Serikali iachane na chaguzi ndogo - Mtatiro

Ukimwonyesha hata mtoto wa darasa la kwanza ushauri huu atakuambia huyu mtu hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi kumi.
 
Huyu vipi si tunafikiria kuwabadilisha wanasiasa kabla ya kumaliza muda wao endapo haturidhii nautendaji wao tofauti hii ya sasa ya kusubiri afe ili uchaguzi mdogo ufanyike yeye anatuletea mipango ya ufalme na usultani hapa?walahi mpemba mie niliyejivua CUF miaka ilee na kuwa miongoni wa wanachadema wa mwanzo pande hizi sikukosea kamwe!
 
Tuogope gharama tutawaliwe nawasio chaguo la Wananchi? Turithishane tu Kama nchi ya kifalme, mbona watauliwa wengi. Tukubali tu gharama kwani ki uhalisia hawafi kivileeeee.
 
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?

Mkuu si watamalizana kwa kuuana? Kama ni kuokoa gharama jimbo libaki wazi hadi uchaguzi utakaofuata
 
Back
Top Bottom