Sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010

sasa kama zinaweza kufikia zaidi ya 50 kwa kweli itabidi tu tumuombe asigombee tena.. kwa hiyo hakuna mipaka..

4 years is a lot of madudu hehehe, think about the first 6 months only then do a linear assesment nakwambia itafika hata 200.....
 
Ingekua nchi nyingine ya bara la ulaya SURELY, JK hawezi kupata term ya pili. Test yangu kwa siasa ya TZ ni next year, hasa kwa CCM, kama wakimpitisha JK ntaamini kweli siasa za TZ bado, wasipo mpitisha JK ntaamini tumeanza kukomaa au tumekomaa tayari. Ila mpaka sasa study hypothesis yangu inaniambia watampitisha JK,though HASTAILI, so HATUJAKOMAA BADO KISIASA.
 
Baada ya kuingia madarakani December 2005 aliahidi umeme kutopanda, lakini by January 2006 Tanesco walitangaza ongezeko la bei la 21%.

Ameligeuza suala la umeme kuwa mradi wake wa kujinufaisha yeye na maswahiba wake tangia akiwa Waziri wa Nishati na Madini.
 
Baada ya kutafakari sana, nimepata sababu 51 za kwanini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi aamue kutoshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani. Ninajua kwamba ni "mtaji" kwa upande wa kina Makamba na vile vile ana "sura nzuri" na bla bla bla..

Sasa kati ya hizo 51 nitaanza na zile mbili za mwisho yaani ya 50 na 51. Bila ya shaka na wewe unaweza kuwa na za kwako.. hivyo nawakaribisha wale ambao wanaweza kukisikia au kuchangia sababu zile nyingine 49!


51: Alisema kuwa akichaguliwa tena ataleta vijana na kuwa watu wa rika "lake" waanze kuachia ngazi. Well, kwa vile yuko rika moja nao basi na yeye aungane nao!

50: Hajui kwanini Tanzania ni maskini licha ya kuwa kwenye utumishi wa serikali kwa karibu miaka 30 sasa! Kiongozi asiyejua chanzo cha tatizo ataweza vipi kuliondoa isipokuwa kuziba tu dalili zake.
Chaguo la Mungu hilo huwezi kucheza na mungu kwa hiyo inabidi uvumilie kwasababu askofu wako kasema hivyo au uko against maaskofu siku hizi?

Hii sababu ya 51 ondoa maana yeye atawaweka vijana sasa akiondoka nani atakayeweka?

Hii sababu ya 5o ondoa maana ume quote sentezi out of context" huwezi chambua jambo bila kujua alisema hivyo wakati gani, ndani ya maongezi gani etc..
 
Ila mpaka sasa study hypothesis yangu inaniambia watampitisha JK,though HASTAILI, so HATUJAKOMAA BADO KISIASA.

This is a risk CCM cannot take.
Kumpitisha Kikwete ni kuua chama machoni kwa watanzania.
CCM is corrupt alright,but not that ignorant.
 
45 Kupitia katibu wake alitangaza kwamba makampuni 13 yalikuwa yameiba pesa za epa kijinai lakini bila kutarajia JINAI ikaundiwa tume kupoteza umda.
44. Hotuba yake bungeni alitueleza kwamba account ya EPA ilikuwa na kiasi cha billion 260 sasa baada ya kuibiwa Bl.133 hakutuweka.wazi ziliko zilizobaki bila kuibiwa.
43: ameshindwa kutekeleza maazimio 23 ya bunge hivyo kusababisha wahalifu waliotuhumiwa kuleta vurugu tunayoishughudia nchini sasa.
Anayetekeleza maagizo ya bunge ni pinda nafikiri tumshauri asimchague hyo kilaza baada ya uchaguzi

Hotuba yake ya bunge hakuwahi kusema hicho unachosema acha uwongo wa mchana

tume zimuundwa ili watu wasije kushtakiwa na serikali bila uhakika na kushindwa mahakamani pamoja na mambo tume ilikuwa inatafuta vielelezo vinavyofaa kwa ajili ya ushahidi mahakama huwezi kwenda mahakamani kama kichaa..kama unavyo suggest wewe.
 
Chaguo la Mungu hilo huwezi kucheza na mungu kwa hiyo inabidi uvumilie kwasababu askofu wako kasema hivyo au uko against maaskofu siku hizi?

Hii sababu ya 51 ondoa maana yeye atawaweka vijana sasa akiondoka nani atakayeweka?

Hii sababu ya 5o ondoa maana ume quote sentezi out of context" huwezi chambua jambo bila kujua alisema hivyo wakati gani, ndani ya maongezi gani etc..

Mambo ya madrassa yanaharibu akili kweli kweli
 
.........Huyu mwakani CCM watamchagua tena kugombea urais, maana hadi afikishe miaka 10 ya utawala.
Kwa akili ya wapiga kura wa Tanzania wataichagua tu CCM hata kama Kikwete hakufanya vizuri katika kipindi hichi alichotawala.Tatizo asilimia kubwa ya wapiga kura wapo vijijini, na huko vijijini hao wanachojua ni CCM tu chama cha Nyerere.
 
42: Migomo ya wafanyakazi isiyokwisha na kupanda kwa gharama za maisha
Migomo ni dalili ya demokrasia na uhuru ambao ndio azma yake..ulifikiri watu hawakogoma zamani kwasababu gani kumbuke enzi zile makaburi walisindikizwa kwa polisi..uhuru ni haki yako migomo na maandamo yanaendelea duniani kote kila siku..labda ugeni wako katika demokrasia ndio tatizo.
 
tatizo sio kikwete, tatizo ni ccm. ling'olewe hili ccm na sera zake za naintiin kweusi.
 
Anayetekeleza maagizo ya bunge ni pinda nafikiri tumshauri asimchague hyo kilaza baada ya uchaguzi

Hotuba yake ya bunge hakuwahi kusema hicho unachosema acha uwongo wa mchana

tume zimuundwa ili watu wasije kushtakiwa na serikali bila uhakika na kushindwa mahakamani pamoja na mambo tume ilikuwa inatafuta vielelezo vinavyofaa kwa ajili ya ushahidi mahakama huwezi kwenda mahakamani kama kichaa..kama unavyo suggest wewe.

bwa ha ha ha...

Halafu inachekesha sana kumsoma anayejiita kuwa mpinzani na "mwanachama mwandamizi wa CUF" akitokwa mipovu kumtetea Kikwete.
 
Anawaogopa wamiliki wa Kagoda na aliingizwa kwenye uongozi kwa pesa Haramu
 
hilo ni somo jingine. Kwa ufupi ni kuwa haiitajiki watu 51 kumreplace JK.. anahitajika mmoja tu!

Huyo mmoja mhh!
1.Je, Kunayo succession plan for this? au ni kubahatisha tu halafu tuje tulalamike tena?
2.Tunadanganyika ni vitu ambavyo havina mchango mkubwa kwenye results mwisho wa siku.
3. Hata aje malaika kutawala.... itachukua miaka zaidi ya 200 kabla ya kuona mabadiliko ya kweli.
4.Tatizo liko kwenye mind-set na siyo vingine.Mindsets za viongozi na waongozi...kote ni problem.
 
Binafsi naona mjadala huu ni km kumpigia paka kengele. Nani anaubavu kutoka CCM kusimama na kumshinda kikwete kwa sasa. Woote waliopo katika madaraka ni wateule wake. Nani yupo tayari kuwa fired. Mie nadhani kupiga kelele Kikwete asigombee hakuna tija kwa sasa. Maana hakuna immediate successor in his presence. Mpaka kipindi chake kiishe.
Halafu pia why focusing on CCM? CCM wao wanamuona Kikwete ndio chaguo lao kwa sasa. Kwanini tuwasemee? Au na sisi ni CCM? Mengi ni CCM ndio maana alimsemea kwenye vyombo vyake vya habari kuwa anakubalika.
Kwahiyo mbadala wa Kikwete unatakiwa kusemwa na vyama vya upinzani kwa kusimamisha mgombea mwenye nguvu (km yupo) wa kumshinda Kikwete na hapio ndio dhana ya vyama vingi.
Otherwise uwepo wake utaamuliwa na CCM wenyewe hizi kelele nyingine kwa takwimu za Kikwete za asilimia 70% wanafuata upepo haziwezi kuleta mabadiliko katika kipindi kifupi.
 
