‘Samaki nchanga’ waangamiza mihogo Newala

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WILAYA ya Newala mkoani Mtwara imeelemewa na tatizo la panya kushambulia mashamba ya mihogo, ambapo kwa sasa imeomba msaada wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Kwa kawaida Wilaya za Mikoa ya Mtwara na Lindi zina historia ya kuwa na panya wengi ambao baadhi ya wakazi waliwabatiza kwa jina la ‘samaki nchanga’.

Lakini sasa tayari panya hao wameteketeza hekta 5,147 za mihogo na hivyo kuyeyusha matumaini ya wilaya hiyo kuwa na chakula cha ziada kwa msimu huu wa kilimo kama ilivyo kawaida yake

Hali hiyo inaripotiwa siku chache baada ya wilaya jirani ya Masasi, kuripoti zaidi ya hekta 305 za mazao mchanganyiko kuharibiwa na viwavijeshi na hivyo kuathiri mwenendo wa kilimo wilayani humo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Dk Rehema Nchimbi aliliambia Mwananchi ofisini kwake mwishoni mwa wiki kuwa ukubwa wa mashamba ya mihogo yaliyoliwa na panya ni sawa na asilimia 63 ya mashamba yote wilayani humo.

“Tumeoomba msaada wizara ya kilimo ili watusaidie dawa za kutosha kutekeleza Panya hao,tatizo ni kubwa kama unavyoona asilimia ya uharibifu ni zaidi ya nusu, mihogo hii ni ile iliyopandwa mwaka jana na ilikuwa inatarajiwa kuvunwa mwaka huu,” alifafanua Nchimbi.

Alibainisha kuwa wilaya hiyo ina hekta 8,073 za mihogo ambazo zingeiwezesha kuwa na chakula cha ziada, na kwamba kuibuka kwa Panya hao kunaiondolea matumaini ya kuwa na zaida hiyo.

“Ni kawaida ya wilaya yetu kila mwaka kuwa na ziada ya chakula ambacho kinatokana na zao la mihogo, kwa hali iliyojitokeza ziada hiyo kwa mwaka huu inaweza isipatikane, hatutakuwa na njaa ila uwezo wa kuasaidia wilaya jirani pindi zinapokabiliwa na njaa hautakuwapo,” alisema Dk Nchimbi

Aliongeza kuwa “Miezi mitatu tangu kuibuka kwa panya wanaoshambulia mihogo, hekta 5,147 sawa na asilimia 63 kati ya hekta 8,073 zimeliwa , na idadi hiyo inaweza kuongezeka licha ya jitihada kadhaa tunazofanya katika kukabiliana”

Nchimbi alifafanua kuwa tayari uongozi wake umewahimiza wakulima kusafisha mashamba yao, sanjari na kutumia mitego na sumu ili kuwaangamiza panya hao.


Aliongeza kuwa miongoni mwa jitihada zinazofanywa na wilaya yake ni pamoja na kuhimiza wakulima kupanda zao la mtama ili kuziba pengo la upungufu huo wa chakula.

Taarifa hiyo inatolewa siku mbili baada ya Wilaya ya Kilombero ,mkoani Morogoro kuripoti taarifa za panya kushambulia mashamba.
 
Back
Top Bottom