Sakata la Mahujaji: Utendaji ATCL na Yaliyojiri Hadi Leo Hii

mkuu mtu wa pwani.........

moja kati ya mahujaji ambao walishushwa juzi,leo alfajiri amenitumia sms kunambia tayarti kuwa wapo makka na yumo ndani ya basi kuelekea mADINA.

sijui kundi la pili litaondoka lini.

hapa kuna mchezo mchafu sana umechezwa,naamini JK akirudi hizo hasira zake sijui zitakuwaje.hii itampa speed kuvunja baraz alote la MAWAZIRI na kutuletea DAMU MPYA ZA VIJANA GRADUATES.

i guess hata zile BODI za serikali nazo hivi sasa mguu ndani mguu nje,naamini JK atatupa zawadi safi sana YA MWAKA MPYA mola akipenda.

hili igizo lmebeba mambo mengi na nnaamini kama tutakaa na kuyachambua tutaweza kupata picha vipi nchi yetu inavoendeshwa.

na rais anaweza kupata picha vipi anavyodanganywa na wajanja.

kazi sio ndogo kwa keli kunahitajika kulitumia vyema hili igizo ili tuweze kupata big picture
 
mtu wa pwani...........

unajua kuna siku sikumbuki thread gani,nilimkemea sana Mzee ES kuwaita watendaji wa serikali yetu JK AMEZUNGUKWA NA KUNDI LA WAHUNI NA WABABAISHAJI...........lkn kila siku zikienda mbele nayakumbuka sana maneno ya mzee ES,kweli JK ana kazi kubwa sana huko mbele.yaani jamaa wamemsubiri ameshapaa angani baadae wakawashusha MAHUJAJI,duh hiyo kweli amepigwa chenga ya mwili.lakini mie bado naamini UKIMUONA KOBE AMEINAMA ujue ANATUNGA SHERIA. tusubiri tuone.
 
kinyau........

mkuu wa KAYA anasema akirudi from DC lazima ale vichwa vya akina KARAMAGI,M/KITI WA BODI YA TANENSCO,ATC na akina chenge na wenzake.

this time nasikia anasema ANAMKOMALIA NYANI KIROHO MBAYA.
 
there you go, kwanini uling'ang'ania ooh waislam mmewasaidiaje wenzenu? suala ni la sisi wengine tusio waislam pia tumewasaidiaje? na ndio maana mreme kaenda kujitafutia ujiko. Mamaa kwenye shida hatuangalii shida ni ya nani ili asaidiwe.
Good day mama.

..swali la mama lao lina mantiki sana,tena nzito!

..kuna mtu kasema waislam wengi hawana fedha,sasa,hii sijui data zimetoka wapi,ila,kitu kama maji ya kunywa,haihitaji hela sana!

..suala ni mshikamano!na kujaliiana!
 
kinyau........

mkuu wa KAYA anasema akirudi from DC lazima ale vichwa vya akina KARAMAGI,M/KITI WA BODI YA TANENSCO,ATC na akina chenge na wenzake.

this time nasikia anasema ANAMKOMALIA NYANI KIROHO MBAYA.

..engineer,

..anasema au umesikia!nyeti kama hiyo nzito!hebu weka clear basi!
 
* Waingizwa kwenye ndege kisha washushwa

*Waambiwa ndege haina kibali cha kutua

* Mrema atangaza kuwa ni janga la kitaifa

*Hatimaye kundi la kwanza laondoka jana jioni

Muhibu Said na Salim Said, MUM

KUKWAMA kwa mahujaji zaidi ya 1,000 kuondoka nchini juzi kwenda Makka, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hijja, kumeingia katika sura mpya, baada ya baadhi yao kushushwa katika ndege waliyokuwa wamepanda kwa madai ya ndege hiyo kutokuwa na kibali cha kutua nchini humo.

Mahujaji hao wapatao 379, walishushwa katika ndege saa 9:00 za usiku wa kuamkia jana baada ya viongozi wa Shirika la Ndege nchini (ATC) kuwaruhusu kupanda majira ya saa 5:00 za usiku huo tayari kuanza safari ya kwenda nchini humo kutekeleza ibada hiyo.

Ndege hiyo DC 10 iliyowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 1:00 ya usiku jauzi, inamilikiwa na kampuni ya Al-wasaa DC 10 ya familia ya Mfalme wa nchi ya Ras-Alkhaima iliyoko katika Umoja

wa Falme za Kiarabu (UAE).

Ilikodiwa na uongozi wa ATC, baada ya ndege ya awali iliyokuwa iwasafirishe mahujaji hao Desemba 3, mwaka huu, kudaiwa kupatwa na matatizo ya kiufundi.

Mahujaji hao walishushwa katika ndege hiyo dakika chache baada ya uongozi wa ATC kumhakikishia Rais Jakaya Kikwete aliyefika uwanjani hapo akielekea nchini Marekani kwamba safari ya mahujaji hao ilikuwa imeiva.

