Maganga Mkweli
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 2,089
- 829
inaumaa sana we are the victimof the systemHao walimu kuna wakati huwa wanakuja kuwatembelea wanafunzi wakati wa field. Mwalimu anafika field na wengi ni hao vijana anashanga tu naye haelewi chochote, mwisho wa siku anauza sura anaondoka zake. Wakati mwingine hata hawaji.
Wapo ambao ni wazuri, angalau walipata bahati ya kufanya kazi labda muda mfupi au walipata sehemu ya field nzuri. Lakini ukweli ni kwamba wanahitaji muda wa kutosha kushiriki kwenye projects mbalimbali ili waje kuwa walimu wazuri.
Serikali itambue kwamba kwa level ya university mwanafunzi anaandaliwa kufanya kazi, sasa kama wanaowafundisha hawajawahi kufanya hizo kazi tutakuwa tunacheza makidamakida.
Labda na suala lingine ni haya makampuni yaliyopo sababu ndio wanaoajili vijana wanapomaliza chuo, watuambie uwezo wa hao wanafunzi, na kama uwezo hawana wamechukua hatua gani. Sababu kuna makampuni mengi ambayo yamekuwa yakilalamika uwezo wa hao freshers lakini hawajaribu kusaidia kusolve hilo tatizo au kusaidia kutafuta kiini cha tatizo.
Tukumbuke kazi za Engineering zinacheza sana na maisha ya watu. Tusipokuwa na maandalizi ya msingi kwa vijana wetu tutakuja kupata madhara makubwa sana huko baadae. Serikali iache kufikiria siasa za kila siku badala yake iinvest kwenye Elimu.
bila wahandisi imara kweli bongo itaendelea
do politician hear this?