Mambo makubwa aliyofanya Rais Samia kwenye sekta ya kilimo

Irene Darton

Member
Feb 25, 2024
18
21
Kwenye Sekta ya Kilimo Serikali ya Rais Samia imeongeza bajeti ya Kilimo kutoka Tsh. 751 mwaka 2022 hadi Tsh. bilioni 970.

Kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula Tani 17,148,290 hadi kufikia Tani 20,402,014 na kufikisha asilimia 124 ya kiwango cha utoshelevu wa chakula.

Ameipatia wakala wa uhifadhi wa chakula NFRA na bodi na nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) kiasi cha Tsh. bilioni 116.

Ametoa ruzuku ya mbolea ya tani 204,818.16 kwa mikoa yote ya Tanzania yenye thamani ya Tsh. bilioni 67.82.

Serikali yake imetenga jumla ya eneo lenye ukubwa wa ekari 201,241 kwa ajili kuwaingiza vijana na wanawake kwenye kilimo kupitia mradi wa BBT

Serikali yake imeendelea kuwekeza katika Skimu za Umwagiliaji kwa kuongeza eneo kutoka hekta 727,000 hadi hekta 822,000.
 
Hakuna hata kimoja kilichomsaidia mkulima hapo angefanya yafuatayo.

Angeshusha pembejeo za kilimo kwa kutengeneza viwanda vya pembejeo hapahap nchini ningehakikisha mazao ya kilimo yana masoko ya uhakika hasa nje ya mipaka.

Mengine wangefanya wakulima wenyewe, ndugu chawa wa mama mkulima anaitaji kitu kimoja tu soko la uhakika hvy vingine ni upumbavu.
 
Hivyo vitu miaka yote yanazungumzwa kwa maraisi wote hata kikwete alikuja na kilimo kwanza hakuna kilichowahi kumkwamua mkulima akaondoka kwenye jembe la mkono mtampa sifa pesa zimeliwa na wajanja mnatangaza nadharia zilizo telekezwa ofisini kwenye makabrasha field hakuna kinachoonekana!
 
Back
Top Bottom