Kagera: Afisa Manunuzi Muleba ashtakiwa kwa Manunuzi Hewa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Machi 15, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Muleba mbele ya Mh Lilian Mwambeleko, imeamriwa kesi ya Jinai namba 3/2024.

Kesi hii ni Jamhuri dhidi ya Bw. Masanja Igolola Afisa Manunuzi VETA, Ndorage pamoja na Denis Rwegalulila Mzabuni.

Walishtakiwa kwa kosa la Hongo katika Manunuzi ambapo wanadaiwa kufanya 'manunuzi hewa' Mwaka 2019 ya Mashine aina ya Porker Vibrator High F na hivyo kujipatia manufaa yasiyo stahiki ya TZS 2,800,000/-.

Kesi iliendeshwa na Wakili Kelvin Murusuri. Mahakama imewakuta na hatia na kuwaamuru walipe faini ya shilingi Milioni Moja (1,000,000/-) au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Vilevile, Mahakama imewataka warejeshe fedha hizo zote TZS 2,800,000/- walizojipatia kwa manunuzi hewa.

Washtakiwa wamelipa faini 1,000,000/- na kurejesha TZS 2,800,000/- katika ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Muleba.

Wakati huo huo katika Shauri la Rushwa Na. O4$/2024.

Kesi hii ni ya Jamhuri Dhidi ya Bw. Raysone Baliyeguje ambaye ni mkusanyaji wa mapato kwa njia ya POS Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.

Alishitakiwa kwa kosa la Hongo kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329/2022 kwa kujipatia manufaa yasiyostahili wakati wa ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali TZS 5,292,900/_ on hivyo kufanya upotevu wa Shilingi 5,292,900/- mali ya Halmashauri ya Muleba.

Kesi iliongozwa na Wakili Kelvin Murusuri Mahakama imemhukumu mshitakiwa adhabu ya kulipa faini ya Laki tano 500,000/- au kwenda jela miaka miwili na kurejesha fedha zote ndani ya miezi Mitatu.
Mshtakiwa ameenda gerezani akisubiria taratibu za kulipa faini.

Chanzo: TAKUKURU
 
Back
Top Bottom