Riwaya ya kusisimua "Kizungumkuti"

junior252

Senior Member
May 3, 2015
141
96
Kizungumkuti #01
Mtunzi..Junior Stories

Simu ilipigwa kwenda makao makuu ya jeshi la polisi kitengo cha Criminal investgator lakini iliita mpaka ikakata bila kupokelewa, mpigaji hakutaka kukata tamaa mapema hivyo akanyenyua simu yake na kupiga tena namba ile ya mkuu wake wa kazi kwa muda ikaendelea kuita bila kupokelewa mpaka ilipokata tena!

"Mbona mkuu hapokei simu?" akauliza kwa hamaki mkuu wa kikosi namba zero cha kitengo kile cha Criminal investgator Shamim.

"Labda ujaribu tena...huenda bosi ametoka nje ya ofisi kidogo!" akajibu kijana mmoja mpole waliyekuwa wakifanya naye kazi.

"Au nipige kwenye simu yake ya mkononi?" akauliza huku akijiuliza mwenyewe pia.
Bila kusubiri jibu la wenzake binti huyu machachari katika kazi yake hii ya kupeleleza na kukamata waharifu walioshindikana alitoa simu yake ndogo ya mkononi na kisha akatafuta namba za mkuu wake wa kazi na kupiga.

Upande wa pili simu iliita kwa muda mrefu mpaka ikakata bila kupokelewa tena!.....wakabaki na mshangao.....mkubwa wao wa kazi yulr hakuwa na tabia ya kutopokea simu tena hasahasa inapokuwa ya Shamim.

Binti yule machachari akapiga tena zaidi ya mara tatu na simu ikaita mpaka ikakata tena bila kupokelewa!......wakaangaliana kwa muda na kuanza kushauriana kwa sababu walichotaka kulipoti kwa mkuu wao kilikuwa kitu cha muhimu sana....kutokana na uchunguzi aliowatuma wakaufanye sehemu flani ya muhimu sana.

"Hebu mpigie Kigwasho......yeye alibaki ofisini...naamini itakuwa rahisi zaidi!" akashauri kijana mmoja.
Shamim akatoa simu yake tena na kupiga namba ya Kigwasho....kijana mwingine aliyekuwa akifanya kazi kitengo kile kile ila kwa siku hiyo hakutoka na wenzake kwenda kwenye tukio.

"Kigwasho..."
"Yes...inspekta"
"Mkuu yupo ofisini?"

""Ndiooo....aaaaa...sijajua...sina uhakika kwa sababu kuna kipindi nilitoka kwenda chumba cha mahabusu hivyo sijajua kama muda huo alitoka au bado yupo ila mimi kama mimi sijamuona akitoka!" akajibu kijana yule.

"Nenda ofisini kwake umwangalie kama yupo...kwa sababu simu yake ya mezani na ya mkononi zote hazipokelewi!" akaagiza Shamim.

"Sawa Inspekta.."
Kigwasho akatoka huku akiwa hajakata simu na kuelekea kwenye ofisi ya mkuu wao wa kazi...kwenye simu Shamim akamsikia Kigwasho akipiga hodi kwa muda bila kuitikiwa na akamsikia akisukuma mlango na kuinga.

"Mamaaaaaaaaaaaaaaa..........mauaji!" Kigwasho aliropoka kwenye chombo kilr cha mawasiliano kwa mshtuko uliomkuta ghafla huku akisahau kama kuna mtu anamsikiliza.

"Kigwasho.......kigwasho.......wewe koplo Kigwasho.....mauaji ya nini?....naomba unijibu Koplo......KOplo"! aliendelea kuita Shamim huku na yeye mshtuko mkubwa ukiwa umemkumba.

"Mauaji?....mauaji ya nani?" vijana waliokuwa naye wakajaribu kumdadisi ila hakuwajibu kitu na akakata ile simu.
"Inaonekana ofisini kuna tatizo!......geukeni twende ofisini haraka!" akaagiza

Vijana aliokuwa nao wakaingia kwenye gari ndogo aina ya Noah nyeusi waliyokuwa wakiitumia katika safari zao zote za shughuli za ofisi na yeye akakaa kwenye usukani na kuiondoa ile gari kwa kasi ya ajabu utafikiri yeye sio mwanamke.
Kijana mmoja alitoa king'ora na kukiweka juu ya bodi ya gari na kisha kikaanza kulia na kusababisha gari kadhaa ziwapishe na wao kuongeza speed ya gari yao ile.

Nusu saa iliwatosha kuingia makao makuu ya Polisi hasahasa kitengo chao cha Criminal investgator...nje ya ofisi zao walikuta watu wengi sana na waandishi wa habari pia wakiwa wamejaa tayali kutaka kujua kilichotokea kutokana na habari ile kusambaa kwa haraka zaidi.

"Pisha....pisha....pisha!" Shamim aliamrisha watu nao wakamuachia njia akapita.
Aliwakuta baadhi ya vijana wa kitengo wakiwa wamezungushia eneo lile kwa karatasi maalum kuzuia watu kuingia huku wengine wakiwa ndani wakiendelea kutafuta ushahidi.

Shamim alitoa glovu zake na kuvaa kisha akanyenyua karatasi ile na kuingia ndani ya kile chumba....alimkuta Kigwasho akiwa kakaa pembeni huku analia kama mtoto mdogo....alimpita na kuufata mwili wa marehemu uliokuwa umefunikwa kwa shuka jeupe.

Akaufunua ule mwili......!!!™ alishtuka!!!! kile alichokiona kilimwacha kinywa wazi!
Mkuu wake wa kazi alikuwa ameuawa kikatili sana...macho yote yalikuwa yametobolewa na muuaji akaondoka nayo..katikati ya paji lake la uso kulikuwa na tundu dogo la risasi!!!!

Itaendelea...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom