Sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Baada ya kutafakari sana, nimepata sababu 51 za kwanini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi aamue kutoshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani. Ninajua kwamba ni "mtaji" kwa upande wa kina Makamba na vile vile ana "sura nzuri" na bla bla bla..

Sasa kati ya hizo 51 nitaanza na zile mbili za mwisho yaani ya 50 na 51. Bila ya shaka na wewe unaweza kuwa na za kwako.. hivyo nawakaribisha wale ambao wanaweza kukisikia au kuchangia sababu zile nyingine 49!

51: Alisema kuwa akichaguliwa tena ataleta vijana na kuwa watu wa rika "lake" waanze kuachia ngazi. Well, kwa vile yuko rika moja nao basi na yeye aungane nao!

50: Hajui kwanini Tanzania ni maskini licha ya kuwa kwenye utumishi wa serikali kwa karibu miaka 30 sasa! Kiongozi asiyejua chanzo cha tatizo ataweza vipi kuliondoa isipokuwa kuziba tu dalili zake.

49: Aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Ahadi hii haionekani kutekelezeka. Inaonekana ametimiza ahadi ya maisha bora kwa kila muwekezaji wa kigeni!

48:Alitangaza kuwa wizi umefanyika Benki Kuu kwa kukombwa mabilioni; badala ya kuacha uchunguzi wa jinai akaunda Kamati kuchunguza jinai. Matokeo yake ni kucheleweshwa kwa upatikanaji wa haki.

47: Serikali yake imeshindwa kutekeleza maazimio yote ya wananchi wa Tanzania kama yalivyoanishwa na wawakilishi wao Bungeni katika maazimio kufuatia Kamati Teule ya Kuchunguza Richmond. Matokeo yake ni kuchochea mgawanyiko mkubwa kabisa wa kimaslahi katika historia ya taifa letu.

46: Aliahidi kupitia mikataba yote mikubwa ya madini ili kutengeneza hali ya "win win win". Hadi hivi sasa hakuna mkataba hata mmoja uliopitiwa na kusahihishwa na badala yake serikali yake imetangaza kuwa mabadiliko ya sheria ya madini yataendelea kuwanufaisha wawekezaji wa sekta hiyo.

45: Akiwa ni Mwenyekiti wa Chama Tawala ameshindwa kuleta nidhamu ndani ya chama na matokeo yake wanachama wake mashuhuru wanatukanana na kuitana majina hadharani. Kile kilichoitofautisha CCM miaka ya nyuma sasa hakipo tena.

44: Aligawa fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa kile kilichojulikana kama "mabilioni ya Kikwete" Hadi hivi sasa haijaoneshwa ni kiasi fedha hizo zimeweza kubadilisha maisha ya waliozipata na kurudisha faida.

43: Aliahidi kuunda Baraza dogo la Mawaziri lakini matokeo yake Baraza lake limekuwa kubwa na lenye ufanisi mdogo.

42: Alidai hadharani kuwa anawajua vigogo wa kuuza madawa ya kulevya na kuwa amewapa muda wajirekebishe. Miaka minne baadaye hajatuambia kama watu wale wamejirekebisha au la.

41: Aliahidi kuwa hakuna mwanafunzi wa Kitanzania anayehitaji elimu ya juu ambaye atashindwa kuipata. Lakini serikali yake iliwarudisha vijana wa Kitanzania waliokuwa wanasomea shahada mbalimbali ikiwemo Uhandisi na Udaktari kutoka Ukraine kwa kudai kuwa serikali haina fedha. Vijana wale 30 ingewagharimu shilingi milioni 400 tu kwa muda wa miaka minne. Kiasi hicho ni sawa na kiasi kilichochangwa na serikali kuipongeza Taifa Stars kwa kuifunga Togo!

40: Amewaruhusu watendaji wake wakubwa kutumia vyeti vya kielemu ambavyo havitambuliki na vyenye utata. Miongoni mwao ni Waziri wa Fedha Bw. Mustafa Mkullo na Naibu Waziri wa Ulinzi na JKT Bw. Emmanuel Nchimbi.

39: Licha ya kuahidi kutatua tatizo la nishati chini ya uongozi wake Tanzania imezidi kukabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kuliko wakati mwingine wowote huku nchi yetu ikiwa na vyanzo vya kutosha kabisa nishati hiyo ambayo serikali yake imeshindwa kuviendeleza.

