Sabodo: Kikwete ni kiongozi anayecheka na rushwa!

Sabodo ni mzalendo halisi wa Tanzania, amechangia ukuaje wa demokrasia kwa kusapoti upinzani wakati wa uchaguzi, pia anatoa mchango mzuri wa mawazo kuhusu utendaji mbovu wa JK. Tumuenzi kwa kuendeleza mapambano dhidi ya JK na kundi lake wanaofuja mali za taifa.. heko sabodo utaingia kwenye vitabu vya historia ya Tanganyika, ahsante
 
Hata Sabodo nae kaliona hilo na ameamua kusema lakini kwa adabu ili asimuadhiri sana hadharani raisi JK. Hatari kweli kweli
 
Mtaongea sana mwaka huu hadi 2015 tuwapige chini tena...lol
Katiba Mpya ndiyo kaburi la CCM................................akilikwepa atakumbana na maandamano yasiyo na kikomo..........................
 
Huu siyo upole wa JK kama Sabodo anavyodai bali JK ameukumbatia ufisadi ....sote tukilitambua hilo safari imeanza ya kuuthibiti ufisadi....


Kikwete anacheka na Rushwa......anatakiwa avute zakutosha,mpaka babu anashtukia hili!!!!!
 
Sabodo ni mzalendo halisi wa Tanzania, amechangia ukuaje wa demokrasia kwa kusapoti upinzani wakati wa uchaguzi, pia anatoa mchango mzuri wa mawazo kuhusu utendaji mbovu wa JK. Tumuenzi kwa kuendeleza mapambano dhidi ya JK na kundi lake wanaofuja mali za taifa.. heko sabodo utaingia kwenye vitabu vya historia ya Tanganyika, ahsante

Ametoa Tshs 1.8 bilion kwa serikali kuchimba visima vya maji nchi nzima ili kupunguza tatizo la maji kwa wananchi, walau anarudisha pesa kidogo kwa wananchi wa TZ
 
Mapya yaibuka Dowans
• Dk. Slaa asema Kikwete anawajua wamiliki wake

na Mwandishi wetu


amka2.gif
WAKATI kampuni ya kuzalisha umeme wa dharula ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd zikiwa zimewasilisha rasmi ombi la kuomba fidia ya sh bilioni 94 isajiliwe katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kulipwa sh bilioni 94, serikali imebakiza siku saba kuanza kuilipa kampuni hiyo kiasi hicho cha fedha.
Hatua hiyo imetokana na serikali kusuasua kuweka pingamizi Mahakama Kuu dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), iliyoipa ushindi Dowans katika kesi yake na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Kusuasua kwa hatua hiyo iliyolenga kuinusuru serikali kukwepa kulipa mabilioni hayo, kunapingana na dhamira ya Rais Jakaya Kikwete aliyelihutubia taifa siku ya kilele cha kumbukumbu ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kwamba serikali kwa kutumia wanasheria waliobobea, inajiandaa kupinga hukumu hiyo mahakamani.
Kikwete ambaye aliungana na kundi la Samuel Sitta, Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), kupinga kuilipa Dowans, aliwatia moyo Watanzania kuwa tayari wameshawaelekeza wanasheria kushirikiana na wale wa TANESCO kutafuta namna ya kukwepa kulipa kiasi hicho kikubwa cha fedha.
Duru za kisiasa kutoka ndani ya Wizara ya Nishati na Madini, zililiambia gazeti hili kuwa pamoja na kauli na msimamo wa Rais Kikwete, hadi jana serikali ilikuwa haijawasilisha pingamizi la hukumu ya ICC, hatua ambayo inaweka mahali mabaya serikali kuanza kulipa sh bilioni 94 pamoja na riba ya sh milioni 17 kila siku kuanzia Februari 16.
Mbali ya serikali kushindwa kuweka pingamizi hilo mahakamani hadi sasa, imebainika kuwa hata kundi la wana harakati lililotangaza awali kwenda mahakamani, halijafungua pingamizi hilo na badala yake limewasilisha mahakamani nia ya kutaka kuweka pingamizi dhidi ya Dowans.
Habari hizo zilisema kuwa kesi hiyo imepewa namba 8/2011 na tayari imeshapangiwa Jaji wa kuisikiliza ingawa tarehe ya kuanza kusikilizwa bado haijapangwa.
Hivi karibuni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Salvatory Bongole, alisema ombi la Dowans dhidi ya TANESCO liliwasilishwa Januari 25 mwaka huu mahakamani hapo na wakili wa kujitegemea anayeiwakilisha kampuni hiyo, Kennedy Fungamtama.
Kwa mujibu wa habari hizo, Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limeiandika barua Wizara ya Nishati na Madini kutaka isaidie kulipa deni hilo baada ya kubaini kuwa hakuna uwezekano wa serikali kushinda au kupunguziwa malipo ya sh bilioni 94.
“Hadi leo, tumebakiza siku saba tu kuanza kuilipa Dowans sh bilioni 94 na tayari TANESCO ilishapata notisi ya siku 21 ambazo zinaishia Februari 15. Ikifika tarehe 16 mwezi huu, tutaanza kulipa na fidia ya sh milioni 17 kwa kila siku.
Hofu ya serikali kuanza kuilipa Dowans, ilielezwa jana na Mbunge wa Bumburi, January Makamba, aliyetaka serikali itoe maelezo lini itawasilisha pingamizi hilo mahakamani kwa hofu ya kubanwa kulipa riba ya sh milioni 17 kila siku.
Tuzo hiyo ya Dowans iliamriwa na ICC Novemba 15 mwaka jana baada ya kampuni hiyo kuishinda TANESCO katika kesi yake ya kudai fidia ya kuvunjiwa mkataba iliyokuwa imefunguliwa rasmi Novemba 20 mwaka 2008 na kupewa namba 15947/VRO.
Tangu ICC itoe hukumu ambayo iliipa ushindi Dowans baadhi ya wananchi, wanasiasa wakiwemo na mawaziri na hata majuzi Rais Kikwete, walijitokeza hadharani kuitaka serikali isilipe fidia hiyo kwa madai kuwa kuilipa ni sawa na kuwazawadia mafisadi waliolidanganya taifa tangu ilipoletwa kwa kampuni dada ya Richmond.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa Rais Kikwete anawajua Dowans na kamwe hawezi kujitenga na kampuni hiyo.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema kuwa Rais Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na maamuzi ya uwekezaji wa kampuni hiyo, yalipitishwa na baraza hilo.
“Rais ana maswali mengi ya kujibu. Kama hawajui Dowans, atuambie nani anahusika nayo? Je, hakuhusika kupitisha azimio la mawaziri wake la kuiruhusu Dowans kuwekeza nchini?” alisema Dk. Slaa na kusisitiza kuwa Rais hawezi kuikwepa Dowans.
 
Kikwete, Makamba nani mkweli?
ban.blank.jpg

Joseph Sabinus

amka2.gif
SAKATA la malipo ya shilingi bilioni 94/- za Tanzania kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited, sasa linawagonganisha uso kwa uso, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi –CCM, Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba.
Mgangano wa kauli zao kwa nyakati tofauti na mazingira tofauti, unazua utata kwa tafakari makini kiasi cha kushindwa kujua nani anamaanisha kile anachokisema; nani msanii au basi kana kwamba wote ni wale wale isipokuwa majina na vyeo tu kwamba wote ni wasanii walewale isipokuwa tofauti ya nyimbo.
Gazeti la Nipashe, Februari 5, 2011, uk. 1 lilikuwa na kichwa cha habari MAKAMBA: RUKSA KUHAMA CCM KUIPINGA DOWANS. Habari hiyo iliyanukuu mazungumzo baina ya Makamba na gazeti hilo huku Makamba akiridhia kuwa ni ruksa kwa mwanachama yeyote wa CCM anayetaka kukikahama chama hicho kama njia ya kupinga malipo ya Dowans.
Mazungumzo hayo yalitokana na tishio lililotolewa na wanachama wa CCM Wilaya ya Rorya mkoani Mara kuwa watarudisha kadi za CCM endapo Serikali itakubali kulipa fidia ya sh bilioni 94 kwa Dowans.
Licha ya Makamba kusema ni hiari ya mwanachama kutoka au kubaki katika chama, kama ilivyo ada yake, alijigamba kwa kusema hata kama wanachama hao wataondoka ndani ya CCM, hali hiyo haiwezi kukiathiri chama hicho.
Anadai tangu zamani wanachama wamekuwa wakitumia hiari yao kujiunga na hata kutoka katika chama lakini, chama hicho kikabaki imara bila kuyumba. Hii ni sawa na kusema kuwa, wabaki au watoke, shauri zao, awike au asiwike jogoo, kutakucha.
Kauli ya Makamba inaonesha kutojali wala kutoona thamani ya wanachama wa CCM wa Wilaya ya Rorya. Hii ni kauli inayotoa taswira kuwa Makamba ni mtetezi mzuri wa kufanyika kwa malipo ya Dowans, hata kama ni kwa gharama ya chama kupoteza wanachama, lakini Dowans ilipwe.
Makamba hajui kuwa TANESCO au serikali haina mahali pengine pa kupata pesa hizo bila kuwakamua Watanzania mithili ya ng’ombe anayeweza kukamuliwa hadi damu kutoka kupitia njia mbalimbali; haijalishi utata wowote uliopo kisheria.
Wakati Katibu Mkuu Makamba akiwa na hilo linalozusha maswali mengi kuliko idadi ya majibu ya kuridhisha huku likijenga hisia kuwa huenda “Makamba ana agenda nyuma ya pazia”, Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, naye amekuja kwa gia tofauti.
Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametoa amevunja ukimya na kukata kiu ya Watanzania. Kiu iliyolenga kumsikia akijibu kama “ana mkono wake ndani yake, au na yeye ni mtazamaji tu wa filamu ya Dowans”.
Amevunja ukimya baada ya watu wengi wakiwamo viongozi wa dini, kuingilia na kuhoji kulikoni awe na kigugumizi mintarafu mambo magumu kama hilo la Dowans linalopasua vichwa vya Watanzania ambao baadhi yao wanaishi katika lindi la umaskini wa kutupwa.
Hawa, ni Watanzania wanaotembea mwendo mrefu kutafuta maji na kituo cha afya au zahanati kisha wakaambulia cheti cha mganga na maelekezo ya kwenda kutafuta dawa, eti ndio walipe shilingi zaidi ya bilioni 90 kwa kampuni yenye mkataba tata. Miongoni mwao wanaolia, wamo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
Kikwete ametema cheche zake zilizowakuna kisawasawa wananchi, lakini kama ilivyo ada kwamba no one is perfect, hotuba ya Kikwete siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika Dodoma, imezua maswali mengine.
Imevutia masikioni mwa wengi kumsikia Rais wa nchi akitamka waziwazi, “Nataka kuwahakikishia kuwa mie ni miongoni mwa wale wasiotaka TANESCO ilipe…; sina uhusiano wowote wa kimaslahi kwa namna yoyote ile na kampuni ya Dowans.
Kauli nyingine aliyosema Kikwete ni pamoja na hii, “Wapo waliosema lazima tulipe, wapo waliosema tusilipe, wapo waliosema tusiharakishe kulipa kwani kuna uwezekano wa kutolipa kwa kutumia sheria. Uamuzi wangu ukawa tusiharakishe kulipa, tutafute njia ya kuepuka kulipa…”
Rais Kikwete; Mwenyekiti wa Kitaifa wa Chama cha Mapinduzi akaenda mbali na kusema, hana hisa na Dowans na wamiliki wake hawajui kwani hawajawahi kumuita maana hawamhitaji.
Licha ya kutotaja jina la mtu siku hiyo, Kikwete alitumia muda mwingi kuwatuhumu baadhi ya wanasiasa akisema, “Akutukanaye, hakuchagulii tusi” kwa kuwa baadhi ya watu wanamhusisha na umiliki wa Dowans.
Hapa kuna pande mbili kama zilivyo pande mbili za shilingi. Kwanza, ninampongeza kwa kuamua kuvunja ukimya na kutoa anayoamini ndiyo “ukweli wa ukweli”.
Pia, nampongeza Rais Kikwete kwa kuona na kutambua kuwa ukimya wake, umesababisha baadhi ya watu wafikie hatua ya kumhusisha na umiliki wa kampuni ya Dowans jambo ambalo ni usiku wa kiza maana ni lile usilolojua.
Hata hivyo, ni kwa vipi Kikwete alitarajia ukimya ule usizae matunda hayo wakati ndicho alichokuwa anapanda? Kwanini akae kimya namna hiyo huku hali ya hewa ikichafuka? Alikuwa anasubiri nini kuweka mambo hadharani mapema?
Ikumbukwe kuwa kabla ya Serikali kutangaza majina “mageni masikioni mwa Watanzania” kuwa ndiyo ya wamiliki wa Dowans, Watanzania walikuwa wakihoji iweje walipe deni la mdai ambaye hajulikani? Yaani mdai hewa?
Baada ya kuanikwa majina hayo watu mbalimbali wamepaza sauti zao akiwamo, mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia anayesema, hakuna sababu kwa serikali kulipa deni hilo wakati watu walioingia mkataba huo ambao serikali imeurithi huku wakijua kuwa ni mchafu, wapo.
Kimantiki kama alivyosema Mbatia, waliohusika na mchezo huo mchafu wapo. Wapo na walifanya huku wakijua faida na hasara zake kwa umma wa Watanzania; kwamba walifanya makusudi ili kulinda “maslahi yao; tena ile yenye maslahi kwao binafsi”. Kama hivyo ndivyo, kwanini mali za Watanzania zichukuliwe au Watanzania walazimishwe kulipa deni hilo?
Basi ndivyo ilivyo kwamba wakati Watanzania wanatamani kusikia serikali ya chama cha kina Makamba ikiwakamata watumishi na wanasiasa waliohusika “kulichezesha taifa segere” ili “licheze na kudundika kama sio kupigika”, Makamba anaona heri wanachama wajitoe.
Ninachojiuliza hapa ni kwamba, hivi kweli huo ndio msimamo wa ndani wa Makamba binafsi, au ndio msimamo wa ndani wa Chama cha Mapinduzi?
Ikumbukwe kuwa Makamba ni mtu mkubwa ndani ya chama hivyo, hata siku moja hatutarajii kusikia utetezi wa kichovu kuwa yalikuwa mawazo binafsi. Ukitaka mawazo binafsi ukiwa kiongozi, sharti ujivue kwanza uongozi.
JK na watendaji wengine wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi na chama chenyewe mbona kauli zenu na maneno mnayoyasema yanagongana uso kwa uso mithili ya treni? Mnayoyasema yanatokna kweli mioyoni mwenu, au yanaanzia tu hapo midomoni kwenu lakini mioyoni hayapo?
‘Kikwete aliyesema analazimika kuyasema hayo licha ya kuwa tayari yalikwishasemwa awali na viongozi wengine akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hakukanusha wala kukemea kauli ya Makamba ya kutoona thamani ya wanachama ndani ya chama, bali uchu wa kulipa Dowans huku yeye Kikwete ambaye ni mwenyekiti, akitamani Dowans isilipwe ovyo ovyo. Hapo tumuamini nani kati ya Kikwete na Makamba?
Rais wangu Kikwete, unaionaje kauli ya Makamba ya kutowajali wanachama wa CCM wilayani Rorya, imekaa sawa? Hivi wanachama hao wana thamani yoyote katika chama, au wamejidanganya tu kuingia katika bwawa kubwa huku wakijijua kuwa ni samaki wadogo maana Wazungu wanasema, you better be a big fish in a small pond, rather than being a small fish in a big pond yaani, ni heri kuwa samaki mkubwa katika bwawa dogo, kuliko kuwa samaki mdogo katika bwawa kubwa.
Samaki mdogo ndani ya bwawa kubwa daima hana thamani hata akifa au kupotea hakuna anayejua wala kujali na hata ndugu zake wakilia, machozi yao yanaishia majini tu. Hakuna jipya.
Haya ndiyo yanawakumba wanasiasa wadogo; wanachama wa CCM wilayani Rorya, kwamba hata wakitoka CCM watoke, haina shida cha msingi ni Dowans kulipwa bilioni 94. Ama kweli akutukanaye, hakuchagulii tusi.
Makamba na CCM yako kumbukeni kuwa wakati wewe unasema “Ya kazi gani”, mwingine atasema, “Nitaipataje”.
Kauli za viongozi hao wakuu wa CCM wakati mwingine zinatia kichefuchefu. Hivi kweli hata kwa imani yake, Rais Kikwete anaweza kuitetea kauli yake mbele ya Mungu kuwa hawajui wamiliki wa Dowan?
Kwamba hawajui wamiliki wa kampuni inayoliyumbisha taifa na serikali yake namna hii? Kama ni kweli, kwa nini asimwajibishe Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ambaye hivi karibuni aliyataja majina kadhaa kwamba ndio wamiliki?
Je, kinachodhaniwa kuwa ni majina hewa, ndicho anachokifahamu pia Rais Kikwete? Hili nalo ni jipya na tamu linaloonesha kuwa, filamu ya Dowans, imeanza kunoga.
Kama alivyosema Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tikiti ya NCCR-Mageuzi, David Kafulila, kitendo cha Rais Kikwete kusema hawajui wamiliki wa Dowans ni ishara ya wazi kuwa wale aliowatangaza Waziri Ngeleja kuwa ndio wamiliki wa Dowans ni “changa la macho” kwa Watanzania vinginevyo kama kweli wangekuwa wamiliki halisi, lazima Rais angewajua.
Hatutarajii Tanzania iwe na Rais asiyejua watu wanaolidai taifa mabilioni mengi namna hiyo huku waziri akiwataja hadharani. Hiki nacho kinaweza kuwa kituko cha kuanzia mwaka 2011.
Kikwete, Makamba na Serikali ya Chama cha Mapinduzi, wakumbuke kwamba huduma nyingi za umma zikiwamo za afya, maji, umeme, barabara na ubora wa elimu zinazidi kuporomoka nchini kiasi kwamba hata Watanzania wengi wanakufa kwa kukosa huduma hizo.
Hivi karibuni televisheni ya taifa, TBC1, ilionyesha moja ya shule za msingi mkoani Shinyanga yenye uhaba wa vyumba vya madarasa kiasi cha kuwafanya wanafunzi wa madarasa mawili tofauti, walimu wawili tofauti, katika masomo mawili tofauti, kutumia chumba kimoja kwa wakati mmoja!
Darasa hili wanatumia ukuta wa mbele, na darasa lingine wanatumia ukuta wa nyuma; aibu kweli kweli katika zama hizi. Mabilioni haya ya pesa yangeweza kutumika vizuri kama yangesaidia kuondoa kero kama hizo nchini.
Kumekuwapo na utitiri wa migomo na maandamano katika vyuo vya elimu ya juu wanafunzi “wakililia” maisha yao. Wengine serikali kwa kusingizia vigezo, imewaacha nyikani bila msaada wala mkopo na badala yake, walio nacho wameongezewa.
Ndiyo maana lugha na matamshi ya Makamba na Kikwete, kwangu zinazua “lugha gongana” na kutia shaka kuhusu umakini wao, la sivyo wanafanya yale yanayowafanya watu washindwe kujua tofauti katika familia ya kambale kuwa nani baba, mama, kaka, dada, shangazi, mjomba, bibi wala wajukuu maana wote wana sharubu.



h.sep3.gif

 
Waliotuficha ukweli Dowans, wametufikisha hapa
ban.blank.jpg

Pascally Mayega

amka2.gif
RAIS wangu imeandikwa kuwa usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako lakini natamani kuanza maandiko haya kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema ili maandiko haya yafanane na yale yaliyomo katika utangulizi wa kitabu cha Mwalimu Mkuu wa watu yasemayo: "Hii ni sauti ya mtu aliaye nyikani. Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake.
Kama nitasema kweli tupu siku zote kuna ubaya gani? Ukisema ukweli daima kila aliye wa ukweli atakuheshimu. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Hapendezi mbele ya binadamu wenye roho mbaya.
Hukimbiwa hata na marafiki zake wenye roho nyepesi. Nikipatwa na mkosi kama huu, sitawaonea wivu watu wawezao kudumu na marafiki zao wote siku zote.
Siwezi kuukana ukweli kwa kuogopa upweke wa muda, nikanyimwa ushirika wa milele unaotazamiwa kutokea baada ya kushindwa kwa uongo!"
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuninyima fursa ya kuwa mshabiki wa vyama vya siasa na kunipatia ukakasi katika siasa. Mwanasiasa aliye wa ukweli hujitoa kwa wale anaowaongoza. Huangaika kule na huku akishirikiana na watu wake katika kutafuta ustawi wao. Wengi tulionao leo siyo wanasiasa wakweli. Wanaganga njaa zao tu. Lakini ni lini mtu anakuwa mwanasiasa?
Ukisimama katika majukwaa na kuzungumza hata kwa kukaza mishipa ya shingo kama wengi wanavyofanya, tayari unakuwa mwanasiasa? Hapana! Lazima kuna zaidi.
Kuna maadili yake. Kuna uelewa na uwezo na mengine kama hayo. Anayeomba kura kwa wananchi na akishakuwa diwani, mbunge, waziri au rais anaanza mipango ya kuwaibia wananchi wale wale waliomchagua, huyu hastahili kuitwa mwanasiasa.
Huyu ni mwizi tu wa kawaida kama walivyo wezi wengine. Kinachotendeka nchini mwetu hivi sasa kuhusu ufisadi ni mafisadi kumaliza majukwaa ya nchi hii kuwaambia wananchi ‘mafisadi walee!' wakiwaonyesha wengine, badala ya kuwaonyesha wengine na kusema, ‘mafisadi wenzetu walee'. Rais wangu wanasiasa wanafiki ni mkosi kwa taifa. Hawafanyi siasa bali kutafuta maslahi binafsi. Wanapoyakosa hugeuza siasa kuwa majungu, chuki na visasi. Hayo huyafanya kwa gharama za wananchi.
Wanapomkosea Mwenyezi Mungu ni pale wanapotumia uelewa mdogo wa watu wetu kuwachanganya na hivyo wao kuonekana kama vile wanawatetea wananchi. Wana dhambi kubwa watu hawa.
Kuiba kuku mmoja wa kienyeji ni wizi sawa na wizi wa kuiba mabilioni. Wizi ni uleule. Ustadi wa mwizi katika kuiba na mazingira aliyomo ndiyo humfanya mwizi mmoja aibe kuku na mwizi mwenzake aibe mabilioni. Wote ni wezi. Mwizi wa kuku akipata fursa na mazingira ya kuiba mabilioni ataiba mabilioni. Vivyo hivyo mwizi wa mabilioni akizidiwa kabisa kabisa ataiba hata kuku. Wizi ni tabia ya mtu.
Kama kuna mbunge au waziri ndani ya Bunge la Jamhuri hivi sasa ambaye alifanya ufisadi wa kupokea posho mbilimbili na kuiba fedha za mafuta kwa kuweka bei ya juu ambayo haipo katika nchi hii hadi sasa kwa hiari yake mwenyewe siyo kwa sababu ilipitishwa na wengi, ajue na atambue kuwa ufisadi wake huo ni sawasawa na fisadi wa Meremeta, Deep Green, EPA na ule unaotawala sasa wa Dowans.
Mazingira waliyokuwamo na ustadi wao katika wizi ndio wamefisadi hicho walichofisadi. Wamethibitisha bila shaka yoyote kuwa wangepata fursa yakuwa katika mazingira ya Meremeta, DeepGreen, EPA, Richmond au Dowans wangefisadi kwa ukubwa uleule wa fursa waliyoipata.
Nani kasema kuna msafi kati yao? Waliofisadi wote ni mafisadi. Hakuna mwenye udhu wakuwaambia wananchi ‘mafisadi walee! Mwenye mdomo wakuwasha au anayejiona kuwa yeye ni ‘fyatu' basi aseme ‘wale ni mafisadi wenzetu'. Mafisadi wote hawakubaliki katika jamii yoyote iliyostaarabika.
Rais wangu katika awamu ya kwanza ya utawala wako, miaka mitatu ya mwisho nchi ilisimama. Bunge lililopita chini ya uongozi wa Spika Samweli Sitta liliibua manabii wa uongo wengi. Huku wao wenyewe wakiwafisadi wananchi kwa ufisadi wao wa posho mbili mbili, kuchakachua fedha za mafuta na kulipwa malipo makubwa yasiyofanana na kazi yao, waliizunguka nchi nzima wakihubiri habari ya vita hewa ya ufisadi.
Taifa likaambiwa kuna mafisadi papa na fisadi nyangumi. Bunge la Samuel Sitta lilitumia muda mwingi kukemea ufisadi wa Richmond hoja ambayo Sitta huyo huyo alikuja kuimaliza kiaina. Meremeta, IPTL, Rada, DeepGreen, EPA, Ununuzi wa ndege ya Rais havikuonekana tena kama ni ufisadi kwa manabii hawa. Hawakugusia popote kote walikokwenda!
Rais wangu wananchi hawajaambiwa ukweli kuwa hoja ya msingi iliyokuwa ipelekwe Bungeni ilikuwa ni kuhoji, ‘imekuwaje kampuni ya Alstom Power Rentals , ilipwe sh milioni 60 kila siku bila kuzalisha hata unit moja ya umeme na ilipwe kwa miezi 24 bila kufanya kazi yoyote? Sambamba na hoja hiyo ya Alstom Power Rentals mpeleka hoja alitaka yachunguzwe maneno yaliyokuwapo juu ya Richmond. Jinsi mkataba ulivyoingiwa na nani hasa mmilki wa Richmond'.
Chakushangaza ni kwamba Bunge chini ya uongozi wa Spika Samweli Sitta likaamua kuunda tume chini ya uwenyekiti wa ndugu Harrison Mwakyembe kuchunguza Richmond ambayo kwa wakati ule ilikuwa haijapokea hata senti tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hoja yenyewe ya kuichunguza Alstom Power Rentals ambayo ilikuwa ikilipwa sh milioni 60 kila siku bila kuzalisha hata unit moja ya umeme kwa miezi 24 bila kufanya kazi yoyote ikatupiliwa mbali! Hii haiwezi kuwa ilitokea kwa bahati mbaya. Masilahi ya taifa hayakuzingatiwa katika kuiunda tume ile. Tume iliundwa kwa malengo fulani ya kibinafsi.
Mbona tume katika kuripoti haikuwaambia wananchi kuwa aliyezuia malipo, Richmond isilipwe ni Waziri Mkuu wa wakati ule Edward Lowassa kwa barua aliyoiandika kwenda kwa waziri wa nishati na madini, akimtaka asikurupuke kuwalipa Richmond kwani walikuwa wanaonyesha kutokwenda na kasi iliyotarajiwa!.
Huko nyuma tumeshuhudia marais wakihojiwa, mawaziri wakuu walihojiwa iweje tume ya Mwakyembe haikumhoji Waziri Mkuu aliyekuwapo wakati ule? Kama angehojiwa majibu yake hayakuwa ya muhimu kuwekwa katika ripoti ili haki ionekane kuwa imetendeka? Au alikwepwa ili asitoe majibu ambayo yamo katika ukweli waliofichwa wananchi?
Hawa wanaosema alilengwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa wanakosea wapi? Mbele ya Mwenyezi Mungu kutotenda haki ni dhambi! ana heri ndugu Lucas Selelii ambaye alipohojiwa alisema waliteleza.
Rais wangu kwa kuficha ukweli Taifa limefikishwa hapa lilipo! Walioficha ukweli wamelihujumu Taifa. Wamewaingiza Watanzania katika magumu mengi. Nchi imesimama tena, inajadili Dowans!
Wananchi hawaelewi wafanye nini! Wametwishwa mzigo mzito wa maisha magumu kwa sababu ukweli ulifichwa. Kama kweli hawa watu wanamwogopa Mwenyezi Mungu wasimame sasa na kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwasababishia janga hili kubwa. Wawaambie ukweli walioficha ili wananchi wapate kuamua kwa haki! Kadiri wanavyozidi kungoja ndivyo mioyo ya wananchi inavyozidi kuvimba dhidi yao! Ogopa hasira ya wananchi walio katika mateso yao, uliyowasababishia.
Leo ndugu Rais wananchi wamehukumiwa kuilipa Dowans bilioni 94. Wale wale Ndugu Samweli Sitta na ndugu Harrison Mwakyembe wameibuka tena. Wanataka serikali isiitii hukumu. Ndugu Sitta amewataka Wananchi waandamane huku akikaririwa kuwa iwapo Dowans watalipwa watakuja kuwasumbua sana katika kinyang'anyiro cha urais 2015.
Kumbe kinachopiganiwa hapa siyo kutetea wananchi ni uroho wa urais 2015. Watu wanaousaka urais hata kwa kutenda dhambi, hawatufai. Lakini Dowans kulipwa au kutolipwa, baba ulisema wazi katika hotuba yako ya Februari 5, 2011 kuwa mkataba ulikuwa halali na umeme wao tuliutumia na kwamba msimamo wako ni uleule kama alivyosema Waziri Mkuu ndugu Mizengo Pinda.
Mzee Pinda alisema nini? Alisema, "Inauma sana lakini hakuna namna ya kukwepa kulipa". Kama kuna watu wanaona kulipwa Dowans kutaathiri juhudi zao za kuusaka urais 2015 basi wabuni mbinu zingine kwa sababu kwa mtazamo huu wa serikali Dowans watalipwa tu.
Na kiongozi mwingine akapigilia msumari akasema kama kuilipa Dowans kutawafanya wana CCM wengine wakihame chama basi, ruksa kuhama! Wajiulize, wanaendelea kuficha ukweli kwa faida ya nani?
Kesi hii imeendeshwa kwa miaka miwili hapa hapa Dar es Salaam katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempski, hawa ndugu walikuwa wapi? Hivyo vipengele wanavyoviibua sasa kwa nini walivihifadhi katika kapu lao asiikabidhi TANESCO huja vingeisaidia wakati kesi ilipokuwa ikiendelea! Ni uhuni kungoja hukumu itolewe ndiyo uikatae!
Rais wangu nitasema kweli daima. Kwa kuficha ukweli hawa ndugu zetu wametufikisha mahali pagumu sana. Ukweli sasa unafunguka. Hawa ni wanasheria. Kama wanaushahidi kuwa kampuni hii ni ya kitapeli kuna taratibu zake za kufuata kisheria. Waisaidie serikali kudai kutapeliwa, fedha zetu zitarudi.
Kusema tu barabarani, oh! Kampuni ya kitapeli, kampuni ya kitapeli! Hakuwezi kuifanya kampuni yoyote kuwa yakitapeli. Hii ni staili wanayotumia watu ambao hawana uelewa wowote wa sheria!
Ndugu Rais tukiwaendekeza watu hawa nchi yetu itatumia miaka mingine mitatu kwa malumbano ya kipuuzi yaliyosababishwa kwa ukweli kufichwa badala ya kujadili maendeleo kwa ajili ya ustawi wa watu wetu. Uroho wa urais wa namna hii ni hatari kwa amani ya nchi.
Wanapigana kwa staili ya kifaru. Kifaru ana nguvu nyingi sana lakini anapopigana hufunga macho. Mwanadamu mwelewa hata akiwa mdogo hadhuriwi na nguvu za kifaru aliyekasirika.
Watanzania wana haki ya kuwadai ukweli uliofichwa na watu hawa. Wauseme ukweli waliouficha ili haki itendeke. Nani ahukumiwe katika sakata hili? Baba umesema huwajui Dowans. Hujawahi kuwaona! Ukaongeza, "Walikuwa hawanihitaji". Inafikirisha sana. Mtu humjui kabisakabisa, unajuaje kama anakuhitaji au hakuhitaji! Mtu anayekuja kuwekeza katika mradi wa mapesa mengi kama huu wa Richmond na Dowans atakosaje kumhitaji Rais wa nchi kama atapatikana? Hii ni akili ya kawaida kabisa.
Tatizo la umeme wakati ule lilikuwa janga kubwa. Nchi ilikuwa inaingia katika gizani totoro!. Kiongozi wa nchi hawezi kupata usingizi. Ilikuwa ni kuhangaika kwa kila njia nchi ipate umeme.
Anapokuja mtu kukusaidia katika wakati mgumu kama huo, akakupatia umeme kwa miezi kumi, ukisimama mbele za watu ukasema simjui mtu huyu wala sijawahi kumwona, du! Inachefua fikra!
Baba una haki zote kuikana Dowans kama huusiki nayo. Kwa nini mtu akuhusishe nayo? Wewe ndiye unayejua kilichotokea nani mwingine? Kinachoshtua hapa umeikana Dowans mno. Umeikana kupita kiasi. Siku zote kupita kiasi ni kutibua! Kupotosha! Kuchepusha! Hapa ndipo shida ya kuambiwa ukweli uliofichwa inapokuwa ni lazima.
Wengine wanasema kama Jogoo wa Petro aliyewika baada ya Petro kumkana Bwana Yesu mara tatu akisema: "Nimekwisha kuwaambia kuwa simjui mtu huyu", angekuwako jumamosi iliyopita, angewika. Kukata mzizi wa fitina au kama wanavyosema wanasheria kukazia hukumu ili kuthibitisha kukana kwako waambie vijana wako ndugu Samweli Sitta na ndugu Harrison Mwakyembe waseme ukweli walioficha tuone kama utaporomoka.
Waliwaambia watu wako kuwa wangesema ukweli waliouficha serikali yote ingeporomoka. Ukweli ni kwamba serikali iliporomoka yote toka Waziri Mkuu ulibaki wewe tu na makamu Dk Shein. Bila kusema ukweli uliofichwa ili wananchi wajue kuwa hutaporomoka wengine wanaweza wakawa na mawazo kuwa ah! Hapa, baba kazuga tu, yumo huyo! Si unajua wanao tulivyo, tumekaa kidadisidadisi!
Ndugu rais ni vema ukweli uliofichwa usemwe sasa ili wananchi wajue wamhukumu nani. Wamhukumu kwa haki! Watanzania, kama hawa watu hawatawaambia ukweli waliouficha sasa, wapuuzeni kwa kila watakachowaambia. Wanachofanya nikuwatumia wananchi kuwakabili mahasimu wao.
Hawana huruma na Watanzania wala na nchi yao!. Siku mahasimu wa wananchi watakapokuwa siyo mahasimu wao hawatakuwa pamoja nanyi. Na wao nawaambia kuwa wakati wao wakuwaambia Watanzania ukweli walioficha ni sasa. Watanzania waliulipia kwa fedha zao katika kuutafuta. Ukweli huo ni mali yao kwa nini kuwafisadi? Wakingoja mpaka Dowans walipwe ndipo wauseme hakuna atakayewasikia! Adhabu kwao itakuwa kali, ngumu na ya kutisha kama nini!.
Watawayawaya na kujutia walichowatenda wana wa nchi hii na roho zao zitawasuta kila watakapowaona waja wa Mwenyezi Mungu wakivuja jasho la damu kuifidia Dowans.


h.sep3.gif

 
Maswali ambayo Kikwete hakuyajibu kuhusu Dowans
ban.kijiji.jpg

M. M. Mwanakijiji

amka2.gif
KUNA baadhi ya maswali ambayo bado yananisumbua kichwani kuhusu suala la Dowans na zaidi kutokana na maelezo ya Rais Kikwete siku ya Jumamosi kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akitumia kejeli kidogo, Rais Kikwete aliwabeza wale wanaomhusisha na kampuni hiyo na kudai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kumtukana bila "kumchagulia tusi".
Akishangiliwa na mashabiki wake, Rais Kikwete aliiruka kabisa kampuni ya Dowans na kudai kuwa yeye hawajui, hajakutana nao na wala wao hawakuwa na sababu ya kukutana naye kwa sababu hawakumhitaji.
Nimesoma hotuba iliyoandikwa na ile iliyotolewa na nimemuelewa vizuri sana japo alinichanganya kidogo. Kuchanganyikiwa huku "kidogo" ndiko kumenifanya nije na maswali yafuatayo ambayo ninaamini bado yanahitaji majibu kwani katika maelezo yake Rais Kikwete hakuyagusia kabisa.
Mosi, katika kauli yake siku ya Jumamosi Rais Kikwete alisema kuwa: "Napenda kuwahakikishia Wana-CCM na wananchi wenzangu kuwa sina uhusiano wowote wa kimaslahi kwa namna yoyote ile na Kampuni ya Dowans. Sina hisa zozote wala manufaa yoyote yale."
Alichotuambia siku ile ni kuwa yeye sasa hivi hana uhusiano wala hisa na kampuni ya Dowans. Miaka karibu mitano baadaye anatuambia tuamini kuwa ‘hana' uhusiano wala maslahi. Lakini kitu ambacho hakukisema ni kuwa "hajawahi" kuwa na mahusiano wala hisa huko nyuma.
Yaani, tangu mwanzo kabisa wa sakata la Dowans Rais Kikwete hakuwa na hisa au maslahi ya aina yoyote na kampuni hiyo?
Swali la pili linatokana na hilo la kwanza kwani nalo linatupa matatizo kidogo. Rais Kikwete anaposema "Kampuni ya Dowans" ambayo hana maslahi nayo ni ipi? Mtu yeyote ambaye amefuatilia kwa karibu suala hili ataona kuwa kuna kampuni mbili za Dowans ambazo zinahusiana kwa namna moja au nyingine.
Hapa ina maana kuwa kuna Kampuni ya Dowans Tanzania Limited ambayo ilianzishwa mwaka 2007 nchini na kampuni ya Dowans Holdings S.A ya Costa Rica. Kampuni ya DTL ilianzishwa chini ya aliyekuwa Meneja wa Kampeni ya Kikwete Rostam Aziz na ambaye pia ni Mbunge wa Igunga na mjumbe wa vikao vya juu vya chama.
Swali ambalo binafsi ningependa kujua sana ni kampuni ipi hasa ambayo yeye hana hisa au masilahi nayo? Ni hii ya DTL au ni Dowans Holdings S.A?
Mtu pekee ambaye anaweza kutoa jibu la maswali yote mawili ni Rostam Aziz. Kwanini Rostam hajasema wazi kuwa Rais Kikwete hana maslahi kwenye kampuni yoyote kati ya hizo?
Kutokana na swali hilo la pili tunajikuta tunakabiliwa na swali jingine ambalo limetokana pia na maelezo ya Rais Kikwete kuwa hawajui Dowans.
Kampuni ya Dowans iliingia nchini baada ya kuletwa na Rostam Aziz kama mwenyewe alivyovikiri mapema mwaka huu; katika wingu lote la maneno na tuhuma za miaka hii mitano ni kweli Rais Kikwete hawajui Dowans? Gazeti la The East African limeandika wiki mbili tu zilizopita juu ya uwezo aliopewa Rostam na Dowans Holdings S.A kufanya kazi kwa niaba ya kampuni hiyo nje ya Costa Rica (ikiwemo Tanzania), kwa maneno mengine mtu ambaye angeweza kumuambia Rais ni nani hasa wanahusika na Dowans Holdings S.A ni Rostam Aziz.
Kwanini hadi leo hii Rais Kikwete hajajaribu kumuuliza Rostam kuwa hivi hawa "jamaa ni kina nani"? Anaogopa nini? Amesema mwenyewe kuwa "Pia sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua kwa sababu ya rafiki yangu au hata kama angekuwa ndugu yangu kahusika." Mbona inaonekana kwa Rostam anasita sita hata kumuuliza swali la msingi sana kama kutaka kujua nani ni wamiliki hasa wa wa kampuni hiyo ambao wameiandikisha huko Costa Rica? Anaogopa kujua au hataki kujua?
Tukiachana na maswali hayo najikuta nalazimishwa kurudi nyuma kidogo ya historia ya sakata zima la Richmond/Dowans na ushiriki wa Rais Kikwete mwenyewe na kwanini siamini na sijashawishika kuwa katika hotuba yake hii ya juzi alituambia ukweli wote. Kuna maswali ambayo bado yanahitaji majibu kwani yasipojibiwa yanalazimisha baadhi ya watu kuhoji, uwezo, uelewa, uthabiti na mtindo wa uongozi wa Rais Kikwete.
Hili si jambo jema hata kidogo. Watanzania wanatarajia Rais wao kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuona mbali, mwenye kutaka majibu ya kuridhisha na ambaye yeye mwenyewe anatafuta majibu hayo kwa mbinde au hata kwa upinde.
Maswali ambayo yanafanya baadhi ya watu kuhoji umakini na uwezo wa Rais Kikwete tunapoangalia jinsi alivyolishughulikia suala la Dowans/Richmond ni haya.
Mosi Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison. Mwakyembe ilitudokeza kuwa maamuzi ya Baraza la Mawaziri yalipindishwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Dk. Ibrahim Msabaha pamoja ana aliyekuwa Katibu wa Wizara hiyo Mwakapugi na hadi leo hilo halijakanushwa.
Baraza la mawaziri lilitoa maelekezo kwa wizara kujaribu kupata ‘dili' nzuri toka Kampuni ya CDC Globeleq na kama uamuzi ule ungepelekwa kama ilivyoamuriwa na baraza la mawaziri siyo Richmond wala Dowans ambayo ingepata tenda baadaye.
Lakini Kamati Teule ilishangazwa kuwa "badala ya kuwatumia ujumbe sahihi CDC Globeleq kuwa serikali inataka wapunguze kipindi cha ukodishaji mitambo, washushe zaidi bei yao ya umeme na wawe tayari kuzalisha umeme ifikapo Mei 2006, ilipeleka ujumbe tofauti kabisa kuwa serikali inafuta mpango wa kukodisha mitambo kutoka kwao" Jambo hilo la kugeuza kabisa uamuzi wa baraza la mawaziri liliacha maswali yafuatayo (kwa mujibu wa Kamati Teule) ambayo hadi leo Ikulu haijawahi kuyajibu na kuchukulia sisi wengine kuwa tumeyasahau:

  1. Je, kulikuwa na kikao kingine cha Baraza la Mawaziri siku hiyo hiyo ya tarehe 10 Februari, 2006 kilichotengua maamuzi yakeya awali ya siku hiyo hiyo?
  2. Ikiwa jibu ni hapana, kwa nini Wizara ilipeleka CDC Globeleq ujumbe tofauti na ule ilioagizwa na Baraza la Mawaziri?
  3. Kwa nini Wizara isitume barua hiyo baada ya kushindwa kuwashawishi CDC Globeleq kubadilisha masharti yao?
  4. Maamuzi kama hayo, siku nne ndani ya mgao wa umeme wa nchi nzima na katika kipindi ambacho Serikali haikuwa na mkakati mbadala uliokuwa umeiva kama wa CDC Globeleq, yalikuwa kweli maamuzi makini ya kunufaisha Taifa?
Ni lazima tutambue kuwa baraza la mawaziri lilipotisha uamuzi wake huo ndio ulikuwa msimamo wa serikali iliyoongozwa na Rais Kikwete juu ya kushughulikia tatizo la umeme. Sasa Waziri na Katibu wake walipopindisha maamuzi ya Baraza la Mawaziri tulitarajia kuwa Rais au Katibu Mkuu Kiongozi angewakumbusha Waziri na Katibu juu ya msimamo wa serikali.
Kuna sababu moja tu kwanini uamuzi wa baraza la mawaziri ulibadilisha na hakuna mtu aliyewajibishwa; Rais Kikwete mwenyewe (Ikulu) ndiye aliyetoa maagizo kwa Msabaha kubadilisha uamuzi wa baraza la mawaziri. Kwa nini?
Mahitaji ya umeme wa dharura yalikuja kwa sababu vyanzo vyetu vya umeme unaotokana na maji vilikuwa na upungufu mkubwa uliosababishwa na ukame. Kumbe umeme wa dharura ulitakiwa kuwepo tu hadi pale vyanzo vyetu vya umeme vingejaa tena maji.
Na kutokana na hili hadi leo mkataba ule wa Richmond na TANESCO uliitwa "Agreement for Emergency Power Supply" yaani "Makubaliano ya Ugavi wa Umeme wa Dharura". Kama hili ni kweli, mkataba ambao ulitakiwa kuingiwa ulitakiwa uwe unahusiana na ile dharura tu na si kitu kingine.
Na huu ndio ulikuwa msimamo uliofikiwa pia na Kamati Teule kwani inatudokeza kuwa "Kwa kuwa madhumuni ya mkataba huu ilikuwa ni kuzalisha umeme wa dharura, Serikali ilipaswa kutilia maanani hali ya kuongezeka kwa maji katika mabwawa yaliyoko nchini ili kuona umuhimu wa kuongeza au kutoongeza muda wakati wa ukomo wake.
Uamuzi wa kuongeza muda kabla ya kutathmini hali ya uzalishaji umeme kwa njia ya maji zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja kilichokusudiwa awali, unatia mashaka."
Kimsingi mkataba ulitakuwa uwe ni kwa ajili ya dharura tu na kama hali isingekuwa imetengemaa basi muda ungeweza kuongezwa na kama hali ingekuwa imetengemaa basi mkataba ungeisha ndani ya miezi kumi na miwili. Lakini ilikuwa ni timu iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Lowassa iliyoongeza muda kutoka miezi 12 na kuwa miaka miwili!
Kwanini muda huu uliongezwa bila kujali hali halisi ya uzalishaji wa umeme? Kwanini Rais Kikwete hakuwasiliana na Waziri wake Mkuu na kuhakikisha kuwa mkataba ni kwa ajili ya dharura tu na akaridhia uwe wa miezi 12? Je, watu wakidai kuwa aidha alikuwa hafuatilii kilichokuwa kinaendelea au aliridhia mkataba uongezwe muda nje ya kushughulikia dharura itakuwa ni makosa?
Swali la pili kwa namna moja linatokana na hilo hapo juu. Katika hotuba yake Rais Kikwete aliwaelezwa wananchi kuwa upungufu wa umeme ulikuwa mkubwa sana kiasi cha vyanzo vyetu vya umeme wa maji kuwa na upungufu mkubwa.
Alisema hivi katika hotuba yake hii kwenye miaka 34 ya chama chake "Aidha, mito mikubwa na midogo ikapungukiwa sana maji na mingine kukauka kabisa. Matokeo yake ni mabwawa yetu yote ya kuzalisha umeme yakakosa maji hivyo uzalishaji wa umeme ukaathirika vibaya sana na nchi ilikuwa gizani."
Hili lilikuwa kweli; lakini, ni lini mabwawa yetu yalikuwa yamejaa maji na kurudi katika hali ya kawaida na hivyo kuondoa ulazima wa umeme wa dharura?
Jibu linapatikana pia kwenye ripoti ya Kamati Teule; wanatuambia hivi kina Mwakyembe "Ukweli ni kwamba maji katika mabwawa nchini yalikuwa yameshajaa mapema Januari, 2007 na muda wa awali wa kuisha mkataba ungekuwa tarehe 11/9/2008; hivyo ingekuwepo nafasi ya kutosha kuamua kuongeza au kutoongeza muda wa mkataba."
Tena ripoti ikaongeza kuwa "Kamati Teule inasisitiza kuwa, udharura wa mradi huu ulimalizika pale mabwawa yetu yalipojaa maji mapema mwezi Februari 2007" Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba kama mkataba ungeingiwa kwa muda wa miezi kumi na mbili (tuseme kuanzia Juni 23, 2006) basi mkataba ungeisha mwishoni mwa mwezi Mei, 2007.
Lakini kwa kuamua kuuweka mkataba kuwa ni wa miezi 24 wajanja wa taifa letu wakauhesabu mwaka mzima wa 2007 kuwa ni mwaka wa dharura. Maana yake ni kuwa TANESCO ingeweza kutoka katika mkataba huo katikati ya 2007 bila kupelekana ICC.
Kwanini Rais Kikwete na serikali yake (Mwanasheria wake Mkuu akiwemo ndani) walikubali kuongeza muda wa Mkataba bila ya kujali hali ya maji kwenye mabwawa yetu? Je, ikidaiwa kuwa ilifanywa hivyo ili kuhakikisha watu wanachotewa mabilioni zaidi itakuwa ni uongo au atadai kuwa anachafuliwa na "kupakwa matope"?
Rais Kikwete katika hotuba yake alitoa madai yafuatayo ambayo tukiyapima katika mwanga wa hilo swali la pili tunayaona hayana msingi wowote katika ukweli: Alisema: "Baada ya hapo Kampuni ya Richmond ikauza mkataba wake kwa Kampuni ya Dowans ambayo ilileta mitambo na uzalishaji wa umeme ukafanyika na kupunguza kabisa makali ya mgao."
Mojawapo ya vitu ambavyo hajavigusia kabisa ni suala la uuzwaji wa mkataba wa Richmond kwenda Dowans. Wiki mbili zilizopita nimeonesha kuwa Richmond na Dowans waligeana mkataba kinyume cha sheria Oktoba 14, 2006 bila ya kupata idhini ya TANESCO kama vipengele 12.1(e), 12.3(a) na 15:12 cha mkataba kati ya Richmond na TANESCO vinavyosema.
Hapa ningependa ieleweke vizuri kabisa kuwa hoja ya TANESCO ya kupinga uhalali wa mkataba kwenye Mahakama ya Usuluhishi (ICC) haikutokana na vipengele hivyo hapo juu. Hoja ya Dowans ikidai kuwa Dowans walirithi mkataba hewa ilitokana na madai kuwa Kamati Teule ya Bunge iliitangaza kuwa kampuni ya Richmond kuwa ni kampuni hewa.
TANESCO hawakupewa nafasi ya kudai kukosa uhalali kwa sababu mkataba ulihamishwa kinyume cha sheria kwa sababu inaonekana kuwa watu pekee waliojua hilo limefanyika ni kina Rostam Aziz, Karamagi, Guy Picard na kina Bernal Zamora Arce. Serikali na TANESCO walifichwa kwa sababu kama ingejulikana kuwa mkataba umehamishwa kinyemela mkataba ungevunjika kwani hata muda wa kusahihisha hayo makosa ulikuwa umeshapita.
Swali tunalobakiwa nalo in kuwa ni kwanini hadi sasa serikali haijataka kujua kilichotokea? Yawezekana Rais Kikwete hataki tujue ilikuwaje rafiki na mshirika wake wa karibu ambaye ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano hakuonyesha uzalendo na kuisadia TANESCO isiingizwe mkenge kwa kusahinishwa mkataba wa geresha wa Disemba 23, 2006.
Je, baadhi ya watu wakidai kuwa Kikwete anamlinda Rostam watakuwa wamekuza mambo madogo?
Kama hamlindi naomba aseme hadharani ni lini mkataba wa Richmond na TANESCO ulihamishiwa kwa Dowans Holdings S.A? Nina uhakika wa asilimia 100 hawezi kufanya hivyo bila kujiingiza yeye mwenyewe na serikali kwenye njia panda ya sheria. Njia panda hiyo iko hivi:
a. Kama mkataba ulihamishwa Desemba 23, 2006 kama Kamati Teule ilivyoaminishwa na Picard, je, Dowans waliweza vipi kuanza kuingiza majenereta ya umeme Oktoba 30, 2006? Miezi karibu miwili kabla ya mkataba kuhamishwa?

b. Kama mkataba ulihamishwa Oktoba 14, 2006 (kitu ambacho ni msimamo wangu) kwanini Waziri wa Nishati na Madini alihoji Novemba 28, kama Mkataba unaweza kuhamishika?
c. Kama mkataba ulihamishwa Oktoba 14, 2006 (kitu ambacho ni msimamo wangu) ni kitu gani walichokuwa wanazungumzia TANESCO na Dowans hadi kukubaliana kuhamisha mkataba toka Richmond kwenda Dowans Desemba 21, 2006 wakati Dowans (Rostam Aziz akiwa ni mwenye mamlaka ya kisheria ya kujua kinachoendelea) walikuwa tayari wanajua wameshauchukua?
Tukumbuke kuwa Rais Kikwete na wengine wanadai kuwa masharti ya mkataba ndiyo yaliwezesha Dowans kufungua kesi ICC (hili ni kweli) na kuwa kwa vile hukumu imetolewa basi ni lazima tutii (kwa kuwalipa Dowans).
Kikwete mwenyewe alisema hivi kuhusu hili hapo juzi "Dowans hawakuridhika, wakashitaki kwenye Baraza la Usuluhishi kama yalivyo masharti ya mkataba waliotiliana sahihi. Madai yamesikilizwa na TANESCO imeonekana ni mkosaji hivyo wakatozwa fidia ya dola za Marekani 64 milioni."
Ni kutokana na hili Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ikiongozwa na yeye mwenyewe ikaja na kusema "Kamati Kuu imetafakari kwa makini suala la TANESCO kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 94 na kubaini kuwa huu ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwamba TANESCO ilivunja mkataba kinyume cha makubaliano na katika hali ya kawaida, kama hakuna njia nyingine ya kujiondoa kwenye kosa, ni busara na ni wajibu kwa muungwana kuheshimu maamuzi ya Mahakama."
Kimsingi ndugu zetu wa CCM wanasema tuheshimu sehemu ya makubaliano yanayoifaidisha Dowans lakini sehemu ya makubalino (Ibara za 12.1e, 12.3a na 15.12 za Mkataba wa Richmond/TANESCO), zinazoinufaisha TANESCO tusizijali!
Hata leo hii tunaweza kuwagomea kuwalipa kabisa Dowans kwa sababu walivunja mkataba na kutulaghai sisi, lakini nani ana ujasiri huo katika viongozi wetu? Si Mhando, si Ngeleja, si Werema na ninathubutu kusema si Kikwete ambaye anaweza kusimama na kusema "walitulaghai hatuwalipi!" Kwanini waungwana tuwe sisi tu? Kwanini wao hawakuwa waungwana na kutuambia wameboronga? Au kuwa muungwana haiendani na kuwa mkweli?
Maswali haya yote na mengine ambayo nimeyaweka pembeni bado yanatufanya tufikie mahitimisho kadhaa ambayo yote si mazuri. Kwanza, Rais Kikwete hajaonesha kujali kinachotokea kuanzia mwanzo. Hivi inawezekana vipi Rais kutokujua wahusika wakuu wa kampuni ambayo imeingia na kupewa mabilioni ya fedha kutatua tatizo la dharura ya kitaifa?
Pili, Rais Kikwete hawezi au hataki kuwasimamia watu walio chini yake kwa uthabiti na umahiri. Inawezekana vipi watu wakafanya madudu ya kuliingiza taifa kwenye mkataba ambao tukifika mwisho Dowans watakuwa wametukomba karibu bilioni 200! Na jambo la tatu ni kuwa Rais Kikwete anamuogopa, anamhofia, na hayuko tayari kumuuliza vizuri (yeye kama Rais au kwa kutumia vyombo vya sheria) Rostam Aziz ili kujua ukweli wa siri iliyoko nyuma ya Dowans.
Serikali ya watu milioni 40 inapotetemeka mbele ya mtu mmoja siyo tu kuwa serikali hiyo iko matatani lakini isipoangalia itajikuta inapoteza haki ya kutawala watu wote hao.
Hadi leo hii hakuna chombo chochote cha serikali yetu kilichomuuita, kumhoji, kumchunguza au hata kuonesha geresha ya hayo Aziz.
Si IGP Mwema, si Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, si Usalama wa Taifa, si mahali popote ambapo wameonesha ujasiri. Hili linatufanya tufikie hitimisho la kusikitisha serikali imeshikwa pabaya na haina pa kutokea.
Kama maswali haya yote yataendelea kuwa na majibu ya uhakika basi hitimisho kuu liko wazi kabisa mbele ya kila mwenye utimamu wa akili; hasa akiulizwa swali "je, unafikiri toka mwanzo Rais Kikwete amehusika katika kuhakikisha kampuni ya Dowans inaingia kwenye mkataba wa nishati?"
Ndugu zangu, tuzo ya Dowans haipunguziki, hailipiki, na hawalipwi; kwani watakapolipwa kama ambavyo naamini itakuwa kwani kinachofanyika sasa ni geresha "ya kujitahidi" ili baadaye waje kutuambia "tulitafuta kila njia ya kutolipa lakini tulishindwa" na nina uhakika hawatatumia vifungu hivyo kama njia moja wapo!
Kwa sababu lilioandikwa limeandikwa, Dowans watalipwa, na wakilipwa wanafunga makampuni yao na kutoweka kama walivyofanya kwenye zile nyingine. Ndiko kutamalaki kwa ufisadi.



h.sep3.gif

Niandikie: Facebook: "mimi mwanakijiji"
 
Hatuna chuki na Kikwete, bali mfumo wa uchaguzi
ban.kalamu.jpg

Samson Mwigamba

amka2.gif
JUMA lililopita Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (mb), alikutana uso kwa uso na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa nchi, Jakaya Mrisho Kikwete. Baada ya kukutana kwenye sherehe za Siku ya Sheria Duniani ambako wote walialikwa, walisalimiana kwa kushikana mikono. Wasomaji wengi wameniuliza tafsiri ya jambo hilo na mmoja ambaye yuko Hai (jimbo ambalo Mbowe ndiye mbunge wake) alinitumia ujumbe mfupi wa simu akisema Mbowe ang'olewe mara moja uenyekiti wa taifa wa chama chake kwa kuisaliti CHADEMA.
Kwa kuwa wanaouliza maoni yangu juu ya hili wamekuwa wakiongezeka, nimeona nilizungumzie leo kupitia kalamu hii. Gazeti moja la kila siku likiripoti tukio hilo liliandika:
"MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe jana alikutana uso kwa uso na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni mara ya kwanza tangu chama hicho kilipotangaza kutotambua ushindi wa Kikwete uliompa fursa ya kuwa rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana.

Tukio hilo la aina yake kutokea tangu kuanza kwa mwaka huu, liliwakutanisha Mbowe na Rais Kikwete katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono.
Mbowe na Kikwete walikutana uso kwa uso ikiwa ni siku 85 tangu Mbowe alipowaongoza wabunge wa chama chake kususia hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 10, Novemba 18 mwaka 2010 kutokana na msimamo wa chama chake kutotambua matokeo ya urais.
Mwaka jana, Mbowe alitangaza chama chake kutotambua matokeo ya rais huku akitoa madai mbalimbali kuhusu taratibu zilizotumika kumwingiza kiongozi huyo madarakani.
Madai ya CHADEMA ambacho mgombea wake wa urais Dk. Willibrod Slaa alishika nafasi ya pili ni pamoja na kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyomweka madarakani Rais Kikwete kwa mara ya pili baada ya kupata kura 5,276,827 ukiwa ni ushindi wa asilimia 61.17.
Katika uchaguzi huo, Dk. Slaa alipata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 huku Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF akipata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06.
Mbali na kutohudhuria hafla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, wabunge wa CHADEMA pia walisusia sherehe za kumwapisha Kikwete zilizofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na pia zile za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda zilizofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino, Dodoma.
Mbali na Sherehe hizo, pia viongozi wa CHADEMA hawakuonekana katika maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 9, 2010.
Katika maadhimisho ya jana yaliyofanyika nje ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam, Mbowe alikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria katika maadhimisho hayo, akiwa ni kiongozi pekee wa chama cha upinzani huku Rais Kikwete akiwa mgeni rasmi.
Tukio hilo lilivuta hisia kwa washiriki wa maadhimisho hayo ya Siku ya Sheria nchini ambapo Mbowe aliwasili katika maadhimisho hayo akiwa peke yake huku akiwa amevaa mavazi maalumu ya chama hicho maarufu kwa jina la kombati pamoja na miwani myeusi.
Baada ya kuwasili alikwenda kukaa katika viti vya mbele karibu na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa. Katika tukio la kupiga picha za pamoja ndipo Mbowe alikutana uso kwa uso na Rais Kikwete ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono na kupiga picha pamoja huku wote wakiwa na tabasamu pana.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa na kutoka hapo napenda nikuletee maelezo ya Mheshimiwa Mbowe kama alivyoripotiwa na gazeti hilo :
"Alipotafutwa na gazeti hili ili kuzungumzia tukio hilo, saa kadhaa baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Mbowe alisema alikwenda katika sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa ni za mahakama na kwamba hata kungekuwa na tofauti gani kusingemzuia yeye kusalimiana na Kikwete.

‘Sherehe zile si zangu wala Rais Kikwete hivyo siwezi kuwa na chuki na mahakama, ni 'Birthday' ya Mahakama yenyewe, ni mhimili wa dola', alisema Mbowe.
Mbowe alisema kuwa katika maadhimisho hayo alialikwa kama mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni. "Hatuwezi kuwa na chuki na mahakama, pale mihimili yote mitatu ya nchi ilikuwepo, ile haikuwa 'Birthday' yangu wala ya Rais Kikwete," alisema Mbowe.
Mbowe alisema kuwa madai waliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana hayakuwa na maana kwamba hawaitambui Serikali wala kutaka Rais Kikwete ang'oke madarakani. Alisema kuwa mambo mawili kati ya matatu yaliyokuwemo katika dai lao yameshaanza kupatiwa ufumbuzi kwa namba moja au nyingine ambayo ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi".
Kimsingi nimekusanya maelezo yote yaliyohusu tukio zima la siku hiyo na maelezo binafsi ya Mheshimiwa Mbowe kuhusiana na issue hiyo. Naomba niweke mambo kadhaa wazi.
Kwanza kabisa ni kuelewa vema msimamo wa CHADEMA kuhusiana na matokeo ya uchaguzi. Hawakusema kwamba hawamtambui rais aliyechaguliwa maana ingekuwa hivyo ni dhahiri hivi leo Tanzania ingekuwa ndani ya machafuko makubwa pengine kuliko hata yale yaliyotokea Ivory Coast.
Wangesema hawamtambui kabisa rais, wanachama, wafuasi na wapenzi wa chama hicho wangeingia mitaani kuandamana na kudai Kikwete ang'oke madarakani. Walichokisema ni kutotambua utaratibu na matokeo yaliyomwingiza Kikwete madarakani.
Na katika hilo pia wakawa wazi kwamba kimsingi walitakiwa kwenda mahakamani kudai haki yao lakini katiba inawazuia. Sasa haki yao itapatikana wapi, ndo wakaamua kutangaza mgogoro ili tu umma wa Watanzania, jumuia ya kimataifa na hatimaye serikali iwasikilize.
Walichokitaka ni kuundwa kwa tume huru ichunguze kilichojiri kwenye uchaguzi huo na kutoa maoni nini kifanyike kuepuka matatizo hayo katika chaguzi zijazo. Pia walitaka kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Kama muijuavyo serikali ya Chama Cha Mapinduzi unaweza kulia kilio mpaka machozi yakaisha bila kusikilizwa.
Ni pale tu utakapolia kwa vitendo ndipo unaweza kuwashtua watanzania wenzako wakaanza kupaza sauti zao kukuunga mkono na kupiga kelele dhidi ya serikali hii na hapo watakusikiliza si kwa sababu wameamua kukusikiliza bali kwa sababu wanaogopa nguvu ya umma.
Ndipo CHADEMA wakaanza kufanya vitendo kwa kususia hotuba ya rais na matukio yote ya rais. Kuanzia tukio la kumtangaza rasmi kuwa rais, sherehe za kumwapisha kuwa rais, sherehe za yeye kumwapisha Waziri Mkuu, na hatimaye hotuba ya kulizindua Bunge.
Hatua hizo tayari zimezaa matunda na sasa mchakato wa katiba mpya unaendelea na ndani ya katiba mpya tutaweza kuweka utaratibu wa kupata tume huru ya uchaguzi.
Lakini pengine ni muhimu kuelewana hapa kwamba msimamo wa CHADEMA ni wa kisiasa na si wa kibinafsi. CHADEMA kutangaza kupinga matokeo yaliyomwingiza mgombea wa CCM madarakani haina maana kwamba sasa kuna chuki binafsi kati ya Slaa na Kikwete, ama kati ya Mbowe na Msekwa, ama kati ya Mbowe na Kikwete, ama kati ya Slaa na Makamba, kwa kiwango cha kutokusalimiana.
Muhimu ni kwamba katika kusalimiana haijaripotiwa kwamba Mbowe alitambua rasmi matokeo yalivyomwingiza Kikwete madarakani wala hakusema sasa amefuta madai ya CHADEMA yaliyofuatia uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Wala haikuelezwa kwamba Mbowe alimwomba radhi Kikwete kwa kususia hotuba yake bungeni.
Ni dhahiri basi kwamba alichokifanya Mbowe ni uvumilivu wa kisiasa (political tolerance) ambayo ni muhimu sana kwa utulivu, umoja na amani ya nchi yetu. Tukianza kuingiza chuki za namna hiyo kwenye siasa hatutafika mbali.
Zao la chuki ya namna hiyo lazima litazaa mapigano na hatimaye mauaji. Tukumbuke kwamba tunachopigana nacho watanzania wa leo si Kikwete wala Makamba bali ni mfumo mzima wa chama tawala ambacho kinapeleka halijojo mustakabali wa taifa hili. Mambo ya wizi wa kura yalikuwepo tangu enzi za Mkapa na Mangula hadi enzi hizi za Kikwete na Makamba.
Nahitimisha kwa kusema Mbowe hajakisaliti chama chake na hatuna haja ya kumshambulia kwa kitendo tu cha kusalimiana na Kikwete. Uvumilivu wa kisiasa ni muhimu kwa mustakabali wa taifa na tuvumiliane ili tuweze kupingana bila kupigana, kukomesha uovu nchini bila kukomoana, kuchukuliana hatua bila kuchukiana, na kadhalika. Mapambano yanaendelea!



h.sep3.gif

Niachie ujumbe kwenye: smwigamba@yahoo.com, 0713953761 / 0767953761 / 0784815499.
 
Hatuna chuki na Kikwete, bali mfumo wa uchaguzi
ban.kalamu.jpg

Samson Mwigamba

amka2.gif
JUMA lililopita Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (mb), alikutana uso kwa uso na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa nchi, Jakaya Mrisho Kikwete. Baada ya kukutana kwenye sherehe za Siku ya Sheria Duniani ambako wote walialikwa, walisalimiana kwa kushikana mikono. Wasomaji wengi wameniuliza tafsiri ya jambo hilo na mmoja ambaye yuko Hai (jimbo ambalo Mbowe ndiye mbunge wake) alinitumia ujumbe mfupi wa simu akisema Mbowe ang’olewe mara moja uenyekiti wa taifa wa chama chake kwa kuisaliti CHADEMA.
Kwa kuwa wanaouliza maoni yangu juu ya hili wamekuwa wakiongezeka, nimeona nilizungumzie leo kupitia kalamu hii. Gazeti moja la kila siku likiripoti tukio hilo liliandika:
“MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe jana alikutana uso kwa uso na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni mara ya kwanza tangu chama hicho kilipotangaza kutotambua ushindi wa Kikwete uliompa fursa ya kuwa rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana.

Tukio hilo la aina yake kutokea tangu kuanza kwa mwaka huu, liliwakutanisha Mbowe na Rais Kikwete katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono.
Mbowe na Kikwete walikutana uso kwa uso ikiwa ni siku 85 tangu Mbowe alipowaongoza wabunge wa chama chake kususia hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 10, Novemba 18 mwaka 2010 kutokana na msimamo wa chama chake kutotambua matokeo ya urais.
Mwaka jana, Mbowe alitangaza chama chake kutotambua matokeo ya rais huku akitoa madai mbalimbali kuhusu taratibu zilizotumika kumwingiza kiongozi huyo madarakani.
Madai ya CHADEMA ambacho mgombea wake wa urais Dk. Willibrod Slaa alishika nafasi ya pili ni pamoja na kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyomweka madarakani Rais Kikwete kwa mara ya pili baada ya kupata kura 5,276,827 ukiwa ni ushindi wa asilimia 61.17.
Katika uchaguzi huo, Dk. Slaa alipata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 huku Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF akipata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06.
Mbali na kutohudhuria hafla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, wabunge wa CHADEMA pia walisusia sherehe za kumwapisha Kikwete zilizofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na pia zile za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda zilizofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino, Dodoma.
Mbali na Sherehe hizo, pia viongozi wa CHADEMA hawakuonekana katika maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 9, 2010.
Katika maadhimisho ya jana yaliyofanyika nje ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam, Mbowe alikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria katika maadhimisho hayo, akiwa ni kiongozi pekee wa chama cha upinzani huku Rais Kikwete akiwa mgeni rasmi.
Tukio hilo lilivuta hisia kwa washiriki wa maadhimisho hayo ya Siku ya Sheria nchini ambapo Mbowe aliwasili katika maadhimisho hayo akiwa peke yake huku akiwa amevaa mavazi maalumu ya chama hicho maarufu kwa jina la kombati pamoja na miwani myeusi.
Baada ya kuwasili alikwenda kukaa katika viti vya mbele karibu na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa. Katika tukio la kupiga picha za pamoja ndipo Mbowe alikutana uso kwa uso na Rais Kikwete ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono na kupiga picha pamoja huku wote wakiwa na tabasamu pana.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa na kutoka hapo napenda nikuletee maelezo ya Mheshimiwa Mbowe kama alivyoripotiwa na gazeti hilo :
“Alipotafutwa na gazeti hili ili kuzungumzia tukio hilo, saa kadhaa baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Mbowe alisema alikwenda katika sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa ni za mahakama na kwamba hata kungekuwa na tofauti gani kusingemzuia yeye kusalimiana na Kikwete.

‘Sherehe zile si zangu wala Rais Kikwete hivyo siwezi kuwa na chuki na mahakama, ni 'Birthday' ya Mahakama yenyewe, ni mhimili wa dola’, alisema Mbowe.
Mbowe alisema kuwa katika maadhimisho hayo alialikwa kama mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni. “Hatuwezi kuwa na chuki na mahakama, pale mihimili yote mitatu ya nchi ilikuwepo, ile haikuwa 'Birthday' yangu wala ya Rais Kikwete,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema kuwa madai waliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana hayakuwa na maana kwamba hawaitambui Serikali wala kutaka Rais Kikwete ang’oke madarakani. Alisema kuwa mambo mawili kati ya matatu yaliyokuwemo katika dai lao yameshaanza kupatiwa ufumbuzi kwa namba moja au nyingine ambayo ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi”.
Kimsingi nimekusanya maelezo yote yaliyohusu tukio zima la siku hiyo na maelezo binafsi ya Mheshimiwa Mbowe kuhusiana na issue hiyo. Naomba niweke mambo kadhaa wazi.
Kwanza kabisa ni kuelewa vema msimamo wa CHADEMA kuhusiana na matokeo ya uchaguzi. Hawakusema kwamba hawamtambui rais aliyechaguliwa maana ingekuwa hivyo ni dhahiri hivi leo Tanzania ingekuwa ndani ya machafuko makubwa pengine kuliko hata yale yaliyotokea Ivory Coast.
Wangesema hawamtambui kabisa rais, wanachama, wafuasi na wapenzi wa chama hicho wangeingia mitaani kuandamana na kudai Kikwete ang’oke madarakani. Walichokisema ni kutotambua utaratibu na matokeo yaliyomwingiza Kikwete madarakani.
Na katika hilo pia wakawa wazi kwamba kimsingi walitakiwa kwenda mahakamani kudai haki yao lakini katiba inawazuia. Sasa haki yao itapatikana wapi, ndo wakaamua kutangaza mgogoro ili tu umma wa Watanzania, jumuia ya kimataifa na hatimaye serikali iwasikilize.
Walichokitaka ni kuundwa kwa tume huru ichunguze kilichojiri kwenye uchaguzi huo na kutoa maoni nini kifanyike kuepuka matatizo hayo katika chaguzi zijazo. Pia walitaka kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Kama muijuavyo serikali ya Chama Cha Mapinduzi unaweza kulia kilio mpaka machozi yakaisha bila kusikilizwa.
Ni pale tu utakapolia kwa vitendo ndipo unaweza kuwashtua watanzania wenzako wakaanza kupaza sauti zao kukuunga mkono na kupiga kelele dhidi ya serikali hii na hapo watakusikiliza si kwa sababu wameamua kukusikiliza bali kwa sababu wanaogopa nguvu ya umma.
Ndipo CHADEMA wakaanza kufanya vitendo kwa kususia hotuba ya rais na matukio yote ya rais. Kuanzia tukio la kumtangaza rasmi kuwa rais, sherehe za kumwapisha kuwa rais, sherehe za yeye kumwapisha Waziri Mkuu, na hatimaye hotuba ya kulizindua Bunge.
Hatua hizo tayari zimezaa matunda na sasa mchakato wa katiba mpya unaendelea na ndani ya katiba mpya tutaweza kuweka utaratibu wa kupata tume huru ya uchaguzi.
Lakini pengine ni muhimu kuelewana hapa kwamba msimamo wa CHADEMA ni wa kisiasa na si wa kibinafsi. CHADEMA kutangaza kupinga matokeo yaliyomwingiza mgombea wa CCM madarakani haina maana kwamba sasa kuna chuki binafsi kati ya Slaa na Kikwete, ama kati ya Mbowe na Msekwa, ama kati ya Mbowe na Kikwete, ama kati ya Slaa na Makamba, kwa kiwango cha kutokusalimiana.
Muhimu ni kwamba katika kusalimiana haijaripotiwa kwamba Mbowe alitambua rasmi matokeo yalivyomwingiza Kikwete madarakani wala hakusema sasa amefuta madai ya CHADEMA yaliyofuatia uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Wala haikuelezwa kwamba Mbowe alimwomba radhi Kikwete kwa kususia hotuba yake bungeni.
Ni dhahiri basi kwamba alichokifanya Mbowe ni uvumilivu wa kisiasa (political tolerance) ambayo ni muhimu sana kwa utulivu, umoja na amani ya nchi yetu. Tukianza kuingiza chuki za namna hiyo kwenye siasa hatutafika mbali.
Zao la chuki ya namna hiyo lazima litazaa mapigano na hatimaye mauaji. Tukumbuke kwamba tunachopigana nacho watanzania wa leo si Kikwete wala Makamba bali ni mfumo mzima wa chama tawala ambacho kinapeleka halijojo mustakabali wa taifa hili. Mambo ya wizi wa kura yalikuwepo tangu enzi za Mkapa na Mangula hadi enzi hizi za Kikwete na Makamba.
Nahitimisha kwa kusema Mbowe hajakisaliti chama chake na hatuna haja ya kumshambulia kwa kitendo tu cha kusalimiana na Kikwete. Uvumilivu wa kisiasa ni muhimu kwa mustakabali wa taifa na tuvumiliane ili tuweze kupingana bila kupigana, kukomesha uovu nchini bila kukomoana, kuchukuliana hatua bila kuchukiana, na kadhalika. Mapambano yanaendelea!



h.sep3.gif

Niachie ujumbe kwenye: smwigamba@yahoo.com, 0713953761 / 0767953761 / 0784815499.
 
Kikwete tuachie kumbukumbu nzuri
ban.blank.jpg

Ruhazi Ruhazi

amka2.gif
KIONGIOZI yeyote muungwana hutaka kuacha jambo jema, ili akumbukwe na umma kwa mambo mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.
Wananchi huendelea kuwakumbuka baadhi ya viongozi kutokana na utendaji kazi wao katika kipindi chao chote ama sehemu ya kipindi cha uongozi wao.
Viongozi kama walivyo binadamu wengine, hukumbukwa kwa namna uongozi ulivyokuwa mbaya ama ulivyokuwa mzuri.
Ingawa kwa kawaida binadamu hupenda kukumbukwa kwa wema lakini kwa viongozi walio wengi katika nchi za kiafrika wamekuwa wakikumbukwa kwa mabaya.
Tanzania kwa sasa iko katika uongozi wa awamu ya nne unaoongozwa na Rais Jakaya Kikwete (JK), ambaye amemaliza ngwe ya kwanza ya kipindi chake cha miaka mitano na sasa ameanza ngwe yake ya mwisho.
Watangulizi wake hayati baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere, aliyeinongoza nchi yetu tangu mwaka 1961 hadi 1984 alipostaafu, hukumbukwa kwa mengi, mazuri yakiwa mengi zaidi kuliko mabaya.
Watu wanaendelea kumuona na kumhesabu kama kiongozi pekee aliyepata kutokea hapa nchini na kuamua kupigania usawa akipinga kuibuka kwa matabaka ya matajiri na masikini.
Mwalimu aliendelea kupigania hili hata baada ya kung'atuka madarakani, alichukia kama alivyochukia na kupi vita rushwa.
Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ‘Mzee Ruksa', atakumbuka kwa jinsi alivyojitahidi kuwakomboa wananchi kiuchumi.
Mzee Ruksa aliyeingia rasmi madarakani mwaka 1985 aliikuta nchi iko katika uchumi tete, aliwakuta Watanzania wapo katika hali ngumu ya kiuchumi na kwa kiasi kikubwa hali hiyo ilisababishwa na vile vita kati ya Tanzania na Uganda.
Hata hivyo aliruhusu biashara na ndiye aliyeruhusu kujenga majumba na hata watu kuwa na ajira mbadala ikiwemo biashara ndogondogo, ili mradi kuwafanya watu waongeze vipato vyao na kuweza kuishi maisha yenye uhakika japo wa milo mitatu.
Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa naye atakumbukwa kwa kuendesha ubinafsishaji wa mashirika ya umma ambayo mengi yalikuwa yapo hoi, yakishindwa kutoa huduma au kuzalisha kile kilichokusudiwa wakati wa uanzishwaji wake.
Pamoja na watu wengi kuendelea kutia wasiwasi baadhi ya mambo yakiwemo ya mikataba yenye harufu ya rushwa wakimtaka ayatolee ufafanuzi lakini bado atakumbukwa kutopandisha gharama za maisha.
Ukiacha Daraja la Mkapa, Daraja la Umoja kati ya msumbiji na Tanzania na barabara nyingi nchini, Mkapa ataendelea kukumbukwa kwa kuijazia serikali akiba ya fedha za kigeni, huku akifanikiwa kuzuia mfumuko wa bei kwa miaka yote kumi aliyokaa madarakani.
Kwa muda mwingi nimekuwa nikijiuliza hivi kipi kizuri ambacho JK, atakiacha hata kuwafanya Watanzania wamkumbuke na kumtaja kwa uzuri baada ya kuondoka madarakani?
JK ameruhusu kupanda zaidi ya mara mia gharama za maisha katika uongozi wake miaka mitano na ushee alichoongoza, hajali na inaonekana bado hajaamua kuzuia mfuko huu wa bei ambao unayafanya maisha hasa kwa watu wa chini kubwa magumu.
Kwa kweli asilimia kubwa ya Watanzania kwa sasa wanaishi katika maisha magumu kupindukia, huku asilimia kubwa wakiamini kuwa Rais ndiye anayechangia wao kuteseka ndani ya nchi yao kwa kutozuia mfumuko wa bei.
Ninahisi kuwa JK anataka atakapoondoka madarakani tumkumbuke kwa mabaya, kwamba ni kiongozi wa kwanza aliyeingia madarakani na kuruhusu kuzaliwa kwa tabaka la Watanzania matajiri na Watanzania masikini.
Tabaka ambalo, vyovyote iwavyo litazaa uhasama, chuki, pamoja na kuleta utengano baina ya wana jamii, pengine linaweza kukaribisha uvunjifu mkubwa wa amani hapo baadaye.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila tabaka linapozaliwa huendelea kutoa kizazi cha tabaka hilo hilo, kwa hiyo wale Watanzania masikini wataendelea kuzaa watoto masikini kupindukia na wale wenye utajiri wataendelea kuwa matajiri kila kukicha.
Matokeo ya matabaka haya kila mmoja anayajua kuwa kuingia katika mauaji yasiyo na mwisho wale masikiti watafikia mahali na kuamua kuchukua sehemu ya kile kinachomilikiwa na matajiri kwa nguvu.
Ni hapo ambapo mauaji ya wenyewe kwa wenyewe yanapoanza, mfano mzuri ni kule Afrika Kusini, ambako vijana wazawa kutoka familia masikini wamekuwa wakiwatimua wahamiaji bila kujali wanatoka ndani ya Afrika Kusini au la.
Wahanga wa kadhia hilo la tabaka ya kimaisha wamekuwa wahamiaji, wa kimaeneo kutoka Afrika Kusini kwenyewe na nchi nyingine za Kiafrika, ambao hawakuwa na shaka ya kugeukwa na kuporwa mali nap engine kuuawa.
Wanachokiamini vijana wazawa kutoka familia masikini ni kwmaba wamedhulumiwa haki yao, kwa kupokwa nafasi za kufanya kazi ambazo zingewaingizia kipato cha kuwawezesha kupata pato la kujikimu.
Siku zote nimekuwa nikiangalia jinsi tofauti ya kipato inavyowagawa wananchi na kuzusha uhasama baina yao, ninajiuliza hivi ni kweli JK hajui kuwa kwa kuachia mfumuko huu wa bei anaipeleka nchi pabaya?
Hivi anataka aje kukumbukwa kwa lipi hasa, ni kwa kuisababishia nchi matabaka ambayo dhahiri yatazaa mauaji hapo baadaye ama anataka tuje kumkumbuka kwa lipi?


h.sep3.gif

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu 0784 au 0713 – 765757, barua pepe:wiruhinda@yahoo.com
 
Hatudanganyiki; JK anawajua Dowans
ban.maswali.jpg

Ansbert Ngurumo

amka2.gif
RAIS Jakaya Kikwete amejiingiza kwenye matope mazito zaidi kwa kutamka kwamba hawajui Dowans na kwamba na yeye ni mmoja wa wananchi wanaotaka kampuni hiyo isilipwe bilioni 94 inazolidai Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO).
Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, kama sehemu ya hotuba yake kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya CCM. Kwangu mimi, hii ilikuwa kauli ya "kujinasua." Na kama fikra hii inawakilisha maoni ya CCM katika umri wake wa miaka 34, basi, hili nalo ni janga la kitaifa!
Kuna mambo matatu ya kumsahihisha Rais Kikwete hapa. Kwanza, anawajua Dowans. Pili, alihusika na ujio wao hapa. Tatu, anataka walipwe pesa zao, tena haraka.
Yote haya yamejikita katika ukweli kwamba Dowans waliingia nchini akiwa Rais, katika kipindi ambacho Watanzania walikuwa hawajamshtukia. Ni katika kipindi ambacho alikuwa ametoa ahadi mpya kwa wananchi kwamba tatizo la ukosefu wa umeme lingekuwa historia.
Akiwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri lililoshiriki kuipa tenda kampuni ya Richmond, ambayo yeye na wenzake walikuwa wanajivunia, hawezi kukosa kuwajua Dowans walioletwa kutekeleza mkataba uliowashinda Richmond – zikiwa harakati za yeye na wenzake kuandika historia aliyoisisitiza.
Kuna la ziada. Vigogo wengi wa CCM ambao wamekuwa wakiisuta serikali kwa miradi ya Richmond na Dowans, wanalindwa na siri moja. Wanajua kuwa wakubwa walihusika katika kuzileta kampuni hizo.
Na wanajua kila mmoja alivyohusika, akiwamo Rais Kikwete. Na ndiyo maana anashindwa kuwachukulia hatua kina Samuel Sitta, Dk. Harrison Mwakyembe na wenzao wanaoisumbua serikali na CCM kuhusu malipo ya Dowans.
Na wanaojua ukweli zaidi kuhusu jinsi Dowans walivyokuja nchini, wanadai kuwa baada ya Rostam Aziz kuwavuta waje kuwekeza katika nishati ya umeme, kuchukua mkataba uliowashinda Richmond, wawekezaji hao walitaka kuhakikishiwa ulinzi wa serikali. Kwa uzito wa jambo lenyewe na kwa kutambua namna Richmond ilivyokwama na namna yeye mwenyewe alivyoshiriki kuinyima fedha, isingewezekana katu Ikulu kutoufahamu undani wa Dowans.
Ni Ikulu gani hiyo ambayo haimhusu Rais Kikwete? Hata kama wasingeunganishwa na Ikulu, Rais wa nchi anawezaje kupata ujasiri wa kusema hawajui wawekezaji ambao wamekuwa kwenye sokomoko na mjadala wa kitaifa kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo? Anataka kuwaambia Watanzania kwamba hajali maslahi yao kwa kiwango hicho?
Hata kama angekuwa hawajui, sokomoko hilo si lingetosha kumfanya aagize vyombo vya dola vimsaidie kujua ni kina nani? Rais Kikwete anataka kutuambia yeye ni kiongozi mzembe wa viwango hivi?
Hapana! Kauli yake ililenga kuficha jambo. Ililenga kufanya propaganda. Ililenga kuwahadaa wananchi na kwa jinsi hiyo kujidanganya mwenyewe kwamba yeye si sehemu ya serikali iliyowaleta Dowans. Anataka kuwa sehemu ya umma unaoipinga serikali. Anataka kumdanganya nani? Ataweza?
Ndiyo! Si lazima Rais Kikwete awe na hisa katika Dowans. Lakini ana maslahi nao – hata kama si ya kipesa. Walau ana maslahi ya kisiasa; maslahi ya kiwajibu. Maslahi ya kikazi na haya ndiyo aliyokuwa anayalinda kwa hotuba ya juzi.
Rais Kikwete alipaswa kuwa na ushupavu wa kusema ukweli. Aseme jinsi alivyohusika na jinsi alivyofuatilia na kuchunguza usajili wao. Awatendee haki Watanzania.
Aseme ukweli kwamba tatizo tulilo nalo hapa halikuletwa na Dowans. Akiri kwamba lililetwa na serikali yake. Akiri kwamba hata mkataba wenyewe ulileta shida, haukuandikwa na Dowans, bali maofisa (wanasheria) wa serikali kupitia TANESCO.
Atwambie kwamba wanasheria na wanasiasa wetu ndio walioingiza vipengele kwa kutubana iwapo tungevunja mkataba huo; na ndio waliotushauri kuuvunja. Akiri kwamba wanasheria haohao ndio waliotumwa na serikali kututetea kwenye kesi kati ya Dowans na TANESCO; na kwamba inawezekana walifanya njama tushindwe au ni kweli kesi ilikuwa nzito sana dhidi yetu.
Na aseme kuwa ndiye aliyewatuma mawaziri Mathias Chikawe, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutamka wazi kwamba "lazima tuwalipe Dowans kwa kuwa wametushinda kwenye kesi." Je, anataka tumuamini kwa kuwaruka mawaziri wake!
Si hilo tu. Rais Kikwete ndiye aliyeongoza Kikao cha Kamati Kuu ambacho wajumbe walisutana kuhusu Dowans, hata baadhi yao wakafika mahali pa kutajana majina kwamba "fulani ndiye Mr. Dowans." Atuambie kwamba ndiye aliwasimamisha kina Sitta na Mwakyembe kujenga hoja zao, halafu akasema: "Sawa, lakini hiyo yote ni historia. Tumeshabanwa na tuna deni hapa, tusaidie tutalilipaje?"
Kama wajumbe walifika mahali wakamtaja Rostam kwamba anahusika na Dowans na Rais akiwa anaongoza kikao hicho alishindwaje kuchimba zaidi – tena kutoka kwa rafiki yake huyo za zamani – ili kujua ukweli wa nyongeza kuhusu Dowans?
Kwa kuwa Rostam Aziz amefika mahali akakubali kwamba ana nguvu ya kisheria katika Dowans na hata akajivuna, Rais anashindwaje kumuuliza kwa kina, "Hebu nieleze, hao wamiliki wa Dowans ni kina nani?"
Haiwezekani kwamba Ngeleja – waziri tu - alidiriki kusema anawajua wamiliki wa Dowans, akawataja – ingawa alikosea kidogo kwa kumtaja mmoja wa wanahisa aliyekwishajitoa; halafu Rais wa nchi anaona ni jambo la kawaida kutamba hadharani, "siwajui."
Kauli yake hiyo inafanana na ile aliyowahi kuitoa akiwa nje ya nchi alipoulizwa sababu zinazoifanya Tanzania kuwa maskini huku ikiwa na raslimali nyingi, akasema, "Hata mimi sijui."
Hakuna mtu aliyemheshimu Rais kwa kutokujua chanzo cha umaskini wa nchi. Maana hata akitokea mtu akamheshimu, atakubaliana nami kwamba Rais wa namna hiyo hawezi kutatua tatizo la umaskini ambalo hajui chanzo chake.
Lakini zaidi, kauli ya "siwajui Dowans" inaweza kufananishwa na kauli ya Mtume Simon Petro mbele ya Wayahudi, siku Yesu alipotiwa mbaroni.
Kwa kuogopa kibano, Simon Petro, ambaye alikuwa mzee kuliko mitume wote, na ambaye muda mfupi kabla ya hapo alimwahidi Yesu kwamba hata ikibidi afe angelikuwa tayari kuliko kumwona Bwana wake akikamatwa, alipohojiwa na kijakazi kuhusu uhusiano wake na Yesu, alijibu mara tatu, "simjui mtu huyu."
Hii ilikuwa kauli ya kijinusuru; kauli ya kisaliti, ambayo sasa inatumiwa na Rais Kikwete kukimbia jukumu lake kwa Dowans na kwa Watanzania.
Kwa kauli hii, Kikwete ameikana Dowans na amewakana Watanzania. Sasa atakuwa mgeni wa nani? Maana anajua fika kwamba lazima atawalipa Dowans. Akichelewa tu kuwalipa, kwa mujibu wa mkataba na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa, serikali italazimika kulipa pesa nyingi zaidi, ambazo kitakuwa kitanzi kikubwa zaidi kwa serikali.
Maana kama anasema hawajui, hizo pesa – ambazo anadai anaunda jopo la wanasheria kusaidia kuzipunguza au kutozilipa kabisa - atawalipa kina nani?
Na kama Rais Kikwete anafanya kazi katika serikali moja na Pinda, basi akubali kutekeleza kile alichomtuma. Afe kiume. Ni bora angekubali kwamba katika hali ambayo tumejifikisha, Dowans lazima walipwe. Lakini aahidi kwamba serikali itawachukulia hatua kali maofisa wake wote – wa sasa na wa zamani – walioshiriki kuliingiza taifa katika mkataba mbovu.
Haya ndiyo maamuzi magumu. Asitafutwe kupendwa na wananchi. Hakumsaidii sasa, maana zamu yao ya kumpenda ilishapita.
Kauli ya Rais Kikwete kwamba hawajui Dowans, ina maana kwamba anawajua. Hatudanganyiki.
 
JK hajatoa kauli yoyote ya maana juu ya dowans zaidi ya kuwa kinyonga tu:
Kwenye kamati kuu ambaye yeye ni mwenyekiti anasema dowans ilipwe;
kwenye baraza la mawaziri ambako yeye ni mwenyekiti anasema dowans ilipwe;
kwenye jukwaa anasema dowans isilipwe na haijui!
Mtu huyo huyo mmoja kauli ....!
 
Wasipobadilika, wataondoka
ban.blank.jpg

Juvenalis Ngowi

amka2.gif
KIONA Mbali amejaliwa kipaji cha kuona mbali kweli kweli. Na umbali anaouna unaweza kuwa wa mbele au wa nyuma. Vyovyote iwavyo, Kiona Mbali anaona mbali. Tena anayaona yale ambayo hata intelijensia pengine haiyaoni au inayaona lakini haiyasemi.
Kiona Mbali yeye yuko tayari kukisema kile anachokiona katika umbali wowote bila kujali kama kwa kusema alichokiona kitamkasirisha, kitamkwaza au kitamfurahisha mtu. Kazi ya Kiona Mbali ni kupaaza sauti yake na kuwaambia anaona nini huko mbali. Atakayenuna, shauri yake.
Jumamosi iliyopita Kiona Mbali hakuwa mmoja wa waalikwa katika karamu ya kukumbukia uzao wa Chama Cha Mapinduzi maarufu kama CCM. Hata hivyo alijua kinachoendela na kwa hakika anakifahamu fika chama hiki ingawa yeye si shabiki wa chama chochote cha siasa.
Kushabikia chama cha siasa ni kujitakia ugonjwa wa moyo bila sababu. Ni sawa na kushabikia soka ya Bongo, raha kwako itakuwa ni jambo la kudhania tu kutokana na kero zisizokuwa na kichwa wala miguu zinazoandamana na mambo haya.
Kiona Mbali akifahamu kwamba wakubwa wako kwenye birthday ya chama tawala (tamka vizuri neno tawala maana kuna wapuuzi wanatamka twawala), aliamua kutumia kipawa chake cha kuonea mbali na kujaribu kuangalia siku wazazi wa chama hiki walipojifungua mtoto CCM walikuwa na matarajio yapi na malengi yapi. Kiona Mbali katika fikra zake akakumbuka namna CCM ilivyoasisiwa mwaka ule wa 1977.
Akakumbuka ngonjera na tenzi zilizoimbwa. Akakumbuka na mitaala ya siasa ilivyofundisha mengi kuhusu chama hiki. Kiona Mbali akabaki kujiuliza ikiwa kumbukumbu zake ndizo zina makosa au uhalisia wa leo ndio umepotosha kile kilichokusudiwa mwaka 1977. Siku ya uzao wa CCM!
Kiona Mbali bado anakumbukumbu nzuri kuhusu umiliki wa CCM katika nyakati za uzao wake. Hiki wamiliki wake walikuwa wakulima na wafanyakazi. Wakulima tuliwaita wakulima tu kwa kuwa hatukupata jina jingine zuri. Wakulima wa hali ya chini kabisa. Wafanyakazi nao ndio hao watu wa vipato vya kati na chini.
Huko ndiko ilikotoka CCM. Jicho la Kiona Mbali linaona nyuma nyakati zile ambapo taifa zima lilikuwa na furaha licha ya kipato duni. Hakuna aliyemnyonya mwingine. Ilifikia wakati watu wenye mitumbo mikubwa waliona soni kutembea hadharani maana walijihisi kupe walionyonya mali ya umma. Madiwani, wabunge na hata rais walitoka katika makundi haya ya watu wa kada ya kawaida kabisa. Kiona Mbali aliangalia huko nyuma akayakumbuka hayo.
Leo hii Kiona Mbali akingalia miaka kumi mbele moyo unamtweta. Tutafika? Mtoto anaonekana ameporwa kwa wenyewe. Sasa anamilikiwa na matajiri na watu wenye uwezo kifedha. Bila vijisenti ni ngumu kweli kweli kuingia katika kinyang'anyiro cha uongozi ndani ya chama hiki.
Kiona Mbali anaona kama hakuna mabadiliko, siku chache zijazo, uchaguzi ndani ya chama hiki utakuwa ni gulio la kura. Mnada utapigwa na mwenye rupia za kutosha ndiye atatawazwa mshindi. Nakumbuka Mwalimu alishasema, kwa kasi tunayokwenda nayo ipo siku watu wanaouza dawa za kulevywa watatuwekea mtu kule Ikulu. Ole wetu.
Kiona Mbali anapoangali mbele na kuona Chama Cha wakulima na wafanyakazi kikimilikiwa na wafanyabiashara na wenye fedha anatabiri kwamba kama hakuna kizuizi kinawekwa mbele ya safari, basi siku si nyingi, tutalazimika kuandamana tukitaka ile alama ya jembe na nyundo kwenye nembo ya chama iondolewe na badala yake iwekwe alama ya sarafu.
Unaweza kubisha lakini kiona mbali anaangalia mbali sana na anaona wakulima wakihoji jembe linamuwakilisha nani pale? Waafanyakazi nao unadhani hawatahoji nyumdo ni alama ya nini? Kama mnadhani Kiona Mbali anatia chumvi, tafuta picha za wabunge wetu halafu anza kutuonyesha wakulima wako wangapi humo.
Tukisema wakulima namaanisha wale watu ambao wanaendesha maisha yao kwa kutifua udongo. Hicho ndicho kilimo cha wengi hapa kwenye kaya yetu.
Kiona Mbali habashiri bali anaona mbali. Anawaona wafanyakazi wakikichukia chama hiki kwa kuwa serikali yao imeshindwa kuwapatia kile wanachotaka. Mshahara mdogo, gharama za maisha kubwa. Wakati mzazi analipwa noti chache kama ujira wa utumishi wake, anaambiwa amsomeshe mwanae elimu ya juu. Jaribio la kumkamua ng'ombe dume. Hapo ujazungumzia kupanda kwa gharama za usafiri, vyakula na kukosekana kwa mahitaji muhimu kama umeme.
Hayo yote ni mambo ambayo tulitarajia yangesimamiwa na chama tulichokizaa mwaka ule wa 1977. Hadi sasa chama kinazeeka na kuishiwa nguvu kikituacha bila matarajio ya kutekeleza yale tuliyoazimia. Hasa kuupiga vita umaskini, ujinga na maradhi. Kiona Mbali haoni utekelezwaji wa mambo yatakayokifanya chama hiki kifanikiwe kuondoa adha inayowakabili watu wake.
Babu yangu alinisimulia kwamba shetani akizeeka huwa kama malaika. Lakini hiki chama hakilandani na msemo huo wa wahenga. Hatuoni kikianza kuwa kama malaika. Lakini kinachomtisha Kiona Mbali kila anapokifikiria chama hiki, sio tu kushindwa kwake kufikia yale malengo ambacho kwayo kilianzishwa bali ni ule mkanganyiko wa chenyewe kwa chenyewe.
Kiona Mbali anaona vyama vingi ndani ya kimoja. Anaona watu wakikenuliana meno na kujidanganya wanatabasamu ili tuamini wapo pamoja. Kiona Mbali anaona mbali sana. Anaona siku inafika ambapo wenye matabasamu ya kuchonga watachoka na kukisema kilichojificha kwenye uvungu wa mitima yao. Siku hiyo Kiona Mbali anaona kama itakuwa siku ya sambaratiko kubwa la chama. Hapo ndipo watakapofukuzana na yale yaliyokipta KANU yatatokea kwa chama hiki.
Rafiki yangu mmoja aliniambia kwamba hawa jamaa chama chao kilianza kufa miaka ya themanini. Kwamba ni kule kuwa chama dola ndiko kumewafanya waendelee kushika hatamu na kupata utamu. Kiona Mbali anapoangalia siasa za mbeleni haoni nafasi ya "udola" kuwabeba hawa jamaa. Watu wameamka hata kama watoto wao huko shuleni wanafeli kuliko wanavyofaulu, bado wana akili za kuzaliwa na kale ka woga ka kusema heri zimwi likujualo kwa kiasi kikubwa kamepotea.
Hata hao waliokuwa waaminifu wakitumia mbinu wazijuazo kukibeba chama nao wana mioyo ya nyama na macho yao yanatoa machozi. Inafika mahali nao wanakata tama ya kumbeba asiyebebeka. Kiona mbali hana haja ya kumung'unya maneno.
Mbele ya safari anaona jambo moja tu ikiwa chama hakizaliwi upya. Mwisho wa chama kushika usukani unakuja. Wachague wenyewe, kubadilika ili kusogeza siku zao za kuwa chama tawala au wapuuze maono ya Kiona Mbali halafu waangukie pua uchaguzi ujao.
(Jina la makala hii ya Kiona Mbali liliasisiwa na mwandishi mashuhuri wa makala, marehemu Condrad Danstan. Makala hizi zinatakiwa kuchapishwa kwa heshima na kumbukumbu yake).
 
Kweli Kikwete hawajui wamiliki wa Dowans?
ban.blank.jpg

Christopher Nyenyembe

amka2.gif
USHINDI wa kesi ya madai iliyopatiwa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans iliyorithi mikoba ya Richmond unaweza kusababisha kila Mtanzania ajikute akilipa deni hilo si chini ya sh milioni mbili, fedha ambazo kama serikali isingeweza kujiingiza kwenye ‘mkenge' huo kiasi hicho kingetumika katika shughuli za kijamii.
Watanzania wapatao milioni 40 ndio wanaopaswa kubeba mzigo huo endapo serikali itakubali kulipa fidia ya dola za Marekani milioni 94 sawa na shilingi bilioni 94 na zikigawanywa kwa idadi hiyo ya Watanzania kila mmoja anapaswa kulipa sh milioni 2.3.
Ni wazi kuwa mzigo wa deni hilo linamgusa hata mtoto mchanga anayezaliwa leo na pia linaweza kuwagusa watoto waliopo tumboni ambao mimba zao zilitungwa wakati kesi hiyo ikiendelea kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) ambayo imeitaka TANESCO kuilipa Dowans sh bilioni 94.
Nashawishika kulichukulia deni hilo kubwa katika nchi masikini kama Tanzania kuwa linawagusa hata watoto wa Kitanzania waliopo matumboni wakisubiri kuzaliwa wakati wowote ambao malumbano ya kutokuilipa Dowans au kuilipa yakiendelea na ndio maana mvutano huo uliovuta hisia za watu wengi na unatia uchungu.
Kwa namna yoyote ile lazima tukubali na tukiri wazi kuwa hawa waliosababisha hali hiyo iwepo wapo na tunaishi nao na hata hilo deni la kila mtanzania anayepaswa kulibeba wao haliwezi kuwaumiza kwa sababu ndani yake wana masilahi makubwa katika fedha hizo, ndiyo maana kati yao umetokea mgawanyiko na mkanganyiko, wale wanaopiga Dowans isilipwe wamekuwa maadui wakubwa kwa wenzao.
Suala la Dowans linapaswa kushughulikiwa kwa nguvu kubwa ya umma, watanzania wengi wanasema kuwa hawapo tayari kuiona serikali ikilipa deni hilo, wanataka kwanza kuwajua wamiliki halali wa kampuni hiyo, ni Watanzania gani waliolifikisha taifa mahali hapo, haya ni maumivu ya hatari ya kiuchumi.
Bila kujali umaskini mkubwa walionao Watanzania, fidia hiyo ya mabilioni ya fedha inamgusa kila mtu, itagusa kwa kiasi kikubwa uzorotaji wa huduma za kijamii, utagusa maisha ya kila Mtanzania na tukilipa deni hilo pia tutakuwa tumeshiriki kuwaua Watanzania wenzetu wasiokuwa na uwezo kabisa hata wa kununua Asprin.
Ni wazi kuwa kulipwa kwa fedha hizo kwenye kampuni tata ambayo inaonyesha wazi kuwa ni genge la mafisadi wachache wa kitanzania wanaoogopa kutajwa na viongozi waandamizi wa serikali kunazidisha hofu na mashaka kuwa fedha hizo si za mtu mmoja isipokuwa ni za mtandao wa kundi maarufu serikalini au mtandao wa chama tawala.
Kwa kuwa kila mtu ana haki ya kuonyesha hisia zake mbaya juu ya sakata hilo lazima ufike wakati kwa taarifa zile zile za Kiintelijensia watanzania waambiwe ni kina nani wanaohusika na umiliki wa Dowans na sio habari za kiintelijensia ziishie kuzuia maandamano ya kisiasa au maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaodai posho na mikopo yao ya elimu ya juu kwa mbinde.
Tumeweza kujionea habari za kiitelijensia zilivyofanya kazi ya kuwatetea mafisadi wa ununuzi wa Rada na namna tulivyoweza kuumbuliwa katika sakata hilo tukisubiri kurudishiwa zaidi ya sh bilioni 60 tulizoibiwa lakini kwa hili la Dowans lazima watanzania wenye uchungu na nchi yao, waseme wanapaswa kusema hapana.
Hapana ya Watanzania sio tu kwamba iwe na lengo la kuyakubali mawazo ya Rais Jakaya Kikwete aliyezungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa anaungana na wananchi wanaopinga hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) inayolitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kuilipa Kampuni ya Dowans fidia ya dola za Marekani milioni 94 kwa kosa la kuvunja mkataba.
Kitendo cha Rais Kikwete cha kuamua kuungana na wananchi katika kadhia hiyo hakuwezi kulinganishwa kwa maana alichotakiwa kukifanya rais ni kwenda mbali zaidi na kwa kuwa hukumu imekwisha tolewa na ICC ni wazi kuwa kwa kupitia taarifa za kiitelijensia anaelewa kabisa Watanzania wanaomiliki Dowans ni kina nani ?
Rais Kikwete kwa taarifa za siri za kiserikali anajua fika kuwa mzigo wa deni hilo wanalotakiwa kutwishwa wananchi wasiokuwa na uwezo kumesababishwa na watu wanaojulikana, basi hana haja ya kuungana na wananchi katika hilo isipokuwa kwa madaraka aliyonayo anapaswa kuwataja na kuwachukulia hatua za kisheria.
Dowans sio jini au msukule ulioletwa na Mungu asiyejulikana. La hasha ni chombo cha biashara kilichoundwa na watu na kusajiliwa kwa kufuata taratibu zote na hapo ndipo watanzania wanapohitaji kujua kuwa akiungana nao kukataa pia awe mwepesi kuwataja wahusika hadharani.
Kama Rais Kikwete alivyojihakikishia kuwa hausiki na Dowans niliweza kumnukuu kuwa "Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka TANESCO ilipe, hivyo kauli za kuhusika na Dowans zinanishangaza, maana nisingeamua hivyo katika Kamati Kuu na Kamati ya Wabunge wa CCM. Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi," alisema Kikwete.
Kwa sababu hiyo na kuonyesha wazi kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi anaweza kuapa hadharani na kuukana uswahiba wake na wamiliki wengine wa Dowans kwa kauli yake anapaswa kuwapa raha watanzania kwa kuwataja bila uoga wamiliki wa Kitanzania walioiingiza mkenge serikali kwa kujua fika kuwa watavuna mabilioni.
Na kwa sababu hizo na kubwa zaidi ambazo zimemsukuma Rais Kikwete aweze kuungana na wananchi wanaopinga kuilipa Dowans atakuwa amefaulu na kuzuia deni ambalo kila mtanzania amelibeba la kulipa kiasi cha sh milioni 2.3 ili waweze kuzifaidi na kuiacha nchi ikitopokea kwenye umaskini usiokwisha.
Kwa hali hiyo, kama Serikali ina fedha za kulipa fidia na wananchi wanapinga ni vyema fedha hizo zikatolewa motisha kwa kila mtanzania anayeshuhudia miaka takriban 50 tangu nchi hii ilipopata uhuru wake ikiwa ni gawio la raslimali na maliasili zilizoiingizia taifa faida kwa muda huo kuliko kuilipa Dowans na fedha hizo ziliwe na watu wachache.
Madhara ambayo yapo mbele ya kila mwananchi ni kuendelea kukosa huduma muhimu za kijamii, kusababisha mfumuko wa bei, kushindwa kuwalipia ada wanafunzi wa vyuo vikuu na kushindwa kutoa ajira ya kutosha kwa walimu wa shule za sekondari na pia kushindwa kuwa na wataalamu wa tiba katika zahanati za vijiji.
Tukilipa deni hilo, huo utakuwa mwanzo wa kuendelea kulipa madeni mengine yaliyofichika kwa kuwa tayari mafisadi watakuwa wameona njia nzuri ya kuiibia nchi maskini kama Tanzania kwa maana ya kuwa na viongozi wazembe wanaoiingizia hasara nchi, wapo lakini hawashughulikiwi na wanaendelea kujifanya wafalme kwenye majimbo yao.
Hakika inauma, kitendo cha nchi masikini kuzipeleka fedha nyingi kiasi hicho kwa watu wasiofahamika ni sawa na kuwavua nguo watu wazima mbele ya watoto wao ili wacheze ngoma ya ‘Kiduku'wote hapo tutaonekana ni wendawazimu, lazima sasa tuseme kwa pamoja kuwa ‘Dowans NO'.


h.sep3.gif

cnyenyembe@yahoo.com 0754 301864, 0715 301864
 
Yusuf Makamba nenda, iache CCM yao
ban.mtazamo.jpg

Irene Mark

amka2.gif
JUZI kwenye moja ya magazeti ya kila siku nilisoma taarifa iliyomnukuu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Rajab Makamba, akisema yupo tayari kuondoka kwenye nafasi hiyo ikiwa itathibitika kuwa yeye ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa umaarufu wa chama hicho.
Nilipoona kichwa cha habari Makamba akisema yupo tayari kutemwa CCM nilishtuka halafu nikashawishika kuisoma habari yenyewe, kisha nikajipa muda wa kutafakuri na ninachokieleza kwenye mtazamo wangu hakina lengo la kumchafua mzee huyu bali kuweka sawa kumbukumbu.
Makamba amesema hatoyumba pindi atakapoondoka ndani ya chama hicho kikongwe kwa madai kuwa wamepita makatibu wakuu wengi na bado chama kipo imara. Ni kweli kabisa, tena wapo wengi kabla yake na bado chama kama taasisi kitaendelea kuwepo.
Kwangu maneno ya Makamba ni kujifariji na kujipa moyo baada ya bosi wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Jakaya Kikwete, kuwaahidi wafuasi zaidi ya milioni nne wa chama hicho kwamba atafanya mabadiliko makubwa hasa kutokana na umaarufu wa chama hicho kuporomoka kwa kasi.
Kilichoniaminisha kwamba katibu mkuu huyo aliyepoteza mwelekeo wake na chama kwa ujumla anajifariji ni pale anaposema eti ikithibitika kwamba yeye ni chanzo cha kushuka kwa umaarufu wa chama hicho, yupo tayari kuondoka.
Namshangaa babu yangu Makamba ambaye mpaka sasa hataki kuamini kwamba uwepo wake ndani ya chama ni mauti ya chama hicho… ninavyofahamu katibu mkuu ndiye mtendaji na msimamizi wa shughuli za kila siku za chama husika.
Mipango mizuri na mibaya ya chama huanzia kwenye ofisi yake, kauli zisizo na mashiko na mikinzano kati yake na mwenyekiti wake ni sababu tosha ya kumtimua Makamba kwenye nafasi hiyo.
Matokeo ya kura wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita ni moja ya tiketi za kuondoka kwa babu Makamba. Kushuka kwa idadi ya kura za urais, kudondoshwa kwa wabunge wengi wa CCM na kuzomewa kwa baadhi ya viongozi wa serikali na chama, sababu ni katibu mkuu.
Kwa chama kikongwe kama CCM matokeo yaliyopita ni mwanzo wa mauti yake. Haiingii akilini ushindi wa mwaka 2005 kwa kura za urais iwe asilimia 80 halafu katika kipindi cha miaka mitano ishuke hadi asilimia 60, kisha unaendelea kumwacha katibu wa chama aliyesababisha watu kukata tamaa na wengi wao kukacha zoezi la kupiga kura.
Mengi anayafanya kwa uonevu kiasi baadhi ya wafuasi wa chama hicho kujengeana chuki. Kwa muda usiopungua miaka miwili nilichunguza na kujiridhisha pasi na shaka kwamba ofisi ya katibu mkuu ni chungu cha makundi ya wafuasi wa CCM.
Babu Makamba ni mtaalam wa kukariri maandiko matakatifu bila kujali matumizi ya mahali, wakati na hadhira anayoifikishia ujumbe… ndiyo maana mara zote amezua ukakasi kwenye matamshi yake.
Anapoulizwa maswali magumu huja na majibu mepesi mno yenye kukera mara zote. Kwangu huyu ni katibu asiye na karama ya uongozi hivyo hafai kuendelea kuwepo kwenye nafasi hiyo.
Mfano mzuri ni siku moja baada ya kunukuliwa na vyombo vya habari akiwataka wana CCM wanaotaka serikali isiilipe Kampuni ya Dowans wajiondoe wenyewe ndani ya chama, bosi wake alikuja na kauli za kujiswafi akiungana na wanaotimuliwa.
Leo hii mzee huyu ambaye binafsi naridhishwa na uwezo wake mdogo wa kumbukumbu ya mambo na kauli zake anadiriki kusema: "Kama tatizo ni Makamba ndani ya CCM basi ni vema mabadiliko yakaanza na mimi kwa sababu chama si Makamba, cha msingi hapa chama changu kibaki katika hali ya usalama."
Kwetu wachambuzi wa masuala ya siasa haya ni maneno ya kuomba huruma kwa bosi wake, kwa mtazamo wa haraka babu huyu anajifariji tuu kwani hata uso wake haumaanishi anachokisema. Ningekuwa na uwezo, mzee huyu angebaki kuwa mfuatiliaji wa siasa za chama tawala kupitia vyombo vya habari pekee, nisingempa nafasi hata ya kuwa kiongozi wa tawi.
Ninachomshauri Mwenyekiti wa CCM taifa afanye haraka kumwondoa mzee huyu. Ampumzishe kwa maslahi na mustkabali mwema wa chama chao, kwa hali ilivyo mbaya sasa anatakiwa katibu mtendaji, mambo ya propaganda si wakati wake huu kwa kuzingatia hoja nzito zinazotolewa na wanasiasa wa kambi ya ushindani.


h.sep3.gif

0784 190066
 
Back
Top Bottom