SAUTI HURU: "CUF yaingia kwa kishindo, yazoa 3,000 wa CHADEMA Arusha!"

Kaka wala usihofu mkutano wa CUF haukuwa hata na watu elfu moja hao 3000 watatoka wapi, walifanya mktano mmoja tu arusha ambao asilimia 60% ya wahudhuriaji walitoka Buguruni, 30% walikuwa wana CCM na Waliobaki ni TLP na Wana usalama wa chadema ambao ni 10%.

CUF ni wahuni tu hawana nia njema ya kuwaletea watanzania mabadiliko. Tuwapuuzeni. Arusha tumeitangaza CUF adui namba 5 wa watanzania, kwenye ili list ya maadui wa taifa by Nyerere.
 
Hata kama ingekuwa na ukweli, kitendo cha chama kinachojiita cha upinzani kwenda eti kujijengea makao makuu ya mapambano ktk eneo linaloaminiwa kuwa strong-hold ya chama kingine ambacho nacho ni cha upinzani huku wakiacha zaidi ya asilimia 70 ya nchi ikiwa ni strong-hold ya chama tawala nin ishara kuwa hakuna mpango madhubuti wa kutaka kuiondoa CCM madarakani miongoni mwa vyama vya upinzani. Inawezekana hii inayoitwa V4C ni mpango wa chama tawala na haishangazi kwani CUF ni CCM B na lengo lake ni kuhakikisha CCM inabaki madarakani ili Seif aendelee kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Visiwa vya Unguja na Pemba. Siwezi kuwapangia CUF wapi pakuanzia ila ukweli ni kwamba yapo maeneo mengi ambayo yanahitaji kukombolewa kutoka katika mikono ya CCM so kujaribu kukidhoofisha chama makini cha upinzani ni kufanya kazi ya CCM. Hii siyo CUF ya 2005 na hakika, itaambulia asilimia 3 katika uchaguzi wa 2015.
 
Nadhani kuna kampeni maalum inayofanywa kisanii kujaribu kupunguza nguvu za CDM. Jumamosi nikiwa maeneo ya Ubungo niliona mabasi mengi yakiwa yamejaa watu huku yakiwa yamefungwa bendera za CUF. Nilipodadisi nikaambiwa wanakwenda kwenye mkutano wa hadhara Arusha. Nilishangaa sana kwa sababu sio kawaida wafuasi wa chama kusafirishwa kutoka mkoa mmoja hadi mwingine eti kuhudhuria mkutano wa hadhara. Hapa kuna jambo! Kingine kilichonishangaza ni kauli ya kiongozi wa UPDP aitwaye DOVUTWA alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari na kumlaani Dk Slaa aliyeiponda CCM kwa kuwakumbatia mafisadi kwenye uchaguzi wao wa NEC. NIONAVYO mimi, baada ya CCM kuelekea kushindwa kuzima nguvu ya CDM (hata baada ya kutumia polisi kuua), sasa wanajaribu kuvitumia vyama dhaifu vya upinzani (ambavyo ni matawi yao) kujaribu kupambana na PEOPLE'S POWER. Wataweza?
 
Ahaa haaa mgosi watafuta habari za ukweli za CUF ndani JF? ni sawa kusema bahari ya Hindi imepita imepita Mashewa!

Chama
Gongo la mboto DSM

Kama jf pamejaa uwongo mbona kila siku unashinda humu na wale magamba wenzako?! Na wale new guest 3800 wa jana ambao naamini hata MSAFIRI alikuwepo kufuatilia rufaa ya lema humu nao walifuata uwongo?!

Habari za cuf ziko kwenye gazeti la sauti huru la kada wa ccm haziko jf hapa tunajadili kama tunavyo jadili masuala mengine. Au unakasirika mwana ndoa wako kujadiliwa kwa kuongopa kuwa kapata wanachama 3000 kutoka chadema wakati hata wewe nafsi inakusuta kuwa si kweli?!

Labda nikuulize, hesabu hiyo ni pamoja na zile coaster zilizo jaza watu kutoka Tanga na Dar? Eti Chama wa mboto!? Jifunze kuwa kama saa mbovu! Pamoja na obovu wake huwa inaongea ukweli mara mbili kwa siku.

Think or sink

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Nadhani kuna kampeni maalum inayofanywa kisanii kujaribu kupunguza nguvu za CDM. Jumamosi nikiwa maeneo ya Ubungo niliona mabasi mengi yakiwa yamejaa watu huku yakiwa yamefungwa bendera za CUF. Nilipodadisi nikaambiwa wanakwenda kwenye mkutano wa hadhara Arusha. Nilishangaa sana kwa sababu sio kawaida wafuasi wa chama kusafirishwa kutoka mkoa mmoja hadi mwingine eti kuhudhuria mkutano wa hadhara. Hapa kuna jambo! Kingine kilichonishangaza ni kauli ya kiongozi wa UPDP aitwaye DOVUTWA alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari na kumlaani Dk Slaa aliyeiponda CCM kwa kuwakumbatia mafisadi kwenye uchaguzi wao wa NEC. NIONAVYO mimi, baada ya CCM kuelekea kushindwa kuzima nguvu ya CDM (hata baada ya kutumia polisi kuua), sasa wanajaribu kuvitumia vyama dhaifu vya upinzani (ambavyo ni matawi yao) kujaribu kupambana na PEOPLE'S POWER. Wataweza?

CDM mti wenye matunda bora kwa afya so lazima UPOPOLEWE KWA MAWE, MITI N.K.
 
swali kwa cuf.
ni kwa nini wakiambiwa ni ccm b wanalalamika?
je ccm si chama kilicholeta maendeleo kwa miaka 50?
je si kilicholeta uhuru?
je si ndicho wanachounda nacho serikali kwa upande mmoja wa muungano?
si ndicho habari zake zinapambwa na magazeti ya ccm?
SIJAWAHI KUONA MTOTO AKIAMBIWA ANAFANANA NA BABA YAKE HATA KAMA NI KIPOFU AKALALAMIKA.
KUFANANA NA MZAZI NI UFAHARI.
 
Hahahaa, kwa hiyo cuf wapinzan wake CDM? Kweli watu wakisema cuf na ccm wamefunga ndoa ni ukweli mtupu na kwa style hii tunaweza kuchukua mda upinzani kuingia madarakani
 
angalieni facebook wall ya Mtatiro uone anavyowashukuru wananchama wa CUF wa Dar kwa kufanikisha ukodishaji wa mabasi mawili toka Dar hadi Arusha kuhudhuria huo mkutano. Tulikuwa tunawazomea CCM kwa kusomba kwa Fusso watu wa maeneo jirani na kuwaleta kwenye mikutano yao, sasa huyu Bi. mdogo wake CUF ametia fora kwa kuwasomba maili zote hizo. Inatia kinyaa na kichefuchefu kuona CUF wakiwa bize na CDM na hii ina-prove kuwa wao ni CCM-B
 
Change is unpreventable,CUF wajitathmini kwa kina walivyokua miaka mitatu nyuma na sasa!C.C.M walileta hoja ya ukabila ikashindwa,udini ikashindwa,wakatumia dola (polisi) na msajili wa vyama ikashindwa na wakapata karipio toka European Union!sasa wameamua kutumia chama kinacho ongozwa na mwenyekiti hasiyejitambua (Cuf) kwa kuwafadhali na kuleta propaganda zisizo na macho!Prof mzima unakubali kushawishiwa na kuongoza propaganda za kitoto,eti mnabeba watu toka Dar to Arusha,kwenda kuleta propaganda kwa chama cha upinzani,alafu eti na nyie mnajiita wapinzani mnaotaka kuikomboa nchi,kichekesho sana!Watanzania wanakomboka kifikra sasa hv,mfano Morogoro tu iliyokua ngome ya C.c.m sasa hv imebaki historia!Cuf ni chama kinacho jichimbia kaburi chenyewe!nampongeza Hamad Rashid kwa kuona usaliti na ubabaishaji wa Lipumba na Seif mapema
 
Ukiangalia kichwa cha habari hapo juu utagundua kuwa unachoenda kukipata si cha kweli na kimejaa uongo ndani yake. Heading hiyo iko kwenye gazeti la sauti huru.

Sauti huru nila kada wa ccm lakini hapa linatumika kujenga uongo wa mchana kweupe! Labda mlioko Arusha mumsaidie muandishi kumuambia ukweli.

Kaka huoni uongo uliopitiliza mkutano wenyewe waliokuwepo walitoka dar sasa hao wanachama wa arusha imewapata wapi kikubwa nilichosikitika mimi ni kuona mwandishi akiandika uongo sasa jiulize ni mangapi wamekuwa wakiandika ya uongo achilia mbali mambo ya siasa
 
Ni kuwa wamepoteza 3000 kwa chadems

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Inawezekana! Kuna coaster 8 kutoka Dar, 1 kutoka Morogoro. 33x9 wanaweza kufika elfu 3. Ila wote ni wageni! Wenyeji waliokupepo ni kama mia tu! Na waliojiunga cuf ni wawili tu!
 
Hilo gazeti ni noma. CUF
wenyewe kwenye risala yao kwa Sultan walisema wamepata wanachama 100 na
hao wanachama 3000 waliwapatia wapi? make kwenye mkutano sijaona mtu
akirudisha kadi

Sultani?!!!!
 
jamani mkutano wenyewe ukitoa watu walioletwa na mabasi kutoka Dar na Morogoro hawakuzidi 100 Na hata ukijumlisha waliotoka Dar na Moro na watu wa Arusha kwa pamoja hawakuzidi 700 sasa hao 3000 wanatoka wapi? au waliimanisha watatu kama ni watatu ni kweli na majina nawafahamu..


Kweli, na hata yule aliyekuwa diwani wa CDM Arusha naye pia makazi yake ni Buguruni Malapa naye pia alisafirishwa na COASTER.
 
Chadema hamna lolote nyinyi na CCM ni wamoja tu nyote mupo kwa ajili ya kuimarisha Kanisa tu na si jengine ni backups Ya CCM tu Kanisa siku ikiona CCM haina maslahi na kanisa ndio mutakabidhiwa nyinyi. Nchi hii inatawaliwa na Kanisa kwa nyuma ya pazia. si mulisema humumtambuwi kikwete ilikuwa ni geresha ya Kanisa tu. kama kweli nyinyi sio Kanisa basi tuwelezeni vipi mutashinda uchaguzi wakati.. 1. Tume ya Uchaguzi ni CCM (kanisa)
2.Polisi Ni CCM (Kanisa) 3. Jeshi Ni CCM (Kanisa) 4.Mahkama Ni CCM (kanisa) 5.JKT ni CCM (Kanisa) Kila Kitu Muhimu kinatawaliwa na CCM kanisa na nyinyi hatuwasikieni kufanya chochote cha kubadilisha hali kwasabau masilahi yenu ni kwa kanisa ivi kweli kama nyinyi sio CCM (kanisa) yule muhindi wa CCM anayewapa mamilioni ya shilingi ccm wangemuacha kweli kama si kwa ridhaa ya CCM?
 
Back
Top Bottom