38: Amekuwa akiendeleza safari za nje yeye na viongozi wa ngazi za juu ambazo zimegharimu zaidi mabilioni ya shilingi kwa safari, posho, matumizi ambayo hataki kuyaweka hadharani.

37: Ameendeleza fikra za uduni wa Mtanzania kwa kutukuza wageni na hivyo kuendeleza kuhukumu taifa letu kwenye utegemezi wa kudumu kwa kupokea misaada ya kiudhalilishaji ya mambo ambayo yamo ndani ya uwezo wa kuzaliwa wa Watanzania.

36: Serikali yake imeendelea kuwaficha wananchi wa Tanzania mambo muhimu yanayohusu serikali yao na hivyo kuwanyang'anya wananchi usimamizi wa serikali yao kwa kuficha mambo ya Meremeta, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, na Tangold.

35: Akionesha kutokujali sifa za watendaji wake amewateua watu mbalimbali wenye utata wa maadili, na elimu na kuwapa nafasi za kuongoza wizara, na idara nyeti. Miongoni mwao:

- Mustaffa Mkullo - Waziri wa Fedha
- Emmanuel Nchimbi - Naibu Waziri wa Ulinzi na JKT
- Andrew Chenge - Alikuwa Waziri wa Miundombinu
- Peter Noni - aliyesimamia akaunti ya EPA ikichotwa na sasa kapewa Benki ya Raslimali (TIB)
- n.k

34: Serikali chini yake imevumilia vitendo vya uharibifu mkubwa wa mazingira na hata kutishia maisha kama yale yaliyotokea huko mgodi wa Mara ambapo watu wamerudhika kutokana na sumu inayotoka mgodini.

33: Alitangaza kwa wananchi kuwa msukosuko wa kiuchumi uliokumba dunia usingeleta matatizo ya kiuchumi kwa Tanzania; miezi michache baadaye serikali yake ikaidhinisha zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya "kusisimua" uchumi bila kuweka utaratibu wowote wa kupima mpango huo na kuonesha kitaalamu haja ya mpango huo zaidi ya kuongeza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali.

32: Ameshindwa kuliongoza Taifa kwa misingi ya Ujamaa ambayo imeanishwa katika Katiba ya Jamhuri na Katiba ya Chama chake na hivyo kuendelea kufanya kazi na kuendesha serikali kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuihifadhi.

31: Licha ya kupigiwa kelele dhidi ya uwekezaji wa kampuni ya India ya Rites Consortium kwenye shirika letu la Reli, aliendelea na kuhakikisha wanawapa mkataba huo. Matokeo yake ni yale yale tuliyoyaona wakati wa Mkapa; mwekezaji kashindwa na anaondoka tajiri!

30: Licha ya kubuni na kuhubiri juu ya umuhimu wa Kilimo, ameshindwa kuiongoza CCM kama chama na jumuiya zake kuwekeza katika kilimo kikubwa cha mfano kama chanzo cha mapato endelevu.

29:Kama ilivyokuwa kwenye sakata la Richmond, serikali yake imeingia mkataba na kufanya kazi na kampuni ya kitapeli ya Dowans ambayo iliingia nchini kinyemela na kuhalalishwa kwa kutumia maelezo ya uongo. Hadi hivi sasa hajakubali kuanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo.
 
49. Anachagua viongozi kiuswahiba. 48. Ameshindwa kuwaajibisha mafisadi 47. Ameahidi uongo "maisha bora kwa kila mtanzania" 46. Anawatumikia watu wa nje ya nchi yake badala ya kuwatumikia wananchi ndiyo maana anasafiri nje ya nchi mara kwa mara
 
Baada ya kutafakari sana, nimepata sababu 51 za kwanini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi aamue kutoshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani. Ninajua kwamba ni "mtaji" kwa upande wa kina Makamba na vile vile ana "sura nzuri" na bla bla bla..

Sasa kati ya hizo 51 nitaanza na zile mbili za mwisho yaani ya 50 na 51. Bila ya shaka na wewe unaweza kuwa na za kwako.. hivyo nawakaribisha wale ambao wanaweza kukisikia au kuchangia sababu zile nyingine 49!

51: Alisema kuwa akichaguliwa tena ataleta vijana na kuwa watu wa rika "lake" waanze kuachia ngazi. Well, kwa vile yuko rika moja nao basi na yeye aungane nao!

50: Hajui kwanini Tanzania ni maskini licha ya kuwa kwenye utumishi wa serikali kwa karibu miaka 30 sasa! Kiongozi asiyejua chanzo cha tatizo ataweza vipi kuliondoa isipokuwa kuziba tu dalili zake.

Orodhesha watu 51 wanaofaa kuchaguliwa if JK steps down...!!!
 
45 Kupitia katibu wake alitangaza kwamba makampuni 13 yalikuwa yameiba pesa za epa kijinai lakini bila kutarajia JINAI ikaundiwa tume kupoteza umda.
44. Hotuba yake bungeni alitueleza kwamba account ya EPA ilikuwa na kiasi cha billion 260 sasa baada ya kuibiwa Bl.133 hakutuweka.wazi ziliko zilizobaki bila kuibiwa.
43: ameshindwa kutekeleza maazimio 23 ya bunge hivyo kusababisha wahalifu waliotuhumiwa kuleta vurugu tunayoishughudia nchini sasa.
 
"Mungu humuumbua kila mwenye kuficha maradhi"
Iko siku hata wakoloni zilifika siku zao walifukuzwa; pia hata wao mafisadi wajiandae maana CCM na watumia bidhaa za mafisadi kama mtandao wa Voda wanawapa mafisadi nguvu na wanaendelea kufisadi zaidi. CCM na wanachama wake wote ni mafisadi.
 
Hivi yale mabilioni "ya Kikwete" yalitoka wapi, na yamerudisha kiasi gani kwenye mtaji? Yaweza kuwemo katika hizi sababu..
 
hana program mahususi ya kujenga uchumi, yaani nikimaanisha hana plan A,B and C. Yupoyupo bora liende.
 
Hivi yale mabilioni "ya Kikwete" yalitoka wapi, na yamerudisha kiasi gani kwenye mtaji? Yaweza kuwemo katika hizi sababu..
Mkapa aliacha fedha nyingi alivyotoka madarakani, na yeye JK alikiri hivyo, nakumbuka katika speech yake ya bunge kama sijakosea.
 
Orodhesha watu 51 wanaofaa kuchaguliwa if JK steps down...!!!

Kaka Vuta subira sababu 51 za JK kutoendelea zifahamike..then tunajadili nani anafaa. Tutakua ni "wehu" kujadili nani mbadala wa JK wakati hatujaweka wazi sababu za kutoendelea kwake.
 
Alizichezea fedha zilizobakia hazina bila maendeleo yoyote, mpaka sasa tumerudi square one.
 
Makamba ameshasema nyie wote mnaomkosoa Mh rais ni wehu na mna wivu kwikwikwikwikwi...
On a serious note Mzee Mwanakijiji, hivi kwa nini umeweka sababu 51 kwa nini isiwe 100.. ni chellenge nzuri lakini naomba muda nije kuweka sababu 50 niwaachie 50 zingine...
 
Kaka Vuta subira sababu 51 za JK kutoendelea zifahamike..then tunajadili nani anafaa. Tutakua ni "wehu" kujadili nani mbadala wa JK wakati hatujaweka wazi sababu za kutoendelea kwake.

hii inaitwa hekima! wabeja!
 
Makamba ameshasema nyie wote mnaomkosoa Mh rais ni wehu na mna wivu kwikwikwikwikwi...
On a serious note Mzee Mwanakijiji, hivi kwa nini umeweka sababu 51 kwa nini isiwe 100.. ni chellenge nzuri lakini naomba muda nije kuweka sababu 50 niwaachie 50 zingine...

sasa kama zinaweza kufikia zaidi ya 50 kwa kweli itabidi tu tumuombe asigombee tena.. kwa hiyo hakuna mipaka..
 
sasa kama zinaweza kufikia zaidi ya 50 kwa kweli itabidi tu tumuombe asigombee tena.. kwa hiyo hakuna mipaka..
hata hazihitajiki kufika hamsini, watu ni kufikiri kitu kidogo tu..toka 2005 mpaka leo kuna nini mtanzania anaweza akasema kafaidika au kaona impact ya utawala huu?.tumeona Obama kaja tu juzi unaona kaanza kuweka health care reforms na mambo mengine mengi. Kwa JK hakuna jipya nchi ipoipo tu.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom