Sera mpya ya kusimamia ajira za walimu ifikapo Septemba 2023

mwakajingatky

JF-Expert Member
May 30, 2018
555
909
SERA MPYA YA KUSIMAMIA AJIRA YA WALIMU IFIKAPO SEPTEMBA 2023

Wasalaamu wapendwa, natumaini tuwazima wa afya
!

Nimesikia chama cha Walimu kimepinga vikali. Mimi nadhani kuna mambo tunachanganya. Tuna haja ya kuwa na chombo maalum cha kusimamia taaluma ya ualimu. Nikimanisha Bodi ya Ualimu.

Hii imekuwa danadana muda mrefu na siasa zimeingia na hata walimu walio wengi wanapinga kwa kigenzo cha eti kutakuwa na kulipia ada ya bodi. Wenzetu madaktari wanalipia ada ya bodi wenzetu manesi na mafamasia wanalipia ada ya bodi na kupewa lesseni. Hii leseni itasaidia kuleta ubora wa kazi na ndipo leseni zitafanya kazi. Na hakutakuwa na ubabaishaji wa kiendesha mambo kufuata siasa.

Sasa kuna hili la kusema walimu watakao ajiliwa (ajira mpya) kufanya mtihani. Hapo ndipo ubabaishaji mkubwa na siasa zinataka kuchukua mkondo wake. Huo mtihani utatoka wapi?

Huo mtihani utatungwa na nani?
Huo mtahani utapima nini?
Huo mtihani nani atagharimia?
Una walimu wa masomo tofauti tofauti. Unaposema wanafanya mtihani una manisha utakuwa na mtihani kila somo kila mwalimu?

Vyuo ndivyo vyenye mamlaka ya ku-train walimu na kujiridhisha pasipo shaka walimu wameiva na vyuo vimeenda mbali zaidi zimewapa mitihani wakafaulu na hata waliofeli wakarudia mpaka wafaulu.

Leo hii wanataka kuajiliwa wanaambiwa wafanye mtihani. Hapo kuna shida. Ina maana vyuo ndivyo vyenye ubovu mpaka kuto aminika na waajiri wanataka kuwapa wafanye mtihani.

Leo ukija na hoja ya kuwa walimu wafanye mtihani wanapo ajiliwa kwa kigezo eti hawana uwezo hapo haupo sahihi. Hata kama walikuwa na ufaulu mdogo wakasoma ualimu. Je unapowafanyisha mtihani ufaulu mdogo waliokuwa nao utakuwa umepanda?

Kuna awamu kadhaa Serikali ilisha kuwa na uhaba mkubwa wa walimu wakaazisha program za walimu wa Voda Fasta, mara certificate walimu wasome mwaka mmoja. Mara degree walimu wasome miaka mitatu badala ya minne. Mara kuna uhaba wa walimu wa Sayansi hivyo program maalum zikaanzishwa ili kusaidia upungufu.

SASA LEO
Baada ya kuonekana kuna kasoro nyingi kwenye elimu eti walimu wanaoanza ajira mpya wafanye paper

USHAURI WANGU
1. Mpaka sasa bado haijaeleweka kama kuwafanyisha paper walimu wa ajira mpya kutaongeza ubora wa elimu Labda hoja iwe wahitimu wa ualimu ni wengi mtaani kwa hiyo kuwapunguza ni kuwafanyisha mtihani.

Angalizo je ikitokea kuna uhaba tena hapo badaye tutafanyaje? Tutafuta mitihani?

2. Kama kiwango cha elimu kimeshuka ili kukipandisha kuna mambo mengi ya kufanya. Mojawapo ni kuanzisha chombo maalum cha kusimamia taaluma ya ualimu. YAANI BODI YA UALIMU. NA walimu watakuwa up todate. Watafanya mitihani ya bodi na watakuwa na leseni.

Nje ya hapo tunajidanganya ndiyo maana chama cha walimu CWT kimekuja juu kupinga hilo. Tusitegemee kufanya paper kwa walimu wa ajira mpya kutaondoa matatizo tuliyonayo sisi walimu yaani matatizo ya kitaaluma.

Asante.

Comments za kujenga tafadhari

By: Mwl Ndangalasi.
Fb: Mtoto wa mkulima.
 
Tatizo la ngozi nyeusi mateso aliyoyapitia yeye mbaka kufanikiwa ndio anataka nyote mpitie hayohayo na sio kuboresha wajao wapite njia Bora zaidi yake isiyo na mateso kama yake.
Hapo issue ni kufanya utaratibu wa kuajiri uwe sawa kwa kada zote ni mambo ya wivu tu na Siasa za wabongo ndio kichochezi Cha jambo hili
 
Wawape

Mishahara minono kuanzia M1 kuendelea kwa wanaoanza kazi

Wawape posho za kufundishia

Wawape posho za nyumba kwa wasiopewa nyumba ya shule.

Wawape posho za overtime.

Huwezi uka impose mambo magumu hivyo halafu unawalipa walimu laki 5. How comes!?

Wao wenyewe waone AIBU kwanza na nafsi ziwasute.

Sidhani kama Kuna ataona ikiwa hayo mambo hapo yakiwepo.

Unataka kuboresha elimu halafu unawasahau walimu it doesn't make sense.

Waache upuuzi
 
Walimu mnapenda sn kulia lia mbona coz nying sn wanafanya mitihan mfano wanasheria au hao wanaopigwa ma interview kila siku manesi ma dr husikii kelele ila nyie kila siku n malalamiko tu nahis ivi vitu ndo vinafanya hii fani ionekane n ya watu wa chini sn kwa kulalamika vitu vya ovyo haiwezekan afsa mifugo ana mshahara mdogo kuliko mwalim but utamkuta anaishi maisha ya juu sn ila mwalim yy n kulalamika tu mshahara hautoshi
 
Wawape

Mishahara minono kuanzia M1 kuendelea kwa wanaoanza kazi

Wawape posho za kufundishia

Wawape posho za nyumba kwa wasiopewa nyumba ya shule.

Wawape posho za overtime.

Huwezi uka impose mambo magumu hivyo halafu unawalipa walimu laki 5. How comes!?

Wao wenyewe waone AIBU kwanza na nafsi ziwasute.

Sidhani kama Kuna ataona ikiwa hayo mambo hapo yakiwepo.

Unataka kuboresha elimu halafu unawasahau walimu it doesn't make sense.

Waache upuuzi
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Yule profesa ni andazi
Mi ningekuwa nafatilia sana siku hizi bila shaka anawachukia walimu halafu Hana anachowasaidia Kila siku kuwananga na kutaka kuweka mazingira magumu kwa walimu.

Sijamsikia akiongelea maslahi ya walimu hata kama sio kazi yake yeye anaongoza wizara ya kisekta.

He should do something kama kweli ana Nia ya dhati kuiokomboa hii elimu yetu iliyo shaghalabaghala
 
Walimu ni washamba sana. Hadi mitihani ya usaili hamjawahi kufanya. Ninyi mnadekezwa sana bora AJIRA zenu ziingizwe Sekretarieti ya Ajira. Kufanya mitihani ya usaili ni utaratibu wa kawaida duniani. Walimu jaribuni kupata exposure basi.
 
Mbona ghafla walimu mmekuwa waoga hivyo?

Hamjiamini

Hamuamini mlichosoma



Serikali kazeni hivo hivo walimu vilaza watajiondoa wenyewe
 
Back
Top Bottom