Sababu za kupinga Bob Sambeke sio bilionea

Na jamaa aliweza kuwabrainwash
wachaga wa moshi,mtu hana hotel,hana kampuni,akitembea na jeep wanamwita bilionea,,,,,,,

bongo watu wanazungumza bila data, ndo maana bongo mtu akinunua vitz m6 anajitangazia m10 na watu wanaamini.
 
Kaeni ki discuss utajiri wa wenzenu tu. Wenzenu wanaongeza hela by the day.

Do you. Kukodolea macho sana utakiri wa watu ni ishara ya kukosa shughuli. Tafuta vyako utuambie na mimi bilionea, hata kama ni bilionea wa senti.
 
Nina pesa kuliko hata huyo bob sambeke,ni mtoto sana kwa hivyo visumni vyake.ndege ya laki tano?
Je nikikupa taarifa ya jamaa tu mwanza mdogo nyumba ndogo yake amemnunulia V8 za wabunge naye utamwitaje?

Kama ni hivyo hata kakaangu mmoja wa humu nI Billionea, Btw kuna umuhimu gani wa kuhoji mali alizonazo mtu aliyekufa, unataka mgao!
 
Vipi kuhusu milionea? atakuwa na asset zinazofikia milioni moja? nikiwa na milioni moja na nusu naweza orodheshwa milionea?
 
Lakini unacho cha kusema kwake kuwa ni mmiliki wa kitu fulani what about bob sambeke?Soma historia ya donald trump,mtu kupata misukosuko ndio inayomuweka strong.

Kwa hiyo kwako wewe mtu ambaye hajawai kupata misukosuko hata akiwa na billioni ngapi bado si billionea? Vipi Riziwani siyo billionea, naona kumbe mnachuki binafsi kwa Sambeke! Kwani Billioni moja kitu gani wazee, mabillionea tunao wengi sana hapa tanzania, ni wengi mno kwa makumi maelfu, ungesema trillionea hapo maneno mengine!
 
Alaa! Kumbe...
Heshima kwenu wanajamvi,

Ni kweli kumekuwa na mtindo wa kuwakweza baadhi ya wafanyabiashara wa kawaida kabisa na kuwaita mabilionea.Mfano mzuri ni huyu Babu Sambeke.Marehemu alikuwa anafanya biashara kubwa ya kukopesha watu fedha binafsi nawajua baadhi ya wafanyabiashara wakubwa waliokopa fedha kwake 1.Ove huyu ni mfanyabiashara ya wa magari na pia anajishughulisha na uchinjaji wa magari kwaajili ya kuuza spares (us 450,000/=) 2. Sunda mfanyabiashara na mchimbaji wa madini ya Tanzanite (Tsh 2 bilioni) 3.Mmiliki wa Snow Crest kiasi hakijulikani. 4 Wachimbaji wa wengi wa Tanzanite wanadaiwa kiasi kikubwa cha fedha walichokopa kwaajili ya kuendesha mashimo ya mawe.

Bado kuna wafanyabiashara wengi wadogo wadogo walioporwa nyumba na magari kupitia mikopo ya Babu,mfano mmojawapo ni dalali wa viwanja anayejulikana kama Simba alikopa fedha akaweka nyumba anayoisha rehani siku ya siku aliposhindwa kulipa nyumba ikachukuliwa siku hizi anaishi Mwanama nyumba ya kupanga ya vyumba viwili,fikiria huyu katoka kwenye nyumba yake self contained,car park,gati kubwa na makorokoro kibao leo anakichukuliaje kifo cha Babu !

Babu Sambeke ni mfanyabishara mkubwa ingawa biashara yake haijulikana rasmi na serekali huyu jamaa ni bilionea usiangalie kigezo cha kumiliki ndege ukadhani wanahabari wamekurupuka la hashaa jamaa alikuwa akimiliki biashara kubwa sana yenye kumuingizia fedha nyingi pasipo kulipa kodi ya serekali.Inashangaza sana jambo kama hili linatendeka wazi wazi huku serekali ikikubali kuibiwa mapato yake kupitia ukwepaji wa kodi mkubwa.Nina hakika kufuatia kifo chake fedha zake nyingi zitapotea (kufa kufaana).

Mwisho serekali ijipange vizuri ihakikishe inapanue uwogo wa walipa kodi wake.Wafanyabiashara wakubwa aina ya Babu ni wengi lakini utashangaa serekali haina taarifa zao za mapato na matumizi.

Marehemu Wakili Nyaga huyu ni bilionea kwa vigezo vyote ukitaka kujua uwezo aliokuwa nao nenda Mawala estate ni zaidi ya eka 200 4 kilometa from city center kaweka miundo mbinu yote kuanzia barabara za lami,mtandao wa maji na umeme.Isitoshe Mawalla alikuwa na connection za matajiri wakubwa wa dunia kama Paul Tudor.Pia ana miliki estate huko South Afrika na Zimbabwe usishangae kwenye mazishi yake mawaziri walikuwa wanapigana vikumbo.
 
Ngongo sitaki kuamini kama wewe ndio umeandika humu. Ila kwa uwepo wa avatar yako na font hiyo nashawishika kuamini. Hivi kweli nawe umeandika kuthibitisha huyo sambeke ni bilionea? Data zako ni zipi, vigezo vyako ni nini? Ulichoandika ni stories tu za kijiweni ambazo mi nimezisikia muda sasa.

Kama ndio hivyo basi na kwa vigezo vyenu Kahama na na Ushirombo pekee kuna mabilionea 50!
 
haha muulizeni ispeka naniliu anajua ato z ya babu sambeke alipopatia hela.,yule aliyejipumzkia morogoro maana babu pale central ya ms palikuwa nyumbani
 
Mkuu Spike Lee hawa jamaa wanamitandao yao sijui tusema ni mitandao ya kihalifu au nakosa neno sahihi la kiswahili.Ni hivi usifikiri hata mara moja Babu akikudai fedha zake atakupitisha kwenye mikono ya dola la hasha atapamaba na wewe binafsi au genge lake.Ndiyo maana nakwambia leo ukienda Njiro,Kimandolu,Baraa,Mitaa ya mjini kati na Sakina nyumba,magari na viwanja alizofanikiwa kuzichukua kupitia mikopo yake utashangaa ni kiasi gani serekali ilikuwa ikipoteza mapato yake.Vuta subira kidogo mtu mwenye uwezo wa kumkopesha Sunda unamweka daraja lipi ?,ngoja kidogo ni kwambie umewahi kujiuliza Sunda ana miliki asset za aina gani ?.Mtu mwenye uwezo wa kutoa mkopo wa tsh 10,000,000,000/= halafu serekali haina habari zake halafu leo unashangaa wanahabari wanamwita bilionea!.

Kifupi sana kuna baadhi ya banks za hapa Arusha na Moshi sipendi kuzitaja ulikuwa ukiomba mkopo na wakiona unaweza kuwasumbua wanakuelekeza kwa Babu Sambeke.Kama hiyo haitoshi pia alikuwa akiulizwa kama mkopaji alikuwa akidaiwa kabla hazijamkopesha sasa nadhani umeelwa maana ya mtandao pia nadhani umeelewa Babu alikuwa na uwezo kiasi gani.

Nadhani wewe umetufahamisha vizuri kuhusu hawa jamaa ambao wanaitwa mabilionea.

Forbes wanautambua utajiri hao jamaa au ndio kazi za kimafia.
 
Last edited by a moderator:
Still bado kama porojo hizo hazina uhakiki

Mkuu Spike Lee hawa jamaa wanamitandao yao sijui tusema ni mitandao ya kihalifu au nakosa neno sahihi la kiswahili.Ni hivi usifikiri hata mara moja Babu akikudai fedha zake atakupitisha kwenye mikono ya dola la hasha atapamaba na wewe binafsi au genge lake.Ndiyo maana nakwambia leo ukienda Njiro,Kimandolu,Baraa,Mitaa ya mjini kati na Sakina nyumba,magari na viwanja alizofanikiwa kuzichukua kupitia mikopo yake utashangaa ni kiasi gani serekali ilikuwa ikipoteza mapato yake.Vuta subira kidogo mtu mwenye uwezo wa kumkopesha Sunda unamweka daraja lipi ?,ngoja kidogo ni kwambie umewahi kujiuliza Sunda ana miliki asset za aina gani ?.Mtu mwenye uwezo wa kutoa mkopo wa tsh 10,000,000,000/= halafu serekali haina habari zake halafu leo unashangaa wanahabari wanamwita bilionea!.

Kifupi sana kuna baadhi ya banks za hapa Arusha na Moshi sipendi kuzitaja ulikuwa ukiomba mkopo na wakiona unaweza kuwasumbua wanakuelekeza kwa Babu Sambeke.Kama hiyo haitoshi pia alikuwa akiulizwa kama mkopaji alikuwa akidaiwa kabla hazijamkopesha sasa nadhani umeelwa maana ya mtandao pia nadhani umeelewa Babu alikuwa na uwezo kiasi gani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ibambasi kiwanja kimoja maeneo ya mjini katikati sasa ni kati ya tsh 800,000,000/= mpaka 1bilioni bado sijaenda Njiro,sakina......huko ni nyumba si nyumba za kijinga la hasha.Bado kuna petrol station,mashamba yaliyo pembezoni mwa barabara kuu na Cash ya kutosha ndiyo maana wafanyabisha wakubwa badala ya kuhangaika kuandika michanganuo ya biashara inayohitajika kwenye mabanks mbali mbali wanamwona Babu wanapatiwa fedha wanaweka dhamana nyumba au viwanja au mashamba au magari ya ukweli.Kama unadaiwa na bank ukimwona ana nunua deni lote anabaki na nyumba au dhamana yoyote anayoina itampatia faida kubwa.

Ngongo sitaki kuamini kama wewe ndio umeandika humu. Ila kwa uwepo wa avatar yako na font hiyo nashawishika kuamini. Hivi kweli nawe umeandika kuthibitisha huyo sambeke ni bilionea? Data zako ni zipi, vigezo vyako ni nini? Ulichoandika ni stories tu za kijiweni ambazo mi nimezisikia muda sasa.

Kama ndio hivyo basi na kwa vigezo vyenu Kahama na na Ushirombo pekee kuna mabilionea 50!
 
Last edited by a moderator:
Ungetufafanulia hizo pia lakionea na milionea tungekushukuru sana mkuu! mie nilikimbia umande wa somo la hesabu
 
Vijana wa kitanzania ni watu wa Ajabu sana. Sasa mtu kuwa bilionea au kuotkua bilionea kunakusaidia nini. Tujadilini ideas na sio ku discuss watu .Kama unadhani alikuwa na business strategy nzuri ambazo vijana wanatakiwa kujifunza then hiyo itakuwa ina maana au labda ni mfano wa kuigwa au labda business strategy zake hazikuwa nzuri na si mfano wa kuigwa na vijana wanaotaka kuwa wajasiriamali hayo ndo mambo ya ku discuss. Sijui mnapata wapi muda wa kuanzisha topic kama hizi. Mi huwa sina muda kabisa sema nikikuta mtu kaandika utumbo kama huu huwa nasikia kichefu chefu inabidi tu niupoteze muda wanguu. Inakera jamani mbona hatubadiliki au mnafurahia kuendelea kuwa maskini tu na kujiona nyie ndo wajajnja wa mjini
 
Kutokana na matukio ya matajiri wa Arusha waliopoteza maisha yao,kumetokea mchanganyiko wa mawazo wengine wakisema ni mabilionea na wengine wakipinga.Bilionea ni mtu ambaye asset zake zimefikia bilioni moja na kuendelea kwa Tanzania.

Ni vema tukaibadilisha hii zana kwa kuita bilionea mtu ambaye hata ajira hajatoa kwa wananchi ama impact kwa taifa lake.

Kuhusu Bob Sambeke na hiyo ndege,inabidi wote tufunguke akili,je unajua kuna ndege zinauzwa hadi laki 5 na serikali?

Je unajua 2c walishawahi uza ndege kwa millioni 60?and guess what aliyenunua ni owner wa precision na mikataba hadi tender zipo wazi.

Kwa hiyo suala la mtu kumiliki ndege ndogo used sio shida labda kama ingekuwa mpya kaitoa kiwandani hapo ni sawa.

Suala lingine alikuwa akimiliki kampuni gani?mfano wa wajasiriamali ambao mtu anaweza kuaccept kuwa ni mabilionea baadhi ni kama wafuatao

ndesamburo-hotels,tours
mansoor-mansoor oil
sunda- mount meru,tanzanite etc
Reginald Mengi - ipp media,cocacola kwanza etc
Mohmd Dewji-Mohamed enterprise tanzania ltd
Erick shigongo-global publishers
Michael ngareko- precision airways
Koola Zadock- CEO ZEK Group and dar village 2nd largest shopping mall in tanzania
bob sambeke-??????

Hayo ni mawazo tu,

Mkuu, vipi mimi ninaye miliki bajaji ya mil 3.5 Tsh, ni sahihi nikijiita MILLIONAIRE??
 
Ngongo sitaki kuamini kama wewe ndio umeandika humu. Ila kwa uwepo wa avatar yako na font hiyo nashawishika kuamini. Hivi kweli nawe umeandika kuthibitisha huyo sambeke ni bilionea? Data zako ni zipi, vigezo vyako ni nini? Ulichoandika ni stories tu za kijiweni ambazo mi nimezisikia muda sasa.

Kama ndio hivyo basi na kwa vigezo vyenu Kahama na na Ushirombo pekee kuna mabilionea 50!
sasa mkuu kahama kuna bilionea hapo?.

Huyo tajiri wenu mkubwa mnaemuona ndo bigboss,matanuzi yake makubwa ni kula supu ya kichwa cha mbuzi na wapambe wake wakati family ikila mchicha.
 
Na mie ni millionaire maana namiliki kiendea ------ cha million 7, kibanda sijui thamani yake lakini ardhi nilinunua million 8, bustani bagamoyo sijui thamani yake ardhi nilinunua million 3,hela yangu NSSF million kadhaaa. Yalah uwiiiiiiiii Millionaire N-handsome............
 
Back
Top Bottom