Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,549
113,728
Wanabodi,

Kwa vile hili ndio bandiko langu la kwanza kwa mwaka huu, kwanza tutakiane heri ya mwaka mpya.

Pili tupeana pole sana kwa msiba mkubwa wa kumpoteza JPM.

Tatu, nitoe pongezi kwa President Samia kuwa rais wa JMT, kuongoza awamu ya Sita, hongera sana Mama Samia, umeanza vizuri kwa kuonyesha kuwa japo una nia ya kuyaenzi mazuri yote ya mtangulizi wako, umeonyesha kila mtu ana size yake ya viatu, sio vema kuvaa viatu vya mtu yoyote, bali viatu vyako vya size yako. Magufuli anazikwa na viatu vyake, huku ametuachia only mazuri yake ambayo ndio yanabebeka, na kwasababu he was a human being, lets carry only his good luggages, but not his baggages zake on his human side, awe amezikwa nazo na ikibidi, tuzungumzie his human side, only his good deeds.

President Samia umeonyeshwa uwezo kwanza ni kwa kulibwaga hilo zigo ulilolikuta hapo mlangoni kwako Ikulu. Pia asante kutuletea a real diplomat pale MFA na sio yule Mwalimu wangu Orator mzuri tuu, pale hapahitaji oration ni diplomacy. Mtihani pekee mkubwa kwako ni kuukubali ukweli kuhusu Corona and do the right thing. Kwenye hili nimewahi kushauri mahali na hapa nashauri tena, "Kwavile Magufuli alikuwa hapendi kupangiwa na hatukumpangia, nawaombeni members humu, tusimpangie Samia". Samia Suluhu yuko vizuri sana, anajua nini cha kufanya, tumwache afanye vile anaona inafaa, please let's give her space ".

Kabla sikaanza, naomba kutoa angalizo muhimu. Kwa vile sasa Samia ndie rais, kuna watu sasa ndio wataanza kujipendekeza kwa Samia, hivyo kila mtu atakayeandika jambo lolote zuri kumhusu Samia akaonekana ana jipendekeza. Naomba usome bandiko hili uone nilisema nini kumhusu Samia na ni lini!.

Baada ya hayo sasa nije kwenye topic hii.
Kwanza mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa karma, everything that happens, it happens for a reason, hivyo lolote likitokea, hakuna ubaya kulitafakari bila kumuuliza Mungu sababu, Mungu ana sababu zake kumchukua Magufuli na pia ana sababu zake kumleta Samia, we don't question God's authority.

Japo kifo cha rais Magufuli ni kazi ya Mungu, lakini pia kuna vitu vya kibinaadamu vimechangia, kama heshima kwa marehemu, naomba nisivitaje, lakini kama kuna kitu unakijua kumhusu Magufuli na kinaweza kuwa kimechangia, na sasa unakiona kinaanzishwa mdogo mdogo kuelekezwa kwa Samia, ukiweza kukizuia, kizuie, mimi sina uwezo wa kukizuia, ila nina uwezo tuu wa kukisema ili wenye uwezo wazuie, wakiona hakuna haja ya kuzuia ni kupuuzia tuu, let it be, mimi kwa upande wangu nitakuwa nimetimiza wajibu wangu, to inform.

Siku zote nimekuwa nikihubiri humu, kauli huumba, hakuna kitu kina nguvu humu duniani kama kauli. Pia nikasema uongo ukisemwa sana na kuachwa kujirudia rudia bila kukanushwa, huwa na mtindo sio wa kuonekana kama ukweli, bali kauli hizo za uongo kuumba huo uongo in reality na kuufanya ukatokea kweli.

Moja ya majarida makubwa kabisa ya kimataifa ya kibeberu, The Economist, kwa miaka yote mitano limekuwa likiandika makala za uongo mwingi na ukweli kidogo za kumsakama rais Magufuli. Uongo huu umekuwa ukirudiwa rudiwa bila kukanushwa, na matokeo yake ukaja kugeuka ukweli, sasa Magufuli hatunaye tena, sasa tuna Samia, jarida hili sasa linajipanga kuanza na Samia!. Jee Tanzania tuendelee kuacha uongo ukisemwa kuhusu taifa letu na viongozi wetu hatu lini?!. Hivi ni hatuna uwezo wa kukanusha, au ni tunapuuza kwa hoja kuwa wasomaji wao hawatuhusu, sisi wanaotuhusu ni Watanzania tuu?!. Sasa tunaishi kwenye global world, ulimwengu wa kiganjani, uongo ukisemwa popote unaingizwa kwenye social media, kila mtu anausoma, mkisingiziwa uongo, msipo kanusha, uongo huo unaonekana ndio ukweli. Tanzania ya Samia must do something on this.

Katika toleo lake la wiki inayoanzia April 3, The Economist limeibuka na makala hii kuihusu Tanzania ya Samia. Katika toleo hili this time angalau limeanza kwa kuonyesha Tumaini Jipya Tanzania: The Economist Baada ya Kumsakama Sana Rais Magufuli, Sasa Angalau Lina Matumaini na Rais Samia!, Laanza Nae Vizuri kwa kumtaka aachane na makosa ya Magufuli kwenye kudeal na Covid!. Yakwepa kuzungumzia chianzo cha kifo kilichotangazwa rasmi, waisingizia...

20210403_map502.jpg

Hoping for change​

Tanzania’s new president surely can’t be worse than the old one​

Will Samia Suluhu Hassan reverse one of the most self-defeating coronavirus policies in the world?
Middle East & AfricaApr 3rd 2021 edition

Apr 3rd 2021
NAIROBI
Tanzania’s new president, Samia Suluhu Hassan, vows to continue where her predecessor left off. Pity the country if she keeps her promise. John Magufuli, whose death was announced on March 17th, was a covid-denying populist who ran a ruthless authoritarian regime. Many believe that the virus killed him.

For the moment liberal Tanzanians are surprisingly upbeat, in part because they do not take Ms Samia, the country’s first female leader, at her word. She is a product of the ruling party, known by its initials ccm, which has held power in different guises since independence from Britain in 1961. But she is no insider. She comes from the semi-autonomous archipelago of Zanzibar, not the Tanganyika mainland, which is the hub of power.

Ms Samia was Mr Magufuli’s vice-president, but it is rumoured that she was foisted on him by ccm bigwigs. Foremost among these was Jakaya Kikwete, Tanzania’s president from 2005 to 2015, who is said to have admired her competent efficiency. Mr Magufuli valued it less and she was excluded from his inner circle. That is now seen as a reason for hope—as are the flashes of principle she has shown. In 2017, for example, she defied a presidential directive by visiting Tundu Lissu, a prominent opposition mp, as he recovered from being shot 16 times.

Still, few are expecting a radical departure from her predecessor’s policies. Not yet, anyway. Lacking a base within the party, Ms Samia will be concentrating on surviving the early stages of her presidency (inherited in accordance with the constitution), when she will be weakest. Mr Magufuli’s faction still holds dominant positions in the cabinet and the party.

She is not totally helpless, however. She may not have a base of her own, but she does have potential allies. With the support of Mr Kikwete’s previously sidelined faction, she was able to resist pressure to appoint Bashiru Ally, a Magufuli acolyte, as her deputy. Instead she tapped Philip Mpango, the finance minister, pleasing international donors. Still, she will have to avoid becoming too reliant on Mr Kikwete.
While foreign investors, often the butt of Mr Magufuli’s nativist policies, would welcome a return to the easy-going pro-market internationalism that marked the Kikwete years, many Tanzanians remember it as an era when corrupt patronage networks flourished. Kikwete factions “smell blood and sense a comeback”, says Thabit Jacob of Roskilde University. It would be sensible to look to the former president for cover rather than guidance.

Ms Samia’s first challenge will be to reverse one of the most self-defeating coronavirus policies in the world. Mr Magufuli responded to the pandemic with a blend of quackery and denialism. Turning his back on science, despite having a phd in chemistry, he prescribed God, communion wafers and steam baths as prophylaxes. Unsurprisingly, the virus spread unchecked through the population.

A more sensible approach is desperately needed. Diplomats and the World Health Organisation hope the new president will again start publishing official data on the virus (after a year-long pause), sack the anti-vaxxer health minister and sign Tanzania up to the covax vaccine-sharing programme. Continuing to deny Tanzanians the jab would stain her reputation from the outset. Whether Ms Samia is for making such changes remains to be seen. In her first public appearances as president, she did not deign to wear a mask.■
This article appeared in the Middle East & Africa section of the print edition under the headline "Hoping for change"

Paskali
 
Huo ni mtazamo wa Gazetti la The Economist, hata raia wanaojielewa ninaamini wana mtazamo huo huo pia.

Katika kitu natamani ndugu mwandishi, siku moja uje kuanzisha thread kuichambua REPORT YA CAG ya mwaka huu bila kuwa biased kwa kusaka uteuzi. Bwana mkubwa hayupo nasi tena. Cha kusikitisha bungeni hayupo Zitto wa kuichambua vizuri hio report.

Key points;

1) ATCL kuendeshwa kwa hasara ya Billion 60 tokea 2016 - 2021.

Au ndio tuseme CAG pengine ana mhujumu Marehemu Rais Magufuli alietuaminisha kwa nguvu kubwa sana kwamba shirika linafanya kazi kwa faida, kufikia hatua shirika kupewa tuzo ya usafiri bora wa mwaka kuliko Turkey Airlines na serikali kupewa Hundi Ya Gawio La Faida na shirika???

Na je, Rais Magufuli angekua hai, angepewa hii hii report ya CAG yenye kulikosoa shirika la ATCL na TTCL, au kuna report nyingine iliopo kwenye makabati yenye mahesabu yaliopikwa ndio angepewa kumtukuza na kutuficha raia???

2) Matumizi ya hela nyingi zilizokua zinapelekwa Wizara Ya TAMISEMI na kutokujulikana matumizi yake, kufikia Rais Samia kumsimanga Waziri Selemani Jafo wazi wazi mbele ya vyombo vya habari, na kumtaka awasilishe mahesabu ya Wizara yake ndani ya muda mfupi, ila kabla hata ya Waziri Jafo ya kuwasilisha hayo mahesabu alioamrishwa na Rais, Rais akaamua kumhamisha Wizara baada ya Siku Mbili (Pengine baada ya kujua kwamba mahesabu hayo akipelekewa hata ridhika nayo kabisa).

3) TPA kukoroga mambo kwenye matumizi ya hela (Kwa viashiria vya ufisadi uliokithiri) mpaka kufikia hatua Rais Samia kumsimamisha kazi Mkurugenzi TPA na TAKUKURU kumshikilia na kufanya upelelezi wa Mabillioni kupotea kwenye account za TPA (Za BOT na NMB).

4) Matumizi ya hela HAZINA kuchotwa hovyo na wachache kwa kigezo cha matumizi (Matumizi yasio na mashiko wala sababu wala kujulikana). Kupelekea Rais Samia kumpa maelekezo CAG afanye ukaguzi upya wa matumizi ya hela zilizotoka hazina kuanzia January 2021 - March 2021.

5) Mikopo mingi sana kuchukuliwa na serikali kimya kimya bila kupitia bungeni, mikopo hio ya kimya kimya mingine bila hata kupitia katika Account za serikali na hela kuwa deposited kwenye Account za contractors na wauzaji wa ndege. Kitu kilicho sababishia serikali kuwa na deni zaidi kwa ukubwa ndani ya miaka 5 kuliko miaka 10 ya Kikwete.

Rais Samia kifupi, ana mashaka makubwa na matumizi ya hazina kuanzia mwaka huu kuanza (Ni aibu kwa watendaji kumfanya Rais awe ana mashaka na taasisi zao) na ana mashaka makubwa hasa na TPA.

Tulikua tunaaminishwa katika utawala ya 2015 - 2021 kulikua hakuna ufisadi kabisa, na mafisadi walikomeshwa kisawasawa sambamba na kutothubutu kuifisadi nchi. Raia walifurahi na kushangilia sana kwa hilo kwani mpambanaji wa mafisadi hatimae alipatikana kuwatetea wanyonge.

Ila katika hali ya kushangaza, na haya yaliotokea hivi karibuni kuna sintofahamu na imani imeanza kubadilika kabisa, kwamba ufisadi ulikuwepo ila "VITISHO VYA KUOGOPA KUIKOSOA NA KUIHOJI SERIKALI YA AWAMU YA 5" ndio sababu ya raia kuaminishwa kwamba hakuna ufisadi na mengineyo, ila sasa raia wanaanza kuamini ufisadi ulikuwepo kama awamu zilizopita (Na wengine wakiamini ufisadi umezidi awamu zilizopita - tuvute subira).

Na sisi wengine tunaamini, waliokua wanapata taarifa za ufisadi (Hasa waandishi wa habari wa kipelelezi) walikua wakiogopa sana kuweka wazi taarifa hizo, kwa kuhofia kupotezwa kama kina Azory Gwanda au kupewa kesi za uhujumu uchumi. Kasoro waandishi mliokua mnasaka uteuzi kwa kusifia hata yasio sifika.

NOTE THAT: baada ya awamu ya 6 kuingia madarakani, ndani ya week moja tu baadhi ya magazeti (Mfano Raia Mwema) wameanza kuisaidia serikali kutoa taarifa za ufisadi unaofanyika katika taasisi za serikali, kama hela zilizotolewa hazina kuanzia January 2021 mpaka March 2021 kwa kuweka wazi mpaka Account Number za benki na kiasi cha pesa zilizokua zikitolewa bila maelezo.

Issue ya Makontena Ya Makinikia, imeanza kuchukua taswira mpya, leak zimeanza kusambaa kwamba tume ya Prof fulani baada ya kufanya uchunguzi, ili baini kwenye makontena ya mchanga ule katika kila kontena la 20Ft kulikua na 0.7% ya dhahabu na sio 7.0% kama walivyolazimishwa kuandika kwenye report na Marehemu Boss Kazi baada ya kuona alikurupuka kwenye maamuzi (For the sake of political sympathy and legal consequences).

Acacia, mtoto wa ndani ya ndoa ya Barrick alikua akilipia kodi ya 0.7% ya dhahabu katika kila kontena la 20Ft kama ilivyotakiwa kisheria, na baada ya Boss Kazi kukurupuka na kufanya maamuzi bila kujiridhisha kwa kuunda tume ya uchunguzi aliamua kuyazuia makontena yale, report ilivyotoka ya tume ilibidi data kugeuzwa na kupikwa kuwa 7.0% ya dhahabu katika kila kontena badala ya 0.7%, Acacia ndio wakakutwa wanakwepa kodi.

Tanzania imepoteza takriban shilingi za kitanzania trilioni 188 (dola bilioni 84 za Marekani ) katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba - Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Tume iliyoundwa na Rais Magufuli.

Rais Magufuli Alionyesha kukasirishwa na matokeo ya tume hiyo:

''Watu hawa hawana huruma, wanachukua dhahabu yote hii, lakini pia hawakulipa kodi,'' alieleza wakati wa kukabidhiwa ripoti hiyo, tukio lililoonyeshwa moja kwa moja kwa njia ya Televisheni.

Mambo ambayo Rais Magufuli alituambia baada ya kukutana na Prof. Thornton (Mwenyekiti Barrick Gold Mine) - Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa, Prof Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) nchini Tanzania.

Tulisubiri sana, mtambo wa kuchenjulia Dhahabu na zile NOAH moja kwa kila Raia kutoka kwa Barrick Gold Mine, ila kimya kilitanda mpaka umauti ukamfika alietupa ahadi ile. Tuliogopa ku hoji kipindi cha uhai wake, kwani tulimzoea kwamba hapendi kubanwa kwenye kona kwa hoja zenye mashiko.

Pia tulimzoea alivokua akimaanisha pindi anaongea kwa kutumia maneno kuhusiana na serikali ya awamu ya tano "SERIKALI YANGU, MIMI NINATAKA, NIMEAMUA", tofauti na Mama anavyotumia maneno hayo na jinsi alivyoyabadilisha SERIKALI YETU, SISI TUNATAKA, TUMEAMUA" - Kwa ufupi, Awamu ya 5 ilikua serikali YAKE, Awamu ya 6 imekua serikali YETU.
 
Welcome back to the forum! You were surely missed sir! Bandiko la the economist liko vizuri , tusubirie approach kwenye covid kama itabadilika, lakini kwa hapa mwanzo tu naona kama hakutakuwa na big changes if any #no face coverings!
 
Mkuu P, ukimya wako huo au hofu ya kuweka bandiko ulitokana na nini mkuu, anyway karma Ina nguvu Sana leo wale waliokua wanaunga mkono juhudi kutokana ushawishi wa Bashiru kwa namna yeyote ile,ndo hao leo Mabosi wa Bashiru,anaenda Bungeni anauliza swali anajibiwa na Gekul,lusinde,waitara aisee
 
Naona dawa zimekusaidia kidogo mkuu, pia huyu mama hatafanya chochote cha ajabu sababu ya mfumo mbovu wa CCM pamoja na katiba yetu ikichangizwa na NEC ya ajabu ya Mahera, tatizo la nchi yetu hatuna mfumo imara isipokuwa tunategemea watu imara kama vile tuna mkataba na MUNGU, mwendazake watu walimchukia sababu ya tabia zake za kujiona yeye ni MUNGU mtu na nchi ilikuwa mali yake binafsi, ndiyo maana wapambe wake akina Bashiru leo wamevuna aibu kubwa sn. Tutengeneze mfumo imara na siyo mtu imara.
 
Heri ya mwaka mpya mkuu Pascal,

Binafsi natarajia ulete hapa uchambuzi kuhusu Dkt Mpango ( and his fate as vice president) na namna

anavyoweza kutusaidia as a country. Na pengine kuhusu vipaumbele (angalau vitatu) ambavyo Rais

Samia akivitekeleza basi tunaweza kupiga hatua kubwa kama taifa
 
Mkuu P, ukimya wako huo au hofu ya kuweka bandiko ulitokana na nini mkuu, anyway karma Ina nguvu Sana leo wale waliokua wanaunga mkono juhudi kutokana ushawishi wa Bashiru kwa namna yeyote ile,ndo hao leo Mabosi wa Bashiru,anaenda Bungeni anauliza swali anajibiwa na Gekul,lusinde,waitara aisee
Aibu tupu kabisa
 
Heri ya mwaka mpya mkuu Pascal,

Binafsi natarajia ulete hapa uchambuzi kuhusu Dkt Mpango ( and his fate as vice president) na namna

anavyoweza kutusaidia as a country. Na pengine kuhusu vipaumbele (angalau vitatu) ambavyo Rais

Samia akivitekeleza basi tunaweza kupiga hatua kubwa kama taifa
Hakuna muujiza wowote utafanyika
 
Mtu akikaa akaandika toka Nairobi, usitegemee lolote zuri litaandikwa kuhusu Tanzania.

Na kwanini tuishi maisha ya kukanusha kila siku, dawa ni kuwapeleka mahakamani wathibitishe hayo wanayoyasema kama JPM amepoteza maisha kwa covid. Huko kwao watu maarufu ndivyo wanafanya kuwafundisha adabu magazeti ya uwongo.
 
Mtu akikaa akaandika toka Nairobi, isitegemee chochote kizuri kutokea Tanzania.

Na kwanini tuishi maisha ya kukanusha kila siku, dawa ni kuwapeleka mahakamani wathibitishe hayo wanayoyasema kama JPM amepoteza maisha kwa covid. Huko kwao watu maarufu ndivyo wanafanya kuwafundisha adabu magazeti ya uwongo.
Tatzo magazeti yetu hayausemi huo ukweli ,tungeanza kuwapeleka mahakamani Kwanza uhuru,jamvi la habari nk
 
Back
Top Bottom