Serikali iachane na chaguzi ndogo - Mtatiro

Nakubaliana na Mtatiro, ni mahela mengi yanatumika!

Ukizingatia wabunge wetu wengi above 50 and 60 ni hatari sana, tunaweza kujikuta kuna mwaka tunafanya chaguzi 10!
 
...nahisi harufu ya umafia kwa washindi wa kwanza kuuwawa ili wa pili achukue jimbo.
 
Gaijini bwana we umeona pesa zina potea kwenye chaguzi ndogo.vp kuhusu kulipana posho,Ulipaji wa zabuni za umeme kam Iptl,Dowans,Songas na mengineo,vp kuhusu wizi wa Eppa,mikataba mibovu ya madini na matanuzi makubwa ya viongozi wa serikali. Au we umeona uchaguzi mdogo tu ndo unapoteza pesa za serikali.
 
kunavichaa wa viwango tofauti,kichaa cha mhe,lusinde kama alivyojiita na ndivyo kichaa cha mtatiro kina aina yake.do!hata kama ni uhuru wa kutoa maoni,maoni haya yana roho ya gubu
 
Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.

Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.

Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.

Source: MWANANCHI

Ninakubaliana na Mtatiro kuhusu pesa nyingi inayotumika katika kuandaa chaguzi ndogo lakini sikubaliani nae pendekezo la kurithishana kichama. Kwani wananchi wanapopiga kura hawachagui chama bali wanachagua mgombea.

Kwahiyo kama mgombea waliyempenda na kumchagua amefariki, wanayo haki ya kuchagua mtu mwingine wa kuwawakilisha, chama hakiwezi kupora madaraka ya wananchi na kuwachagulia muwakilishi wao.

Jambo la msingi kwa sasa ni kuhakikisha kwamba kunakuwa na udhibiti wa matumizi makubwa ya fedha katika chaguzi zetu. Kwakuwa sheria ya gharama za uchaguzi ipo ni vizuri vyombo husika yaani serikali, vyama vya siasa, msajili wa vyama vya siasa pamoja na vyombo vya dola vikasimamia utekelezaji wa sheria hiyo, na kama ina mapungufu ifanyiwe marekebisho ili tuweze kudhibiti matumizi makubwa na yasiyokuwa ya lazima katika chaguzi ndogo.

Tatizo lililopo katika utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi kwa sasa ni kwamba watumiaji wakubwa fedha nyingi katika chaguzi ni ccm kwahiyo serikali na msajili wa vyama wanashindwa kuiwajibisha.

Ushauri kwa mdogo wangu mtatiro, aache kuwaza ki-ccm, ni muhimu akajitahidi kuwa na mawazo ya kimapinduzi na mtazamo wa mageuzi wenye kuruhusu demokrasia shirikishi. Kutoa wito wa kutaka chama kiteue muwakilishi wa wananchi bila ridhaa yao huo ni uvunjwaji wa makusudi wa demokrasia kwa wananchi kumchagua muwakilishi wao. Kama cuf nayo imefika mahali sasa inataka kufifisha mamlaka ya umma, basi huko inakoelekea ni kaburini.
 
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?

Hii nayo pia itasababisha watu kuzuliana mizengwe au hata kupanga njama za kuuana ili tu kukidhi haja ya kuwa mbunge.
 
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?

Mkuu hapa si watakuwa wanauana ili nafasi ipatikane? Refer Kiwia/Machemli case. Just thinking loudly!
 
Anasema baada ya Chadema kushinda? Wanamtungua jicho!

Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.

Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.

Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.

Source: MWANANCHI
 
kwa kuweka utaratibu wa mshindi wa pili achukue jimbo pindi mbunge akifa.nadhani wabunge wengi watakua kwenye hatari zaidi ya kufa hasa ukizingatia chaguzi nyingi zinakuwaga za mizengwe.
 
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?

kwa statement yako watu watawekeana bifu na matukio ya vifo kwa wabunge yataongezeka,mtu anakuvizia anakupa ya chemba unatapka damu wanasema majambaz wamekuvamia.kumbe ni dili
 
Tusipoangalia hii hoja imetoka kwa nani, nadhani tunaweza kuijadili vizuri.

Serikali inaingia gharama sana na hizi chaguzi za kila siku. Watanzania tunakufa mno na nafasi za kuchaguliwa ni nyingi mno vile vile. Miaka mitano hii tutafanya chaguzi mpaka tutakinai

Kuna Muakilishi wa CCM kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar jimbo la Bububu amekufa mwezi uliopita, mwezi ujao kutakuwa na uchaguzi huko

Tunahitaji kukaa chini kama taifa na kutafakari namna ya kuokoa hizi fedha zinazotumika kwenye chaguzi ndogo

"Ukipenda waridi penda na miiba yake" na hii gharama ndo miiba ya democracy!
 
Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.

Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.

Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.

Source: MWANANCHI

Huyu Mtatiro vipi?ni mambo mangapi yasiyo na tija yanafanywa kwa hela za walipa kodi na yeye ameliona ili la chaguzi ndogo tu ambalo Watanzania wengi tunaliona lina tija?eti analeta mifano ya vi nchi viwili,mbona nchi nyingi duniani zinafanya utaratibu wa chaguzi ndogo?anataka kulazimisha eti ateuliwe mtu kutoka chama kile kile,kama hana uwezo je?hasitake kutuletea u***** wake huyu Mtahaira!
 
Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.

Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.

Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.

Source: MWANANCHI

Arithiwe na mgombea aliyemfuatia kwa wingi wa kura, kwakua ndiye chaguo la pili la wananchi (kama hakukuwa na uchakachuaji), na si kurithiwa na mtu kutoka chama chake ambaye wananchi hawamjui wala hawakumpigia kura zozote kumchagua. Kwani ukidesa Msumbiji au Ghana, ndo ukopi mpaka jina la mtahiniwa!
 
Ninakubaliana na Mtatiro kuhusu pesa nyingi inayotumika katika kuandaa chaguzi ndogo lakini sikubaliani nae pendekezo la kurithishana kichama. Kwani wananchi wanapopiga kura hawachagui chama bali wanachagua mgombea.

Kwahiyo kama mgombea waliyempenda na kumchagua amefariki, wanayo haki ya kuchagua mtu mwingine wa kuwawakilisha, chama hakiwezi kupora madaraka ya wananchi na kuwachagulia muwakilishi wao.

Jambo la msingi kwa sasa ni kuhakikisha kwamba kunakuwa na udhibiti wa matumizi makubwa ya fedha katika chaguzi zetu. Kwakuwa sheria ya gharama za uchaguzi ipo ni vizuri vyombo husika yaani serikali, vyama vya siasa, msajili wa vyama vya siasa pamoja na vyombo vya dola vikasimamia utekelezaji wa sheria hiyo, na kama ina mapungufu ifanyiwe marekebisho ili tuweze kudhibiti matumizi makubwa na yasiyokuwa ya lazima katika chaguzi ndogo.

Tatizo lililopo katika utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi kwa sasa ni kwamba watumiaji wakubwa fedha nyingi katika chaguzi ni ccm kwahiyo serikali na msajili wa vyama wanashindwa kuiwajibisha.

Ushauri kwa mdogo wangu mtatiro, aache kuwaza ki-ccm, ni muhimu akajitahidi kuwa na mawazo ya kimapinduzi na mtazamo wa mageuzi wenye kuruhusu demokrasia shirikishi. Kutoa wito wa kutaka chama kiteue muwakilishi wa wananchi bila ridhaa yao huo ni uvunjwaji wa makusudi wa demokrasia kwa wananchi kumchagua muwakilishi wao. Kama cuf nayo imefika mahali sasa inataka kufifisha mamlaka ya umma, basi huko inakoelekea ni kaburini.

Mkuu umemaliza kila kitu,kama Mtatiro ataiona hii hoja yako atajiona ni jinsi gani alivyo kiongozi aliyekosa maono,asante 7ana mkuu
 
KAFU ingekua inashinda, angesema serikali ifikirie kuwa na chaguzi ndogo hata kama wabunge hawajafa... LOL

Nilikua namwamini sana mtatiro alipokua pale udsm,alikua mpinaganaji hasalakini toka apewe rungu cuf naona ameshindwa kupambana.chama kimekosa muelekeo.I think yeye kuwa cuf it was a wrong choice,
 
Mtatiro usichanganye umma. South africa na baadhi ya nchi za africa wanachagua chama na chama ndo kinamteua mwakilishi wake kwenye urais, ubunge nk. Hawa wanao uwezo na haki ya kumteua mrithi pale anapo kufa wa awali. Sie tunachagua mtu anaye pendekezwa na chama. Akifa lazima vyama vipendekeze tena na umma umchague mmoja wapo.
Huyu jamaa Mtatiro ana akili fupi, hapo ndio uwezo wake wa kufikiria umeishia. Yeye ni mtu wa kutumwa tu pale CUF hawezi kujiamulia mambo yake mwenyewe ndio maana anataka kugeuza watanzania wote kuwa watu wa kutumwa na CCM. Faida ya chaguzi ndogo sio tu kupata mbunge lakini pia zinawezesha kujua upepo wa kisiasa nchini, mfano kwa sasa tumejua kuwa watanzania hawaitaki CCM na 2015 wanaizika kaburini
 
Kwani chama cha mtatiro bado kipo? Kwanini hawakuungana kuweka nguvu ya kupata KATIBA mpya? Haya mambo hayawezi kufanyika kutoka mawazoni mwa watu. Kuna mapendekezo mengi yenye uzuri na ubaya wake katika kukwepa gharama nizo. Ila kwa katiba ya sasa hiyo ndiyo demokrasia.

Tunajua hawezi kusema mshindi wa pili ateuliwe kuongoza, maana sasa CUF inakuwa ya tatu kuendelea. Ref. chaguzi za karibuni (Igunga-Tabora, Uzini-Unguja), na hapo walikuwa hawajasambaratika bado. Tunamshauri wakakijenge chama chao kwanza. Hatuwezi kukubali mawazo ya watu waliochangia kuuwa chama chao, tukiwakumbatia hawa tutabomoa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom