Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Na mimi napenda kumshukuru rais na wanakamati teule angalau kwa kudhibitisha uvumi tulio kuwa nao muda mrefu,japo kuwa uhalisia wa mambo yenyewe na hatua za kuchukuliwa vinaweza kuwa vya kisiasa zaidi.

On top of that, I have got this email below from one of my friends, basically it is a summary of the Mwakyembe's Report! Anyone seen it too?
''MWAKYEMBE AMWAGA LAZI BUNGENI

MH. HARRISON MWAKYEMBE

MBUNGE WA KYELA NA MWENYEKITI WA KAMA TEULE YA KUCHUNGUZA MADUDU KAMPUNI YA RICHMOND, MH. HARRISON MWAKYEMBE, DAKIKA TANO ZILOPITA AMEHITIMISHA KUSOMA RIPOTI YA KAMATI YAKE KWA UWAZI NA UKWELI KWA MUDA WA DAKIKA TAKRIBAN 80.

KAMATI TEULI HIYO IMEBAINI KWAMBA MKATABA WA RICHMOND ULIFIKIWA KWA UPENDELEO, RUSHWA NA UBABE WA VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALINI, NA KWAMBA LICHA YA USHAURI WA KITAALAMU NA HALI HALISI WAKUBWA WALILAZIMISHA USAINIWE. hIVYO PAMOJA NA MAMBO MENGINE KIBAO IMEPENDEKEZA MIKATABA YOTE YA NISHATI IPITIWE UPYA KAMA ILIVYO MIKATABA YA MADINI

KAMATI TEULE HIYO KUPITIA MDOMO WA MH. MWAKYEMBE IMETO MAPENDEKEZO KAMA 15 HIVI, BAADHI YAKE YAKIWA:

1. WAZIRI HUSIKA WA WAKATI HUO (MH. DR MSABAHA) NA KATIBU MKUU WAKE WAKATI HUO WAPEWE ADHABU KALI

2. WAZIRI WA SASA WA NISHATI NA MADINI MH. NIZAR KARAMAGI NA MWANASHERIA MKUU WAWAJIBISHWE KWA KUWEZESHA MKATABA WA RICHMOND KUHAMISHIWA KAMPUNI INGINE

3. UONGOZI WA TAKURU (SASA TAKUKURU) UFANYIWE MABADILIKO HARAKA KWA KILICHODAIWA KUTOA TATHMINI ISIYO SAHIHI JUU YA MAZINGIRA YALIYOUZUNGUKA MKATABA WA RICHMON.

4. MKATABA WA RICHMOND AMBAYO IMEIPASIA KAMPUNI YA DOWANS UCHUNGUZWE UPYA.

5. MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUAMUA NINI CHA KUFANYA BAADA YA RIPOTI KUANIKWA HADHARANI

AIDHA JUHUDI ZINAFANYIKA KUIPATA RIPOTI YOTE HIYO NA KUANGALIA NAMNA YA KUWEKA HADHARANI ILI HADHIRA IJUE KILA KITU KWA UWAZI NA UKWELI.

PSSST! SASA TUNASUBIRI RIPOTI YA MADINI YA KINA KABWE''

Festo G
 
JK
...as you did to Balali.......the same logic should be applied to your kiranja Mkuu
 
Wapinzani wajiandae kujenga hoja nyingine CCM na JK wanaelekea kujipanga kusafisha Chama...wakingangania hoja hii soon wanaishiwa mashiko maana CCM watasema tulikosea na sasa tumerekebisha.


Hapa hakuna cha Msimamo wa Chama zaidi ya kuomba watu flani wajiuzuru.na saa si Nyingi kuna watu watajiuzuru.Si Rahisi kutetea Jambo ambalo linaweza kukiathiri chama na wanachama

Unadhani wakisimamia pande tofauti na kina Mwakyembe itakuwa ni kama kuwasaliti kina Mwakyembe na jambo gumu sana.

Kuna Jambo ambalo linafichika hapa,Je JK anataka Kumtosa Swahiba wake?Je Ujasiri kautoa wapi?au ndio sababu ya kumteua Mwakyembe kamati zote mbili pamoja ile ya Madini,kabla hajajitoa katika madini?

Ngoja niwamegee jambo ambalo limo katika ripoti ya CAG.Hata Rostama na the so callled "BWana Mkubwa" walihusishwa ila CAG nashangaa katiakExecutive summary ya CAG hakusoma mabo yote zaidi ya kuweka blaah blaah.

