Sakata la vyeti vya shule TANESCO, wafanyakazi waomba likizo za muda

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Kama kuna mtu anayepata shida sasa na hili sakata la TANESCO ni HR,

Habari zilizotufikia kuna vituko vitupu watu wana vyeti vya copy na walipobanwa wapeleke original kila mtu anamuomba Mungu kama ni mapenzi yako basi kikombe hiki kinipite.

Sasa basi pengine si suala la kucheka hili ni tatizo la kudumu kama mabalozi wetu tunavyowahalalisha huko UN na kwingineko.

Pamoja na kwamba hawana vyeti, wengi wao unakuta wana uzoefu wa miaka 10 nk. Na hapa ndipo vichwa vinawaka moto hata mabosi wanajiuliza wamekaaje kwenye vyeo hivi bila ya kuhalalishwa shule zao tangu mwanzoni.

Naamini matatizo haya ni wakati muafaka wa kuwapa nafasi watu waliosoma na kuachana na watoto wa momba, shangazi na wengineo.

Kaimu Mkurugenzi mtumishi wa Mungu Mramba najua uko na wakati mgumu lakini kutokana na maombi yako na jinsi unavyomjua Mungu naamini utapita kwenye vita hivi vizito.

Ni wakati sasa wa kukutana na majaribu kama ulikuwa ukiyasikia utaanza kuyaona live, wapo wanaokimbilia Bagamoyo na Tanga wanajua wanafuata nini.

Lakini kama uliyenae ni mkuu kuliko hao wanaokimbizana nao, tunaomba suala la vyeti liendeelee kila sehemu kwenye sekta za serikali kuwapa nafasi wanaostahili.

Kuna uchafu mwingi sana wa vyeti huko serikalini, wengi wao hata original ni vya kufoji.

Raha ya milele ampe ee ex director na mwanga wa milele apumzike kwa amani na hela zetu za tanesco milli 800 loh!!
 
we Pdidy vipi naona maombi mengi sana, kunamtu ataachia nafasi ambayo unaweza kuipata kwa vile wewe unavyeti vyako halali na sifa stahiki wakati bosi wako amefoji vyeti?
 
Kidundulima kwa hali inayoendelea mpwa huko tanesco inawezekana kaka yangu macho namwonea tu huruma mkurugenzi na hr watakavyopambana na mhimili huu wa vyeti
 
mbaya zaidi ni kwamba wana vyeti vya kufoji na hawana uzalendo. wao ndo wamejaa mizengwe mpaka wanatia hasira. kama wangekuwa wanafanya kazi inayoonekana, ningewaombea angalau dua njema, lakini kwa jinsi tanesco ilivyojaa wafanyakazi wahuni ni bora wakatimuliwa wasio na sifa ili tupate wafanyakazi wenye sifa za kuliendesha shirika kwa ufanisi liweze kuhudumia watanzania wengi kuliko ilivyo kwa sasa. wafanyakazi wa tanesco msio na sifa mtanisamehe, ila mimi nawaombea kwa Mungu mtimuliwe, kwa sababu mlipewa dhamana mkaitumia vibaya huku mkitupatia huduma mbovu kupindukia. sasa tuwaombee dua njema ili iweje, muendelee kutuuzia nguzo moja kwa sh. milioni moja???
 
Tuanze na Badra Masoud, alipata division 0 na wenzake walishtuka sana walipomuona chuo kikuu kwenda kusoma Sociology!!! Na kwa aibu ile aliahirisha mwaka!!!!!!! Naomba vyeti vya kidato cha nne na cha sita cha Badra Masoud vipitiwe kwa makini!!!!!!! Angalizo la uhakika!!
 
Tuanze na B***a M****d, alipata division 0 na wenzake walishtuka sana walipomuona chuo kikuu kwenda kusoma Sociology!!! Na kwa aibu ile aliahirisha mwaka!!!!!!! Naomba vyeti vya kidato cha nne na cha sita cha B***a M****d vipitiwe kwa makini!!!!!!! Angalizo la uhakika!!

Mwache mtoto wa watu ale maisha,mjini mipango!!!
 
Kweli mjini mipango,lakini kinachoudhi hata kama mjini ni mipango wewe ukiingia kwa mpango jitahidi kutafuta wengine wasioingia kwa mpango ili waweze kufunika gepu lako_Otherwise kama kila kitu mipango mipango wataharibu.Mfano kama IT Manager kaingia kwa mpango basi inatakiwa aajiri waliochini yake wataalam ili waweze kumfunikia uozo lakini akizidisha mipango nakuambia ataharibu.
 
Wanaogopa kufanya hvyo wanaofua watawanyang'anya position zao.
 
mbaya zaidi ni kwamba wana vyeti vya kufoji na hawana uzalendo. wao ndo wamejaa mizengwe mpaka wanatia hasira. kama wangekuwa wanafanya kazi inayoonekana, ningewaombea angalau dua njema, lakini kwa jinsi tanesco ilivyojaa wafanyakazi wahuni ni bora wakatimuliwa wasio na sifa ili tupate wafanyakazi wenye sifa za kuliendesha shirika kwa ufanisi liweze kuhudumia watanzania wengi kuliko ilivyo kwa sasa. wafanyakazi wa tanesco msio na sifa mtanisamehe, ila mimi nawaombea kwa Mungu mtimuliwe, kwa sababu mlipewa dhamana mkaitumia vibaya huku mkitupatia huduma mbovu kupindukia. sasa tuwaombee dua njema ili iweje, muendelee kutuuzia nguzo moja kwa sh. milioni moja???

Kaaazi kweli kweli!
 
Ha ha haa mpwa una hasira kama yule mwananchi wa kisarawe anaitwa kondo nilimsoma kwenye gazeti la mwananchi anapendekeza kwenye katiba mpya usiwepo wimbo wa taifa kwakuwa tunawaombea heri viongozi wetu wanaendelea kutuibia.
 
Km sikosei huyu B.Masoud kasoma pia IFM na Nyegezi miaka ya 90' kweli katafuta Elimu pengi.km wanasafisha Tanesco acheni mgawo umetiumiza na hizi LUKU
 
... kuna chafu mwingi sana wa vyeti huko serikalini wengi wao hata origin ni vya kufoji ...
Hakiwezi kuwa cheti original halafu wakati huo huo kiwe cha kufoji. By the way tupunguzieni tatizo la sukari, tujengeeni viwanda. Haya mengine ni kutaka kuwahadaa wajinga ili watoke nje ya mstari
 
Yaaani Tanesco mavyeti ya kufoji yamejaa has a huko mikoani. Hr mkuu fanyia kazi hizo taarifa
 
wawatimue tuu kwa kweli mana hao utumish wanavotukaguaga vyet tukienda kwnye usahili na bado michongo hawatupi bc inabid wawakague na hao waliopo huko hvyo hvyo
 
Back
Top Bottom