Kabla ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kumsindikiza Rais Kikwete, Waziri Mkuu, Edward Lowassa alifika na kuwaomba radhi Waislamu na Watanzania kwa jumla kutokana na yaliyowakumba mahujaji hao.

Lowassa aliwaambia mahujaji hao kuwa kitendo kilichofanywa na uongozi wa ATC ni kibaya na kwamba ana wasiwasi kuwa ndani ya shirika hilo kuna viongozi wasio waaminifu.

Kutokana na hali hiyo, Lowassa alisema Rais Kikwete ametoa pole kwa mahujaji kutokana na usumbufu uliowapata.

Lowassa alisema taarifa za kukwama kwao kuondoka, walizipata usiku wa Desemba 9 na kuongeza kuwa hali hiyo imemuudhi Rais Kikwete kupindukia.

�Sijawahi kumuona Rais akikasirika kama siku hiyo na alikuwa akihangaika akipiga simu kwa falme mbalimbali za Kiarabu ili msafiri,� alisema Lowassa kauli ambayo iliwapa matumaini mahujaji hao kuondoka.

Habari zilizopatikana uwanjani hapo na kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa serikali na viongozi wa taasisi zinazoratibu safari za mahujaji hao, zinaeleza kuwa baada ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo, alikataa kuondoka mpaka mahujaji wote waondoke.

�Viongozi wa ATC wakaona rais hataondoka. Ndipo wakaamua kuwaingiza mahujaji ndani ya ndege, huku wakimhakikishia kuwa safari yao imeiva na wakati wowote wangeondoka,� alisema mmoja wa maofisa wa serikali uwanjani hapo jana.

Ofisa huyo alisema kauli hiyo ilimridhisha Rais Kikwete ambaye aliondoka, lakini saa chache baadaye uongozi wa ATC ukawafuata mahujaji hao ndani ya ndege na kuwashusha.

Akisimulia mkasa huo, Imamu wa Msikiti wa Mtoro, ambaye ni mmoja wa mahujaji waliotarajiwa kuondoka, Sheikh Abbas Ramadhani, alisema baada ya kupatwa na mkasa

huo, hadi kufikia jana saa 7 mchana, walipoteza matumaini ya kuondoka kwani wakati huo mji wa Madina, nchini Saudi Arabia ambako walitakiwa waingie milango ya kuingia ilikuwa imeshafungwa na pia milango ya kuingia mahujaji nchini humo, ilitarajiwa kufungwa usiku wa kuamkia leo.

Mbali na hilo, Sheikh Abbas alisema jambo lingine lililowakatisha tamaa ni kauli za kuwakanganya zinazotolewa na rubani wa ndege hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATC, Balozi Mustafa Nyang�anyi kuhusu hatima ya safari yao.

�Wakati rubani anasema kuwa hajapata kibali cha kutua Madina, Balozi Nyang�anyi naye anasema hakuna nafasi ya kutua uwanja wa ndege wa Saudi Arabia. Tunasikitika kwa kunyang�anywa nguzo yetu ya msingi ya kuabudu,� alidai Sheikh Abbas.

Hata hivyo, wakati Sheikh Abbas akisema hayo, jana saa 4:00 asubuhi, ilielezwa na mtangazaji kupitia vipaza sauti vya uwanjani hapo kuwa kibali hicho kilikuwa kimepatikana

kutoka Ikulu nchini, lakini safari ya kundi la kwanza la mahujaji 379

iliyotarajiwa ianze muda huo isingewezekana kutokana na kibali cha ndege kutua katika uwanja wa ndege wa Jeddah, nchini Saudi Arabia kutokuwapo.

Tangazo hilo liliwakatisha tamaa zaidi mahujaji hao, hasa baada ya muda ambao walitangaziwa kuwa wangeondoka, kuisha bila kupewa taarifa zozote na wahusika.

Kutokana na hali hiyo, mahujaji watatu kutoka visiwani Zanzibar walikata tamaa wakaamua kuahirisha safari na kurejea nyumbani.

Mwenyekiti wa taasisi ya Zanzibar Istiqama Hajj and Travell tawi la Dar es Salaam, Sheikh Abdallah Mohamed, alithibitisha hilo uwanjani hapo jana.

�Kuna mwingine yuko kwenye chumba amenitaka nikamchukulie tiketi yake, lakini sijaenda, kwa sababu nakwenda kwenye kikao na Mustafa Nyang�anyi ili kujua hatima ya safari yao. Binafsi tunaona uwezekano haupo...,� alisema Sheikh Mohamed.

Wakati hayo yakijiri, mahujaji zaidi ya 300 waliotarajiwa kuondoka jana, wamefungiwa katika chumba cha kuondokea, huku wakikosa huduma za chakula na maji na mahujaji wawili walianguka uwanjani hapo, kutokana na shinikizo la damu na

kifafa.

