Binadamu na Pesa, Wajinga ndiyo waliwao

Tsyamatsy

Senior Member
Sep 9, 2023
109
155
Binadamu Kila kukicha ni kutafuta pesa tu! Uhai autafutwi, kwani kuishi ni bahati tu bali kufa ni lazima, iwe unapenda au haupendi utakufa tu! Hakuna mwenye uhalali wa kuishi milele hapa duniani Kila mtu ni marehemu mtarajiwa.

Pesa ndio Kila kitu humu duniani ISIPOKUWA UHAI TU! Hata uwe billionaire wewe utakufa tu!
Pesa inanunua haki, pesa inaheshimisha mtu, pesa ndio chanzo Cha furaha na mateso humu duniani, na mengineyo.

Pesa inatafutwa Kwa njia nyingi tu, lakini katika njia hizo, nimezigawa katika njia kuu mbili; moja, Pesa inapatikana Kwa njia HALALI, na pili, Kwa njia HARAMU!
Sijui wewe pesa zako unazipata Kwa njia Gani?

Njia Halali zinajulikana kama kutokana na mshahara Halali Kwa aliyeajiriwa mahala popote pale iwe ofisini, walimu, aina yoyote ile ya ajira, vibarua vya kulima au kubeba mizigo na kazi yoyote Halali.

Kwa njia HARAMU, Hapa ndipo sokomoko lilipo. Kwa kukisia asilimia 98% wengi wanapata fedha Kwa kutumia njia hii.
Usikatae, jiulize iwapo wewe ni muajiriwa , je, unafanyakazi masaa yaliyoko ndani ya mkataba wako? Huchelewi kazini? Unatoka kazini muda unaotakiwa?

Je, wewe sio mtoro kazini? Uwapo kazini unafanyakazi kweli au ni kuvuta muda tu, masaa yapite ndio siku imeshaingia hiyo, na mwisho wa mwezi mshahara unaingia kamili japo wewe nafsi yako inajua fika kwamba Kuna masaa ulikuwa unasogeza muda tu, hii ni njia haramu.

Je, wewe ni mfanyabiashara lakini unauza bidhaa zilizo chini ya kiwango ili kujipatia faida kubwa huna habari na madhara Kwa watumiaji, Cha muhimu wewe unatengeneza faida kubwa basi!

Mwenzangu Mimi una duka au biashara yako inahitaji kutumia mizani, lakini huo mzani ushaurekebisha badala ya kilo unapima kilo kasoro, huo ni uharamia!

Njia nyingine Haramu ni Hawa viongozi na wataalamu wetu. Pesa inayotengwa Kwa ajili ya kazi Fulani, wanaimega Kwa Kila hatua ili kujinufaisha binafsi, hii ni njia haramu kabisa.

Katika utafutaji huu wa Pesa Kuna wengine njia zao za kutafuta pesa ni kuwahadaa wengine, kuwafanya wapumbavu na kuwachukulia uto tuShilingi twao, nasikia njia hii inaitwa UTAPELI.

Ebu tusaidiane kati ya Hawa wafuatao ni nani tapeli anae hadaa watu na hafai katika jamii;

Wa kwanza ni Mganga wa kienyeji Ambae umekwenda kumweleza matatizo yako ya kimaisha, yeye Mganga akakupa tiba na kukueleza kuwa malipo ya kazi aliyokufanyia utalipa baada ya Kuona matokeo ya iyo tiba aliyokupa, ukiona umetibikà ndio uje ulipe na kama tiba haikufanya kazi basi usilipe chochote. Je, huyu ni Tapeli?

Wa Pili ni watu wanaojiita watu wa Dili, anakwambia wanamtambo wa kutengeneza pesa, unachotakiwa ni kutoa Milioni moja wakanunue vifaa vya kazi halafu wanakutengenezea Milioni 20.

Ukitoa subiri danadana! Hawa nao ni matapeli?

Wa tatu ni Mchungaji anahubiri na kutakiwa tumchangie akanunue gari au ajenge nyumba, alafu yeye atuombee waumini ili tupate pesa tukanunue gari au tujenge, nyumba! Je, huyu nae ni mkweli au Tapeli ndani ya kivuli Cha uchungaji?

Wote Hawa wanatafuta pesa, je, kati Yao nani mkweli?
 
Back
Top Bottom