RPC Mbeya, Kamanda Msangi azuia maandamano ya kumpokea Lowassa

TITHO SANGA

Member
Jul 20, 2015
99
13
Barua ya Jeshi la Polisi ambayo imetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Z. Msangi ikikataza maandamano na kukubali kufanyika kwa mkutano tu.

Tangazo kwa umma
11825198_738454619631748_4331759803681161275_n.jpg

Mnamo tarehe 10/08/2015 ofisi ya mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya ilipokea barua toka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe. Lengo la mkutano huo ni mgombea wa Rais kuomba wadhamini Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilikutana na uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo akiwemo mbunge wa Mbeya mjini na baadhi ya madiwani katika eneo la usalama wa chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano.

Hii inatokana na; Sababu za kiusalama Kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja.

Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki.hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Ni sawa.Wana Mbeya nendeni mkahudhurie mkutano na kumsikiliza mgombea.Hakuna haja ya kuandamana kama Polisi imezuia.LOUD AND CLEAR!
 
Maandamano katika dhana hii wanayotueleza, nashindwa kabisa kuona weledi wa Jeshi la Police. Uhalali ama uharamu wa maandamano umejikita kwenye ile nia ama sababu ya wahusika kufanya hivyo. Kwa uelewa wa police wetu basi inabidi kila siku pale mtaa wa congo Dar es salaam wakazime maandamano. Ama nyakati za jioni pale Barabara ya Msimbazi Dar es salaam. Asubuhi barabara zote kuelekea katikati ya jiji la DSM huwa kuna maandamano. Weledi uko wapi hapa. Tukisema wanatumika tutakuwa tunakosea!!!!???
 
Kula like mkuu,Msafara wa Kikwete tu wa magari huwa ni full maandamano na kero haswa katikati ya jiji kwa foleni!!
 
Barua ya Jeshi la Polisi ambayo imetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Z.Msangi ikikataza maandamano na kukubali kufanyika kwa mkutano tu.

Tangazo kwa umma
Mnamo tarehe 10/08/2015 ofisi ya mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya ilipokea barua toka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya Ruanda nzovwe. Lengo la mkutano huo ni mgombea wa Rais kuomba wadhamini Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilikutana na uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo akiwemo mbunge wa mbeya mjini na baadhi ya madiwani katika eneo la usalama wa chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano. Hii inatokana na; Sababu za kiusalama Kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja.

Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki.hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Siku 64 za maajabu
 
Barua ya Jeshi la Polisi ambayo imetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Z.Msangi ikikataza maandamano na kukubali kufanyika kwa mkutano tu.

Nampongeza kamanda Msangi.Misafara ya kisiasa ya maandamano barabarani inazuia shughuli za kuchumi.Jana mabasi toka Moshi,Arusha na Nairobi kwenda Dar es SALAAM yamechelewa kufika sababu ya msafara wa maandamano wa LOWASA na maboda boda yake ya kukodi yaliyokuwa yametanda barabara zima.Mabasi yalikuwa hayawezi ku-overtake YANAZOMEWA na vibaka wa BODA BODA waliokuwa msafara wa Lowasa.

Kamanda msangi ana hoja barabara ziachwe wazi zifanye shughuli za kiuchumi watu waende huko kwenye mikutano yao ya kisiasa waache watu waendelee na shughuli za kiuchumi.Anayependa kwenda mkutanoni aende na anayependa kuendelea na shughuli zake kama za daladala nk aendelee na kazi zake bila bughudha kutoka kwa waandamaji kwenye barabara.

Ombi langu ni kuwa wanaporudi pia kwenye hiyo mikutano wasirudi na maandamano tena ya kuleta siasa mabarabarani na kuanza kupora watu na maduka.Mihemuko yao ya kisiasa iishie huko huko mikutanoni kwao wasianze kurudi kimakundi na michaka michaka na kufanya vurugu na kupuliza mahoni ya bajaji nk.Wamalize mikutano yao kwa amani watawanyike kwa amani waende kama ni boda boda warudi sehemu zao za kazi waendelee na maisha yao.

Hongera kamanda Msangi
 
Intelijensia ya polisi huwa inaona tu mikatano na maandamano ya upinzania kuwa hakuna usalama.

Subirini hako ka chama kenu kasukumwe pembeni na wananchi halafu tulifumue jeshi hilo na kuifanya kuwa la kisasa zaidi na kuwajibika kwa wananchi zaidi.
 
CCM wanajichanganya sana...Sasa umati wa WATU UNATUA TOKA MBINGUNI...!??

Sbb watu wanakuja kwa miguu hadi uwanjani...sbb ni wengi sanaaaaaaa....wataonekana ni maandamano tu...!!! Uwingi wa watu kwenda uwanjani tayari ni maandamano...!!!

Ni sawa na kula chakula usisikie harufu...CCM washashikwa kila kona...!!! Inakufa vibaya sana...!!
 
Kinacho onekana ni polisi kulishwa maneno na hao wanaodai ngazi za juu.mimi ninashauri hao ngazi za juu wafute kampeni tukapige kura hata kesho tumalize upuuzi huu maana wanachi wengi tayari uamuzi wanao wanasubiri kupiga kura tu.
Maandamano katika dhana hii wanayotueleza, nashindwa kabisa kuona weledi wa Jeshi la Police. Uhalali ama uharamu wa maandamano umejikita kwenye ile nia ama sababu ya wahusika kufanya hivyo. Kwa uelewa wa police wetu basi inabidi kila siku pale mtaa wa congo Dar es salaam wakazime maandamano. Ama nyakati za jioni pale Barabara ya Msimbazi Dar es salaam. Asubuhi barabara zote kuelekea katikati ya jiji la DSM huwa kuna maandamano. Weledi uko wapi hapa. Tukisema wanatumika tutakuwa tunakosea!!!!???
 
Kula like mkuu,Msafara wa Kikwete tu wa magari huwa ni full maandamano na kero haswa katikati ya jiji kwa foleni!!

Wacha uongo.Yule ni kiongozi wa nchi.Anatanguliwa na pikipiki moja.Sio boda boda 300 AU kama lowasa.Msafara wake unaende spidi ya kuua mtu KIASI KUWA DAKIKA TU NJIA INAKUWA NJEUPE.Hauendi taratibu kama wa Lowasa ambao kutoka biguruni tu hadi posta mpya kufika unatumia masaa matano mazima!!!!.
 
Nampongeza kamanda Msangi.Misafara ya kisiasa ya maandamano barabarani inazuia shughuli za kuchumi.Jana mabasi toka Moshi,Arusha na Nairobi kwenda Dar es SALAAM yamechelewa kufika sababu ya msafara wa maandamano wa LOWASA na maboda boda yake ya kukodi yaliyokuwa yametanda barabara zima.Mabasi yalikuwa hayawezi ku-overtake YANAZOMEWA na vibaka wa BODA BODA waliokuwa msafara wa Lowasa.

Kamanda msangi ana hoja barabara ziachwe wazi zifanye shughuli za kiuchumi watu waende huko kwenye mikutano yao ya kisiasa waache watu waendelee na shughuli za kiuchumi.Anayependa kwenda mkutanoni aende na anayependa kuendelea na shughuli zake kama za daladala nk aendelee na kazi zake bila bughudha kutoka kwa waandamaji kwenye barabara.

Ombi langu ni kuwa wanaporudi pia kwenye hiyo mikutano wasirudi na maandamano tena ya kuleta siasa mabarabarani na kuanza kupora watu na maduka.Mihemuko yao ya kisiasa iishie huko huko mikutanoni kwao wasianze kurudi kimakundi na michaka michaka na kufanya vurugu na kupuliza mahoni ya bajaji nk.Wamalize mikutano yao kwa amani watawanyike kwa amani waende kama ni boda boda warudi sehemu zao za kazi waendelee na maisha yao.

Hongera kamanda Msangi

Haisaidii mkuu bado dawa iko pale pale...... na ili iingie vizuri lazima sindano itumike kwa hiyo kuwa mpole dawa iingie hakuna namna nyingine ya kufanya.
 
Tusishangae polisi wakizuia mikutano na maandamano wakati wa kampeni. Tanzania ni yetu sote,polisi tekelezeni wajibu wenu kisheria,acheni kujipendekeza kuwafurahisha CCM
 
Back
Top Bottom