utoke wapi. Wachina na Waarab wanaongoza kutoa rushwa na kuleta deal kwa nchi afu eti upate ubora anakuzid ufaham wa MRADI anaokuletea then uta challenge vipi?.
Nitaanzisha chama cha wazee WASTAAFU (CWW) katika "All field quality control _AFQC . hawa wanakuwa wameishapunguza tamaa, na ni Sehem ya worship yao kutenda wema. (Kama NGO).
FB_IMG_1679420626388.jpg
FB_IMG_1679554151172.jpg
IMG_20230323_162947_MP.jpg
FB_IMG_1679546845614.jpg
 
Ukiwa unajua Jambo moyo unakwambia kuwa kimya usiongee. (Tz is a master of reverse projects)
Inabidi iwe hivi: TARURA/TANROAD welete wazo lipite Wizara ya fedha, arafu liende kugafanyiwa kaza (implementation) Alafu tender itangazwe apatikane Mkandras , MWISHO mwananchi afaidike na kulipa kodi (hiyo ndo circle halis), LEO SASA, mkandras atengeneze demand/deal apeleke TARURA/TANROAD, ALAFU NDO LISOGEZWE MBELE mpaka mkandras apate kazi aliyoianzisha yeye. Alafu unadai ubora utoke wapi. Wachina na Waarab wanaongoza kutoa rushwa na kuleta deal kwa nchi afu eti upate ubora anakuzid ufaham wa MRADI anaokuletea then uta challenge vipi?.
Nitaanzisha chama cha wazee WASTAAFU (CWW) katika "All field quality control _AFQC . hawa wanakuwa wameishapunguza tamaa, na ni Sehem ya worship yao kutenda wema. (Kama NGO). View attachment 2563497View attachment 2563498View attachment 2563499View attachment 2563500
Hivi ninaweza kupata majibu kwa nini madarasa ya nayojengwa kwa shule za msingi na sekondari za serikali, mafundi wanalaza Matofali kuanzia kwenye msingi mpaka juu ya renta??

Kwa ujenzi wa namna hiyo unaweza kupata Karibu ya mara mbili ya darasa!!! Na kwenye "manunuzi na ugavi" tumeambiwa tusizidishe asilimia 15 ya gharama.

Naomba majibu tafadhali.
 
Back
Top Bottom