SENGEREMA: Afisa TAKUKURU amlamba mwalimu makofi

Aisee kumbe na TAKUKURU nao wanaihati KATIKIKIRI iwachunguze.
Sasa si angetumia Lugha nzuri tu kumuambia,maana kama ni kusimama inawezekana lengo ilikuwa ni kumfahamisha pale kwenye utata.

Halafu sijui kwanini TAKUKURU mpaka issue itoke kwenye vyombo vya habari ndio wao waende wakachunguze,yaani haiwezekani wao wenyewe kuhisi sehem kuna kitu wafuatilie mpaka issue ikitolewa na wanahabari basi na wao mbioo.
Halafu Number yao waliotuma kwenye sim ya 113 kama sikosei naona majanga tu,yenyewe inatakiwa ichunguzwe
 
Huyo jamaa ni Mkuria nini.Natania tu.
Taarifa zilizonifikia ni kwamba;

Kama kichwa kinavyo jieleza tukio limetokea leo Halmashauri ya Wilaya ya BUCHOSA wilaya ya SENGEREMA MKOA WA MWANZA ambapo Afisa mmoja wa TAKUKURU amemlamba makofi mwalimu wa kike (jina linaifadhiwa) wa shule ya msingi (jina linahifadhiwa) wakati wa uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma wa Halmashauri hiyo kwa kosa la kusimama nyuma yake wakati zoezi likiendelea.

Afisa huyo anashikiliwa na polisi mpaka sasa, kwenye kituo cha polisi cha KATA YA NYEHUNGE ambapo zoezi hilo linafanyika, wakati mwalimu akiwa hospitali kwa matibabu ya michubuko aliyoyapata.

Hii ni mwendelezo wa vichapo na udhalilishaji kwa waalimu ambao wanaonekana kutokuwa nathamani mbele ya kada zingine za kiutumishi.

Mpaka sasa suala hilo lipo mikononi mwa polisi, wizara usika na vyombo vyenye dhamana mtende haki kulinda heshma ya mwalimu.
 
Madame nawewe siumsaidie kumwelekeza aweke ukiweka kilasaa iposiku atashindwa chomoa
 
Huyu angekuwa amempiga mama yangu muda huu ungekuta yupo ICU anapumulia mashine mambo yanaudhi sana kwa nini amemwonea huyo mwanamke?
 
Ungesema mapema ningeshuka hapo Sengerema, ndio nimepita jioni hii maeneo hayo! Walimu na CWT isiyo na meno
 
Msilikuzeee sana hiyo ni involuntary act inaweza kukutokea, iliwahi kukutokea na baada ya kitendo unajilaumu mwenyewe kwa kile ulichokitenda. Duniani kuna viumbe wengine wasioonekana wanaoweza ku ku control bila wewe kujijua hivyo wakati unalaumu hilo jiangalie wewe mwenyewe hujawahi kukutwa na kitu kama hicho au kinachofanana na hicho?
Sawa lakini kuna sheria, taratibu zinazoiongoza Nchi
 
Huu ni udhalilishaji sana, na unaweza kumkuta mtu yeyote maana kuna watu wanajiona wao wako juu mbinguni hawawez guswa na mtu hapo ndo tunaitaka ile kitu wanaita CWT wasimamie haki ya uyo Mwl kwa kumbuluza mahakaman ili uyo mtakukuru apate kinachostahiki
ila hapa napo tatizo laweza kuwa uyo dada Mwl ameshamsamehe mshtakiwa coz hawa watu wana huruma sana
 
Si ndyo hii takukuru iliyokamata waliokuwa wakinunua vitambulisho vya kupigia kura na hawakuchukua hatua yoyote.
 
Huyo mtakukuru kakosea sana,Hiyo kazi ya kukagua vyeti isifanye wajione wapo juu ya sheria,wakati wametokea mikononi mwa waalimu hao hao ambao leo wanaaona wana vyeti FEKI.
Mfumo mbovu uliosimamiwa na serikali hii ya sisiem ndio uliruhusu haya.Saa hizi wanapiga makofi ya nini
 
Msihukumu mpeni haki ya Kusikilizwa huyo ofisa wa takukuru ' henda aliingziwa kidole katikati ya kalio' na hivyo kuwa provocade, yaweza kuwa ni nbinu pia.......ya Kuharibu party iliyokuwa inawakabili waalimu.... kuhakikiwa.....who knows!
Mwanamke kusimama nyuma ya mwanaume mimi sioni kama linaweza kuwa tatizo kama mwanaume kusimama nyuma ya mwanaume mwenzie au nyuma ya mwanamke...
Lakini ninachojiuliza kama issue ilikuwa ni kusimama tu nyuma yake bila kufanya jambo lolote baya ni kwa nini huyo ofisa achukie bila sababu yoyote ya msingi??
 
Jinsi ulivyoandika title ni kama ulifurahia. ndani ukachanganya hisia. Ni kama magazeti yetu yanavyoandika.
 
Kulikua hamna wanaume hapo ? Si wangemvunja hata jino ndio apelekwe polisi ,Unampiga mwalimu wa kike ? Ila ndio hulka za hawa jamaa wa Mwanza ,hata kaka yao alisema "siwezi kumtanguliza mwanamke mbele yeye ndio ataonekana kama raisi wakati mimi ndie rais"

Anyway pigeni tu ,nimeshachoka mimi
 
Taarifa zilizonifikia ni kwamba;

Kama kichwa kinavyo jieleza tukio limetokea leo Halmashauri ya Wilaya ya BUCHOSA wilaya ya SENGEREMA MKOA WA MWANZA ambapo Afisa mmoja wa TAKUKURU amemlamba makofi mwalimu wa kike (jina linaifadhiwa) wa shule ya msingi (jina linahifadhiwa) wakati wa uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma wa Halmashauri hiyo kwa kosa la kusimama nyuma yake wakati zoezi likiendelea.

Afisa huyo anashikiliwa na polisi mpaka sasa, kwenye kituo cha polisi cha KATA YA NYEHUNGE ambapo zoezi hilo linafanyika, wakati mwalimu akiwa hospitali kwa matibabu ya michubuko aliyoyapata.

Hii ni mwendelezo wa vichapo na udhalilishaji kwa waalimu ambao wanaonekana kutokuwa nathamani mbele ya kada zingine za kiutumishi.

Mpaka sasa suala hilo lipo mikononi mwa polisi, wizara usika na vyombo vyenye dhamana mtende haki kulinda heshma ya mwalimu.
Ashitakiwe.
 
Back
Top Bottom