Komredi Riziki Kingwande Akagua mradi Ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Mwaikisabe Wilaya ya Chemba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

CDE. RIZIKI KINGWANDE AKAGUA MRADI WA UJENZI WA VYUMBA 4 VYA MADARASA NA OFISI 3 KATIKA S/MSINGI MWAIKISABE - CHEMBA

Asema UWT Yaridhishwa na Utekelezaji wa Mradi huo.

Pia, Ametembelea na Kuona utoaji huduma wa Zahanati ya Soya

Awataka Wazazi kuwajibika katika Malezi bora kwa Watoto

23 Novemba, 2023

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Mary Chatanda , umeendelea na ziara yake ikiwa ni siku ya pili katika imefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani humo.

Uongozi huwa ukiwa katika ziara yake umegawanyika katika timu mbalimbali ambapo Naibu Katibu Mkuu Ndg. Riziki Kingwande amefanikiwa kutembelea mradi wa Ujenzi wa Vyumba 4 vya madarasa na Ofisi 3 katika Shule ya Msingi Mwaikisabe wenye thamani ya Shilingi 90,000,000 (Millioni tisini) na Zahanati ya Soya iliyopo kata ya Soya pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Kata zote mbili .

Akizungumza na wananchi, amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao na kuwalinda wakiwa ndio walinzi namba moja kwani maadili yameporomoka hivyo amewasihii kutoka kuamini watu kwa urahisi kwani Dunia imeharibika .

" Wazazi naombeni tuwajibike katika kuwalea watoto wetu kwenye msingi mzuri kwani ndio viongozi wa leo na kesho yao ambayo bado wanayo kubwa ,hatuwezi kukaa kimya hii hali ya sasa hivi ambayo watoto wetu wanaharibiwa kwa kukatishwa ndoto zao na miili yao utasikia huko mara mtoto amelaitiwa mara kabakwa hizi tabia tuzikomeshe " Amesisitiza Ndg. Kingwande

Vilevile, Ndg.Kingwande amefanikiwa kusikiliza kero za wananchi hao na kuzipatia majibu ikiwemo ahadi ya muda mrefu ya gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati ya Soya na zingine ameielekeza Halmashauri ya Chemba kuwafanikishia wananchi wake likiwemo suala la TASSAF ,Barabara, ujenzi wa shule Vyumba vya madarasa 4 katika Shule ya Chang'ombe na Kata hio,pamoja mengine ambayo yatapatiwa ufumbuzi mara baada ya UWT kuyapokea na kwenda kuweka msukumo kwa Serikali.

#UWTImara
#UWTJeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.38.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.38.jpeg
    154.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.39.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.39.jpeg
    150.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.39(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.39(1).jpeg
    132.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.40.jpeg
    150.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.40(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.40(1).jpeg
    136.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.40(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-24 at 14.49.40(2).jpeg
    173.8 KB · Views: 3
Back
Top Bottom