Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Siasa za dunia yetu ni ngumu sana wanasiasa huwa mara zote wanataka kupinda taratibu walizowaka hili waongoze.Museven anabadili mkatiba awe rais wa uganda tena na tena.Huyo Nape naye amezaliwa 26 november 1977.Hivi inabidi kuwa na degree ya hesabu kujua kuwa wakati wa uchaguzi ujao mwezi dec 2008 atakuwa amevuka umri uliowekwa kwa kanuni ya uvccm?yani mgombea awe na miaka chini ya 30.Hio ni dalili ya kuwa ata yeye Napeana kaugonjwa ka tamaa ya madaraka.

Mkuu heshima kwako!! nadhani nikushauri ufuatilie vizuri taratibu za uchujaji majina UVCCM na CCM kwenyewe ili tujadili vizuri swala hili,wanalodhani ndio kizingiti pekee cha kumfanya Nape asiwe mwenyekiti wa UVCCM (T).Isije mwisho wa safari mkaanza kukanyagana ka vile kapendelewa.Kwanza Nape inasemekana kazaliwa tarehe 07/11/1977 na sio 26/11/1977 ka usemavyo!! Pili nijuavyo umri unatazamwa pale anapochukua fomu na si uchaguzi unapofanyika so si hoja hiyo!!Bahati yenu tu kwamba mpaka sasa anaonekana kutoitaka nafasi hiyo,pamoja na mashinikizo mengi ya wapambe wake!!!
 
Mkuu heshima kwako!! nadhani nikushauri ufuatilie vizuri taratibu za uchujaji majina UVCCM na CCM kwenyewe ili tujadili vizuri swala hili,wanalodhani ndio kizingiti pekee cha kumfanya Nape asiwe mwenyekiti wa UVCCM (T).Isije mwisho wa safari mkaanza kukanyagana ka vile kapendelewa.Kwanza Nape inasemekana kazaliwa tarehe 07/11/1977 na sio 26/11/1977 ka usemavyo!! Pili nijuavyo umri unatazamwa pale anapochukua fomu na si uchaguzi unapofanyika so si hoja hiyo!!Bahati yenu tu kwamba mpaka sasa anaonekana kutoitaka nafasi hiyo,pamoja na mashinikizo mengi ya wapambe wake!!!

Nina habari kwamba Nape anasoma upepo maana hataki kuwa kama akina Makamba ambao huwa hawajui upepo unavyo vuma .Nape kwa kuwa najua unasoma hapa JF hebu jitokeze basi useme ukweli maana kila siku uko online na hasa JF ushahidi upo .Sema basi tujue mwelekeo wako
 
Mkuu heshima kwako!! nadhani nikushauri ufuatilie vizuri taratibu za uchujaji majina UVCCM na CCM kwenyewe ili tujadili vizuri swala hili,wanalodhani ndio kizingiti pekee cha kumfanya Nape asiwe mwenyekiti wa UVCCM (T).Isije mwisho wa safari mkaanza kukanyagana ka vile kapendelewa.Kwanza Nape inasemekana kazaliwa tarehe 07/11/1977 na sio 26/11/1977 ka usemavyo!! Pili nijuavyo umri unatazamwa pale anapochukua fomu na si uchaguzi unapofanyika so si hoja hiyo!!Bahati yenu tu kwamba mpaka sasa anaonekana kutoitaka nafasi hiyo,pamoja na mashinikizo mengi ya wapambe wake!!!
Sasa kwa kusema Nape amezaliwa 07/11/2008 ndio kusema inaondoa hoja kuwa ameshapita umri wa miaka 30?????jamani mapenzi binafsi yasitupe upofu wa kujua ukweli.Hakuna anaemuogopa Nape ndani ya uvccm kinachofanywa ni kusimamia kanuni.Hana uwezo wa kushindana na Beno wala Jerry wala Zaiab.Wote ni WANEC na wamempita elimu japo yeye kavuka umri.
 
NIliwaambia mapema kuwa hii thread itakuwa moto hapa na naona so far mambo ni mpwito kama kawa.... All in all I am glad kuwa Nchimbi is gone! zee zima bado linajiita kijana! goooooosh - damu ya Amina Chifupa na Ipyana Malecela inadai haki toka kwako mnafiki na mloz - Nchimbi!
 
Siasa zetu ndivyo zilivyo, hata Kingunge usishangae akiitwa kijana au akawa kamanda wa vijana. LOL
 
Na Mwandishi Wetu

WIKI mbili tu baada ya kuanza kwa hatua za mwanzo za uchaguzi mkuu wa ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kampeni za "kuchafuana" majina miongoni mwa wanachama wanaokusudia kugombea Uenyekiti wa Taifa wa jumuiya hiyo muhimu kisiasa nazo zimeanza.

Hatua hiyo inakuja licha ya Baraza Kuu la Taifa la UVCCM lililokutana Dodoma Februari 9, mwaka huu, kuwaonya mapema wanachama wanaotaka kugombea uongozi katika uchaguzi huo "kutopakana matope", msimamo uliosisitizwa tena hivi karibuni na Mwenyekiti wa Taifa anayemaliza muda wake, Dk. Emmanuel John Nchimbi.


Wiki iliyopita, gazeti moja la kila wiki lilibeba makala ndefu iliyoandikwa na mtu aliyedai kuwa mwanachama makini wa UVCCM, ile ambayo ilikuwa "ikimshambulia" kwa mafumbo na hata waziwazi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo (Tanzania Bara), Beno Malisa.


Hata hivyo, vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa kuna kundi limezindua kampeni maalum ya "kumpaka matope" Malisa pamoja na mtoto wa Rais Jakaya Khalfani Mrisho Kikwete, Ridhiwani Jakaya Kikwete, ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Malisa amesema kwamba kuna lengo la "kumchafua" kisiasa kutokana na kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa UVCCM na kushangaa ni kwa nini.


"Wanasema uanachama wangu katika UVCCM hauna hata miaka mitatu, hapa ndipo uongo unapoanzia. Mimi nilikata kadi mbili kwa wakati mmoja: Ya CCM na ya Umoja wa Vijana wakati nasoma Chuo Kikuu (cha Dar es Salaam) mwaka 2001 na zote nilikabidhiwa na (aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Philip) Mangula", anasema Malisa na kuongeza:


"Kwa hiyo, yeyote anayejaribu kudanganya vinginevyo ana nia yake mwenyewe na hili kwangu siyo tatizo. Mimi naijua siasa, nafahamu kwamba siwezi kukubaliwa na watu wote maana hata Mitume walioleta dini kama Muhammad (SAW) na Yesu nao pia wanapingwa hadi leo. Kwa nini iwe ni ajabu kwangu ambaye ni binadamu wa kawaida kabisa?"


Lakini wakati kiongozi huyo wa juu wa UVCCM akiyasema hayo, vyanzo vingine vya habari vimeeleza kwamba anayetajwa kwa kisingizio cha minong'ono mitaani kuwa mwanasheria na mtoto wa "kigogo" wa CCM aliyejipa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya rafiki yake waliyesoma naye kuanzia shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siyo mwingine isipokuwa Ridhiwani Jakaya Kikwete.


"Huyo anayelengwa ni Ridhiwani Kikwete na yule anayetajwa kuwa rafiki yake mkubwa waliyesoma pamoja huko kote ni Beno Malisa", kinasema chanzo kimoja cha habari hizi.


Akizungumza kwa simu yake ya mkononi, Ridhiwani amethibitisha kuwa amesoma na Beno Malisa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini akakanusha tuhuma kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM na wala hajui kama anataka kugombea uongozi wa kuchaguliwa.


"Mimi siyo mwendawazimu nifanye kampeni za Uenyekiti unaosemwa wakati nafasi hiyo yenyewe hadi sasa bado haina mgombea", amesema.


Amesema Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM atachaguliwa Desemba 14, mwaka huu, na wale wanaotaka kugombea nafasi hiyo watachukua fomu miezi minne ijayo, kisha vitafuatia vikao vya mchujo ili hatimaye Kamati Kuu ije kuteua wagombea watatu watakaopigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, hivyo haelewi tuhuma za yeye kumfanyia mtu kampeni hivi sasa zinatoka wapi.


Alipouliuzwa kuhusu kwenda katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kuendesha mikutano ya kampeni, Ridhiwani amesema kila uongo unaotengenezwa juu yake unajengewa mazingira yanayoweza kukubalika.


Kwa mfano, amesema mkoa wa Pwani anakwenda muda wowote kwa vile ni kwao ambako kuna babu zake, bibi zake, baba zake, shangazi zake, kaka zake, dada zake, binamu zake, watoto wa ndugu zake na hata marafiki aliocheza nao alipokuwa mtoto.


"Hivi mtu anawezaje kupangiwa vipindi vya kwenda kwao? Mimi ninatoka Pwani na huko ndiko sehemu kubwa ya ndugu zangu kwa baba wanakoishi. Utaniambiaje nikienda Bagamoyo au Chalinze ninakwenda kufanya kampeni wakati ni nyumbani kwetu?" Amehoji.


Ameeleza kuwa hata baba yake mzazi alikuwa akienda Chalinze na Bagamoyo muda wowote alipokuwa hayupo chini ya itifaki kama sasa kwa vile ni kwake, na pia siku nyingine alikuwa akilala na kutokea huko asubuhi wakati akienda ofisini kwake Dar es Salaam, hivyo haiwezi kuwa "ishu" kwa yeye naye kwenda wakati ni kwao ambako ataishi hata baada ya kustaafu kazi za utumishi anazofanya hivi sasa.


Kuhusu Lindi na Mtwara, Ridhiwani amesema huko pia kuna babu zake, bibi zake, wajomba zake, mama zake wakubwa na wadogo, kaka zake, dada zake, binamu zake, watoto wa ndugu zake na marafiki aliocheza na kusoma nao, hivyo amekuwa akienda mara kwa mara katika mikoa hiyo miwili kuwatembelea ndugu wa ukoo wa mama yake anayetokea huko na pia Mkuranga katika mkoa wa Pwani.


Mbali na safari anazokwenda peke yake, nyingine amekuwa akifuatana pamoja na wadogo zake au mama yake, na kwamba katika miaka iliyopita alikuwa pia akienda na baba yake kabla "hajabanwa" na itifaki alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kana kwamba haitoshi ameshangazwa na madai kwamba anafanya kampeni wakati hata Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM watakaopiga kura za kumchagua Mwenyekiti na viongozi wengine nao bado hawajajulikana.


Amesema zaidi ya asilimia 75 ya wajumbe wanaomaliza muda wao hawana sifa za kugombea tena, hivyo kamwe hawatakuwepo katika uchaguzi huo huku waliobaki kama watawania tena ujumbe huo pia hakuna anayejua kwa uhakika endapo atashinda.


"Hivi anayetuhumu wenzake kwamba wameanza kampeni anaijua vizuri Kanuni ya Umoja wa Vijana au tumwelewaje?" Amehoji na kusema yeye ameiva kisiasa kwani amekuwa ndani ya UVCCM tangu akiwa mtoto mwenye umri wa miaka sita akianzia uanachama na uongozi wa Chipukizi.


Amewataka wanachama wanaotaka kugombea uongozi katika Umoja wa Vijana kuheshimu maadili pamoja na kanuni za uchaguzi na siyo kuogopana na kuanza "kuchafuana" majina.


"Kama mtu unataka kugombea Uenyekiti wa Taifa, Mkoa, Wilaya au nafasi nyingine kwa nini uanze kuchafua wenzako? Mimi ninadhani hiyo siyo njia sahihi ya mtu kushinda ila ni kujipotezea ushindi.


"Ukitaka kugombea uongozi wowote unaangalia kanuni na vigezo vilivyowekwa. Ukiona unakidhi vyote unaeleza kuwa mimi ninataka na sifa zangu ni hizi ili wapiga kura nao wakupime, wakutathmini na wewe uwaambie mikakati yako kuwa ukichaguliwa utafanya moja, mbili, tatu na kadhalika", amesema.


Akionyesha kiasi gani alivyo makini, Ridhiwani ametahadharisha kuwa yeyote "anayewapaka matope" wenzake iwe kwenye vyombo vya habari na hata vinginevyo ili kutaka uongozi ajue anajaribu kulima shamba kwa kutumia wembe badala ya kulimia jembe.


Naye kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Tanzania Bara), Beno Malisa amesema uongozi wa kisiasa siyo sawa na uongozi wa kitaaluma kama vile Ugavana wa Benki Kuu, Udaktari Mkuu wa Mkoa, Uhasibu Mkuu wa Wizara, Ujaji wa Mahakama Kuu ama Uhandisi Mkuu wa Kiwanda.


Malisa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM amesema kabla hajateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu alikuwa Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Utumishi katika Makao Makuu ya UVCCM, na pia amekuwa mwanasheria wa kujitolea wa jumuiya hiyo na amefanya kazi inayoonekana.


Ili kuepuka majungu amewataka wenye mashaka naye waende ofisini kwa Katibu Mkuu wa UVCCM na kupata maelezo ya kesi alizoutetea mahakamani Umoja wa Vijana na kushinda zote, hatua iliyouepusha kulipa mamilioni ya fedha kwa walalamikaji waliokuwa wameushtaki ili kudai fidia kwa namna moja ama nyingine.


Pamoja na mifano mingine, kiongozi huyo wa juu wa UVCCM amesema kupanda au kushuka kwa madaraka ya kisiasa ni tofauti na yale ya kitaaluma kama Ukuu wa Kitivo cha Chuo Kikuu ambako mfanyakazi hupanda ngazi moja baada ya nyingine kwa mpangilio wa lazima.


"Katika siasa hakuna hayo. Leo unaweza kugombea ubunge na kuchaguliwa, kesho ukiapishwa tu unateuliwa kuwa Waziri na kuwaacha Wabunge waliokaa bungeni kwa miaka ishirini hata ishirini na tano na huwezi kusema eti huyu amechaguliwa jana.


"Asiyejua hilo atuambie ni kwa nini Mbunge kama (Chrisant Majiyatanga) Mzindakaya ambaye amekuwepo bungeni tangu mwaka 1965 siyo Waziri, lakini Lawrence Masha aliyechaguliwa kuwa Mbunge mwaka 2005 tu hapa tayari ni Waziri, au aseme ni kwa nini Dk. Maua Daftari amekuwa Naibu Waziri kwa zaidi ya miaka 12 mfululizo lakini William Ngeleja amekaa na wadhifa huo kwa takriban miezi 14 tu na kupanda kuwa Waziri kamili", amesema na kuendelea:


"Ni polisi gani aliyeanza kazi mwaka 2005 ambaye sasa ni Kamanda wa Mkoa? Ni daktari gani ameajiriwa mwaka 2005 ambaye sasa ni Mganga Mkuu wa Mkoa? Hiyo ndiyo mifano ya tofauti ya madaraka ya kisiasa na kitaaluma".


Kuhusu kuchaguliwa kwake kuwa Mjumbe wa NEC, kijana huyo amesema anashangazwa na madai kwamba "alibebwa" na UVCCM wakati nafasi hiyo hakuipata kwa kuteuliwa isipokuwa kwa kupigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM huku zaidi ya asilimia 99 miongoni mwao akiwa hafahamiani nao hata kidogo.


"Katika uchaguzi ule unakutana na wajumbe karibu 2,000 kutoka nchi nzima palepale ukumbini. Unaitwa jina lako na Mwenyekiti (wa Taifa wa CCM), unakwenda mbele na kupewa dakika tatu za kujieleza kwao ili wakujue wewe ni nani na kwa nini unadhani unafaa kuwa Mjumbe wa NEC. Wao ndio wanakutathmini na kuamua kila mmoja katika nafsi yake mwenyewe kama akupe ama akunyime kura. Hapo unawezaje kusema eti nilibebwa?" Amehoji.


Habari zilizolifikia gazeti hili muda mfupi kabla ya kuingia mitamboni jana usiku zinaeleza kuwa mbali na kuzinduliwa kwa kampeni maalum za "kumpaka matope" Beno Malisa anayeonekana kuungwa mkono na wengi katika UVCCM, jina la Ridhiwani Kikwete limekuwa likitumiwa bila yeye kujua ili "kumchafulia" Naibu Katibu Mkuu huyo kama ana nia ya kuchukua fomu ya kuwania Uenyekiti wa Taifa.


Vyanzo vya habari kutoka mikoa ya Pwani, Morogoro na Tabora, vinasema mkakati huo unasimamiwa na kugharamiwa kifedha na kundi la wafanyabiashara wenye asili ya Somalia ambao ndugu yao ni miongoni mwa vijana wanaotajwa kuwa na mipango ya kuisaka nafasi hiyo.


"Hao ndio wanatumia jina la mtoto wa Kikwete kuwatengenezea fitina walengwa hasa Beno Malisa kwa kumtungia uongo", vimedokeza vyanzo hivyo na kumtaja anayesaidiwa kwa njia "chafu" na kundi hilo ambaye hata hivyo jina lake hivi sasa tunalihifadhi.


SOURCE: GAZETI LA TAZAMA
 
Naomba nishukuru sana kwa ufafanuzi yakinifu kama huo, hii itatusaidia sisi tulio mbali na makao makuu ya UVCCM kujua ukweli na uongo kwa yale yanayoendelea kujitokeza siku hadi siku lakini pia itatusaidia kutathmini dhana nzima ya ukweli na uwazi kama ni uongo kuwa hakuna mtu anayejipanga kumsaidia mtu, tunashukuru na pia kama nikweli kuna mtu/watu wanaojipanga kumsadia mtu na taarifa hizo kuandikwa katika vyombo mbali mbali vya habari hali inayopelekea kundi husika kukanusha tuhuma hizo kwa nguvu kubwa hilo nalo tunashukuru ! cha msingi the messege will be sent and derivered !

M-bongo !
 
Last edited:
3. Marehemu Nauye, hakuacha kitu chochote cha urithi, ninasema nothing, yeye ni mmoja wa viongozi wachache walioamini sana maneno ya Mwalimu, aliishia kuwa na apartment moja ndogo sana pale Upanga, ambayo mke wake mkubwa anaishi mpaka leo kwa hiyo alipofariki hakukuwa na urithi aliouacha zaidi ya hiyo apartment basi.

4. Rais wetu anaweza kuwa ana wake zaidi ya mmoja, hivi kweli nayo hiyo inapaswa kuwa ishu ya taifa? Naaamini kwamna viongozi wetu wengi kuanzia upinzani mpaka CCM wana wake na watoto zaidi ya wake zao wanaofahamika, hivi hiii nayo inatakiwa kuwa kipimo cha uongozi bongo? Hivi kweli hii ikifuatiliwa kwa undani kuna kiongozi yoyote wa upinzani na CCM atakayebaki? I mean unless kuna something sielewi hapa kwenye hiii topic kwa sababu kwa ufahamu wangu kama ni viongozi na wanawake wasio wake zao na watoto sidhani kama kuna hata mmoja anayeweza kusimama kwenye pande zote mbili, au anayeweza kumtukana mwenziwe wa upande wa pili, sasa nashangaa what is the buzz for?, labda sana sana dogo Mnyika tu ndiye sijawahi kumsikia kwenye viwanja, wakuu hebu tu-stick na ishus kama alivyosema mtoaji wa hii mada.

Kaka wakati nikielewa mantiki ya wewe kuwa na muono huu napenda kupingana nawe haswa katika hili la maadili binafsi, familia na uongozi.

Kwanza kabisa naamini kama kuna watu ambao wanajua madhara ya kutokuwa na stable family haswa kwa viongozi wetu na watoto wao hivyo ninaamini unaweza kufungua kichwa na kufikiri kwa mapana yake suala hili.

Mimi binafsi ninaamini kabisa kuwa unapokuwa na tabia za kushindwa kucontrol matamanio ya kimwili ni wazi itakuwa vigumu kucontrola matamanio mengine ambayo yanatuzunguka kama viongozi ama hata wanafamilia.Kama unashindwa kujizuia na urembo wa biadamu utawzaje kujizui urembo wa mabilioni kama yale ya EPA?

Lakini zaidi ni kuwa kwa binadamu yoyote kukosa stable family kunaathiri uwezo wako wa kufikiri na kufikia maamuzi kwani stress na depresion inakuwa ni sehemu ya maisha yako.

Lakini vilevile, unstable familiy ni mwanzo wa matatizo yasiyokwisha kiuchumi kwani majukumu ya kifedha yanakuwa mengi usiyoweza kuyacontrol. Kinachofuata ni uhitaji usiokwisha wa kuongeza kipato. Naamini unajua wapi uhitaji huu unapowafikisha viongozi wetu kama sio kukwapua fedha za wananchi basi hongo na hata kukuwadia ufisadi kwa ajili ya kulinda maslahi binafsi na wakati mwengine hata kuuza nchi yako kwa vijizawadi kutoka kwa maadui zetu wa nje.

Kila nisikiapo kuwa fulani amekufa akiwa hana kitu huwa najiuliza, hivi sababu alikuwa msafi na mwaminifu kwa nchi ama hakuwa na mpango mzuri wa matumizi ambao moja ya chanzo chake ni nyumba za pembeni na za nyongeza.....bado sijapata jibu

Mwisho, wakati nakubaliana nawe kuwa hili linaweza kuwa nje ya mjadala lakini pia naamini suala la maadili binafsi, familia na uongozi linapaswa kujadiliwa zaidi na zaid na kama kweli tunataka kujenga Tanzania makini ni wazi haya nayo tunapaswa kuyaingiza katika mchujo wa vigezo wa viongozi wetu haswa hawa wa kizazi cha baada ya mwalimu na enzi za mtandao.

Tanzanianjema
 
Asante kwa Mjadala Mziti hapa JF,So far soo GOOD Jerry Silaa keshatangaza nia yake ya kugombea kiti hicho ila hakuna mtu aliyejitokeza kumpinga.Lets wait and see
 
Lunyungu Kama Zinawahusu Kwa Nini Tuwapotezee Muda Watu Waanze Kumaliza Thread Hii Warudi Nyingine Wakati Wanauwezo Wa Kuendeleza Mswano Mpaka Moro????????
 
Benno bado ni mchanga sana kisiasa aachane na hizo ndoto za alinacha.Yaliyowapata wenzake tena watoto wa vigogo sio madogo. Siasa si suala la kusema niko na fulani ni suala la kusoma nyakati wakati mwingine huwa halitabiriki.
 
TATIZO LA UANDISHI !
Historia ya darasa langu la Kindergaten nililoishia linanikumbusha mapambano ya kupigania uhuru wa Nchi yetu yalivyopambana na vikwazo vingi! Elimu duni,silaha duni n.k lakini pamoja na yote hayo hayakupelekea wazalendo wa Nchi hii kukata tamaa ya kupigania uhuru hadi walipofanikiwa, cha msingi ilikuwa ni mawasiliano yaliyojenga moyo wa uzalendo na upendo wa Nchi yetu kwa hiyo Ndg yangu aliyekwazwa na mandishi ya haraka haraka huenda yakikimbizana na TIMEWATCHER yasimtishe wala kumsumbua cha msingi watu wanawasiliana, wanaelewana ili kuhakikisha lengo linatimia iwe kusini au kaskazini mwa nchi zaidi ya hapo mwandishi bora ataheshimika 14/12/2008 nadhani Dodoma!
M-bongo
 
Benno bado ni mchanga sana kisiasa aachane na hizo ndoto za alinacha.Yaliyowapata wenzake tena watoto wa vigogo sio madogo. Siasa si suala la kusema niko na fulani ni suala la kusoma nyakati wakati mwingine huwa halitabiriki.

Nilidhani umoja wa vijana ni kwa ajili ya wanasiasa wachanga ama?

Tanzanianjema
 
Ridhiwani nae anataka kujiletea balaa..sasa kwanini yeye asigombee huo uenyekiti???
 
Vijana CCM wataka Lowassa, Chenge waachie Ubunge

*Pia wamo Karamagi na Dkt. Msabaha


Na Mashaka Mhando,Tanga

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Tanga umewataka viongozi wote wanaotuhumiwa kuhusika kwa namna yoyote na vitendo vya ufisadi kuachia mara moja nyadhifa zao za uongozi ndani ya chama ili kukinusuru na chuki dhidi ya umma.

Viongozi hao wametakiwa kukaa na kutafakari kama kweli bado wana uwezo wa kusimama majukwaani na kunadi sera na Ilani ya chama hicho mbele ya umma baada ya kukumbwa na kashfa hizo.

Akitoa tamko la Kamati ya Utekelezaji ya Umoja huo Mkoa wa Tanga kwa waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, Bw. Emanuel Kiondo, alisema viongozi walioachia nyadhifa zao serikalini hivi karibuni kutokana na kashfa za ufisadi, wameendelea kubaki na madaraka makubwa ndani ya chama hicho jambo ambalo ni hatari katika kujenga imani ya umma.

Bw. Kiondo ambaye pia ni Katibu wa Idara ya Uenezi na Siasa Mkoa wa Tanga, alisema viongozi hao hawana budi kutafakari upya na kupime kama bado wanaheshima ya kusimama mbele ya jamii na kunadi sera bora na Ilani ya CCM na kama hawataaminiwa, wajiondoe haraka.

"Kuachia ofisi za serikali hakutoshi, bado wengine ni wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu, wabunge na hata Kamati ya Madili na hizo zote ni ofisi za umma...Kwa kuwa CCM ndicho chama kikongwe na wananchi wengi wanakitegemea kutoa mwongozo na mwelekeo wa Tanzania ya leo na ijayo, tunawaomba wote waliojiuzulu nafasi zao serikalini wafanye hivyo kwenye chama ili kukinusuru kusemwa vibaya," alisema Bw. Kiondo.

Mwenyekiti huyo huku akinukuu mifano mingi kutoka katika vitabu mbalimbali vya marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Dkt. Ibrahim Kaduma, alisema viongozi hao kwa kuziachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama kutasaidia kupunguza kilio cha wanachama, wapenzi na mashabiki wa chama hicho.

Alisema wakijiondoa watakuwa wamekubali kujisafisha na kukinusuru chama chao na wakati huo huo kumuenzi Mwalimu Nyerere katika kutoa maamuzi mazito likimwemo la kukubali kukosolewa na kujikosoa.

Miongoni mwa viongozi waliowajibika hivi karibuni kutokana na kashfa mbalimbali ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa aliyeachia wadhifa huo kwa kashfa ya Richmond sambamba na mawaziri wengine wawili, Bw. Mustafa Karamagi aliyekuwa Waziri wa Madini na Nishati na Dkt. Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Afrika Masharki.

Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge pia alijizulu kutokana na kashfa ya ununuzi wa rada iliyomhusisha na kutunza mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, UVCCM Tanga imekitaka Chama cha Wananchi (CUF) kukubali kwenda kwa wananchi kupata maoni yao juu ya kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar na kukaa meza moja na CCM kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

"Kitendo cha CUF kukataa kwenda kwa wananchi ili watoe maoni yao si cha kiungwana hata kidogo, wanapingana na jina la chama chenyewe, 'Chama cha Wananchi' halafu wanaogopa kwenda kwa wananchi hao hao," alisema Bw. Kiondo.

Bw. Kiondo alisema UVCCM inapinga kauli ya CUF kutaka Rais Jakaya Kikwete naye ajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi na kukariri maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa "Kuwajibika kuna ngazi zake, hatuwezi kusema mtendaji akifanya kosa Rais ajiuzulu, hapana aliyetenda kosa likathibitika awajibike mwenyewe."

Aliwataka Watanzania kutambua kwamba CCM ni kama familia kubwa wanamozaliwa watu wenye hekima , waadilifu, vilema, mataahira, majambazi, vichaa na wengine hivyo si busara watu kuisakama familia hiyo kwa kuwepo jambazi moja wakati kuna wengi wenye hekima zao.

Alitetea kuwa CCM imekuwa na viongozi wengi wenye busara na uadilifu mkubwa na kuongeza kuwa chama hicho ni kikubwa ndio maana Rais Kikwete hivi karibuni alikaririwa akisema umefika wakati wa kutenganisha siasa na biashara.


majira
 
"Those who cannot remember the past are condemned to repeat it". Huu msemo ulipendwa sana na mhubiri mmoja wa kimarekani kwa jina Jim Jones aliyeendesha maisha yake na ya waumini wake kwa mtindo uleule wa Joseph Kibwetere wa Uganda, na aliangamiza waumini wake zaidi ya 900 katika mji wa porini walikokuwa wakiishi huko Guyana, ambako walipaita Jonestown mwaka 1978. Kuthibitisha ukweli wa kauli yake, miaka zaidi ya 20 baadae waumini wa Kibwetere huko Uganda walikufa katika mtindo huohuo!

Haya maneno ya vijana wa UVCCM dhidi ya "baba" zao hayakuanza leo, na siku zote huwa yanamalizwa kwa kutishiwa na kunyamazishwa kwa mtindo wa "nidhamu ya chama". Mwaka 1995 katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM wa urais, John John Guninita akiwa mwenyekiti wa UVCCM taifa na mwenzie Sukwa Said Sukwa akiwa Katibu Mkuu walikuja na tamko lililodai kuwa ati wao wangemuunga mkono mgombea "kijana" kwa kuwa ati ilikuwa zamu ya "vijana", enzi hizo JK na mwenzie Lowassa ndio waliokuwa vijana wakienda kwa jina la "Boyz 2 Men"! Mbona walikomeshwa! Waliitwa na wazee kina Kingunge na kukoromewa hadi wakalazimika kufuta kauli yao hadharani na kuomba radhi kuwa haukuwa msimamo wa chama! Baada ya uchaguzi ule Guninita "alitemwa" akalazimika kukimbilia upinzani, na njaa ilipomzidia akarudi CCM kwa magoti!

Nasema nini? Kumbukeni historia, la sivyo mtalaanika kuirudia! Mbinu hiyo ya mapambano ilishawashinda wengine toka enzi, nyie leo mmeongeza nini hadi muweze? Huwezi kukata tawi la mti ulilolikalia, ondoka penye tawi hilo ndipo ulikate! Hali kadhalika huwezi kukata mti ambao ndio uliouparamia, utaanguka nao, au wenye mti wao watakushusha! Shuka mtini humo, kamata chain-saw yako ukate mti huo kwa nafasi bila kukerwa na mtu! Na kama unajali miti, ule msemo maarufu wa "Panda mti kata mti" ndio wa kuzingatia, ukijaribu kukata mti kabla hujapanda mti mwingine mwishowe utaishia kutangatanga tu kama hawa wanaohama vyama kila siku. Mtu anayeikemea CCM akiwa ndani yake ilhali bado anahangaika kuhonga ili apate ujumbe wa halmashauri nk ndani ya hiyohiyo CCM kwa ajili ya "ulaji", anatupa mashaka kuhusu umakini wa anachokisema, ni mnafiki tu! Huko kwenye nyumba ya kioo mnakoogopa kutupiana mawe, leo hii nitaaminije kuwa hayo unayorusha sasa si usanii tu wa kurushiana vifurushi vya sufi au pamba? Tumeshamichokeni na usanii wenu!
 
Back
Top Bottom