�Tunaiomba serikali ilete huduma ya kwanza,� alisema Sheikh Abbas.

Saa 9:30 mchana, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alifika uwanjani hapo na kuwafariji kwa kuwapa mahujaji hao katoni 10 za maji safi, huku akiiita kukwama kwa mahujaji hao kuondoka nchini kuwa ni tatizo la kitaifa.

Mrema alisema ameshangazwa kuona karne ya 21 serikali ikishindwa kuwasifirisha mahujaji ambao wamelipa fedha zao wenyewe, huku rais akithubutu kuondoka na

kuwaacha wakikaa uwanjani hapo kwa zaidi ya siku tisa.

Kiongozi wa Muda wa Mahujaji hao, Seifullah Rajabu huku akibubujikwa na machozi, alisema matumaini ya nia zao kufika Makka na Madina kwa ajili ya ibada ya Hijja,

yameanza kufifia.

�Shida ndio vazi la Waislamu, matatizo ndio chai ya Waislamu na huzuni ndio chakula cha Waislamu wa nchi hii. Sijui Waislamu tumekosa nini?,� alihoji Seifullah na kuwafanya mahujaji na baadhi ya ndugu na jamaa waliowasindikiza kuangua kilio uwanjani hapo.

Dakika chache baadaye, viongozi wa harakati za Kiislamu, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ponda Issa Ponda, Sheikh Mussa Kundecha na Maalim Ali Bassaleh, walifika uwanjani hapo na kuwahutubia mahujaji hao.

Kabla ya kuwahutubia, mahujaji hao walisimama na kukusanyika katika kundi moja na kuanza kutoa vivumo vya sauti za maneno ya �Takbiyr, Allahu Akbar� kama ishara ya

kuwaunga mkono masheikh hao.

Maalim Bassaleh alisema kadhia iliyowakuta mahujaji hao, ni dhulma dhidi ya Waislamu na kusema kuwa wataendelea kudai haki yao.

�Haki yetu ya kudhulumiwa tutaidai kwa njia yoyote. Kama ni kwenda mahakamani au ni barabarani, tutaidai. Hatukubali...,� alisema Maalim Bassaleh.

Sheikh Ponda alidai kuwa kuna watu ambao wamepandikizwa ili kuwafanya Waislamu waone kuwa matokeo hayo, ni mipango ya Mungu, wakati si kweli.

Naye Sheikh Kundecha alisema dhulma, imekuwa ni mwendelezo wa mambo mengi mabaya

wanayofanyiwa Waislamu nchini na kuwataka waumini hao kuwungana kudai haki zao.

�Hivyo, cha msingi Waislamu tuwe kitu kimoja ili kujua namna ya kuwaambia hawa

mabwana waliotudhulumu,� alisema Sheikh Kundecha.

Katika hatua nyingine, jana jioni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro alitangaza kwamba kundi la kwanza la mahujaji 379 lingeondoka, kundi la pili litarajiwa kuondoka leo leo saa 11 alfajiri na la tatu litaondoka leo saa 11 jioni.

Alisema kwamba serikali ya Saudia imekubalia serikali ya Tanzania mahujaji kuweza kutua Madina na kwenda kwa njia ya basi hadi katika sehemu ya kufanya ibada ya hijja.
 
Tatizo letu tunafikiri kila tatizo ni la kisiasa. Hili halikuwa tatizo la kisiasa, ni tatizo la ki-uwezo (incompetence) ndani ya ATC na wateja wao kwa upande mwingine. in the first place walipaswa kufanya utafiti wa kutosha kupata shirika zuri kabla ya kutoa mapesa yao. Kitendo cha kukubali kuingia mkenge kwa ATC wanapaswa kujilaumu wao kwanza, then ATC na sioni kwa nini serikali ihusike katika jambo la shirika la usafiri na wateja wao.

Kama tunafikiri kila tatizo linalotokea ni la kisiasa na hivyo liwe solved kisiasa, tunajiua wenyewe. Mbaya zaidi tunafikiri kila tatizo lazima liwe solved na Rais au Waziri Mkuu, how stupid we have become! Sasa kama Rais anasema lazima waondoke, bila hata kujua technicalities zilizopo unafikiri ATC wangefanyeje? Ndio maana wakaswaga kwenye ndege halafu walipoona Rais ameondoka wakawashusha maana walijua politically yes, but technically haiwezekani!

Tujifunze kuziamini taasisi zilizopo katika kushughulikia matatizo, hii ya kila kitu kuwakimbilia wanasiasa ni ujinga. Wanasiasa wanapenda short cut ili wapate sifa hapohapo, katika hali ya kawaida ya maisha, mambo hayaendi hivyo. Lazima kufuata taratibu.

Next time waislamu wajifunze kwamba ATC ni bomu na wasikubali kuweka hela zao huku. Hakuna swala la dini hapa wala waislamu kunyanyaswa. Ni swala la incompetence ya ATC na wahujaji wenyewe kukubali kuwekeza hela zao kwenye shirika fake wakati kuna mashirika kibao yaliyo smart. It is that simple.
 
Mwenye ez Mungu awazidishie moyo wa subira Mahujaji wote na watekeleze ibada yao vyema kabisa na awalipe kheri duniani na akhera. Hii ni ishara njema kuwa kila mtu ana hamu ya kwenda kutekeleza nguzo hii tukufu. Mwenye ez Mungu atamlipa kila mmoja kwa mujibu wa nia yake.

Kama mtu hana uwezo wa kifedha au kiafya lakini nia yake ni safi basi Mwenye ez Mungu atamlipa sawa na walioenda Hija. Mwenye ez Mungu atuwezeshe kuhiji kama sio mwaka huu iwe mwakani. Tuende tukalidhuru karibu lake habibina Mustafa Muhammad rehema na amani na baraka zimmiminikie. Tuende tukaone historia ya ajabu ya babu wa mitume wetu Nabii Issa na Nabii Muhammad rehema na baraka za Mungu ziwamiminikie nae ni Mtume Ibrahimu rehema zimmiminikie.

Tunashauku kubwa nasi tukusanyike katika viwanja vitukufu vya Arafati, tuitufu nyumba tukufu Kaaba, tusali katika msikiti wake kipenzi cha Mwenye ez Mungu Muhammad rehema na baraka zimmiminikie. Na ikiwezekana Mwenye ez Mungu atufishe katika miji hii mitukufu Makka au Madina au baina yake AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN AMIN
 
haya ndiyo mambo yanayoniudhi mara tunaambiwa ohhh tusichanganye DINI na SIASA huku serikali iko involved na mambo ya kidini utafikiri nini sijui....

Hii ni mess ya waislam na ATC na probably baraza kuu na Hajj trust sasa waziri mkuu anahirisha mambo muhimu ya serikali ili ili awaccomodate waislam. Najua ni un popular opinion humu JF lakini huu ni unafiki wa hali ya juu kabisa, sitoshangaa serikali ikaanza kutumia kodi za wasio waislam na wasio na dini ili kuwafurahisha hawa watu

Game
Naungana na wewe Serikali inatakiwa kuwa crystal clear kuwa isingilie mambo ya dini, this is cheap politics. Hiyo ni weakness aliyoonesha EL na serikali kujaribu kujipendekeza. Naona kama kuna kitu anatafuta.
Kuna jumuiya zinazoshughulikia mambo hayo kwa nini asiziachie? Mimi naona opinion yako sio un popular, it is very genuine and it needs to be discussed. Kuna mahali pia nimesoma kule kwenye thread ya dini, wanataka kumsomea Mataka itikafu. Haya mambo mimi naona kama nikuwadhalilisha waislamu na kuleta ujinga kwenye serikali.
 
hapa kuna mchezo mchafu sana umechezwa,naamini JK akirudi hizo hasira zake sijui zitakuwaje.hii itampa speed kuvunja baraz alote la MAWAZIRI na kutuletea DAMU MPYA ZA VIJANA GRADUATES.
.

Kama unategemea JK atafanya mabadiliko yoyote unaota, kitakachofanyika hapa ni kuwaumiza wale wasio mtandao na kuwasifu wengine. Na inawezekana yeye mwenyewe naye amewauza mahujaji, hii ndio bongo.
 
Uwanja Wa Ndege Wageuzwa Mahali Pa Hija Poa Tu Tutaingiza Pesa Zakigeni
 
Game na wenzako..JK na EL walikuwa ktk SAFARI zao..hawakwenda airport eti kuwasaidia waislam...its like EL/JK wapite Morogoro njiani wakute barabara imefungwa na ipo AJALI..obvious..watasimama na kutoa Pole...magazeti yameandika EL alikwenda kumsindikiza JK..hapa JF source zimekuwa millions..kila mtu na yake...
Kimsingi Game na Wenzake usifafanishe na watu walotoa pesa zao kuipa serikali MTAJI wa Kunnua Ndege...ATC ipo Taabani..ilichofanya for my personal understanding..ku-loby viongozi wa safari za Hijja kuwa wao watawapeleka Hijja...HAPA JF mmeanzisha thread Maalum ya Kuwa ATC wananunua ndege MPYA 2..so mitaji itaokotwa..hata ukikopa lazima ulipe...Viongozi wa Kiislam kama watanzania wengine ambao wanaona kwanini FEDHA iende kwa Shirika ya NCHI..kwani wasiwape wa-TZ wenzao?

Ofourse kama wengine walivvyosema ATC inamilikiwa na Serikali...so mtoto akikutukana lazima umshitaki kwa babake...
 
mkuu mtu wa pwani.........

moja kati ya mahujaji ambao walishushwa juzi,leo alfajiri amenitumia sms kunambia tayarti kuwa wapo makka na yumo ndani ya basi kuelekea mADINA.

sijui kundi la pili litaondoka lini.

hapa kuna mchezo mchafu sana umechezwa,naamini JK akirudi hizo hasira zake sijui zitakuwaje.hii itampa speed kuvunja baraz alote la MAWAZIRI na kutuletea DAMU MPYA ZA VIJANA GRADUATES.

i guess hata zile BODI za serikali nazo hivi sasa mguu ndani mguu nje,naamini JK atatupa zawadi safi sana YA MWAKA MPYA mola akipenda.

engneer kwa namna serikali hii inavyoendeshwa kisanii na kishkaji lolote linawezekana,usishangae kama rais pia alikuwa akijua kuwa wale abiria wanaingizwa ndani ya ndege kuwazuga tu....wewe unafikiri angepitaje pale na angewaambia nini kipya ..kama si kuwaambia usafiri tayari pandeni ..at least ilileta hali ya utulivu ...sio rahisi kwa uamuzi wa kuwapiga chnga la macho abiria ufanyike na kina mustapha nyanganyi..tena mbele ya waziri mkuu ,makamu wa rais ,na watu wa vyombo vya usalama..ambao definatelly walikuwapo pale uwanjani kumsubiri rais na amiri jeshi mkuu.....itakuwa ulikuwa uamuzi wa pamoja ..lakini msalaba wake ukaamuliwa waubebe kina mustapha [kwamba wao ndio wamehadaa]....haingewezekana kabisa wafanye vile bila baraka ...

uamuzi wa rais kuzuga kuwa hapandi kwenye ndege hadi mahujaji waondoke ...ulikuwa ni wa kisiasa..na kujikosha...huku akijua wazi kuwa safari usiku ule haingewezekana ,huku kibinadamu akikosa ujasiri wa kuwaambia wazi abiria walikwisha subiri siku 9 kuwa ...jamani safari itakuwa tayari baada ya masaa 18!!!

ni wazi katika mchakato huu wengi lazima wafukuzwe kazi kihalali na wengine wazi lazima watolewe kafara kama mbuzi au kondoo wa shughuli kama sabuni ya kuosha jina maarufu la muungwana na serikali yake!!!!!
 
Game na wenzako..JK na EL walikuwa ktk SAFARI zao..hawakwenda airport eti kuwasaidia waislam...its like EL/JK wapite Morogoro njiani wakute barabara imefungwa na ipo AJALI..obvious..watasimama na kutoa Pole...magazeti yameandika EL alikwenda kumsindikiza JK..hapa JF source zimekuwa millions..kila mtu na yake...
Kimsingi Game na Wenzake usifafanishe na watu walotoa pesa zao kuipa serikali MTAJI wa Kunnua Ndege...ATC ipo Taabani..ilichofanya for my personal understanding..ku-loby viongozi wa safari za Hijja kuwa wao watawapeleka Hijja...HAPA JF mmeanzisha thread Maalum ya Kuwa ATC wananunua ndege MPYA 2..so mitaji itaokotwa..hata ukikopa lazima ulipe...Viongozi wa Kiislam kama watanzania wengine ambao wanaona kwanini FEDHA iende kwa Shirika ya NCHI..kwani wasiwape wa-TZ wenzao?

Ofourse kama wengine walivvyosema ATC inamilikiwa na Serikali...so mtoto akikutukana lazima umshitaki kwa babake...

chuma nilisikiliza mahujaji waliokuwa wanaongea na mustapha nynganyi pale ATC HOUSE..wanasema kuwa mara zote huwa wanachangishana pesa kupitia taasisi mbali mbali..na baadaye wanalipa shirika la emirates au mengine ya ghuba yanawasafirishaga bila wasi...na ndio maana hapajakuwa na tatizo la mahujaji huko nyuma...wakasema kuwa ATC walishaacha kuitumia miaka mingi iliyopita kutokana na uswahili....

mwaaka huu wanasema mustapha nyanganyi baada ya kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi...aliwapitia na kuwaomba kuwa mwaka huu walipe kazi shirika lake[ATC]...yule kiongozi wao akasema kwa kuzingatia nyanganyi ni muislamu mwenzao ..walimuamini na ndio kisa cha wao kuamua kutumia ATC MWAKA huu....

kitu kingine ambacho bado sijapata jibu..naambia mahujaji walokwama ni wa taasisi za kiislamu tu...wale wa BAKWATA ambao miaka yote mahujaji wanakataa kuitumia kwenda hijja ukizingatia haiaminiki na inaonekana ni ya serikali ..mwaka huu ni safiii na wameondoka kwa wakati bila tatizo...sidhani kama wao wametumia ATC..
 
kuwafuka kazi uongozi wa ATC ni kuwaonea tu,wao JK na EL walitudanganya umeme wa richimiduli na mpaka leo haupo ,wajuidhulu wao kwanza ndio sisi tufuatie apendwi mtu.
 
Posted Date::12/13/2007
Usanii watawala safari ya mahujaji
* Waingizwa kwenye ndege kisha washushwa

*Waambiwa ndege haina kibali cha kutua

* Mrema atangaza kuwa ni janga la kitaifa

*Hatimaye kundi la kwanza laondoka jana jioni

Muhibu Said na Salim Said, MUM
Mwananchi

KUKWAMA kwa mahujaji zaidi ya 1,000 kuondoka nchini juzi kwenda Makka, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hijja, kumeingia katika sura mpya, baada ya baadhi yao kushushwa katika ndege waliyokuwa wamepanda kwa madai ya ndege hiyo kutokuwa na kibali cha kutua nchini humo.

Mahujaji hao wapatao 379, walishushwa katika ndege saa 9:00 za usiku wa kuamkia jana baada ya viongozi wa Shirika la Ndege nchini (ATC) kuwaruhusu kupanda majira ya saa 5:00 za usiku huo tayari kuanza safari ya kwenda nchini humo kutekeleza ibada hiyo.

Ndege hiyo DC 10 iliyowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 1:00 ya usiku jauzi, inamilikiwa na kampuni ya Al-wasaa DC 10 ya familia ya Mfalme wa nchi ya Ras-Alkhaima iliyoko katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Ilikodiwa na uongozi wa ATC, baada ya ndege ya awali iliyokuwa iwasafirishe mahujaji hao Desemba 3, mwaka huu, kudaiwa kupatwa na matatizo ya kiufundi.

Mahujaji hao walishushwa katika ndege hiyo dakika chache baada ya uongozi wa ATC kumhakikishia Rais Jakaya Kikwete aliyefika uwanjani hapo akielekea nchini Marekani kwamba safari ya mahujaji hao ilikuwa imeiva.

Kabla ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kumsindikiza Rais Kikwete, Waziri Mkuu, Edward Lowassa alifika na kuwaomba radhi Waislamu na Watanzania kwa jumla kutokana na yaliyowakumba mahujaji hao.

Lowassa aliwaambia mahujaji hao kuwa kitendo kilichofanywa na uongozi wa ATC ni kibaya na kwamba ana wasiwasi kuwa ndani ya shirika hilo kuna viongozi wasio waaminifu.

Kutokana na hali hiyo, Lowassa alisema Rais Kikwete ametoa pole kwa mahujaji kutokana na usumbufu uliowapata.

Lowassa alisema taarifa za kukwama kwao kuondoka, walizipata usiku wa Desemba 9 na kuongeza kuwa hali hiyo imemuudhi Rais Kikwete kupindukia.

Sijawahi kumuona Rais akikasirika kama siku hiyo na alikuwa akihangaika akipiga simu kwa falme mbalimbali za Kiarabu ili msafiri,� alisema Lowassa kauli ambayo iliwapa matumaini mahujaji hao kuondoka.

Habari zilizopatikana uwanjani hapo na kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa serikali na viongozi wa taasisi zinazoratibu safari za mahujaji hao, zinaeleza kuwa baada ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo, alikataa kuondoka mpaka mahujaji wote waondoke.

Viongozi wa ATC wakaona rais hataondoka. Ndipo wakaamua kuwaingiza mahujaji ndani ya ndege, huku wakimhakikishia kuwa safari yao imeiva na wakati wowote wangeondoka,� alisema mmoja wa maofisa wa serikali uwanjani hapo jana.

Ofisa huyo alisema kauli hiyo ilimridhisha Rais Kikwete ambaye aliondoka, lakini saa chache baadaye uongozi wa ATC ukawafuata mahujaji hao ndani ya ndege na kuwashusha.

Akisimulia mkasa huo, Imamu wa Msikiti wa Mtoro, ambaye ni mmoja wa mahujaji waliotarajiwa kuondoka, Sheikh Abbas Ramadhani, alisema baada ya kupatwa na mkasa
huo, hadi kufikia jana saa 7 mchana, walipoteza matumaini ya kuondoka kwani wakati huo mji wa Madina, nchini Saudi Arabia ambako walitakiwa waingie milango ya kuingia ilikuwa imeshafungwa na pia milango ya kuingia mahujaji nchini humo, ilitarajiwa kufungwa usiku wa kuamkia leo.

Mbali na hilo, Sheikh Abbas alisema jambo lingine lililowakatisha tamaa ni kauli za kuwakanganya zinazotolewa na rubani wa ndege hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATC, Balozi Mustafa Nyang�anyi kuhusu hatima ya safari yao.

Wakati rubani anasema kuwa hajapata kibali cha kutua Madina, Balozi Nyang�anyi naye anasema hakuna nafasi ya kutua uwanja wa ndege wa Saudi Arabia. Tunasikitika kwa kunyang�anywa nguzo yetu ya msingi ya kuabudu,� alidai Sheikh Abbas.

