Sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010

MMM,

Kutaka Kikwete asigombee si ni KINYUME cha "UTARATIBU" wetu CCM? Au?

Mkuu,

Sidhani kama kuna mtu ambaye amemilikishwa uongozi wa maisha nchini kwetu,hivyo basi kila mtu anayo haki kabisa kikatiba kugombea nafasi yeyote ile kwenye uchaguzi ili mradi tu awe ametimiza minimum requirements.Huwezi ukanishawishi kuwa hata kama mtu amechemsha kipindi chake cha uongozi,apewe tu 'eti' kwa sababu 'UTARATIBU' ni kuwa lazima vipindi viwili(2) amalize.Tukifuata misingi hii tutaendelea kujenga taifa lisilo na misingi imara.Tukubali kuwa demokrasia ya kweli ni kukubali pia kupingwa.Usipokubali haya basi hautokuwa tofauti sana na dikteta.Kuna nini cha kuogopa mpaka tusikubali wagombea wengine?Kama kweli mtu yupo makini na rekodi yake ni nzuri(kwa kulinganisha mafanikio aliyoyapata kwenye kipindi chake cha kwanza na ahadi alizozitoa)then atadhibitisha kwenye kinyang'anyiro na siyo kukubali tu matokeo kuwa aendelee.

Kuendesha vyama kidikteta sio pia demokrasia.Kwani demokrasia inaanzia ndani na kuonekana nje.Kama ndani ya chama ndio kama haya,unategemea kweli nje mtu ataonekana anahubiri demokrasia?Hapa itakuwa ni kujidanganya na kudanganya wananchi.Kila mtu ana mtizamo wake na he/she is entitled to it.Kila mtu basi yupo responsible kutetea mtizamo wake kwa kutoa maelezo anayoona yana-support huo mtizamo.

Tusijenge tena msingi wa matope tena tukitegemea kuwa kesho utakuwa wa saruji!

Nawasilisha.
 
Sisi tumejiwekea utaratibu ndani ya cham na si katiba,Rais ambaye ni mwenyekiti wa Cham ndiye atakuwa mgombea pekee ili amalizie yale yalibaki na yatakayokuwepo kwenye 2010-15 CCM manifesto

Wenye Chama mnatuletea mtu safi - another 'Mr. Clean'?

Kutaka Kikwete asigombee si ni KINYUME cha "UTARATIBU" wetu CCM? Au?






Ni kweli kumwachia rais aliye madarakani kipindi kingine cha miaka 5 ndio utaratibu uliotumiwa na CCM kwa Mzee Rukhsa na Mkapa. Lakini hii sio sheria wala katiba ya CCM. Ila zipo sababu zilizowafanya wakapewa hiyo ridhia.
  1. Mzee Mwinyi aliweza kuiunganisha nchi kwa amani baada ya Mwalimu kuondoka madarakani. Pia aliweza kuifungua nchi kwenye soko huria ingawa iliingiza na tusiyoyapenda, rushwa ya wazi kwa viongozi.
  2. Mkapa alianza vema kwa kujenga insititution za uongozi na kuweka misingi ya maendeleo. Pia kipindi chake cha kwanza kabla ya Mwalimu kufariki, rushwa kwa viongozi ilikuwa nadra. Ingawa miaka 5 iliyofuatia bado alifanya kazi nzuri, lakini kulikuwa na mapungufu mengi.
  3. JK zaidi ya kutalii ulimwengu wote , fanikio lake pekee ninaloliona lingekua kumleta Maximo. Lakini nalo pia ni wazi kachemsha. Chini ya uongozi wake wa miaka 4 na ushee;
    • Umasikini umeongezeka,
    • Elimu imezidi kuwa duni,
    • Umeme aliokuta una matatizo umezidi kuwa mahututi,
    • Viongozi wake wamekuwa na utendaji mmbovu lakini wote wameweza kujilimbikizia utajiri,
    • Ameshindwa kushurutisha watendaji wake kuwashughulikia mafisadi
    • Mwelekeo wa maendeleo ya nchi haueleweki n.k, n.k.
Kwa hiyo JK hana sababu yoyote inayomfanya aombe kuruhusiwa kuendelea kuongoza nchi. Akijiuzulu hivi sasa ingekuwa nafuu kubwa kwa nchi.

Nakubalina 100% na MMJJ kuwa, kumpigia debe JK sio uzalendo.
 
Ukweli wenyewe JK has not done that bad in his first term. Yeah najua wengi tayari mnaguna. Ni raisi wa kwanza wa Tanzania ambae ame jaribu kuleta demokrasia yenye ukweli kwenye kipindi chake.

Tuna demokrasia ambayo ni changa na inachukua mkondo wake kwa namna moja au nyingine magazetini, mtandaoni na hata uraiani. Ingawa ni demokrasia ambayo bado ina tinted glass lakini imesaidia kuleta maendeleo fulani, kuwahamsha watu fulani na kufanya baadhi ya watanzania waweke hata sikio moja kwenye Siasa za nyumbani ni mwamko huo. Ambao unatokana na demokrasia leo hii mabomu mengi wanayo yamwaga wana JF humu ndani tunayachangia kwa matusi na kuwa-simulia hata wasiokuja humu, na wao kuchukizwa na matendo ya viongozi ni mwanzo huo.

Hivyo hii ni hatua muhimu kwetu na ni ya kumpongeza JK. Vile vile amejaribu kuwafanya viongozi wa mali za Umma wa ngazi za kati kufikiria mara mbili michezo ya fauli. Mfano ni jinsi alivyodili na baadhi ya laana ambazo zilianza na Mwinyi na kudekezwa na Mkapa, Ujambazi wa kutupwa na majambazi yalioukuwa yanaona kama kupora ni legitimate career au majambazi ya Benki ambayo assets za Benki walikua wakiziona kama mali zao. Mfano wa karibu na Liyumba na bwana Zombe hawa ni products wa awamu zilizopita.

Ndio kuna mapungufu mengi lakini JK unaweza sema ametuanzishia safari yenyewe, bado kuna mapungufu ambayo yamejijenga kwa zaidi ya miaka ishirini kwa sasa, ambayo ni muhimu tuyamalize kama hayo ya makundi Mzee MKJJ anayoyasema.

Kwani si Makundi tu bali ndio balaa lenyewe letu, lilipo hapo. Kila kundi lina nia ya kutumaliza kama hawa wa sasa wanavyotumaliza, kwa namna ya kusajili mikataba mibovu, kujilimbikizia assets za taifa na sasa mpaka kurithishana madaraka as if tunaishi kwenye Kingdom fulani hivi.

Hivyo alitukua jambo la busara kumnada kiongozi asie jinada. Ni lazima mwenye nia kuongoza nchi aje na ajitambulishe akaguliwe mapema sifa zake kabla atujaanza kumpigia debe. Vinginevyo tutajikuta tunaleta kiongozi ambae anaturudishia akina Zombe wengine. Wakati ni hatua ambayo tunataka kuifuta ktk historia yetu.

Ni kweli JK ametuangusha na ahadi zake nyingi, lakini tunasikia kutoka kwa takuruku kuna kesi kazaa uko jamaa wanazikwamisha. Mi naona JK has done phase one kuleta kitu muhimu scrutany, considering the context of our political history before he got into office ni mafanikio kutupa kiji sauti fulani ingawa ni kichanga. Phase ya pili iwe kujipunguzia madaraka au majukumu na kugawa sheria kihalali ili kuwe amna mwenye uwezo wa kulindwa na hilo ndio kongamano tunalolisiburi.
 
Mengi umesema ukweli na mengi hayana msingi....Ni vigezo gani hivyo umevitumia kusema kuwa safari zilizopita urais ulikwenda kwa mgombea kwa kustahili tofauti na huo unaodai alishinda kwa kuuza sura?Wakati wa Mr Clean?Mwinyi?

Kwanza si kweli kuwa JK alichaguliwa kutokana na sura ama tabasam,JK amechaguliwa(urais) kwasababu yeye ni CCM period,kama kuna waliompigia kura kwasababu ya sura ama tabasam,basi hiyo first inaweza kuwa percent ndogo sana,secondly kama hicho kilikuwa ni kigezo,basi kilikuwa ni kigezo cha wana CCM hao wakati wa uteuzi wa mgombea urais kupitia chama chao na certainly siyo kigezo cha kwanza vs kile cha uana CCM pale inapokuja kwenye kura za urais,mbona Mkapa na sura yake ya ajabu ajabu alichaguliwa?Tena kipindi chenye upinzani mkubwa?Unataka kusema tabasam lake lilizidi la Mzee wa kiraracha?lol!

Kama issue kweli ni kuuza sura na tabasam,kwanini wapinzani wasitafute mgombea urais mwenye sifa hizo kumzidi JK?

Naelewa ni kweli tuna hamu sana ya mabadiliko na kwahiyo we want change in any means or form.

Hivyo mwishoni nakubaliana kuwa ukijiweka kwenye viatu vya mwana ccm,basi inawezekana kuwa JK alipitishwa kwasababu ya sura na tabasam,lakini kwenye uchaguzi wa urais,JK alishinda kwasababu kura za CCM zilizidi za upinzani...Hivo unaweza kuona picha kwamba mabadiliko ya kweli yaje vipi.

Usiwe na uhakika sana. Mimi nina wasichana wenzangu kama watano hivi ambao tulimpigia kura Kikwete kwa ajili ya kuipenda sura yake! He is handsome kusema ule ukweli!!
 
Ni kweli kumwachia rais aliye madarakani kipindi kingine cha miaka 5 ndio utaratibu uliotumiwa na CCM kwa Mzee Rukhsa na Mkapa. Lakini hii sio sheria wala katiba ya CCM. Ila zipo sababu zilizowafanya wakapewa hiyo ridhia.
  1. Mzee Mwinyi aliweza kuiunganisha nchi kwa amani baada ya Mwalimu kuondoka madarakani. Pia aliweza kuifungua nchi kwenye soko huria ingawa iliingiza na tusiyoyapenda, rushwa ya wazi kwa viongozi.
  2. Mkapa alianza vema kwa kujenga insititution za uongozi na kuweka misingi ya maendeleo. Pia kipindi chake cha kwanza kabla ya Mwalimu kufariki, rushwa kwa viongozi ilikuwa nadra. Ingawa miaka 5 iliyofuatia bado alifanya kazi nzuri, lakini kulikuwa na mapungufu mengi.
  3. JK zaidi ya kutalii ulimwengu wote , fanikio lake pekee ninaloliona lingekua kumleta Maximo. Lakini nalo pia ni wazi kachemsha. Chini ya uongozi wake wa miaka 4 na ushee;
    • Umasikini umeongezeka,
    • Elimu imezidi kuwa duni,
    • Umeme aliokuta una matatizo umezidi kuwa mahututi,
    • Viongozi wake wamekuwa na utendaji mmbovu lakini wote wameweza kujilimbikizia utajiri,
    • Ameshindwa kushurutisha watendaji wake kuwashughulikia mafisadi
    • Mwelekeo wa maendeleo ya nchi haueleweki n.k, n.k.
Kwa hiyo JK hana sababu yoyote inayomfanya aombe kuruhusiwa kuendelea kuongoza nchi. Akijiuzulu hivi sasa ingekuwa nafuu kubwa kwa nchi.

Nakubalina 100% na MMJJ kuwa, kumpigia debe JK sio uzalendo.
Nipe sababu moja tu kwamba kumpigia debe JK siyo uzalendo bali kuipigia debe CCM ni uzalendo....Sababu moja tu, ili niweze kupambanua vigezo mnavyotumia magreat thinker kuhusiana na upi ni uamuzi sahihi kati ya kuipigia debe CCM vs JK,hapo ndio uonevu unapojitokeza....Shida hapa ni kwamba,mnaupima ufanisi wa JK kwa kutumia vigezo vya mafanikio ya kitaifa kama maendeleo ya wananchi nk, na wakati huo huo mnatumia vigezo vya kichama wakati wa uamuzi wa either apigiwe debe ama la.
Tatizo mmesahahu kwamba ufanisi kwa maendeleo ya Taifa si kigezo cha kuchaguliwa kwa tiketi ya CCM,Hilo halipo na tuache unafiki,hakuna kiongozi utakayesema ni mzalendo wa kweli amewahi kupitishwa na ccm....Kigezo cha kuchaguliwa kwa tiketi ya CCM si uzalendo msi mix issues hapa.
 
Usiwe na uhakika sana. Mimi nina wasichana wenzangu kama watano hivi ambao tulimpigia kura Kikwete kwa ajili ya kuipenda sura yake! He is handsome kusema ule ukweli!!

Kwa hiyo una maana kwamba wewe si mwana CCM lakini uliamuwa kumpigia kura mwana ccm kwasababu ya sura?
 
Usiwe na uhakika sana. Mimi nina wasichana wenzangu kama watano hivi ambao tulimpigia kura Kikwete kwa ajili ya kuipenda sura yake! He is handsome kusema ule ukweli!!

Kwa hiyo nyie mliochagua sura yake inaelekea mlipata kweli ingawa hujasema kama katika miaka minne ya uongozi wake mlifanikiwa kupata mgao wenu, ila siye tuliotaka kiongozi tuliliwa ile mbaya.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna watu wanajaribu kuwafanya wengine wajisikie vibaya wanapotoa mawazo yao kuwa Rais Kikwete afikirie adhma yake ya kugombea ngwe ya pili. Wanajaribu kuwafanya watu wajisikie kama wasaliti au waonevu wanapotoa mawazo kuwa Taifa letu linahitaji uongozi mpya kabisa mwakani na siyo wa Rais Kikwete. Ukweli ni kuwa watu wengi wanampenda Kikwete kama mtu binafsi; ana sura nzuri, sauti nzuri, tabasamu n.k n.k lakini linapokuja suala la uongozi wapo wanaoona kuwa ana mapungufu makubwa mno kiasi kwamba kumpa nafasi nyingine mwakani ni kuendeleza kile ambacho tayari kimeshaonekana miaka hii minne.

Tunapoelekea mwaka huu mpya ambao ni mwaka wa uchaguzi kambi za "kikwete agombee" na "Kikwete asigombee" zitazidi kuibuka na kwa mara ya kwanza tutashuhudia mgongano wa wazi kati ya kambi hizi. Tatizo kubwa ni la wale ambao wanaamini kuwa kutaka Rais aliyemadarakani asigombee tena ni sawa na uhaini na kumtaka afikirie kutokugombea ni sawa na kumsaliti.



Hii si kweli. Rais wa Tanzania anachaguliwa kwa kipindi kimoja tu na akitaka nafasi nyingine basi anapitia mchakato ule ule na hawezi kutawala kwa vipindi zaidi ya viwili. Katiba haisemi kuwa vipindi hivyo viwili ni lazima viwe vimefuatana. Kutokana na ukweli huu ni lazima watu wakubali kuwa utawala wa demokrasia una gharama yake na gharama mojawapo kubwa ni wananchi kuweza kumkataa kiongozi wao na hata kutaka asigombee!



Lakini wazo hili ni gumu kwa watu ambao wanaongozwa na ushabiki wa mtu; watu ambao wanaona kuwa Kikwete ame"fika" hapo kwenye Urais na mtu yeyote anayetoa mawazo kuwa asigombee au hana sababu ya kutosha kugombea tena basi ni kama mhaini; tumewasikia watu wazima na ambao ni wanasiasa wakongwe wakianza kutukuza huu ubia wa Bw. Kikwete na Urais wa Tanzania.

Wanataka kumfanya Kikwete kuwa ni mfalme na kuwa yeyote atakayejitokeza kupingana naye basi ni msaliti wa aina fulani au mhaini. Haya ni mawazo potofu. Kama watu hawa wanataka Kikwete agombee milele na kuwa hakuna mtu mwingine yeyote mwenye uwezo kumzidi basi wajitokeze hadharani na wabadili Katiba ili wamtangaze Kikwete kuwa ni Rais wa Maisha na sisi wengine tutakaa kimya (kwenye njozi zao).



Mwaka 2005 kinyume na inavyosemwa Kikwete hakupitia kwenye tanuru ya moto; hakuwa na rekodi ya kusimamia lakini safari hii bila ya shaka tunayo rekodi yake ya kutosha na tunaweza kumpima kwa kile alichokifanya kama Rais. Na ni kipimo hicho tu ndicho ambacho kitatuamulia kama ana sababu ya kugombea tena au tutafute mtu mwingine.

Safari hii Kikwete kama anataka kuwa Rais wetu tena itabidi ajibithibitishe kwa kufanya midahalo na wagombea wengine, kusimamia rekodi yake na kujibu hoja zitakazotolewa dhidi yake. Safari hii Urais hauji kwa kuuza jina, sura, au tabasamu; safari urais utakuja kwa kuustahili.

Na wana CCM ambao wanaona Rais Kikwete hawezi kuwa chaguo lao wasijisikie vibaya wala kujiona kama wanasaliti chama; watambue kuwa wana wito mkubwa zaidi na sababu kubwa zaidi na kama wanaona kuwa Bw. Kikwete anahatarisha hata maslahi ya Chama basi ni jukumu lao kutokumpendekeza na yeye kama Mkapa atakaa pembeni na kula pensheni yake na kuendelea kufurahia ving'ora na saluti za hapa na pale. Kama Gen. Powell aliweza kumuunga mkono Obama wakati yeye ni Republican na mtu aliyefanya kazi na marais wa Republican kama Reagan, Bush na GW Bush basi mwana CCM yeyote anaweza naye kumpendekeza mtu mwingine zaidi ya Kikwete.



Kwa upande wetu tutaendelea Jumatano hii kwenye gazeti la Mwanahalisi na fungu la pili la sababu 51 za kwanini Rais Kikwete asigombee. Ni matarajio yetu kuendelea kuwakera watu wachache na kuwaudhi wengi.

Kupinga ngwe ya pili kwa JK si uhaini -kweli kabisa lakini toa ufafanuzi kwanza hakuna mwenye ubavu wa kupinga hilo kwakuwa kila mtanzania ana haki ya kugombea nafasi hiyo wakati tume itakapotangaza kwamba iko vacant kupitia chama cha siasa kilichosajiliwa...JK anayo haki hiyo kama mwanachama mwingine wa CCM, briefly hakuna mwenye haki ya kikatiba kumpinga JK asigombee ila wanachama wa CCM wataamua kumpitisha JK au wataamua kumpitisha mwingine kwa utaratibu wao....

Kumpigia debe si Uzalendo ...duh! hapo ndiko ulikochemsha uzalendo ni nini? unapimaje uzalendo? unafikiri kwamba wewe unayepigia debe asichaguliwe ni mzalendo zaidi kuliko yule ambaye anampigia debe achaguliwe? unataka kufikiri wewe na kundi lako mna haki zaidi kuliko wengine wanaompigia debe?

wewe toa sababu zako za kutompigia debe 51 na waache wengine watoe sababu zao za kumpigia debe JK..wote nyinyi ni wazalendo na mwamuzi ni "wapiga kura" kupitia uchaguzi huu ndio ustaarabu wa nchi yetu..labda kama unataka ustaarabu wa madagascar! ala

Lakini kujibatiza kwamba wewe na kundi lako linalopinga kumpigia debe JK ni wazalendo zaidi kuliko wale wanaompigia debe JK ni udikteta na ujinga ambao hautapita hivi hivi bila kupingwa..
 
kIKWETE ajiulize mwenyewe kama bado ana nguvu zinazostahili kuhimili vishindo vya miaka mingine mitano.Kwa vyovyote vile, kuna mengi ambayo hayaturidhishi walio wengi na naona kama vile hayaoni kama ni tatizo kwa uongozi wake.Ingekuwa mimi ningeenda kufanya retreat na kutafakari kama bado ni sawa kuendelea kugombea uongozi wa nchi
 
Nitaomba sana ufanyike mdahalo na wana ccm wenzake wataoomba kugombea...wasimuone kama mfalme maana akirudi kugombea anatakiwa awe mnyenyekevu na kufuata sheria...(Utaratibu) sasa wapambanishwe na waombaji wengine tuone nguvu ya hoja na demokrasia ichukue mkondo wake...ila tu isiwe ni mazoea na kuja kulipizana visasi na kujenga chuki!!iwe demokrasia ya kweli....hayo maturity yake anayosofiwa nayo aiweze ku practise!!
 
Hivi ni nani haswa tunayetaka achukue nafasi ya Kikwete? Nakubali kabisa Kikwete ana upungufu wake mkubwa tu. Lakini siko tayari kuona nchi inarudi enzi zile za kina Mkapa! Au hata za Mwinyi!

Kama kuna kitu kinachonivutia mimi ni jinsi Tanzania inavyokuwa kidemokrasia. Kwa mara ya kwanza sasa tutaona upinzani ukichukua dola Zanzibar. Hii ni kwa sababu haitawezekana tena masanduku ya kura kupelekwa kwa wakuu wa wilaya kuhesabiwa na watu kuuwawa wanapojaribu kuzuia hilo na kutetea haki yao ya kidemokrasia.

Na kwa mara ya kwanza sasa kama kina Zitto watatulia na kujenga upinzani imara tutaona wabunge zaidi ya 100 wa upinzani bungeni. Na ni kwa mara ya kwanza pia katika historia ya Tz tumeona na tutazidi kuona jinsi wabunge wa ccm na spika wao wanavyowaumbua mawaziri na viongozi wa chama chao.

Hivi mnataka nini zaidi ya hapo jamani? Au mnataka JamiiForum ifungiwe kwa kusema Rais wa TZ anauza sura na kucheka cheka hovyo ndio tuamini kwamba JK sio dhaifu? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni jamani!

Give me a break!
 
Kikwete kuendelea kutawala (siyo kuongoza) kwa miaka mingine mitano ni kukaribisha maafa kwa taifa letu. Kipindi cha kwanza ambacho anahitaji kuungwa mkono kupata kipindi kingine ameharibu kiasi hiki na kuicha nchi mikononi mwa mafisadi huku yeye akipasua anga kutalii ughaibuni je kipindi kingine ambacho hahitaji tena kura zetu si ataiteketeza kabisa nchi? Hebu tuache ushabiki wa kijinga katika jambo nyeti kama hili . Huyu mtu hafai kupewa nafasi nyingine hao wanaoshabikia ni wachumia tumbo tu. Tanzania ni yetu sote
 
Hata kidogo; utaratibu wa kumpata mgombea wa CCM utafanyika kama vile ni mara ya kwanza; mwana CCM yoyote ambaye anaamini ana uwezo wa kuliongoza Taifa letu atajitokeza na kuchukua fomu na kufuata mchakato ule ule. Hadi hivi sasa JK inaonekana ameshapigiwa debe na viongozi wetu; lakini miezi michache ijayo atapata upinzani wa kihistoria na mwamko huo utakapoiva atakuja na sababu ya kwanini asigombee kama nilivyodokeza karibu miezi kadhaa iliyopita.

Tunamshukuru kwa utumishi wake lakini naamini hatokuwa na kinyongo pale ambapo mtu mwingine atapitishwa badala yake.

Nani atakayempitisha huyo 'mtu mwingine'? Vikao vyote vya mchakato wa kupata mgombea wa urais vinaongozwa na mwenyekiti ambaye ni JK. Sijawahi kuona wala kusikia mtu akiongoza kikao cha kujifuta kwenye mchakato. Na hata kama ataongoza mwingine vikao hivyo, kuna usemi wetu wa kiswahili kuwa 'meno ya mbwa hayaumani', tumeyaona Zimbabwe na Uganda, na hata Tanzania katika lile suala la 'kumwacha mzee wetu Mkapa apumzike' bila bughudha.
 
Wenye Chama mnatuletea mtu safi - another 'Mr. Clean'?

Mimi nadhani mtu safi tuu haitoshi! Tunataka awe pia ni competent in leadership. Awe imara na mwenye kufanya maamuzi muhimu na yenye tija kwa taifa na si chama ama wachache.
 
Nilisema mwanzoni kuwa mtu anaweza kuwa safi kwa sababu hajawahi kuwa karibu na uchafu; na mtu mwingine anaweza kuwa safi kwa sababu aliuondoa uchafu..
 
Je uchaguzi utafanyika ilhali kuna kesi ya msingi mahakamani?? (waliyoifungua NCCR-Mageuzi kudai tume huru ya uchaguzi)
Jamaa atatumia mwanya huo kupeta bila kura zenu
 
Hivi ni nani haswa tunayetaka achukue nafasi ya Kikwete? Nakubali kabisa Kikwete ana upungufu wake mkubwa tu. Lakini siko tayari kuona nchi inarudi enzi zile za kina Mkapa! Au hata za Mwinyi!

Kama kuna kitu kinachonivutia mimi ni jinsi Tanzania inavyokuwa kidemokrasia. Kwa mara ya kwanza sasa tutaona upinzani ukichukua dola Zanzibar. Hii ni kwa sababu haitawezekana tena masanduku ya kura kupelekwa kwa wakuu wa wilaya kuhesabiwa na watu kuuwawa wanapojaribu kuzuia hilo na kutetea haki yao ya kidemokrasia.

Na kwa mara ya kwanza sasa kama kina Zitto watatulia na kujenga upinzani imara tutaona wabunge zaidi ya 100 wa upinzani bungeni. Na ni kwa mara ya kwanza pia katika historia ya Tz tumeona na tutazidi kuona jinsi wabunge wa ccm na spika wao wanavyowaumbua mawaziri na viongozi wa chama chao.

Hivi mnataka nini zaidi ya hapo jamani? Au mnataka JamiiForum ifungiwe kwa kusema Rais wa TZ anauza sura na kucheka cheka hovyo ndio tuamini kwamba JK sio dhaifu? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni jamani!

Give me a break!


Kwa hiyo udhaifu wake unaweza kugeuka kuwa faida kwa Taifa!!!!
 
Back
Top Bottom