Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Hii ishu ya ndoa ukikurupuka kama mwendawazimu hutoweza kuelewa.
Hii ishu kuna kipindi ilishajadiliwa sana mpaka tukapata kuelewa kuwa kisheria mtu ukikaa na mpenzi within a 6 mnth basi huyo atahesabika kuwa mke wako kihalali na hata siku mkitengana basi utalazimika kugawana nae mali mlizochuma.

Tuchukulie hicho kipengele ni kweli (kuwa ni miezi sita na sio miaka miwili) basi kuna uwezekano wa kuwa Dr.Slaa ni mume wa Rose Kamili kama mwenyewe (Rose Kamili) anavyodai kuwa waliishi pamoja kama mke na mume na hivyo inabidi aachane na Rose Kamili kwanza ndio aoe mwanamke mwengine.

Tukichukulia kuwa hilo halipo, hakuishi na Rose Kamili, walikuwa wanapeana ngono tu hadi kuzaa watoto wawili basi kuna hili la Josephine. Ya kuwa, hata kama Dr.Slaa anaishi na Josephine sasa kwa zaidi ya miezi sita, haiondoi ukweli kuwa Josephine ni mke wa mtu mwengine kisheria na serikali haiwezi kuandika cheti cha ndoa kati ya Josephine na Slaa kwa sababu tayari ni mke wa mtu kisheria [Unless useme mwanamke mmoja anaweza kuwa na waume wawili KISHERIA kwa wakati mmoja]
 
Hayo si masuala binafsi! Rose Kamili, Josephine, Mahimbo, Dr. Slaa. Wanaume wawili akina mama wawili, si wagawane tu yaishe manake leo Mahimbo yupo mahakamani kesho Rose Kamili wanamfanya Dr. Slaa awe mtu wa mahakama kila kukicha. Hii inaweza kudhoofisha utendaji ndani ya chama.
 
fmpiganaji MBINU NYENGINE BWANA KAMA MUVI VILE! wacha tuone busara za mahakama, the outcome will tell whether the allegations are logical au ni kutaka kujipatia umaarufu na kijitangaza na kupata umaarufu
 
Last edited by a moderator:
Tusiwe biased bwana, kama mwanasiasa ambae ni kioo cha jamii lazima social responsibilities zitimizwe! Josephine (first lady wangu binafsi) hajapata hati ya talaka kwa mumewe na ndo iko mahakamani. Kama Rose Kamili nae hajatalikiwa na mumewe, ana haki ya kumshika ugoni na kudai matunzo ya watoto. Hili sio suala la chadema, ni suala lao binafsi.

Well said King'asti
 
Last edited by a moderator:
Hayo si masuala binafsi! Rose Kamili, Josephine, Mahimbo, Dr. Slaa. Wanaume wawili akina mama wawili, si wagawane tu yaishe manake leo Mahimbo yupo mahakamani kesho Rose Kamili wanamfanya Dr. Slaa awe mtu wa mahakama kila kukicha. Hii inaweza kudhoofisha utendaji ndani ya chama.

Aisee Kimbunga!
 
Last edited by a moderator:
Yaani wana-CHADEMA mna mahaba ya ajabu kama sio ya kushangaza!! Yaani kwenu Dokta Slaa ni kama mungu ambae ni kufukuru kumsema kwa mabaya!!! Tuache ujuha....mapenzi yetu kwenye vyama vya siasa si busara hata kidogo kututia upofu na kujifanya hamnazo!! Jambo la msingi hapa ni kuangalia uhalali wa madai badala ya kuleta siasa!
1. Kweli Dr Slaa amezaa na Bi. Rose?
2. Kweli Dr Slaa amemkimbia Bi. Rose?
3. Kama Na. 1 above ni sahihi, je ni kweli Dr Slaa hatoi matunzo kwa familia yake?

Hayo ndio masuala ya kujadili na kama yote hayo ni sahihi basi si busara hata kidogo kwa mtu kama Dr. Slaa kufanya kitendo cha kinyama kama hicho. Madai kwamba amelipwa na CCM wala hayana msingi na wala hayana mashiko. Endapo mtu makini ataamua kuangalia ni madai yapi yana mashiko kati ya Bi, Rose kupewa ubunge wa viti maalumu ili kumnyamazisha na madai kwamba Bi. Rose analipwa na CCM; basi hapo madai yenye mashiko ni hayo ya yeye(Rose) kupewa ubunge ili kumnyamazisha!!
Kama nimesoma vizuri habari ya hilo gazeti ni kwamba kuna hati hati ya Bi. Josephine na Dr. Slaa kufunga ndoa hivi karibuni.....hivyo madai ya Bi. Rose kwa sasa ni muafaka na wala haileti mantiki kwa wale wanaodai "WHY NOW" baada ya Dr Slaa kuishushia makombora serikali. Hii ni perfect timing kwa Madai kama hayo kwa vile ni muda unaotarajiwa kuhalalisha ndoa batili. Yeyote yule, hata wale walio nje ya siasa angeweza kufanya jitihada ya kuzuia jambo hilo. Na wale wanaodai kwamba Bi. Rose na Dr Slaa hawakuwahi kuwa mke na mume bali walizaa tu nayo ni madai yasiyo na mashiko kisheria. Kwa mujibu wa sheria, mtu ukishakaa nae kwa muda usiopungua miezi sita tayari hapo wahusika wanakuwa entitled na haki zote za wanandoa.

Vyovyote iwavyo, alichofanya Dr Slaa sio kitu cha busara hata kidogo kwa mtu ambae ni kioo cha jamii! Hakuna serious crime katika masuala ya kijamii kama kutelekeza familia na kuamua kuishi na mwanamke mwingine. Wale wanaotetea upuuzi huu labda wachukue nafasi kwamba huyo Bi Rose ni mama yao mzazi na Dr Slaa ndo baba na Baba amekimbia familia na kwenda kuishi na mwanamke mwingine!
 
The solution here is if the allegations are true,just to give the said Kamili the amount of cash she is demanding. This will make Dr Slaa and his Josephine free from this stupid nonsense....!
 
Huyu mama Rose ndio wale wale akina shibuda kwani yeye hadi leo hajapata tu mzazi mwingine wa.......hadi amn'gang'anie Dr.Slaa?
 
Hayo si masuala binafsi! Rose Kamili, Josephine, Mahimbo, Dr. Slaa. Wanaume wawili akina mama wawili, si wagawane tu yaishe manake leo Mahimbo yupo mahakamani kesho Rose Kamili wanamfanya Dr. Slaa awe mtu wa mahakama kila kukicha. Hii inaweza kudhoofisha utendaji ndani ya chama.

Na hii ndio nia yao hasa.
 
Hiki kitu huenda imeanzia ndani ya CDM; kwa Urais 2015 chochote chaweza kutokea na yeyote aweza kutumiwa na yeyote.
 
Kuna mambo mwengine nadhani tunaingiza siasa hata katika mambo yasiyohusu.

Kama Rose Kamil hapati haki zake za msingi kwa baby daddy wake asichukue hatua kwa sababu za siasa?

Slaa angeondoa hizo loop holes wala asingeshtakiwa pahali

Duh! Rais mtarajiwa huyu naye hajatulia. Anakimbia mke! Inaezekana hata upadri aliukacha sababu ya chuchus. Kweli ma rais wetu marijali kwelikweli.
 
Sishangai na hiyo process inachukua muda gani, nashangaa na maadili ya Dk.Slaa linapokuja suala la ngono, tena ngono zembe at that.

Kisha nashangaa alivyomwepesi wa kusema uongo.....juzi mbele ya waandishi wa habari alitutangazia zaidi ya Mara moja kuwa Josephine ni mkewe wakati kumbe kisheria Josephine ni mke wa mtu mwengine

Mkuu ngono zembe si ndiyo yenye utamu? Unataka alage pipi na maganda?
 
Hiki kitu huenda imeanzia ndani ya CDM; kwa Urais 2015 chochote chaweza kutokea na yeyote aweza kutumiwa na yeyote.

Inawezekana isihusiane na siasa kamwe na wala si kwa nia ya kumkomoa Dr.Slaa........

Inaweza kuwa Josephine na Rose ni wanawake wanaopimana ubavu tu, baada ya mmoja kuwa wa zamani na mmoja wa sasa. Wa sasa kataka kumpanda kichwani wazamani, wazamani kaona amnyooshe kidogo .........


:bump2:
 
josephine ana mume wake halali na walifunga ndoa ya kikristo pale kijitonyama lutheran na mumewe ni mfanyakazi wabandari........Rose Kamili ni mke wa Slaa
 
Tusiwe biased bwana, kama mwanasiasa ambae ni kioo cha jamii lazima social responsibilities zitimizwe! Josephine (first lady wangu binafsi) hajapata hati ya talaka kwa mumewe na ndo iko mahakamani. Kama Rose Kamili nae hajatalikiwa na mumewe, ana haki ya kumshika ugoni na kudai matunzo ya watoto. Hili sio suala la chadema, ni suala lao binafsi.
Kama ni suala binafsi kwa nini unalitolea povu??
 
Josephine si mke wa Slaa, hapo ameudanganya umma. Nakubali kuna kutokuheshimu sacrament ya ndoa au family as an institution kwa upande wa Slaa, na hii sio character nzuri ya kiongozi yeyote, especially wa umma.

japo ni mshabiki wa slaa kisiasa, pia mshabiki wa mitazamo mingi ya chadema siungi mkono kabisa public life ya huyu slaa, ni bora aifunge ndoa na huyo jose, je ndoa yake imeisha? Ila huyo rose anapoteza muda wake, atafute kazi afanye,
dr slaa pls maliza hii issue, najua upadre umekushinda, je hata ukristo au uaminifu pia unakushinda?
Ukijua kuwa personal life yako ni public, na tunakujudge kwa hilo pia, jirekebishe
 
Masuala ya ndoa ni magumu sana,tofauti na jinsi wana jf tunavodhani.rose kamili ana haki na yuko sahihi kikubwa ni dr slaa kumsikiliza na kumpa anachohitaji,
 
Uhusiano wa ndoa ni suala binafsi na kamwe rose kamili hawezi kulazimisha penzi toka kwa dr slaa wala kumshtaki dr hakuwezi kuwa kete ya kumuangusha kisiasa;kwani dr ni nyani mzee kisiasa aliyekwepa mishale mingi!
 
fmpiganaji Sidhani kama hapo ni mbunge wa CDM kamshtaki katibu mkuu wa CDM. bali ni Rose Kamili kamshtaki mzazi mwenzie Dr. W.Slaa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom