Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,131
- 35,164
Kama ulidhani hilo jambo halikuhusu basi anza sasa kufikiri tofauti. Yanayoendelea baina ya NHIF na watoa huduma za afya binafsi ndio mwanzo wa picha itayokuja kwenye suala la bima ya afya kwa wote, ambayo itapaswa kuwa ya lazima kwa watu wote. Kwa kifupi sana Yatakayofuata yatakuwa marudio tu.
Kwa kuufungua mjadala, nitaweka baadhi ya hoja zinazojadiliwa na pande zote. Kwa mfano:
1. DAWA
NHIF wanasema wameongeza orodha ya dawa kwenye kitita hivyo wagonjwa watafaidika, wamiliki wa vituo vya afya binafsi wanasema bei ya dawa kwa NHIF imepunguzwa na kuwa chini zaidi ya bei ya soko hivyo ni hasara kwao, hawataweza kutoa baadhi ya dawa kwa wagonjwa wa NHIF.
2. VIPIMO
NHIF inasema vipimo vingi zaidi vimeongezwa katika kitita kipya hivyo wagonjwa watafaidika. Watoa huduma binafsi wanasema, malipo ya vipimo vingi yamepunguzwa sana kiasi cha wao kushindwa kuzifidia gharama za kuendelea kuvifanya kwa wagonjwa wa NHIF.
3. HUDUMA ZINGINE (Procedure)
Mfuko wa NHIF unasema umeongeza huduma ambazo hapo awali hazikuwepo kwenye mfuko wa NHIF. Wamiliki wa vituo binafsi wanasema malipo ya kufidia kuzitoa hizo huduma yako chini na hayakidhi gharama ambazo wao huziingia hapo kabla ili kuwezesha utoaji wa hizo huduma.
4. HUDUMA YA KUMUONA DAKTARI (Medical consultation)
NHIF wanasema pesa kwa ajili ya consultation ni hisani (motisha) kwa watoa huduma lakini sio jambo la lazima kuwepo kama mshahara au posho na kwa sasa wigo umepanuliwa kwa ngazi zote za utoaji huduma kulipwa malipo hayo. Wamiliki wa vituo vya afya wanalisema, msingi wa kutoa huduma za afya huanzia na kuishia kwenye medical consultation, hivyo wataalamu wa afya ni haki yao kulipwa kikamiliki medical consultation fee kulingana na soko la utoaji huduma za afya na siku zote inapaswa kuwa ni malipo ya lazima na sio hisani kutoka NHIF. Viwango vipya vimepunguzwa na vimeshindwa kuendana na soko lilivyo.
MAONI YANGU
NHIF imepanua wigo wa kutoa huduma kwa wanufaika wa mfuko lakini kwa gharama ya kuwabebesha mzigo wamiliki wa vituo binafsi vya afya.