Hata hivyo, wakati Sheikh Abbas akisema hayo, jana saa 4:00 asubuhi, ilielezwa na mtangazaji kupitia vipaza sauti vya uwanjani hapo kuwa kibali hicho kilikuwa kimepatikana kutoka Ikulu nchini, lakini safari ya kundi la kwanza la mahujaji 379

iliyotarajiwa ianze muda huo isingewezekana kutokana na kibali cha ndege kutua katika uwanja wa ndege wa Jeddah, nchini Saudi Arabia kutokuwapo.

Tangazo hilo liliwakatisha tamaa zaidi mahujaji hao, hasa baada ya muda ambao walitangaziwa kuwa wangeondoka, kuisha bila kupewa taarifa zozote na wahusika.

Kutokana na hali hiyo, mahujaji watatu kutoka visiwani Zanzibar walikata tamaa wakaamua kuahirisha safari na kurejea nyumbani.

Mwenyekiti wa taasisi ya Zanzibar Istiqama Hajj and Travell tawi la Dar es Salaam, Sheikh Abdallah Mohamed, alithibitisha hilo uwanjani hapo jana.

Kuna mwingine yuko kwenye chumba amenitaka nikamchukulie tiketi yake, lakini sijaenda, kwa sababu nakwenda kwenye kikao na Mustafa Nyang�anyi ili kujua hatima ya safari yao. Binafsi tunaona uwezekano haupo...,� alisema Sheikh Mohamed.

Wakati hayo yakijiri, mahujaji zaidi ya 300 waliotarajiwa kuondoka jana, wamefungiwa katika chumba cha kuondokea, huku wakikosa huduma za chakula na maji na mahujaji wawili walianguka uwanjani hapo, kutokana na shinikizo la damu na kifafa.

Tunaiomba serikali ilete huduma ya kwanza,� alisema Sheikh Abbas.

Saa 9:30 mchana, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alifika uwanjani hapo na kuwafariji kwa kuwapa mahujaji hao katoni 10 za maji safi, huku akiiita kukwama kwa mahujaji hao kuondoka nchini kuwa ni tatizo la kitaifa.

Mrema alisema ameshangazwa kuona karne ya 21 serikali ikishindwa kuwasifirisha mahujaji ambao wamelipa fedha zao wenyewe, huku rais akithubutu kuondoka na kuwaacha wakikaa uwanjani hapo kwa zaidi ya siku tisa.

Kiongozi wa Muda wa Mahujaji hao, Seifullah Rajabu huku akibubujikwa na machozi, alisema matumaini ya nia zao kufika Makka na Madina kwa ajili ya ibada ya Hijja, yameanza kufifia.

Shida ndio vazi la Waislamu, matatizo ndio chai ya Waislamu na huzuni ndio chakula cha Waislamu wa nchi hii. Sijui Waislamu tumekosa nini?,� alihoji Seifullah na kuwafanya mahujaji na baadhi ya ndugu na jamaa waliowasindikiza kuangua kilio uwanjani hapo.

Dakika chache baadaye, viongozi wa harakati za Kiislamu, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ponda Issa Ponda, Sheikh Mussa Kundecha na Maalim Ali Bassaleh, walifika uwanjani hapo na kuwahutubia mahujaji hao.

Kabla ya kuwahutubia, mahujaji hao walisimama na kukusanyika katika kundi moja na kuanza kutoa vivumo vya sauti za maneno ya �Takbiyr, Allahu Akbar� kama ishara ya kuwaunga mkono masheikh hao.

Maalim Bassaleh alisema kadhia iliyowakuta mahujaji hao, ni dhulma dhidi ya Waislamu na kusema kuwa wataendelea kudai haki yao.

�Haki yetu ya kudhulumiwa tutaidai kwa njia yoyote. Kama ni kwenda mahakamani au ni barabarani, tutaidai. Hatukubali...,� alisema Maalim Bassaleh.

Sheikh Ponda alidai kuwa kuna watu ambao wamepandikizwa ili kuwafanya Waislamu waone kuwa matokeo hayo, ni mipango ya Mungu, wakati si kweli.

Naye Sheikh Kundecha alisema dhulma, imekuwa ni mwendelezo wa mambo mengi mabaya wanayofanyiwa Waislamu nchini na kuwataka waumini hao kuwungana kudai haki zao.

�Hivyo, cha msingi Waislamu tuwe kitu kimoja ili kujua namna ya kuwaambia hawa mabwana waliotudhulumu,� alisema Sheikh Kundecha.

Katika hatua nyingine, jana jioni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro alitangaza kwamba kundi la kwanza la mahujaji 379 lingeondoka, kundi la pili litarajiwa kuondoka leo leo saa 11 alfajiri na la tatu litaondoka leo saa 11 jioni.

Alisema kwamba serikali ya Saudia imekubalia serikali ya Tanzania mahujaji kuweza kutua Madina na kwenda kwa njia ya basi hadi katika sehemu ya kufanya ibada ya hijja.
 
