Serikali iachane na chaguzi ndogo - Mtatiro

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.

Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.

Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.

Source: MWANANCHI
 
Kweli huyu ni vuvuzela la ccm, yaani! Baada ya ccm kuona hali ni tete, ndicho walicho kutuma?
 
Wengine wanasema, 'aliyekuwa mshindi wa pili ndio akabidhiwe jukumu'. Mimi nasema yote ni mawazo mazuri, lakin inabidi yatekelezwe kwa tahadhari. Ni mpaka tutakapokuwa na Tume Huru ya uchaguzi, uchaguzi huru na wa haki, sheria nzuri za uchaguzi na katiba bora, ndio mambo haya yatakuwa na mashiko zaidi.

Nadhan itakuwa busara kama tutayaangalia mambo haya kwenye mchakato wa katiba MPYA. Na lazima tutayaangalia tu
 
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?
 
Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.

Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.

Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.

Source: MWANANCHI

If democracy has to take its course huwezi kuwapa watu mtu ambaye hawakumchagua. Mtatiro should make a distinction between a party and a party contestant- In Africa, people choose people and not parties
 
  • Thanks
Reactions: Zed
Hilo wazo kapewa na CCM, maana ndio mpango wao. Kwa isiwe kwamba mbunge akifa aliyemfuatia kwa kura akapewa ubunge kwa kuwa pia alichaguliwa na baadhi ya watu? Na iweje kama uchaguzi unatenguliwa? CCM A ikiacha kumwaga rushwa, kutumia raslimali za umma, ghara za chaguzi ndogo zitapungua
 
Mtatiro usichanganye umma. South africa na baadhi ya nchi za africa wanachagua chama na chama ndo kinamteua mwakilishi wake kwenye urais, ubunge nk. Hawa wanao uwezo na haki ya kumteua mrithi pale anapo kufa wa awali. Sie tunachagua mtu anaye pendekezwa na chama. Akifa lazima vyama vipendekeze tena na umma umchague mmoja wapo.
 
wivu wa kijinga huu

serikali iachane vipi na utaratibu huu bila ridhaa ya wananchi ambayo ni sheria itokanayo na katiba ya nchi

angeshauri wananchi watoe mapendekezo ya kuridhia utaratibu wa mrithi wa kiti cha ubunge kwenye mchakato wa katiba mpya unaotarajiwa kuanza

again .... poor thinking
 
Kumbe mtu unaweza kuwa taahira ukubwani? Sasa huyu naye ametumwa kuisemea CCM? Au kwa vile ni mke wa magamba? Uchaguzi mdogo haukwepeki. Vinginevyo tuseme kama Mbunge akifariki basi mgombea wa chama kilichoshika nafasi ya pili achukue nafasi hiyo moja kwa moja kwa maana huyu naye alikuwa anatakiwa na wananchi. Shida inayoambatana na hili ni ujuzi wa magamba kutumia Pollolium, sijui kama watu watabaki?!!
 
Demokrasia ina gharama zake brother. Sasa huyo wa kuteuliwa atakuwa na tofauti gani ni kina Vicky Kamata?

Labda tuwe tunachagua kama raisi na makamu wake, at least tunajua tunachagua mtu na atakayemrithi kama kutakuwa na tatizo. Kuteuana, hell no.

umenena mkuu
 
Tusipoangalia hii hoja imetoka kwa nani, nadhani tunaweza kuijadili vizuri.

Serikali inaingia gharama sana na hizi chaguzi za kila siku. Watanzania tunakufa mno na nafasi za kuchaguliwa ni nyingi mno vile vile. Miaka mitano hii tutafanya chaguzi mpaka tutakinai

Kuna Muakilishi wa CCM kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar jimbo la Bububu amekufa mwezi uliopita, mwezi ujao kutakuwa na uchaguzi huko

Tunahitaji kukaa chini kama taifa na kutafakari namna ya kuokoa hizi fedha zinazotumika kwenye chaguzi ndogo
 
Wameona hali ni mbaya sana kwa upande wao na wanajua kbs endapa atakufa mbunge wao tayari watakua wameshapoteza jimbo kwani chadema watashinda.
 
Ni wazi anaandaa mazingira maalum ili CCM itakapoleta hiyo sheria haramu waseme hata wapinzani walipendekeza hivyo
 
Back
Top Bottom