Sakata la vyeti vya shule TANESCO, wafanyakazi waomba likizo za muda

Tuanze na Badra Masoud, alipata division 0 na wenzake walishtuka sana walipomuona chuo kikuu kwenda kusoma Sociology!!! Na kwa aibu ile aliahirisha mwaka!!!!!!! Naomba vyeti vya kidato cha nne na cha sita cha Badra Masoud vipitiwe kwa makini!!!!!!! Angalizo la uhakika!!

Kwani Badra yuko TANESCO?!
 
Tanzania, ukisafiri kwenda nchi za nje na ukaa huko miaka mitatu tu, ukirudi nusu ya Rafiki zako wana master's degree.
Ukiuliza walisoma wapi hapo ndipo unaambiwa mjini mipango.
Tunachezea Sana elimu
 
Kama kuna mtu anayepata shida sasa na hili sakata la TANESCO ni HR,

Habari zilizotufikia kuna vituko vitupu watu wana vyeti vya copy na walipobanwa wapeleke original kila mtu anamuomba Mungu kama ni mapenzi yako basi kikombe hiki kinipite.

Sasa basi pengine si suala la kucheka hili ni tatizo la kudumu kama mabalozi wetu tunavyowahalalisha huko UN na kwingineko.

Pamoja na kwamba hawana vyeti, wengi wao unakuta wana uzoefu wa miaka 10 nk. Na hapa ndipo vichwa vinawaka moto hata mabosi wanajiuliza wamekaaje kwenye vyeo hivi bila ya kuhalalishwa shule zao tangu mwanzoni.

Naamini matatizo haya ni wakati muafaka wa kuwapa nafasi watu waliosoma na kuachana na watoto wa momba, shangazi na wengineo.

Kaimu Mkurugenzi mtumishi wa Mungu Mramba najua uko na wakati mgumu lakini kutokana na maombi yako na jinsi unavyomjua Mungu naamini utapita kwenye vita hivi vizito.

Ni wakati sasa wa kukutana na majaribu kama ulikuwa ukiyasikia utaanza kuyaona live, wapo wanaokimbilia Bagamoyo na Tanga wanajua wanafuata nini.

Lakini kama uliyenae ni mkuu kuliko hao wanaokimbizana nao, tunaomba suala la vyeti liendeelee kila sehemu kwenye sekta za serikali kuwapa nafasi wanaostahili.

Kuna uchafu mwingi sana wa vyeti huko serikalini, wengi wao hata original ni vya kufoji.

Raha ya milele ampe ee ex director na mwanga wa milele apumzike kwa amani na hela zetu za tanesco milli 800 loh!!


Naona umeanzisha mada itakayokufanya usakwe kama Osama. Kuna mtu alichapisha kitabu cha viongozi wenye vyeti vya kufyetua haraka sana TCU ilisema swala la kuhakiki vyeti vya vyuo ni kazi hivyo wapewe muda, mpaka leo kimya. Kuna wakati hili zoezi lilianza kwa wale wazee wa sare za mabakamabaka ilibidi lisitishwe haraka kwani tungekosa hata watu kumi wale wanaonogesha siku ya kumshinda mkoloni. Kwa kifupi hili ni zoezi gumu na hatari.
 
Tanzania, ukisafiri kwenda nchi za nje na ukaa huko miaka mitatu tu, ukirudi nusu ya Rafiki zako wana master's degree.
Ukiuliza walisoma wapi hapo ndipo unaambiwa mjini mipango.
Tunachezea Sana elimu

Mkuu pengine ni wafuasi sugu wa yule mwanafalsafa wa Kiroma; Machiavelli aliposema, " The end justifies the means"
 
Mkuu pengine ni wafuasi sugu wa yule mwanafalsafa wa Kiroma; Machiavelli aliposema, " The end justifies the means"
Tunakuwa na taifa lenye watu wengi wenye vyeti lakini uweredi hamna.
Ukiwa kwenye interview panel ndio unaweza kuona, yaani mtu Ana vyeti vizito lakini kichwani mweupe...

The end justifies the means ILA wanapotupeleka sipo kabisa.....
 
tutafute njia ya kutatua tatizo la ajira, ukiwatoa hao wenye vyeti bandia utabadilisha na kuajiri wengine, ni sawa ila tatizo litarudi uliowaondoa hao nao hawatakuwa na ajira, itakuwa kubadilishana!! watu na serikali tubuni ajira binafis na si kusubiri wafukuzwe ili tuajiriwe!! hata marekani kuna jobless, hata marekani/ulaya kuna wanaochangia pato la taifa kwenye sekta binafsi kwa kujiajiri wenyewe. tutafute mbunu za kujiongezea ajira, hatuna viwanda vya kuajiri kila mtz, kila mwaka wanamaliza vyuoni maelfu ya vijana, idadi ya hao bandia ni ndogo kuliko wanaomaliza shule kila mwaka...leo tusubiri vyeti bandia wafukuzea...
 
Back
Top Bottom