PM..........

analysis yako naikubali mzee,ina maana unataka kusema jamaa wwalipigwa CHENGA LA MWILI?duh hii hatari sasa.
lakini mie naamini kuna somethings will happened,MUUNGWANA sio mjinga.naamini akirudi DC anakuja kula vichwa vya watu.
tuombe uhai na uzima tuone mambo yatakuwaje mwaka mpya.

MWAKA MPYA.....MAMMBO MAPYA
 
Dege laja ila bovu

2007-12-13 16:05:03
Na Simon Mhina, Airport

Dege lililoondoka jana usiku kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam kuwapeleka mahujaji nchini Saud Arabia, limeshindwa kulipeleka kundi lingine leo baada ya kubainika kuwa ni bovu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Abbas Kandoro amesema ndege hiyo baada ya kufanyiwa uchunguzi ilibainika kuwa paipu moja ya maji imepasuka na hivyo kusababisha maji yaende kwenye mfumo wa umeme na kuharibu kifaa kimoja muhimu.

Amesema kifaa hicho kimeagizwa nchini Afrika ya Kusini na kitaletwa na ndege ya ATC itakayotua Jijini Dar es Salaam saa 12:00 jioni leo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa, baada ya ndege hiyo kuwasili, ufungaji wa kifaa hicho utaanza mara moja na huenda ukachukua kama lisaa lizima.

Licha ya matatizo hayo, Bw. Kandoro amesema safari ya mahujaji iko pale pale.

``Bado ninaamini mahujaji wataondoka saa 2:00 usiku leo`` amesema Bw. Kandoro.

Awali ilielezwa kuwa mahujaji walikuwa wameshapanda kwenye ndege hiyo lakini wakashushwa baada ya kubainika kuwepo kwa hitilafu.

Akizungumza na Alasiri uwanjani hapo, Alhaj Abdallah Salimu ambaye ni mmoja wa mahujaji wanaoendelea kusota uwanjani hapo, amesema baada ya ndege hiyo kuwasili leo asubuhi walijawa na matumaini ya kusafiri, hasa baada ya kupewa habari njema kuwa kundi la kwanza lililoondoka jana jioni limefika Makka salama.

Akasema mahujaji waliokuwepo uwanjani hapo walianza kupanda ndani ya ndege hiyo wakiamini kuwa muda wao wa kuondoka kwenda hijja ulikuwa umewadia.

Hata hivyo amesema baada ya kupanda, marubani waliwaamuru kushuke.

Awali Mkuu wa mkoa aliliambia gazeti hili kwamba mahujaji wote wangeweza kusafiri kwa makundi.

``Tumeshafanya taratibu zote za kuhakikisha kuwa mahujaji wote wanakwenda hijja, hivyo hakuna kitakachoshindikana na taratibu zote zinakwenda vizuri,`` alisema Bw. Kandoro.

Alisema ndege hiyo aina ya MC Doglas ya Shirika la ndege la Global Aviation la Afrika Kusini inatumia masaa manne kusafiri mpaka Makka na masaa manne mengine kurejea Dar es Salaam.

Aikizungumzia muda wa mwisho wa ndege zinazosafirisha mahujaji kutua nchini Saud Arabia, ambao unamalizika saa 6:00 usiku wa leo, Bw. Kandoro alisema Serikali imeshalifanyia kazi suala hilo na kuweka mambo sawa.

``Sisi tumeshapewa kibali cha ndege yetu kutua hata kama muda huo utakuwa umemalizika,`` akasema Bw. Kandoro.

Mahujaji hao walipaswa kuondoka tangu Desemba 2 mwaka huu, na wamekuwa wakisota uwanjani hapo kwa zaidi ya siku nane, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ndege waliyokuwa wameandaliwa na Shirika la ndege la Tanzania, ATC, kuharibika.

Mahujaji ambao bado wanasota Jijini Dar ni 758 wakati wenzao 379 waliondoka jana usiku.

SOURCE: Alasiri
 
Pamoja na yooooooooote yaliyotokea binafsi najiuliza hivi serikali hii ya awamu ya nne haina watendaji wengine? Kila kitu Lowasa/JK, mahujaji Lowasa/JK, ujenzi wa nyumba NHC Lowasa/JK, madini Losawa/JK, Richmond Lowasa/JK, mpira Lowasa/JK, HIVI MAWAZIRI WALE 60 WAKO WAPI?? HIVI ILIKUWA NI LAZIMA LOWASA AHAIRISHE SAFARI KWA SABABU YA MAHUJAJI ? IS THERE NO OTHER COMPETENT TANZANIAS WHO CAN SOLVE THAT SMALL MAHUJAJI PROBLEM ?
 
Nimewaambia hapo awali huu ni usani wa kuchota pesa, mwakimbilia siasa. Sasa dege walilokodi ni bovu na utasikia gharama zilivyokuwa kubwa na Serikali kuu itafutia ATC deni!
 
Back
Top Bottom