hatuhitaji mtu safi; tunahitaji mwenye uwezo na aliyeonesha uwezo wa kutocheza kwenye uchafu.
Hii sentensi nakuomba uipitie tena na tuijadili. Haiwezekani kwamba unamaanisha hivi? Pls ufafanuzi kwa heshima zako otherwise edit.
 
Sisi tumejiwekea utaratibu ndani ya cham na si katiba,Rais ambaye ni mwenyekiti wa Cham ndiye atakuwa mgombea pekee ili amalizie yale yalibaki na yatakayokuwepo kwenye 2010-15 CCM manifesto
 
Mzee Mwanakijiji said:
Safari hii Kikwete kama anataka kuwa Rais wetu tena itabidi ajibithibitishe kwa kufanya midahalo na wagombea wengine, kusimamia rekodi yake na kujibu hoja zitakazotolewa dhidi yake. Safari hii Urais hauji kwa kuuza jina, sura, au tabasamu; safari urais utakuja kwa kuustahili.
Mengi umesema ukweli na mengi hayana msingi....Ni vigezo gani hivyo umevitumia kusema kuwa safari zilizopita urais ulikwenda kwa mgombea kwa kustahili tofauti na huo unaodai alishinda kwa kuuza sura?Wakati wa Mr Clean?Mwinyi?

Kwanza si kweli kuwa JK alichaguliwa kutokana na sura ama tabasam,JK amechaguliwa(urais) kwasababu yeye ni CCM period,kama kuna waliompigia kura kwasababu ya sura ama tabasam,basi hiyo first inaweza kuwa percent ndogo sana,secondly kama hicho kilikuwa ni kigezo,basi kilikuwa ni kigezo cha wana CCM hao wakati wa uteuzi wa mgombea urais kupitia chama chao na certainly siyo kigezo cha kwanza vs kile cha uana CCM pale inapokuja kwenye kura za urais,mbona Mkapa na sura yake ya ajabu ajabu alichaguliwa?Tena kipindi chenye upinzani mkubwa?Unataka kusema tabasam lake lilizidi la Mzee wa kiraracha?lol!

Kama issue kweli ni kuuza sura na tabasam,kwanini wapinzani wasitafute mgombea urais mwenye sifa hizo kumzidi JK?

Naelewa ni kweli tuna hamu sana ya mabadiliko na kwahiyo we want change in any means or form.

Hivyo mwishoni nakubaliana kuwa ukijiweka kwenye viatu vya mwana ccm,basi inawezekana kuwa JK alipitishwa kwasababu ya sura na tabasam,lakini kwenye uchaguzi wa urais,JK alishinda kwasababu kura za CCM zilizidi za upinzani...Hivo unaweza kuona picha kwamba mabadiliko ya kweli yaje vipi.
 
Ingawa sipdni nipigwe kabisa mwilini mwangu, ikitokea kuwa ni lazima nipigwe, basi kati ya rungu na fimbo mimi nitachagua nipigwe kwa fimbo.

(a) Kuzuia tusipigwe kabisa, tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya kikatiba na kupunguza madaraka ya rais. Kwa kufanya hivyo tukishajenga tume huru ya uchaguzi, na tume huru ya utumishi wa umma tutaweza kupambana kirahisi na viongozi wabovu.

(b) Sasa kwa vile (a) haijaweza kufanyika, basi tutaendelea kupigwa tu, na hapo ndipo ninaona kuwa ni afadhali tuendelee na fimbo ya Kikwete kwani kinyume chake tunaweza kuja kukaribisha marungu ya akina Lowasa & co.
 
Back
Top Bottom