Sakata la malipo ya korosho sehemu ya pili, Tandahimba kimenuka..!

Saa ya ukombozi imewadia.

Dalili ya mvua ni mawingu na mjinga akielevuka mjanja yuko mashakani.

Watanzania wa leo wameelevuka na watawala wasome alama za nyakati ukutani kama ilivokuwa kwa Roma empire na CCM .........
 
Huu ndiyo mwisho wa kufikiria wa Kikwete na Pinda, kwamba watu wakiandamana kudai haki yao suluhisho ni mabomu ya machozi na risasi za polisi. Lakini na hao wananchi wana sababu gani ya kuwapora wenzao? Mgomvi wao ni serikali au wavuja jasho wenzao? Waandamanaji nao ni wendawazimu kama ndiyo hivyo!

Ndiyo hivyo yaani...

Kuna fujo zisizopimika huku..
 
hawa dawa yao ni kuwaletea vijana wa mwamnyange ndiyo watafungu njia kwani wa mwema wamechemka,hapa nina taarifa kijana mmoja wa said wamebonda na saä amelazwa hospitali ya wilaya

una uhakika kuwa hakuna juhudi walizofanya kabla hawajachukua hatua hii?
 
Nachelea risasi za moto kutumika maana waandamanaji hao sasa wanaelekea Kituo cha Polisi cha Wilaya..

kama nakuelewa vizuri ni kuwa hayo mabomu na risasi zikipigwa waandamanaji wanasema "maajii" na kuendelea kusonga mbele, au hali ikoje?
 
CDM .... Mko wapi? Sauti zackika zikiwahitaji huko Kusini inakuaje mkae kimya? Peleka jembe Lema kule awasilimishe....
 
Duh!nashindwa kutabiri Tanzania ya kesho itakuwaje!Mwalimu Nyerere alisema CCCCCCM ikiyumba na nchi iatayumba,yakitokea haya iondoeni CCCCCCM madarakani kabla hajaleta madhara zaidi!

Kusini huku Chama tawala ni kama kimechokwa hivi.. Na huku CUF ndiyo yenye umaarufu zaidi..(LINDI NA MTWARA)..
 
mkuu, watu wa mtwara hawaeleweki kabisaa! Ukitaka ku-prove peleka tshirt za njano na kijani na cape za ccm, halafu kile kizee chenye mamvi kiende kuwatembelea wataacha maandamano na kucheza ngoma kukitumbuza kile kizee kwa shangwe isiyo na kifani!!!

ha,ha,ha,haa haya bana we umeona hivyo! Ila nadhani mtwara ya leo hususani tandahimba si hiyo uijuayo wewe!
 
Kikwete kikwete kikwete hata pesa za wakulima wa korosho jamani unashindwa kuwalipa mbona dowans na wengineo tena wasio stahili unawalipa hawa waliovuja jasho la haki unawadhulumu,kumbe mlianzisha utaratibu wa stakabadhi ghalani ili muwadhulumu wakulima,Kilio chao kimemfikia manani subiri adhabu yako,najua wakulima hawawezi kupora vitu vya watu wakati wa maandamano bali ni hao kenge waliozamia msafara wa mamba.
 
Waache wakome kwa kukaliwa kohoni na magamba
Utaona uchaguzi ujao wanawachagua magamba kwa kishindo tena
Ngoja wateseke kidogo kisha tunaenda kuwapa ukombozi

Mkuu kuna kesi inaendelea mahakamani ya uchaguzi dhidi ya mgombea wa CCM..

Na wengi wanaamini kuwa mgombea wa CCM hakushinda..

Ilitokea hadi amri ya kutotembea usiku.. Maana watu wengi hawakuwa na imani na matokeo..
 
Mkuu gambachovu tuwekee basi updates hapo juu kwenye post yako ya mwanzo ili tuweze kufatilia kwa masikitiko jinsi nchi yetu inavyoendelea kwenda kusiko.. :(
 
Huko ni kwenda nje ya utaratibu; jana bungeni waziri mkuu katoa tamko, serikali ipo katika hatua za mwisho kulipa deni kwa wakulima; Ikumbukwe 80% thamani ya mazao walishalipwa bado 20% wakulima wawe makini wasije kutumiwa kisiasa na CUF

mkuu hizo ni kauli za kisiasa. kwani wastaafu wa East Africa si wanakufab bila mafao yao tokea 1977?
Ukitaka kuchangia uzi huu vizuri, jaribu kuulizia hali ya wakulima wa korosho huku kusini kwanza ndo utajua kama Pinda anamaanisha akisemacho au anasikitika kama kawaida yake. Wananchi wana hali mbaya. korosho ziko kwenye maghala ya vyama vya ushirika na wahindi hawatakii kuzinunua kila ukipigwa mnada watu wanaleta bei za chini. Na msimu wa palizi ndo unakaribia. watalipwa lini, na sulphur ya msimu mpya italetwa lini?
Na kule Tandahimba wale wamamkonde hawana masihara hata kidogo.
Na yule Mama Mwilima (DC) anawaletea utani kama ule aliokuwa anamfanyia Sophia Simba kwenye UWT. Kazi anayo
 
Hakuna haja ya kuwakejeli cha msingi hapa ni kutoa elimu ya uraia ya kutosha!ni imani yangu kuwa watabadilika tu!

Siyo watabadilika.. Walishabadilika,sema ndiyo hivyo tena,siwezi kuita ni uchakachuaji ama ni nini... Ila, inaaminika Mh. Juma Njwayo,hakushinda!
 
Saa ya ukombozi imewadia.

Dalili ya mvua ni mawingu na mjinga akielevuka mjanja yuko mashakani.

Watanzania wa leo wameelevuka na watawala wasome alama za nyakati ukutani kama ilivokuwa kwa Roma empire na CCM .........

Ni kweli..
 
CDM .... Mko wapi? Sauti zackika zikiwahitaji huko Kusini inakuaje mkae kimya? Peleka jembe Lema kule awasilimishe....

Huku kwao chama pendwa ni CUF..

Yawezekana,kuja lakini hao CDM,kwani mwezi au miwili iliyopita,alikuja Mr Mbatia,Mh Machali,na wengine na NCCR yao,na waliiponda sana CCM kwa kuwaambia mkutano uliohudhuriwa kuwa mgombea wa wananchi 'alichakachuliwa'
 
Back
Top Bottom