Sakata la Mahujaji: Utendaji ATCL na Yaliyojiri Hadi Leo Hii

This is unforgivable! Yaani mtu aliyegharamia safari yake anacheleweshwa kwa siku zote hizo? Imagine tangu tarehe 3, ni karibu siku 9! Jamani, this is extremely unfair, na yeyote anayewatetea hao ATC sitamwelewa kamwe! Ucheleweshaji wa siku 1 au 2 nadhani ungevumilika, tunaosafiri mara kwa mara tunaelewa mambo haya hutokea na mashirika husika huwajibika ipasavyo. Lakini siku 9! This is utterly ridiculous, unacceptable by any description on earth! Nasubiri kuona hatua itakayochukuliwa, na namshauri anayehusika asiogope kutuhumiwa udini kwani huu ulikuwa utaratibu wa KIBIASHARA, si wa kidini. Sidhani kama ATC walikuwa wanajitolea sadaka kusaidia mahujaji, ingekuwa hivyo tungelalamika udini. Lakini ATC walichangamkia nafasi ya biashara kusafirisha abiria hao, na imekiuka mkataba na kuwadhalilisha abiria wake. Mwungwana kaka yetu JK kwa kuwa alishaingilia kati hili suala, namwomba amalizie, asiishie tu kukodisha ndege imetoka, no! Ni suala la kutetea haki za watumiaji wa hivi vyombo. Kama watu zaidi ya 1,000 wanaweza kufanyiwa uzembe kiasi hicho na yakapita hivihivi, sijui nikiwa peke yangu na mke wangu tumedhulumiwa nani atakayetutetea? Anzia hapa, lazima tujenge utamaduni wa uwajibikaji na kuwatetea raia wetu. Narudia: Nasubiri kuona hatua atakayochukua mheshimiwa Rais katika sakata hili.

Sawa kabisa, Mkuu! Kinachosikitisha ni pale wateja wanaposema 'inshaallah, kama Mungu amepanga safari kuwepo itakuwepo'. Pamoja na kumuomba mungu wangekuwa wanawasiliana na mawakili wao kutafuta namna ya kuwashikisha adabu ATC! Yaani Mheshimiwa Rais anashinda kupiga simu kuwatafutia usafiri watu wake? Kama ulivyosema, yasiishie hapa!
 
Hofu yangu ni kuwa Tanzania tunataka kuingia kwenye mtego wa "entitlement". Kuna vitu ambavyo watu wanastahili na ni haki yao kimsingi. Lakini wakati mwingine hii entitlement inakuwa misplaced kwa namna fulani.

Wakati mamia ya wananchi wa Kigoma walipocheleweshewa treni wiki ile ya uchaguzi wa CCM tena kwa wiki moja na wengi wao kupoteza muda wa shughuli zao, tena wakaandamana na kulia serikali ifanye kitu, siyo Waziri Mkuu wale waziri kivuli aliyejitokeza kwenda kuwasaidia, kwa sababu inakubalika "hivyo ndivyo ilivyo".

Kitu pekee ambacho kimemfanya Waziri Mkuu afuatilie ni maslahi ya CCM. Tayari kuna manung'uniko kuhusu suala hili na tangia juzi minong'ono ya "njama" na "wabaya wetu" imeanza kusikika chini kwa chini. Kitendo cha Sheih Issa Ponda kujitokeza pale na kuwahamasisha Waislamu kukutana Magomeni na baadaye kuamua kupanga kama ni maandamano au chochote kile kimewashtua CCM na serikali yake.

Kama vile walivyofanya suala la Richmond, Madini n.k Serikali inajaribu kupiga hatua moja ya haraka ili watu wasichukizwe na serikali yao. Tayari takwimu zimeonesha wameanza kupoteza umaarufu, sasa watakuwa wamefilisika kisiasa kama watashindwa kusoma alama za nyakati na hivyo lazima watengeneze mashujaa!. Hapo ndipo kiongozi mahiri, hodari, shujaa aliyetamba Bungeni anapoingia.

Unapokuwa na suala nyeti na muhimu kama hili halafu unampango mmoja tu ni dalili ya kutokuwa na uongozi mzuri kwenye taasisi zinazosimamia hija hapo Nyumbani. Hivi kuna mashirika mangapi yanayorusha watu hadi Saudia kutoka Bongo?
 
mbona serikali hii hii haikuingia kati kuwasaidia wanafunzi wa UKRAINE?

Mjomba hii ni PR excercise at the expense of walipa kodi ambao si waislam

JF mnasifika kwa kuwa ma free thinkers mbona hili hamtaki kuliangalia kwa undani zaidi?


Hapa niko nawe GT. Hii ni PR-show. Mazingaombwe kama kawa.

Ninachosikitika tu ni kwamba wakati mazingaombwe haya yakifanyika, na cameramen wakiwa busy kuchukua snap ya Suka(jk) na Konda(el) wake kwa ajili magazeti; wanaoumia ni mahujaji hao.
 
Hebu tuache suala la udini tujadili hili: Kuna abiria zaidi ya 1000 wamelipa mamailioni ya fedha zao kwa kampuni fulani iwasafirishe kwenda huko wanakotaka, lakini kampuni hiyo haijatimiza wajibu wake na badala yake imewashindisha na kuwalaza airport kwa zaidi ya siku 9. Serikali ikae kimya tu? Isiwatetee wananchi wake? Kama serikali isipoingilia kati masuala kama haya, nani atawatetea wananchi hawa?

Lakini mshangao wangu ni jinsi serikali inavyoshughulikia suala hili, ati haya ni ya kufanywa na waziri mkuu hadi anaahirisha mambo mengine ya kiserikali? Nini kinachowashinda hao walioko kwenye nafasi hizo za ukurugenzi na hata waziri wa usafirishaji nk? Wapo kwa lengo gani kama kazi zao zinafanywa na waziri mkuu. Na huyo waziri mkuu anapoahirisha safari ya Bukoba na kubaki Dar, lipi la ziada analofanya ambalo asingeweza kufanya akiwa Bukoba au ambalo wenzake wangeshindwa? Atawabeba hao mahujaji mgongoni mwake kuwaingiza kwenye ndege? Damn ridiculous!
 
Hebu tuache suala la udini tujadili hili: Kuna abiria zaidi ya 1000 wamelipa mamailioni ya fedha zao kwa kampuni fulani iwasafirishe kwenda huko wanakotaka, lakini kampuni hiyo haijatimiza wajibu wake na badala yake imewashindisha na kuwalaza airport kwa zaidi ya siku 9. Serikali ikae kimya tu? Isiwatetee wananchi wake? Kama serikali isipoingilia kati masuala kama haya, nani atawatetea wananchi hawa?
Lakini mshangao wangu ni jinsi serikali inavyoshughulikia suala hili, ati haya ni ya kufanywa na waziri mkuu hadi anaahirisha mambo mengine ya kiserikali? Nini kinachowashinda hao walioko kwenye nafasi hizo za ukurugenzi na hata waziri wa usafirishaji nk? Wapo kwa lengo gani kama kazi zao zinafanywa na waziri mkuu. Na huyo waziri mkuu anapoahirisha safari ya Bukoba na kubaki Dar, lipi la ziada analofanya ambalo asingeweza kufanya akiwa Bukoba au ambalo wenzake wangeshindwa? Atawabeba hao mahujaji mgongoni mwake kuwaingiza kwenye ndege? Damn ridiculous!

Mimi nadhani hili ni suala la utapeli na hawa wananchi waliotapeliwa wanaweza kuwapeleka wahusika mbele ya vyombo vya kisheria. Ukisema serikaliiingilie wananchi wake wanapopata taabu nitakupa mfano moja hai: Juzi nilikuwa mikoani nikaona mama moja ameungua vibaya na mtoto wake katuambia shemeji yake alimwagia uji. Lakini alikuwa hana pesa ya matibabu. Sasa kwa nini serikali isiingilie hilo? Watoto kibao wanapoteza maisha yao mikoani na akina mama, kwa ajili ya kukosa dawa, kwa nini serikali isiahirishe safari za nje za waheshimiwa EL na JK badala yake ikimbie huko Rukwa, Lindi kuokoa maisha ya watoto hawa? I mean vitu ni vingi sana na kazi ni kubwa!
Ukisema kwamba wahujaji ni wengi 1,000, ndiyo maana ni lazima serikali iingilie, nitakataa pia, hawa watu ni lazima watafute suluhisho kupitia vyama vyao na familia zao.
Wakristo wanaenda kuhiji pia hivi karibuni kwa ajili ya Xmas huko Bethlehem na Jerusalem na kanisani wametangaza ya kuwa ni usd 1,800, hii si mara ya kwanza je umewahi kusikia wamekwama na wakaandamana?
Mi nadhani hili suala lina udini ndani yake na siyo kwa sababu mimi nataka iwe hivyo mbali ndivyo ilivyo. Hatuwezi kujadili suala hili bila udini.
Nakubaliana na wewe kwamba EL na serikali yake inajitafutia umaarufu hapo na ni katika kujaribu kuficha mapungufu ya viongozi wa ATC na Bakwata or whichever organization is responsible.
But there's nothing new under the sun!
 
Let me be a devil's advocate and spin issues!

Ndugu zangu waenda Hajj, wamelipa $2400.00 hiyo ni nauli na kadhalika. Siku ya nane inaingia hawajatinga Mecca kwenda kumpiga mawe shetani na kumuenzi Mungu wao.

Kisingizio, ndege koko ni bovu!

What if I was to tell you that this is a set up of Mlo Mkubwa (ulua)as an outcome of Serikali bailing out ATC?

Now, if they had paid for the fair, why doesn't ATC seek to lease one KQ, SA or Saudi Arabia arilines and send these Watakatifu for Hajj? what is so difficult to call KLM, PIA or Emirates and request a bail out? Is it that ATC has no money to compensate British Airways or Qatar airlines?

Nope! Huu ni mkao maalum wa kula. Lowassa kakatisha ziara (makusudi) eti kusaidia Waislamu waende hajj! Nanyi mwamsifu eti ni shujaa!

Nope, the GVTZ will bail out ATC and pay out to Air Richmonduli 3 times the costs of asking Njoroge or Mengistu to give us KQ or ET and send these humble brothers in Allah to join hands with other brothers and sisters from all over the world to cherrish the great symbol of their religion and faith.

Hivo basi, Mugawo wa "uzembe" wa ATC utakwenda kwa walionusuru ATC, ATC watabakia na nauli walizolipwa na ndugu zetu waislamu, deni la Taifa litaongezeka kwa ajili ya kuhudumia "Uzalendo" (au kama GQ anavyodai walipa kodi), mtamsifu Lowassa kwa umahiri wa kuokoa jahazi, mtamlaani Mataka na Nyang'anyi eti hawafai.

At the same time, Saudi Arabia Airlines wametoa ndege ya bure, kutusaidia siye masikini (in addition to kondoo and probably refund on all expenses!), lakini GAO report ya 2011 itaonyesha matumizi ya dharura ya $10.5million kuwasaidia mahujaji walikowama kwenda hija 2007!

Case closed! mtaji wa ugombea urais 2015 ushapatikana, jiandaeni kuvaa kofia za Kisungura!

Ama kweli Watanzania tu mbumbumbu!
 
Let me be a devil's advocate and spin issues!

Ndugu zangu waenda Hajj, wamelipa $2400.00 hiyo ni nauli na kadhalika. Siku ya nane inaingia hawajatinga Mecca kwenda kumpiga mawe shetani na kumuenzi Mungu wao.

Kisingizio, ndege koko ni bovu!

What if I was to tell you that this is a set up of Mlo Mkubwa (ulua)as an outcome of Serikali bailing out ATC?

Now, if they had paid for the fair, why doesn't ATC seek to lease one KQ, SA or Saudi Arabia arilines and send these Watakatifu for Hajj? what is so difficult to call KLM, PIA or Emirates and request a bail out? Is it that ATC has no money to compensate British Airways or Qatar airlines?

Nope! Huu ni mkao maalum wa kula. Lowassa kakatisha ziara (makusudi) eti kusaidia Waislamu waende hajj! Nanyi mwamsifu eti ni shujaa!

Nope, the GVTZ will bail out ATC and pay out to Air Richmonduli 3 times the costs of asking Njoroge or Mengistu to give us KQ or ET and send these humble brothers in Allah to join hands with other brothers and sisters from all over the world to cherrish the great symbol of their religion and faith.

Hivo basi, Mugawo wa "uzembe" wa ATC utakwenda kwa walionusuru ATC, ATC watabakia na nauli walizolipwa na ndugu zetu waislamu, deni la Taifa litaongezeka kwa ajili ya kuhudumia "Uzalendo" (au kama GQ anavyodai walipa kodi), mtamsifu Lowassa kwa umahiri wa kuokoa jahazi, mtamlaani Mataka na Nyang'anyi eti hawafai.

At the same time, Saudi Arabia Airlines wametoa ndege ya bure, kutusaidia siye masikini (in addition to kondoo and probably refund on all expenses!), lakini GAO report ya 2011 itaonyesha matumizi ya dharura ya $10.5million kuwasaidia mahujaji walikowama kwenda hija 2007!

Case closed! mtaji wa ugombea urais 2015 ushapatikana, jiandaeni kuvaa kofia za Kisungura!

Ama kweli Watanzania tu mbumbumbu!
 
Kitendo Cha Mahujaji Kuagwa Na Rais Tena Mbele Ya Kamera Za Tv Zote Wakati Alipopita Pale Uwanjani Akienda Marekani...na Mara Baada Ya Kuwaaga Waliingia Kwenye Mdege...ni Kitendo Cha Aibu Kugundua Kuwa Ulikuwa Usanii Kwani Baada Ya Kupanda Kwenye Ndege Na Rais Kuwa Ameshapaa ..maafisa Wa Uwanja Waliwafuata Na Kuwashusha Wakisema Kuna Mambo Bado Hayajatendamaa...

Naamini Kuwa Kitendo Hicho Ni Kama Usanii..uliofanywa..ili Kumuondolea Kadhia Rais...
 
Mengi Yamezungumzwa Hapa.

Ndugu Yangu Game Theory Nnaamini Ametaka Kuleta Game Theory Hapa. Mie Nnaamini Kuna Mambo Alikuwa Anayachokonoa Ndio Mjadala.


Ukweli Waislamu Kwa Muda Mrefu Tun Ailaumu Serikali Kuwa Ina Udini Na Tunasema Serikali Inawapendelea Wakristo Na Ss Waislamu Ni Daraja La Pili.

Serikali Inatambua Wazi Kuwa Hakuna Ugomvi Mbaya Kuliko Wa Kidini, Na Ss Waislamu Tunaamini Wazi Kufa Kwa Kupigania Maslahi Ya Dini Yetu Ni Utukufu Na Heshma, Ni Wajibu Wa Kila Muislamu Kulinda Heshima Ya Dini Yake Isichezewe Au Kudhalilishwa.

Sasa Viongozi Wasingechukua Hatua Za Haraka Kuonesha Kuwa Uzembe Huu Ss Serikali Hatuungi Mkono, Na Nyny Kama Wananchi Wa Nchi Hii Serikali Inao Wajibu Wa Kutatua Matatizo Yenu.

Na Zaidi Muda Wa Kutatua Suala Hili Ulkuwa Mdogo Na Serikali Haikuingilia Huko Mwanzo Ilikaa Kimya Ili Kuwatazama Hao Wahusika Watalitatua Vp, Lkn Kimya Wameshindwa Na Mahujaj Wakaanza Kuielekezea Vidole Serikali.

Nnaamini Kwa Hili Serikali Imejitahidi Kun'gamua Na Imecheza Heko Karata Yake La Si Hivyo Wasingeondoka Wale Bongo Pasingekalika Ingekuwa Pata Shika Nguo Chanika.


Serikali Ina Mapungufu Yake, Na Nnaamini Kuna Sehemu Nyingi Walitakiwa Wachukue Hatua Za Kufaa Lkn Ndio Hivyo, Lkn Hili Wamejitahidi
 
mama lao sasa huo uchokozi dada. Uliza watu wa dar mmewasaidiaje wenzenu?
au we ulitaka wafanyeje?
Oh Mama Lao una lako jambo....ona sasa Mrema na TLP wana score points kwa katoni 10 tu za maji! Sina hakika kama maji ni Kilimanjaro au Uhai!
 
Mkuu Mtu Wa Pwani

Naona umejaribu kutetea Serikali ni vizuri sana lakini mimi naomba kuelewa hasahasa tatizo la hili suala nini?

Nasikia mpaka leo asubuhi hawa watu bado wako Bongo. Je kuna nini ambacho mpaka waziri mkuu anaingilia lakini hakuna suluhu. Je ni utapeli, ni siasa, ni UFISADI, au nini?

Nafikiri tumechoka kusikia kila wakati maujaji.
 
there you go, kwanini uling'ang'ania ooh waislam mmewasaidiaje wenzenu? suala ni la sisi wengine tusio waislam pia tumewasaidiaje? na ndio maana mreme kaenda kujitafutia ujiko. Mamaa kwenye shida hatuangalii shida ni ya nani ili asaidiwe.
Good day mama.
 
Serikali kuuweka kitimoto uongozi ATC

* Lengo ni kujua mchakato safari ulivyofanywa

* Atayebainika kuchukuliwa hatua kali


SAKATA la kukwama kwa baadhi ya mahujaji wa Tanzania kwenda Makka, Saudia limeitikisa serikali na sasa watendaji wakuu ndani ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC) watawekwa kiti moto kwa kutakiwa kueleza mchakato mzima wa jinsi walivyompata dalali wa ndege za waumini hao.

Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, alilithibitishia gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana kuwa baada ya mahujaji kusafiri serikali itataka kujua mchakato mzima uliotumika kuipata kampuni ya ndege ambayo ingepaswa kusafirisha mahujaji hao.

Chenge alifafanua kwamba, haiwezekani kampuni yenye ofisi na inayofanya kazi zake kwa uhakika ishindwe kupata kibali cha kutua na kuegesha ndege mjini Makka kwa siku karibu kumi.

Waziri Chenge aliongeza kwamba, huu si wakati wa kumtafuta mchawi kwani jukumu la kwanza la serikali ni kuhakikisha mahujaji hao wanasafiri na kurudi nchini, baada ya hapo serikali lazima ijue mchakato huo.

Chenge alisema serikali ina mkono mrefu ambao ni lazima ijue kila hatua ya mchakato huo na kuongeza kwamba, lazima mahujaji hao wasafiri.

"Sasa hivi hatutaki kumtafuta mchawi, lengo la serikali ni kuhakikisha mahujaji wanasafiri na kurudi nchini, tutahakikisha wanasifiri na kurudi," alisema na kuongeza kuwa baada ya hapo watataka kujua mchakato uliotumika kuipata kampuni husika.

"Serikali ina mkono mrefu, hatutashughulikia watu wote kwa pamoja, tutataka kujua hatua kwa hatua, nani alihusika, kisha tutamuuliza, alianzaje, na baada ya hapo atasema hivi, sisi tutaangalia na kama kutakuwa na kosa tutawaambia kwa heri," alisisisitiza Chenge.

Chenge alifafanua kwamba, suala hilo kwa sasa linashughulikiwa kidiplomasia kwa dharura na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia ubalozi wa Tanzania wa Saudi Arabia.

Alisema lengo la kulishughulikia suala hilo kidiplomasia ni kutafuta kibali cha kutua na kuegesha ndege nchini humo, ambacho ki utaratibu kinapaswa kupatikana ndani ya kipindi cha wiki moja kabla.

Waziri Chenge alisema hadi jana kibali hicho kilikuwa bado hakijapatikana na kuongeza kwamba, serikali ilikuwa ikifanya juhudi kipatikane kwani upatikanaji wa ndege za kukodi si tatizo.

"Tatizo siyo ndege, ndege ni fedha tu na ukiwa na fedha hata leo unakodi ndege ila tatizo ni eneo la kutua," alisema Chenge.

Alisema tatizo la kukosekana eneo la kutua ndege linaweza kuwa na athari, kwani kila nchi ina utaratibu wake ikiwa ni pamoja na kuangalia taratibu za kiusalama.

"Siwezi kuilamu serikali ya Saudi Arabia, hata Tanzania ina utaratibu wake, ndege zinazotua katika kipindi hiki nchini humo ni nyingi, kuna mambo mbalimbali ya kuangalia ikiwemo la usalama," alisema.

Alisema yeye binafsi (Chenge), wiki nzima hii halali kutokana na sakata hilo na kuongeza kwamba atajisikia vema baada ya mahujaji hao kuondoka.

Waziri huyo aliongeza kwamba, haiingi akilini kwa watu kukaa siku karibu kumi wakisubiri kwenda Makka kutekeleza nguzo ya dini yao halafu wapande ndege kisha waambiwe ndege hiyo siyo yenyewe.

"Chukulia ni wewe, unakaa siku karibu kumi halafu unapanda ndege wakati huo huo unaambiwa ndege siyo, utajisikiaje?" alihoji.

Hali hiyo ilimfanya Waziri Mkuu, Edward Lowassa jana kuitisha mkutano na watendaji wa ngazi za juu wa wizara hiyo wakiongozwa na Chenge.

Wengine waliokwenda katika mkutano huo wa Lowassa ni pamoja na Katibu Mkuu wizara hiyo, Dk Enos Bukuku, Naibu Katibu Mkuu Omar Chambo na mmoja wa wakurugenzi kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) aliyefahamika kwa jina la Manongi.

Kwa karibu siku kumi sasa, baadhi ya mahujaji ambao walipaswa kuondoka kwenda Makka kutekeleza moja ya nguzo ya dini ya Kiislamu wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kutokana na kukosekana ndege ambazo zilipaswa kukodiwa na ATC.
 
Usanii watawala safari ya mahujaji
* Waingizwa kwenye ndege kisha washushwa

*Waambiwa ndege haina kibali cha kutua

* Mrema atangaza kuwa ni janga la kitaifa

*Hatimaye kundi la kwanza laondoka jana jioni


Muhibu Said na Salim Said, MUM


KUKWAMA kwa mahujaji zaidi ya 1,000 kuondoka nchini juzi kwenda Makka, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hijja, kumeingia katika sura mpya, baada ya baadhi yao kushushwa katika ndege waliyokuwa wamepanda kwa madai ya ndege hiyo kutokuwa na kibali cha kutua nchini humo.


Mahujaji hao wapatao 379, walishushwa katika ndege saa 9:00 za usiku wa kuamkia jana baada ya viongozi wa Shirika la Ndege nchini (ATC) kuwaruhusu kupanda majira ya saa 5:00 za usiku huo tayari kuanza safari ya kwenda nchini humo kutekeleza ibada hiyo.


Ndege hiyo DC 10 iliyowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 1:00 ya usiku jauzi, inamilikiwa na kampuni ya Al-wasaa DC 10 ya familia ya Mfalme wa nchi ya Ras-Alkhaima iliyoko katika Umoja

wa Falme za Kiarabu (UAE).


Ilikodiwa na uongozi wa ATC, baada ya ndege ya awali iliyokuwa iwasafirishe mahujaji hao Desemba 3, mwaka huu, kudaiwa kupatwa na matatizo ya kiufundi.


Mahujaji hao walishushwa katika ndege hiyo dakika chache baada ya uongozi wa ATC kumhakikishia Rais Jakaya Kikwete aliyefika uwanjani hapo akielekea nchini Marekani kwamba safari ya mahujaji hao ilikuwa imeiva.


Kabla ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kumsindikiza Rais Kikwete, Waziri Mkuu, Edward Lowassa alifika na kuwaomba radhi Waislamu na Watanzania kwa jumla kutokana na yaliyowakumba mahujaji hao.


Lowassa aliwaambia mahujaji hao kuwa kitendo kilichofanywa na uongozi wa ATC ni kibaya na kwamba ana wasiwasi kuwa ndani ya shirika hilo kuna viongozi wasio waaminifu.


Kutokana na hali hiyo, Lowassa alisema Rais Kikwete ametoa pole kwa mahujaji kutokana na usumbufu uliowapata.


Lowassa alisema taarifa za kukwama kwao kuondoka, walizipata usiku wa Desemba 9 na kuongeza kuwa hali hiyo imemuudhi Rais Kikwete kupindukia.


?Sijawahi kumuona Rais akikasirika kama siku hiyo na alikuwa akihangaika akipiga simu kwa falme mbalimbali za Kiarabu ili msafiri,? alisema Lowassa kauli ambayo iliwapa matumaini mahujaji hao kuondoka.


Habari zilizopatikana uwanjani hapo na kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa serikali na viongozi wa taasisi zinazoratibu safari za mahujaji hao, zinaeleza kuwa baada ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo, alikataa kuondoka mpaka mahujaji wote waondoke.


?Viongozi wa ATC wakaona rais hataondoka. Ndipo wakaamua kuwaingiza mahujaji ndani ya ndege, huku wakimhakikishia kuwa safari yao imeiva na wakati wowote wangeondoka,? alisema mmoja wa maofisa wa serikali uwanjani hapo jana.


Ofisa huyo alisema kauli hiyo ilimridhisha Rais Kikwete ambaye aliondoka, lakini saa chache baadaye uongozi wa ATC ukawafuata mahujaji hao ndani ya ndege na kuwashusha.


Akisimulia mkasa huo, Imamu wa Msikiti wa Mtoro, ambaye ni mmoja wa mahujaji waliotarajiwa kuondoka, Sheikh Abbas Ramadhani, alisema baada ya kupatwa na mkasa

huo, hadi kufikia jana saa 7 mchana, walipoteza matumaini ya kuondoka kwani wakati huo mji wa Madina, nchini Saudi Arabia ambako walitakiwa waingie milango ya kuingia ilikuwa imeshafungwa na pia milango ya kuingia mahujaji nchini humo, ilitarajiwa kufungwa usiku wa kuamkia leo.


Mbali na hilo, Sheikh Abbas alisema jambo lingine lililowakatisha tamaa ni kauli za kuwakanganya zinazotolewa na rubani wa ndege hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATC, Balozi Mustafa Nyang?anyi kuhusu hatima ya safari yao.


?Wakati rubani anasema kuwa hajapata kibali cha kutua Madina, Balozi Nyang?anyi naye anasema hakuna nafasi ya kutua uwanja wa ndege wa Saudi Arabia. Tunasikitika kwa kunyang?anywa nguzo yetu ya msingi ya kuabudu,? alidai Sheikh Abbas.


Hata hivyo, wakati Sheikh Abbas akisema hayo, jana saa 4:00 asubuhi, ilielezwa na mtangazaji kupitia vipaza sauti vya uwanjani hapo kuwa kibali hicho kilikuwa kimepatikana

kutoka Ikulu nchini, lakini safari ya kundi la kwanza la mahujaji 379

iliyotarajiwa ianze muda huo isingewezekana kutokana na kibali cha ndege kutua katika uwanja wa ndege wa Jeddah, nchini Saudi Arabia kutokuwapo.


Tangazo hilo liliwakatisha tamaa zaidi mahujaji hao, hasa baada ya muda ambao walitangaziwa kuwa wangeondoka, kuisha bila kupewa taarifa zozote na wahusika.


Kutokana na hali hiyo, mahujaji watatu kutoka visiwani Zanzibar walikata tamaa wakaamua kuahirisha safari na kurejea nyumbani.


Mwenyekiti wa taasisi ya Zanzibar Istiqama Hajj and Travell tawi la Dar es Salaam, Sheikh Abdallah Mohamed, alithibitisha hilo uwanjani hapo jana.


?Kuna mwingine yuko kwenye chumba amenitaka nikamchukulie tiketi yake, lakini sijaenda, kwa sababu nakwenda kwenye kikao na Mustafa Nyang?anyi ili kujua hatima ya safari yao. Binafsi tunaona uwezekano haupo...,? alisema Sheikh Mohamed.


Wakati hayo yakijiri, mahujaji zaidi ya 300 waliotarajiwa kuondoka jana, wamefungiwa katika chumba cha kuondokea, huku wakikosa huduma za chakula na maji na mahujaji wawili walianguka uwanjani hapo, kutokana na shinikizo la damu na

kifafa.


?Tunaiomba serikali ilete huduma ya kwanza,? alisema Sheikh Abbas.


Saa 9:30 mchana, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alifika uwanjani hapo na kuwafariji kwa kuwapa mahujaji hao katoni 10 za maji safi, huku akiiita kukwama kwa mahujaji hao kuondoka nchini kuwa ni tatizo la kitaifa.


Mrema alisema ameshangazwa kuona karne ya 21 serikali ikishindwa kuwasifirisha mahujaji ambao wamelipa fedha zao wenyewe, huku rais akithubutu kuondoka na

kuwaacha wakikaa uwanjani hapo kwa zaidi ya siku tisa.


Kiongozi wa Muda wa Mahujaji hao, Seifullah Rajabu huku akibubujikwa na machozi, alisema matumaini ya nia zao kufika Makka na Madina kwa ajili ya ibada ya Hijja,

yameanza kufifia.


?Shida ndio vazi la Waislamu, matatizo ndio chai ya Waislamu na huzuni ndio chakula cha Waislamu wa nchi hii. Sijui Waislamu tumekosa nini?,? alihoji Seifullah na kuwafanya mahujaji na baadhi ya ndugu na jamaa waliowasindikiza kuangua kilio uwanjani hapo.


Dakika chache baadaye, viongozi wa harakati za Kiislamu, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ponda Issa Ponda, Sheikh Mussa Kundecha na Maalim Ali Bassaleh, walifika uwanjani hapo na kuwahutubia mahujaji hao.


Kabla ya kuwahutubia, mahujaji hao walisimama na kukusanyika katika kundi moja na kuanza kutoa vivumo vya sauti za maneno ya ?Takbiyr, Allahu Akbar? kama ishara ya

kuwaunga mkono masheikh hao.


Maalim Bassaleh alisema kadhia iliyowakuta mahujaji hao, ni dhulma dhidi ya Waislamu na kusema kuwa wataendelea kudai haki yao.


?Haki yetu ya kudhulumiwa tutaidai kwa njia yoyote. Kama ni kwenda mahakamani au ni barabarani, tutaidai. Hatukubali...,? alisema Maalim Bassaleh.


Sheikh Ponda alidai kuwa kuna watu ambao wamepandikizwa ili kuwafanya Waislamu waone kuwa matokeo hayo, ni mipango ya Mungu, wakati si kweli.


Naye Sheikh Kundecha alisema dhulma, imekuwa ni mwendelezo wa mambo mengi mabaya

wanayofanyiwa Waislamu nchini na kuwataka waumini hao kuwungana kudai haki zao.


?Hivyo, cha msingi Waislamu tuwe kitu kimoja ili kujua namna ya kuwaambia hawa

mabwana waliotudhulumu,? alisema Sheikh Kundecha.


Katika hatua nyingine, jana jioni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro alitangaza kwamba kundi la kwanza la mahujaji 379 lingeondoka, kundi la pili litarajiwa kuondoka leo leo saa 11 alfajiri na la tatu litaondoka leo saa 11 jioni.


Alisema kwamba serikali ya Saudia imekubalia serikali ya Tanzania mahujaji kuweza kutua Madina na kwenda kwa njia ya basi hadi katika sehemu ya kufanya ibada ya hijja.



http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=3376
 
mkuu mtu wa pwani.........

moja kati ya mahujaji ambao walishushwa juzi,leo alfajiri amenitumia sms kunambia tayarti kuwa wapo makka na yumo ndani ya basi kuelekea mADINA.

sijui kundi la pili litaondoka lini.

hapa kuna mchezo mchafu sana umechezwa,naamini JK akirudi hizo hasira zake sijui zitakuwaje.hii itampa speed kuvunja baraz alote la MAWAZIRI na kutuletea DAMU MPYA ZA VIJANA GRADUATES.

i guess hata zile BODI za serikali nazo hivi sasa mguu ndani mguu nje,naamini JK atatupa zawadi safi sana YA MWAKA MPYA mola akipenda.
 

Hivi Nyanganyi na Mataka wanahitaji msaada wa serikali nzima kufanya kazi yao?

Mbona BAKWATA wako kimya?

Mbona SHURA YA MAIMAMU kimya?

Mbona ANNUR liko kimya?

Mbona DAR ES SALAAM ISLAMIC CLUB wako kimya?

Mbona MSAUD wako kimya?

Mbona MWAMKO wako kimya?

Mbona HAJJ TRUST wako kimya?

au ndio mamabo ya ku pick and chosing battles?

No wonder serikali inawaburuza waislam kila angle kwani hawa wanajuana
Mkuu Game unataka taasisi hizi za kiisalm ziseme nini? ikiwa waislam taratibu zote na ATC wamekamilisha. ATC ndio wadaiwa na wao ndio wakujieleza.
Serikali pia lazima itatue hii kitu kwani ATC ni ya waislam? Hata Bungeni Waziri akijikanyaga na majibu then Spika anamsimamisha Waziri mkuu kuweka mambo sawa.
Usanii mtupu. kudadadeki!
 
Lowassa aliwaambia mahujaji hao kuwa kitendo kilichofanywa na uongozi wa ATC ni kibaya na kwamba ana wasiwasi kuwa ndani ya shirika hilo kuna viongozi wasio waaminifu.


Vyema amegundua kuwa uongozi una watu wasio waaminifu-sasa anafanya nini kuhusu hili? maana tumezoea huyu mkuu ana order za upesi upesi, ingekuwa ni katibu kata wa Tandahimba kakosea angemfuta kazi hapo hapo tena mbele ya wananchi. Sasa atumie panga lile la kuwaadhibu viongozi hadharani kuwawajibisha viongozi wa ATC.


Lowassa alisema taarifa za kukwama kwao kuondoka, walizipata usiku wa Desemba 9 na kuongeza kuwa hali hiyo imemuudhi Rais Kikwete kupindukia.

watanzania tunasubiri impact ya hasira za mkuu wa kaya.maana ameudhika kupindukia.



Wakati hayo yakijiri, mahujaji zaidi ya 300 waliotarajiwa kuondoka jana, wamefungiwa katika chumba cha kuondokea, huku wakikosa huduma za chakula na maji na mahujaji wawili walianguka uwanjani hapo, kutokana na shinikizo la damu na


kifafa.

this is totally against human rights,kama walifungiwa kiasi cha kupata magonjwa inasikitisha, tunaomba vyombo husika vya sheria viingilie ili ATC washtakiwe kwa kudhalilisha wateja na kuwasababishia maafa ya magonjwa.
 
Back
Top Bottom