- Thread starter
- #21
Punguza hamasa mkuu...
Tanesco wanachoweza kufanya ni kushauri...na walifanya hivyo kwa ushahidi wa maneno ya waziri malima....kwamba walishauri nchi iwe na back up ya umeme na ready made solution ilikuwa ni kununua dowans...kilichotokea ni historia...lakini tunachojua kwa hakika ni kuwa dowans ilikataliwa na wizara ilishindwa kuanzisha mchakato wa kutafuta mitambo mipya...na hilo ndio limetufikisha hapa.....je lawama iende kwa tanesco au wizara...jazba itatuongoza kuinyooshea kidole tanesco lakini busara ni wizara kwani mwisho wa siku si tanesco ambayo ingekuwa na ultimate responsibility ya kununua dowans....si tuliona richmond...au ndio tumeshasahau maana lowasa alikuwa kipenzi chetu...mwanamtandao mwenzetu?????
Naona sualahili inabidi litufikishe mahala ambapo kuwe na mgawanyo halisi wa madaraka kati ya serikali na Bunge. Kwa hali ya kawaida, jukumu la kuchukua maamuzi na kuyatekeleza katika kuleta maendeleo ya nchi ni jukumu la serikali. jukumu la Bunge ni kutunga sheria na kuisimamia serikali. Si jukumu la Bunge kuchukua maamuzi ya utendaji wa serikali kama ilivyofanya katika suala hili la Dowans.
Hapa Kamati ya Bunge iliikataza serikali kutekeleza majukumu yake. Kilichotakiwa kufanywa na kamati hiyo ni kutoa ushauri tu na sikuingilia na kukataza. Ingefanya hivyo (kutoa ushauri) serikali ingepima kuendelea na mpango wake au la. Katika hali hiyo, kamati ya Bunge ingekuja kuidhibiti serikali baadaye endapo maamuzi hayo yangeliingiza taifa katika hasara.
Kwa kuwa serikali ilikwisha kubali maamuzi ya kitaalamu ya Tanesco na ikawa tayari kuyatekeleza, na kamati ya Bunge ikatishia in advance kuwa wakitekeleza watawajibishwa, basi ili kuinusuru serikali ya CCM kuangushwa na Bunge wakaamua shingo upande kuachana na wazo hilo ingawa lilikuwa na maslahi kwa taifa.
Katika hali hiyo, kamati ya Bunge haiwezi kukwepa lawama katika hili kwani kama isingeingilia maamuzi ya kitaalmu, hizo mega wati 72 zilizopungua leo lingekuwa si tatizo.