Bila Mercy, huenda tusingekuwa na bilionea Mengi

Apr 11, 2011
5
70
Mercy Mengi na kadhia ya wenza wa matajiri

Na Ezekiel Kamwaga

KUNA msemo mmoja mashuhuri wa wahenga wetu kwamba kwenye mafanikio ya mwanamume, kuna mwanamke pembeni yake. Kama kuna mahali msemo huu umesadifu ukweli huu, basi ni kuhusu maisha ya aliyekuwa pengine bilionea maarufu zaidi nchini Tanzania, Reginald Abraham Mengi na mkewe wa kwanza, Mercy Anna Mengi.

Wawili hao sasa wametangulia mbele ya haki. Mercy alikuwa wa kwanza kufariki dunia mnamo Oktoba 31, mwaka 2018 na aliyekuwa mumewe akafuatia miezi sita tu baadaye yaani Mei 2, 2019. Kwa sababu ya tabia zao tofauti, Mengi alikuwa mtu mashuhuri na sura yake ikijulikana na karibu kila mtu mzima Mtanzania aliyejua kusoma na kuandika au angalau kumiliki televisheni – lakini mkewe Mercy hakuwa maarufu kwa sababu ya tabia yake ya kupenda kufanya mambo yake mbali ya kamera za waandishi wa habari.

Matokeo ya tofauti hizi za kitabia ni kwamba Mercy alipofariki dunia alikuwa hajulikani na wengi zaidi ya wale waliowahi kuguswa na maisha yake moja kwa moja iwe kwa kufanya naye kazi, kuishi katika jumuiya moja au kufanya shughuli zinazofanana.

Hadithi ya maisha ya Mercy na Reginald Mengi ni hadithi ya maisha ya wanaume wengi waliofanikiwa kwenye maisha yao. Tatizo kubwa ni kwamba jamii zetu huwa hazina tabia ya kuonesha upande wa pili wa maisha ya wenza waliofanikiwa. Leo, takribani miezi miwili kabla ya maadhimisho ya miaka minne ya kifo cha Mercy Anna Mengi, pengine huu ni wakati wa kuangalia nafasi yake – na kwa kioo hicho, kuwasilisha ukweli halisi katika jamii yetu kuhusu nafasi ya wenza hususan wanawake katika mafanikio yao kama washirika kibiashara.

Hapo mwanzo, Mengi hakuwa bilionea

Mengi na Mercy walioana Novemba mwaka 1971. Wakati huo, Mengi hakuwa maarufu nchini wala hakumiliki mali. Ndiyo kwanza alikuwa amerejea nchini baada ya kumaliza masomo yake ya uhasibu huko Scotland na kipindi kifupi cha kufanya kazi nchini Uingereza. Mercy tayari alikuwa ameajiriwa katika lililokuwa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki (East Africa Airways).

Kimsingi, wakati huo, ungeweza kusema Mercy alitoka ‘matawi ya juu’ kumzidi Mengi maana alizaliwa kwenye koo za kichifu katika jamii ya Wachaga. Mercy ni mtoto wa Chief Abdiel Shangali wa Machame. Mengi alizaliwa katika familia ya kawaida na kwa maana hiyo, ndoa yake na Mercy ilimfanya kuwa mmoja wa wanafamilia katika mojawapo ya koo mashuhuri katika jamii yake.

Ingawa Mengi hakuwa na damu ya kichifu, lakini alikuwa mtu mwenye akili na maarifa. Wakati akimaliza masomo yake ya uhasibu ughaibuni, Tanzania haikuwa na wahasibu wengi wa hadhi yake. Kama angetaka, angeweza kubaki Uingereza na kufanya kazi huko lakini aliamua kurejea nyumbani alikoona kuna fursa zaidi.

Simulizi za watu waliowafahamu wawili hawa tangu wangali vijana, zinaeleza kuhusu wapenzi waliotengeneza kombinesheni ya kipekee. Mengi alikuwa mchapakazi, mwenye maarifa na mpambanaji huku Mercy alikuwa mwenye maono, mchapakazi, msimamizi, mlezi na aliyekuwa tayari kufanya maamuzi magumu ikibidi.

Si wengi wanaofahamu kwamba ni Mercy aliyekuwa wa kwanza kukubali kuacha ajira yake kwenye shirika la ndege ili kuanzisha na mume wake na kusimamia biashara ya familia. Na ingawa Mercy aliamua kuacha kazi ili ajikite zaidi huko, walikubaliana Mengi aendelee na ajira.

Biashara ya kwanza kwa familia ya Mengi – iliyokuja kuwa msingi wa mafanikio yao yote yaliyofuata, ilikuwa ni ile ya kutengeneza kalamu. Biashara hiyo ilianzia sehemu ya kula chakula (dining room) nyumbani kwao, Upanga jijini Dar es Salaam, kwa vile hawakuwa na uwezo wa kumiliki ofisi wakati huo.

Kazi ya kutengeneza kalamu wakati huo haikuwa rahisi kama ilivyo sasa. Waliowafahamu miaka hiyo walishuhudia jinsi ilivyolazimu kuingiza wino katika bomba la ndani la kalamu moja moja kwa kutumia aina fulani ya sindano. Hatua hiyo ilifuatiwa na kuingiza bomba la wino ndani ya kasha la kalamu, kufunga ncha ya mbele na vizibo vyake. Kazi hiyo ilifanywa kwa kalamu moja baada ya nyingine hadi boksi zima la kalamu likamilike.

Mercy aliamua kufanya uamuzi mgumu wa kuacha ajira yake ili aweze kutunza familia changa, ikiwa ni pamoja na mume wake, na kufanya kazi hizo za kufunga kalamu na kushughulikia mambo mengine ya biashara yao kama kupokea mizigo inapoagizwa, mambo ya benki, na kadhalika. Wakati Mengi akiwa kazini na watoto shuleni, jukumu lote hilo lilimwangukia Mercy.

Kuondoa miaka ya baadaye wakati walipopata uwezo wa kuajiri watu wa kuwasaidia kazi, shughuli hiyo ya kufunga kalamu ilikuwa ikifanywa wakati wote na Mercy peke yake. Mengi aliungana na mkewe kwenye jukumu hilo jioni alipotoka kazini. Watoto wao; Regina na Rodney Mutie ambao walikuwa wangali wanasoma shule ya msingi walifundishwa kazi na kushiriki kidogo walipotoka shule mchana.

Katika kitabu cha historia ya maisha ya Mengi kiitwacho I Can, I Must, I Will kilichotolewa mwaka mmoja kabla ya kifo chake, tajiri huyo alieleza kwamba ni kwa kupitia biashara hiyo ndipo walipotengeneza zaidi ya shilingi bilioni moja. Jambo moja la kuzingatia hapa ni kwamba ni Mercy ndiye aliyekuwa akifanya shughuli hizo tangu awali, kwa muda mwingi zaidi na pia ndiye aliyechukua uamuzi mgumu wa kuacha kazi!

Pamoja na mafanikio hayo, bado Mengi aliendelea na ajira yake kwenye moja ya kampuni mashuhuri za kimataifa za ukaguzi wa kihasibu.

Mmoja wa marafiki wa karibu wa Mzee Mengi aliyezungumza nami miezi michache baada ya msiba wake alinieleza kwa mara nyingine kuwa Mercy ndiye alimshawishi Mengi kuacha ajira yake katika kampuni iliyokuwa inajulikana kama Coopers & Lybrand (na sasa inaitwa PwC) ili kuongeza nguvu kwenye biashara zao.

Hatimaye Mengi alisikiliza ushauri wa mkewe na kuacha kazi ili kuendeleza makampuni na biashara za familia. Biashara hizo ni kama Anche Mwedu - kiwanda kilichokuwa kinatengenza sahani na vikombe. Kampuni ya IPP ilizinduliwa rasmi, na waliunganisha nguvu ya biashara na makampuni ya awali na kuendeleza uanzishwaji wa makampuni mengine vikiwamo vyombo vya habari kama luninga za ITV na EATV na magazeti ya The Guardian na Nipashe.

Baada ya Mengi na mkewe kuingia kwenye biashara kwa miguu yote miwili, huo ndiyo ukafungua milango ya utajiri mkubwa kiasi cha kwamba kufikia katikati ya miaka ya tisini, Mzee Mengi, aliyekuwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP alikuwa akionekana kama Mtanzania mweusi mwenye ukwasi zaidi nchini kwake kuliko wengine.

Mercy aliendelea kubaki kwenye kivuli cha mumewe. Tabia ya Mercy ya kutotaka kutajwa au kutangazwa ilikuwa ikijulikana hadi kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front alikokuwa akisali. Wakati wa ibada ya msiba wake iliyofanyika kanisani, baadhi ya waombolezaji walikumbusha kuhusu mambo mawili aliyokuwa akijulikana nayo mke huyo wa kwanza wa Mengi.

Mosi, wakati wa Sikukuu za Mavuno, siku ambayo waumini huwasilisha sadaka zao za mavuno na shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Mercy alielezwa kushiriki bila kuwa na mbwembwe wakati wa minada iliyokuwa ikifanyika kanisani. Hata hivyo, lililokuwa linajulikana kwa viongozi wa Kanisa ni kuwa yeye alikuwa akiwasilisha sadaka yake mapema bila watu kujua. Mchango wake alitaka uwe siri yake na Mungu wake.

Jambo la pili ambalo waumini walisema wanakumbuka ni tabia yake ya kutopenda ‘kujionyesha’ kama kukaa kwenye viti vya mbele. Pamoja na umaarufu wake kama mke wa mfanyabiashara tajiri – huku naye tayari akiwa ana ukwasi wa kutosha, Mercy alipenda kukaa kwenye viti vya nyuma na usingeweza kumbaini kwamba ni mtu wa daraja tofauti.

Naamini kwamba kama ilivyokuwa kwa kitabu cha mumewe, kuna siku tutasoma historia kamili ya Mercy Mengi kupitia maandishi ili mchango wake naye uweze kutanabaishwa bayana. Watanzania na wengine waliosoma kitabu cha Mengi wamepata upande mmoja tu wa shilingi kwa sababu kwa bahati mbaya kitabu hakikueleza sana kuhusu uhusiano wa utajiri wao na ushiriki wa kila mmoja wao katika kutafuta na kumiliki mali zote walizochuma pamoja.

Itakuwa si haki iwapo kumbukumbu pekee ya Mama Mercy itahusu mambo mengine yaliyotokea katika uhusiano wake na mumewe huyo kwa kuwa historia hiyo inadogosha mchango mkubwa wa mwanamama huyu katika utajiri wa familia yake na mumewe.

Bahati mbaya ni kwamba hadithi hii ya Mercy Anna Mengi ni hadithi ya wanawake wengi katika historia ya bara la Afrika. Ukisoma historia ya viongozi wakubwa na makubwa yao – kwa kiasi kikubwa, utasoma historia ya wanaume.

Kama ukitazama orodha ya mabilionea na mamilionea wa Afrika, utakachoona ni utajiri wa wanaume na hakuna maelezo yoyote kuhusu wake zao. Kama utasikia habari za wanawake wa watu mashuhuri, utakachosikia zaidi ni habari kuhusu wanavyopenda maisha ya anasa, wasivyojua kutafuta pesa na pengine migogoro ya mali baada ya vifo vya waume zao.

Ukizungumza na watu binafsi na taasisi ambazo zilifaidi misaada ya Mercy Mengi wakati angali hai, utapata picha ya watu wanaotamani mama huyo akumbukwe kwa kumcha Mungu, kwa upendo wake, kwa upambanaji wake, kwa malezi na kwa misaada yake. Pamoja na kulea watoto wake, alilea pia sehemu kubwa ya wanafamilia wa Mengi na wa Shangali katika kipindi chote cha uhai wake. Ukizungumza na wale waliosaidiwa naye, utaona matamanio yao ya kutaka shughuli alizokuwa akisaidia nje ya kamera za vyombo vya habari zisikome na badala yake ziendelee.

Kama matajiri wanaume wa Kitanzania na watu wengine waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kimaisha wakiendelea na utamaduni wa kuonyesha mafanikio yao hayakutokana na wenza wa kimaisha hususan wa kike, tutachukua muda mrefu kukuza mabinti wenye ndoto kubwa na zenye manufaa kwa taifa lao. Namna pekee ya kuepusha taifa letu na balaa ni kuhakikisha stori za wanawake kama Mercy Anna Mengi zinaandikwa na kusimuliwa kama zilivyo.

Kama mwandishi wa habari, nimeanza kuchoshwa na hadithi hizi za mafanikio ya wanaume ambazo sasa zinaniboa kwa kujirudiarudia na kuzungumza yale yale ambayo tumeyasikia kwa miaka alfu lela ulela sasa. Huu ni wakati wa mabadiliko.

Mercy hakuwa mama wa nyumbani tu, hakulea familia tu, alikuwa mwanzilishi mwenza na mwenye mchango mkubwa wa tunachojua kama makampuni ya IPP. Huu ni wakati wa kuibua michango ya akina mama wa aina ya Mercy Anna Mengi.

Mwenyezi Mungu na azilaze mahali pema peponi roho za Reginald na Mercy- Mengi. Amina.

The End
 
Weka na historia ya Klyn au Jack Ntiyabaliwe alivyosababisha anguko la Mengi ili wanaume tujifunze

Kwa upande wangu Mengi alichemsha kuoa mtoto wa mjini, nina imani nakanisani na kwenye maofisi ya IPP kuna wajane watu wazima wengi tu between 40-50 angechukua humo

Klyn bila viagra kwa mzee huwezi kumtimiza haja zake
 
Nafasi ya mwanamke katika maendeleo ya iwe ya familia au taifa ni kubwa kwa kiasi chake.

Nikichukulia mfano katika kanisa lau kama sio wakina mama kuna mahali kanisa lisingekuwa kama lilivyo leo.

Pia hata taifa letu kuna mahali mwanamke au wakina mama walisimama ambapo kama isingekuwa hivyo kuna kitu kisinge kua kama lilivyo sasa.

Hata kwenye vyama mfano vya siasa mwanamke amekua nguvu kubwa ya chama mfano ccm .

Tukirudi kwenye mada mimi binafsi naami kabisa hilo mleta mada alivyo wasilisha ni sahihi, ila kwa kiasi chake sisi wanaume tumekua tuki ignore mchango wa wenzetu katika maendeleo yetu, sifa zote njema tunapewa sisi.

Lakini ukweli ni wanaume wachache sana ambao wamekua na maendeleo ya moja kwa moja bila ya mwanamke.

Lakini pia wanawake hao hao ndio wanasabisha anguko kwa mwanaume na jamii kwa ujumla.
 
Mzee nae alichemka sana Mungu amrehem mke kapambana mmefikia hapo leo unakuja kuchukua kupe inataka kuchukua mali zote bila jasho kisa tu imezaa na mzee wale watoto wasimamie mali za baba na mama yao na huyo kupe azitafute km alivo tafuta mke wa kwanza
Hakuchemka. Hayo ndiyo matumizi ya fedha alizohangaija kwa miaka mingi kuzitafuta.

Na siyo kweli kwamba K-Lyne hakutoa jasho. K-Lyne anevuja jasho Sana kumlea mzee Mengi. Msichana mdogo Kama K-Lyne kumpakat mzee kana Mengi siyo Jambo dogo.

Na mwisho,. Mali ni za Mengi na Mengi ndiye aliyeamua ampe K-Lyne Mali zote. Wewe nani upinge??
 
Mwanamama Mercy anastahili pongezi sana ktk maeneo 3 yanayowashinda wanawake wengi Sana;-
1. Kutoka kwenye familia ya wenye nazo (kichifu) na kukukubali kuolewa na mtu kawaida. Wanawake wengi hukataa

2. Kukubali kuacha kazi ya maana ili kuanzisha na kusimamia biashara huku mume yeye akiendelea na kazi. Hngera Sana kwa mama yetu Mercy. Wanawake wengi hukataa

3. Kuwa na uwezo wa kusimamia biashara billa tamaa. Wanawake we go ukiwaachia hata duka tu siku hizi wanachepusha fedha na kuzipeleka kwenye koo/ndugu zao halafu duka linakufa.
 
Halafu anaibuka mwanamke uzeeni na kudai mali yote kuwa aneachiwa yeye yaani hata watoto wa marehemu mama wasipate chochote.

Sheria zetu za ndoa na mirathi inabidi ziangaliwe upya, haiwezekani hawara wa uzeeni awe na haki na,mali za marehemu zilizochumwa tangu ujanani na wawili kisa tu naye anefunga ndoa na mwanaume huyo.

Walau sheria ingetamka nusu ya mali tu ndiyo zingeweza kuchukuliwa kuwa ni za mume ili kama urithi basi wanaomhusu wote wagawane hiyo nusu na nusu nyingine igawanywe kwa wanaomhusu mke wa ujanani.
 
Mercy Mengi na kadhia ya wenza wa matajiri

Mercy hakuwa mama wa nyumbani tu, hakulea familia tu, alikuwa mwanzilishi mwenza na mwenye mchango mkubwa wa tunachojua kama makampuni ya IPP. Huu ni wakati wa kuibua michango ya akina mama wa aina ya Mercy Anna Mengi.

Mwenyezi Mungu na azilaze mahali pema peponi roho za Reginald na Mercy- Mengi. Amina.

The End
Mkuu Ezekiel Kamwaga , asante sana kwa bandiko hili, huku ni kumtendea haki marehemu.

Mimi japo ni msoma vitabu mzuri, na kitabu cha I Can, I Must, I Will, kipo kwenye my home library, ila naomba kukiri sijakisoma, ila hadithi ya mchango wa Mercy kwenye utajiri wa Bilioneo Mengi, unasemwa tuu kwenye viunga vya Machame, kuna vitu vingine sisi wanaume tunasaidiwa na wake zetu enzi za mapenzi kabla ya kuona, havisemwi au vikijulikana ni aibu kwetu wanaume!.

Mtoto wa masikini unapopendwa na binti wa tajiri, binti wa Kichagga akipenda ni amependa!, binti ukiisha wathibitishia wazazi wake kuwa moyo wake umelalia pale hivyo uko tayari kuolewa na mtoto wa masikini, wazazi wa binti watahakikisha wanamuwezesha binti akusaidie ili usimame na kuweza kumtunza binti yao kwenye ndoa yenu!.

Huko moshi kuna story ya mtoto tajiri, baba yake alikuwa Chief, akampenda mtoto wa masikini tangu shule!, from then mtoto wa masikini huyo aliishia la 7, ila tajiri huyu alumlipia ada ya sekondari ya kulipia, akawezeshwa hadi kwenda nje ya nchi, si wengi wanaojua kuwa zile scholarship za watoto wa machifu kwenda kusoma UK, ziliendelea hata baada ya Uhuru!. Hivyo chief aka-facilitate mtoto wa masikini apate, akapata akaenda UK, aliporejea ndipo akapewa binti tajiri, tena sijui kama mahari alilipa au alilipiwa!, la sherehe ya harusi ilibebwa na Chifu!.

Mimi pia kwenye maisha yangu nilipitia mumo humu, ile TSJ yule binti ni mtoto wa Tajiri wa Sanya Juu!, zile ponda raha zote za TSJ ni mfuko wa binti!. Ile harusi ya kifahari, honeymoon London, kuhamia US, yote ni familia ya binti!. Tofauti yangu na Mengi, yeye alikuwa Mchagga pesa ndio kila kitu, lakini mimi Msukuma, kuponda raha ndio ilikuwa kila kitu!.

Bandiko hili ndio limenifungua macho kumbe the gap between the demise of husband and wife ni 6 months only!. Then hoja za bandiko hili Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata! could be true!.
P
 
Back
Top Bottom