Wizara ya Kilimo na Arab Contractors ya Egypt Wasaini MoU ya Mradi wa Umwagiliaji Ziwa Victoria

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838
Mama anaendelea kufanya Mageuzi ya Kilimo Kwa ku engage private sector Ili kujifanya Tanzania kuwa ghala la chakula Afrika.

Huyu Mwarabu wa Bwawa la Nyerere asizingue kama kule afanye kweli

==============

Tume ya Umwagiliaji imesaini Hati ya Makubaliano na Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa bonde la Bugwema katika Ziwa Victoria.

Baada ya kushuhudia utiaji saini, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) amebainisha kuwa mradi huo una jumla ya hekta elfu 30, ambapo kwa awamu ya kwanza utaanza na hekta elfu 10.

Mhe. Waziri Bashe amefafanua kuwa mradi wa Bugwema ni moja kati ya miradi iliyotangazwa Bungeni kuwa itatekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, yaani Public Private Partnership (PPP).

Hekta elfu kumi? kweli ? Hawa waarabu mbona wanakuja kwa kasi sana?

Wapi tumekosea?
 
Wakifanikiwa hii aah tumetoboa , ukweli ni aibu nchi kubwa kama yetu tunafaa kuilisha africa , ila kwa kutegemea mvua haiwezekani, hii ni nzuri sana na itafumbua watu macho interms of skills na technology ,watanzania tuna tabia ya kuiga hii utashangaa kila mkulima atapambane afanye akiona jamaa wanavyozalisha kwa wingi na kuvuna mara nyingi kwa mwaka
 
Waziri anasema Kuna mabonde makubwa 22 lakini hakuna tunachofanya.

Ila Hawa Waarabu na Waisrael wako vizuri kwenye irrigation farming so tutegemee wafaukulu.
 
Back
Top Bottom