Ruvuma: Mkurugenzi wa Tunduru asema kuna Bajeti ya Tsh. Milioni 56 zimetengwa kujenga madarasa Shule ya Msingi Magomeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Baada ya picha ya madarasa ya Shule ya Msingi Magomeni ya Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kusambaa zikionesha uhaba wa Madawati na miundombinu chakavu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Chiza Marando amesema wanafahamu kuhusu changamoto hizo na kuna bajeti ya maboresho.
Magomeni.JPG

Marando ameiambia JamiiForums “Mipango ya maboresho ya Shule ipo katika mpango wa Mwaka 2023, kuna Tsh. Milioni 56 na mafundi wameshaanza ujenzi wa madarasa matatu mapya, kuhusu maboresho ya madarasa yaliyopo (pichani) itategemea na bajeti ya ujenzi itakayosalia kwa kuwa tunajenga kwa kutegemea makusanyo ya ndani.”
Magomeni3.JPG

Ameongeza “Upande wa Madawati tumepanga hadi kufikia Desemba 15, 2023 yawe yamefika shulebi, kwa madarasa mapya tumepanga hadi kufikia Januari 2024 yawe yamekamilika."

Pia, soma;

Ruvuma: Sinema na siasa vilivyoingia kwenye sakata la miundombinu ya Shule ya Msingi Magomeni (Tunduma)
 
Back
Top Bottom