Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri

Wanabodi,
Kwa vile hili ndio bandiko langu la kwanza kwa mwaka huu, kwanza tutakiane heri ya mwaka mpya.

Pili tupeana pole sana kwa msiba mkubwa wa kumpoteza JPM.

Tatu, nitoe pongezi kwa President Samia kuwa rais wa JMT, kuongoza awamu ya Sita, hongera sana Mama Samia, umeanza vizuri kwa kuonyesha kuwa japo una nia ya kuyaenzi mazuri yote ya mtangulizi wako, umeonyesha kila mtu ana size yake ya viatu, sio vema kuvaa viatu vya mtu yoyote, bali viatu vyako vya size yako. Magufuli anazikwa na viatu vyake, huku ametuachia only mazuri yake ambayo ndio yanabebeka, na kwasababu he was a human being, lets carry only his good luggages, but not his baggages zake on his human side.

President Samia umeonyeshwa uwezo kwanza ni kwa kulibwaga hilo zigo ulilolikuta hapo mlangoni kwako Ikulu. Pia asante kutuletea a real diplomat pale MFA na sio yule Mwalimu wangu Orator mzuri tuu, pale hapahitaji oration ni diplomacy. Mtihani pekee mkubwa kwako ni kuukubali ukweli kuhusu Corona and do the right thing. Kwenye hili nimewahi kushauri mahali na hapa nashauri tena, "Kwavile Magufuli alikuwa hapendi kupangiwa na hatukumpangia, nawaombeni members humu, tusimpangie Samia". Samia Suluhu yuko vizuri sana, anajua nini cha kufanya, tumwache afanye vile anaona inafaa, please let's give her space ".

Kabla sikaanza, naomba kutoa angalizo muhimu. Kwa vile sasa Samia ndie rais, kuna watu sasa ndio wataanza kujipendekeza kwa Samia, hivyo kila mtu atakayeandika jambo lolote zuri kumhusu Samia akaonekana ana jipendekeza. Naomba usome bandiko hili uone nilisema nini kumhusu Samia na ni lini!.

Baada ya hayo sasa nije kwenye topic hii.
Kwanza mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa karma, everything that happens, it happens for a reason, hivyo lolote likitokea, hakuna ubaya kulitafakari bila kumuuliza Mungu sababu, Mungu ana sababu zake kumchukua Magufuli na pia ana sababu zake kumleta Samia, we don't question God's authority.

Japo kifo cha rais Magufuli ni kazi ya Mungu, lakini pia kuna vitu vya kibinaadamu vimechangia, kama heshima kwa marehemu, naomba nisivitaje, lakini kama kuna kitu unakijua kumhusu Magufuli na kinaweza kuwa kimechangia, na sasa unakiona kinaanzishwa mdogo mdogo kuelekezwa kwa Samia, ukiweza kukizuia, kizuie, mimi sina uwezo wa kukizuia, ila nina uwezo tuu wa kukisema ili wenye uwezo wazuie, wakiona hakuna haja ya kuzuia ni kupuuzia tuu, let it be, mimi kwa upande wangu nitakuwa nimetimiza wajibu wangu, to inform.

Siku zote nimekuwa nikihubiri humu, kauli huumba, hakuna kitu kina nguvu humu duniani kama kauli. Pia nikasema uongo ukisemwa sana na kuachwa kujirudia rudia bila kukanushwa, huwa na mtindo sio wa kuonekana kama ukweli, bali kauli hizo za uongo kuumba huo uongo in reality na kuufanya ukatokea kweli.

Moja ya majarida makubwa kabisa ya kimataifa ya kibeberu, The Economist, kwa miaka yote mitano limekuwa likiandika makala za uongo mwingi na ukweli kidogo za kumsakama rais Magufuli. Uongo huu umekuwa ukirudiwa rudiwa bila kukanushwa, na matokeo yake ukaja kugeuka ukweli, sasa Magufuli hatunaye tena, sasa tuna Samia, jarida hili sasa linajipanga kuanza na Samia!. Jee Tanzania tuendelee kuacha uongo ukisemwa kuhusu taifa letu na viongozi wetu hatu lini?!. Hivi ni hatuna uwezo wa kukanusha, au ni tunapuuza kwa hoja kuwa wasomaji wao hawatuhusu, sisi wanaotuhusu ni Watanzania tuu?!. Sasa tunaishi kwenye global world, ulimwengu wa kiganjani, uongo ukisemwa popote unaingizwa kwenye social media, kila mtu anausoma, mkisingiziwa uongo, msipo kanusha, uongo huo unaonekana ndio ukweli. Tanzania ya Samia must do something on this.

Katika toleo lake la wiki inayoanzia April 3, The Economist limeibuka na makala hii kuihusu Tanzania ya Samia. Katika toleo hili this time angalau limeanza kwa kuonyesha Tumaini Jipya Tanzania: The Economist Baada ya Kumsakama Sana Rais Magufuli, Sasa Angalau Lina Matumaini na Rais Samia!, Laanza Nae Vizuri kwa kumtaka aachane na makosa ya Magufuli kwenye kudeal na Covid!. Yakwepa kuzungumzia chianzo cha kifo kilichotangazwa rasmi, waisingizia...

20210403_map502.jpg

Hoping for change​

Tanzania’s new president surely can’t be worse than the old one​

Uongo humu ni upi na una madhara gani, endelea kuandamana nami.

Paskali
Njaa mbaya sana

Ridhika na mkate wako wako wa kila siku hiyo ndio riziki yako

Kama kipo kikubwa zaidi kitakuja tu we ishi kwa misingi ya haki na ukweli kikubwa unachokitumaini kitakuja tu

Propaganda hazitakuinua never kinyume chake zitakupoteza
 
We ni mwandishi gani wa habari,gazeti halikumsakama bali lilikuwa linatimiza wajibu wake wa kiuandishi wa habari
 
Pascal una lugha chonganishi sana Kaka, Magufuli hakuwahi kusakamwa sema hamkutaka kuambiwa ukweli. Yote yaliyozungumzwa yalikuwa kweli na kweli tu, ndio Maana hata Samia kaanza kuwaondoa watu wa karibu wa Magufuli, hili tu linatosha kuhitimisha kuwa Magufuli alikua na mambo mengi kama unga wa ngano
 
Hawa ni kinyongo chao ilikuwa inshu ya madini, ndio sheria zimesha andikwa, hata aje nani zitaendelea tu ...
Mbona mimi ni mkulima tu lakini nakubaliana nao kwa asilimia mia, kuwa huyu mama kamwe hawezi kuwa mbaya zaidi ya meko?je na mimi nina ishu ya madini?!!acha hizo, eti zimeshaandikwa hiyo ni biblia??mangapi mazuri aliyakuta huyo meko, akaja kuyavuluga?jana bungeni umesikia juu ya sheria ya bodi ya mkopo??tayari wamekubali kuiangalia upya, pole pole tu, mambo mengi yalitungwa kwa ajili ya mtu mmoja tu.
 
Paschal unacheza na wakati vipindi, ahahaha...

Ulipamba sana kipindi kile ila leo unapabomoa, now umeanza kujenga wakati huu, hebu ngoja tusubiri tuone😁!.
 
Vifo vya vigogo vilivyofatana mwaka huu chanzo chake ni corona.
OVER
Kwani haya ya hili gazeti si yanaandikwa na yule kibaraka wao aliyekuwa akitumiwa pesa ili awape vijana kumchafua JPM kwenye mitandao ya kijamii? Bahati mbaya baadaye aliposhtukiwa akashtakiwa kihalali kwa kutakatisha pesa? Ulitegemea aandike nini baada ya rais mwingine kiingia madarakani? Ajue tu kuwa hata akijipendekeza vipi historia yake ipo na akirudia transactions zake za money laundering yale yale yatamrudia.
 
Serikali inajua nini kifanyike katika kusimamia mambo ya nchi, kuhusu Covid-19 si lazima tufanye kama walivyofanya wenzetu, hakuna mtu aliyekatazwa kujitenga mwenyewe, hakuna mtu aliyekatazwa kuvaa barakoa, hakuna mtu aliyezuiwa kusafiri kwenda kutafuta chanjo kama inaihitaji. Tuwaheshimu viongozi wetu ndipo nao viongozi watakapokuwa na huruma kwa wanaowaongoza. Sisi ni mashahidi tuliona jinsi gani wale waliyokejeli na kudhihaki viongozi kwa kisingizio cha upinzani tumeona yaliyotokea. Huenda Pascal ni mwanahabari mahiri lakini si mwanasiasa au mwanadiplomasia makini. Na si kila habari inayoandikwa kwenye magazeti ya nje inapaswa kusomwa na watanzania au kuichambua na kuijibu kwani huwezi kumrushia mawe kila mbwa anayebweka hutoweza fika anapopakusudia kwa wakati. Naomba tujikite sana katika habari za ndani ili tuweze kuchangia mawazo katika kuleta maendeleo. Ikiwa tutaamini Covid-19 ni tatizo basi tuwaachiye wataalamu wa afya wafanye yao na tuwache kufananisha kati ya mtu na mtu au taifa na taifa. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom