Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Muungwana JK,haya mambo yameshawekwa hadharani na Dr Mwakyembe,kazi kwako.

wakati wa KATA FUNUA UMEFIKA BABA,usimtazame mtu USONI.

Itakuwa safi ukichagua mmoja kati ya hawa Prof Mark Mwandosya au Dr Huseein Mwinyi.
 
Da! jamini nimeisoma kwa muda wa kutosha hiyo ripoti! Inaondoka na watu wengi kiasi kwamba siamini kama serikali ya CCM na bunge lake wanao ujasiri wa kutosha. nadhani ndio wakati muafaka wa upinzani kuchukua nchi. CCM imeshasambaratika ndugu zangu. Labda John Mnyika utuambie tofauti!!!!!
 
Acha usanii umetumia vigezo gani kuwapata hawa unawapendekeza? si lazima wawe watu wanaojulikana sana. Mbona Makamu wa rais Dr Shein anaperform wakati hakujulikana. Tuache kuangalia majina.
 
Nilipoipinga kamati ya Madini na kuiunga mkono hii ya Bunge niliamini katika hili. Wakati maswali ya 10 au zaidi kuhusu Richmond yalipochapishwa kwenye Tanzania Daima zaidi ya mwaka mmoja uliopita walijibu "hakukuwa na rushwa"

Dr. Mwakyembe amefanya kile ambacho Taifa lake lilimwomba. Natoa pongezi za wazi na dhati kwa timu nzima iliyofuatilia jambo hili Dr. Mwakyembe, Mhe. Selelii, Injinia Stella na wengine.

Today, you have brought hope back to the hearts of millions of Tanzanians scattered around the world. Now it is the turn of your fellow MPs kama wataweza kukipokea kijiti!!

I salute!
 
Hongera Dr. Mwakyembe na wajumbe wa kamati yako. Kama ni kidonda umejitahidi haswa kukisafisha na kutoa ushauri mzuri wa namna ya kukiuguza. Tuangalie sasa kama mwenye kidonda atafuata ushauri ili kupona ama ataendelea kukijaza mavumbi na kuendelea na staili yake ya kukitunza katika mazingira ya uchafu.
 
Heh heh, Huyu Prof Mwand. kwanza huko kwao hawakaliki na wenzake, anajidai dai na hivi, amewanyima mwanza uwanja akapeleka kwao. Huyu mwingine ni wa Kutangatanga mara leo, Mbunge wa Kisarwe mara Kesho Mbunge wa Zanzibar. Asubiri tu Urais wa Visiwani.

Waziri Mkuu safari hii ni Asha Migiro ataacha kazi hiyo ya UN kujua kusaidia vichwa ngumu.

Mungu na asikie. Wengine sioni, karibu kila mmoja anauturi wa Ufisadi kwenye baraza hili la kishikaji
 
Kama kawaida JK ataunda kamati ya kumchunguza FISADI Lowasa, FISADI Karamagai FISADI Rostam na wenzake na atawapa miezi 6 (sita) kukamilisha kazi hiyo.
 
Huu ndio msumari kwa Lowassa

Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.

Nimpongeze Mwakyembe na kamati yake kwa kuweka uchi suala hili, ambalo kwa kiasi kikubwa limeivua nguo sirikali! Shida ya Mwakyembe katika kunukuu ibara hii ni kwamba kashindwa kabisa kuita spedi ni spedi, kasema ni kijiko kikubwa! Kwa nini asiseme kwamba waziri mkubwa inabidi ajuzulu? Badala ya kusema ataamua kungalia kuchukua maamuzi yanayofaa!

jamani nimeelemewa Dr. kweli amefanya kazi. Ndio maana sita alitaka kuondoka(kukimbia)

Sijajua mpaka sasa nani alimzui Sitta kuondoka, alikuwa akikwepa nini? Kwamba na yeye yuko katika dili hili ama anataka kumlinda waziri mkuu mchafu? Mwalimu Nyerere alisema huyu Bw Lowassa ni mchafu tangu mwaka 1995, sema tu tulikuwa na kiburi! Utabiri wake umetimia!

Gembe JK akiwaacha hao waliotajwa live bila kuuma maneno nitaungana na wewe barabarani tuandamane kama wanatuua wacha watuue tu haina maana kuishi katika aibu kama hii ya kuwa na serikali ya kifisadi juu mpaka chini.

Katika kipindi chote cha miongo mitatu na ushee niliyoishi humu duniani sijawahi kusikia serikali ikivuliwa nguo kama inavyotokea sasa. JK HATA KAMA EL,KARAMAGI,ROSTAM NA WENGINE WALIKUPA MABILIONI YA KAMPENI LAKINI KUMBUKA HAWAKUKUPA 80% YA KURA NI WATANZANIA NDIO WALIOKUCHAGUWA. THE BALL IS ON HAND USIJEKUTULAUMU 2010 AMBAYO HAIKO MBALI SASA.

Na mimi mnipe bango niwaunge mkono huko barabarani, tushachoka, kama ni kuuwawa basi na tuuwawe! Hatuna cha kupoteza! Liwalo na liwe! Spedi ni spedi, sio kijiko kikubwa!

whistling... tik tak tik tak

Now time has come for president Kikwete to make "Tough decisions" he promised in 2005 during his election campaigns. Long Live Tanzania
 
Wapinzani huu ndio wakati muafaka wa kufanya maandamano ya kuunga mkono ripoti ya Dr Mwakyembe (regardless yeye ni CCM) na pia kushinikisha Serikali na hasa JK amwajibishe Lowassa, Msabaha, Karamagi na wote waliotajwa kwenye Riport.
 
Kama kawaida JK ataunda kamati ya kumchunguza FISADI Lowasa, FISADI Karamagai FISADI Rostam na wenzake na atawapa miezi 6 (sita) kukamilisha kazi hiyo.

Siamini kama raisi atafanya ujinga huo, ingawa inawezekana kabisa, kwa sisiemu ya kulindana ninayoifahamu mie!. Hii ni Tanzania bwana!
 
CCM wangekuwa fair wangeandaa maandamano ya kuipongeza Kamati ya Mwakyembe kufanya kazi nzuri...kufichua madudu ya Richmondi na viongozi wasiofata maadili....lakini mmmhhh ngoja tusikie watatoka vipi na msimamo wa chama.....

"Kidumu chama cha mapinduzi na fikra sahihi za mwenyekiti"
 
Back
Top Bottom