Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Heshima Mbele wana Bodi,

Kwa tarifa ambazo nilizipa tangu last week na jana zilitoka katika Gazeti la MWanahalisi,ni kwamba yule Kijana Mtoto wa Rais ,Ndugu Ridhwani amekuwa akiendesha kampeni za kichini chini ili rafiki yake amabye anaitwa Benno Malisa achukue Uenyekiti wa UVCCM taifa,na vikao vya kampeni zao vimekuwa vikifanyika pale Rose Garden,

Suala la Benno ambaye ni Mjumbe wa NEC kupitia Vijana kugombea uenyekiti wa UVCCM sio jambo baya na ni jema kwa sababu ni haki ytake,ila tatizo hili la kuhusika na mtoto wa Rais Kugombea ndio linaanazx akuleta picha mbaya.Kwanini wameeza kampeni mapema sana,Je wanatoa wapi pesa za Kampeni??sababu Benoo ni mwajiliwa wa Chama cha Mapinduzi.Tukilfumbia mamcho sula hili ndio mambo ya kagoda yanapoanzia,

Naomba wanabodi kuanzia hivi sasa tuanze kufuatilia vikao vyao na kujua wapi wanatoa pesa na wametumwa na nani.

Pia naomba tuwajadili kwa kina wale wote ambao wameonesha nia ya kugombea uongozi wa Uenyekiti UVCCM,nimeanisha majina hapa sabbu nimepewa majina hayo ndio wanaojipanga kwuania uongozi huo

1.Benno Malisa
2.Jerry Slaa
3.Nape Mnauye
4.Zamaradi Kawawa
5.Mussa Mnyeti

1-1.jpg

haya wazee , naona Nnape ndio ashapewa kkiti kikubwa zaidi yake, je atakiweza?
 
Nape ajibu mapigo

Na Mwandishi Wetu

BAADA ya kufukuzwa kwenye Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Baraza Kuu la umoja huo, Nape Nnauye ameibuka leo asubuhi na kuwataka wanaomuunga mkono wasikate tamaa kwa sababu mapambano bado yanaendelea.

"Najua kuna wanachama wengi wananiunga mkono. Nawahimiza wasikate tamaa kwa sababu haki itajulikana vikao vya juu vya chama vitakapokaa na kubaini ukweli wa jambo hili. Bado tunaendelea," amesema Nnauye alipozungumza na mwandishi wa habari hizi leo asubuhi.


Amesema kwamba anajua wapo wanachama na wasiokuwa wanachama wa CCM wanaomuunga mkono na kuwataka wasikatishwe tamaa na yaliyotokea Dodoma jana mjini Dodoma.


Kuhusu kauli ya Baraza Kuu la UVCCM kwamba alisema uongo kuhusu mradi wa jengo la UVCCM, amesema asingeweza kulizungumzia hilo kwa sasa kwa sababu linashughulikiwa na Kamati Kuu ya CCM lakini akasema anatarajia kwamba haki pia itatendeka.


"Sitaki kulizungumzia zaidi suala hilo kwa sasa lakini ninaamini penye haki, dhuluma hujitenga na wananchi watakuwa mashahidi," amesema.


Amemlaumu Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akisema kwamba akiwa Kamisaa Mkuu wa uchaguzi wa UVCCM maamuzi yake yameegemea upande mmoja.


Baraza Kuu la UVCCM jana lilimvua uanachama Nape katika kinachodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya chama pamoja na kumwengua rasmi katika kinyang'anyiro cha kuwania uenyekiti wa umoja huo katika uchaguzi unaotazamiwa kufanyika baadaye mwaka huu.


Nape amekuwa gumzo kubwa katika uchaguzi huo kutokana na kulipua alichokiita bomu la ufisadi kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM jijini Dar es Salaam.


Kijana huyo amekuwa akiwataka mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake, Dk. Emmanuel Nchimbi, Katibu Mkuu, Kaimu Katibu Mkuu, Francis Isaac na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Edward Lowassa wawajibishwe kwa kupitisha mradi ambao anadai hauna maslahi kwa umoja huo.


Alitoa hoja hiyo muda mfupi baada ya kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti wa UVCCM, nafasi ambayo ni nyeti kwa vile inampa mhusika kushiriki kwenye vikao vya juu vinavyotoa maamuzi mazito kwenye chama tawala.


Mwanasiasa huyo chipukizi amekuwa akinukuliwa mara kwa mara akidai kwamba mkataba huo ulipitishwa kinyemela hata kabla haujafikishwa kwenye vikao vya juu vya CCM.


Nape pia amekuwa akiweka alama ya kuuliza kwenye uhai wa mradi huo hasa katika kipengele kimojawapo ambacho kinasema kwamba mwekezaji ataendeleza mradi huo milele, huku Jumuiya hiyo ikipata asilimia 25 na mwekezaji akipata asilimia 75.



Tusubili news kamili kesho au jioni hii hii

mpaka sasa hivi Nnape yuko kifua mbele?
 
:bolt:
Hivi kuna ubaya gani hasa kwa mtoto wa Rais kumfanyia kampeni rafiki yake? Ina maana ukishakuwa mtoto wa Rais basi ukae tu nyumbani. Ridhiwani ni mwanasiasa na ana haki ya kufanya siasa ikiwemo kumfanyia kampeni mtu yeyote anayeona anafaa kwa utashi wake. Tuache longolongo zisizo na kichwa wala mkia. I mean what is the exact problem here, are we becoming obsessed with witch hunting?

Safi sana sasa wamchukue na Nape katika hili kundi timu itakuwa imekamilika:A S 465:
 
ishu nadhani iwe ni kuwa of all 3,000,000 members wa chama and so hakuna watoto wa kina ngonyani, masalakwilanga, arifo, mkumbo.... na wengine wenye uwezo wa kuongoza? au uongozi ni kitu iko damuni kwa watu fulani tu?? eg makamba....mnauye.....kikwete....kawawa....kasela bantu.....etc???

mi nadhani sasa umefika muda tuwe na MFALME
 
Back
Top Bottom