Naye nadhani anatakiwa kung'oka??you better find the report
 
Mliopo huko bungeni jamani hakuna ambaye ameachia ngazi hadi sasa hivi?

Yaani hata ambao wameshajua kuwa watakuwa mbuzi wa kafara hawajaachia ngazi?

This is just too much hata la BoT halijapoa mara hili...na inashangaza kuona haya mambo yanatendeka as if nchi haina Rais au haambiwagi yanayoendelea kwenye wizara zake?

JK this is high time kuonyesha uko firm kama ulivoahidi 2005...kama hawang'oki wenyewe, wang'oe kama 'ulivomg'oa' gavana!

Act now befor it is too late!
 
Nafikiri, sasa umefikawakati kwa Wadanganyika kuwa Watanganyika, kwani mambo kama haya si ya kufumbia macho hata kidogo, Sina uhakika kama Mhe Rais pia hahusiki moja kwa mmoja na hawa Richmond, ukizingatia alivyokuwa karibu na Mheshimu PM, mimi sitaki mambo yaishie kama ya BOT, nilitarajia Mhe. Balali awe anatumikia kifungo muda huu, naomba sana Mhe. Raisi awawajibisho wote waliohusika na sakata hili, wote wajiudhuru na wapelekwe kwenye vyombo vya sheria, tangu lini mtu mmoja akawana na kashfa zote, kila deal yeye naye yupo, huyu ni mtu waaina gani na anampango gani na nchi yetu?
 
Hii Ripoti ya Richmond Mbona haifunguki?

najaribu kudownlod ile iliyokatika PDF bila mafanikio, kulikoni?
 
JK hana ubavu wa kuwachukulia hatua. Kinachofanyika ni kuwapoza wananchi kwamba mambo yanafanyiwa kazi. Ripoti alishaiona tayari ila mazingaombwe yanafanya Dododoma.
 
Kwa kweli nchi yetu IMEOZA kabisa. Bila ya hatua madhubuti kuchukuliwa,TUMEKWISHA !
 
Ja`mani mwenye picha ya RA naomba aiweke hapa tumfahamu. Hiwi ni kijana au mzee? Kuna wakati nilisikia kuwa ni kijana yuko kwenye late 30s. Je ni kweli????
 
Napenda kuwapongeza wana JF kwa kuleta habari motomoto kwenye forum hii ili watanzania wengi hasa wapenda maendeleo ya kweli yasiyo ya kibinafsi wapate kujua ukweli halisi wa mambo yanayo endelea Tanzania na duniani kote. - Haya maripoti yanaonyesha wazi kwamba viongozi wetu wengi wanakazana na sera za ''MUKUKUBI'' yaani MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI BINAFSI kwa kutumia nafasi walizo nazo na rasilimali za taifa, huku wakitupumbaza majukwaani kwamba wanatekeleza MUKUKUTA!!
Wana JF tupeni taarifa zote zenye manufaa kwa taifa hili.

Festo G
 
Kwanza shukran kwa hiyo ripoti hapo juu.

Katika mtandao fulani niliuliza katiba yetu inasemaje kuhusu spika na mikutano ya Bunge?
Kumbe kipo kifungu na huyo mfedhuli Sita mwenyewe anakifahamu. Sasa kwa nini alitaka kudhereu katiba ya Tanzania?

“Mheshimiwa Sita amesema Katiba ya Jamhuri, ibara ya 84 inamtaka spika awepo bungeni wakati wa kujadili hoja nyeti kama hiyo.”

Mtu huyu hafai kuongoza Bunge la Tanzania.MWENDA WAZIMU HUYU!

“Moshi wa Richmond wafukuta

2008-02-06 08:57:32
Na Gaudensia Mngumi, Dodoma
Riroti ya Kamati ya Bunge ya kuchunguza mkataba wa Richmond inayosubiriwa na Watanzania wengi kujua kilichomo inatarajiwa kuanza kugawiwa kwa wabunge leo tayari kwa kujadiliwa muda wowote kuanzia sasa.

Habari ambazo hazikuthibitishwa jana, zilisema kuwa huenda ripoti hiyo ikaanza kujadiliwa na wabunge wa CCM leo katika vikao vyao vya siri.

Habari za uhakika zilizopatikana bungeni jana jioni zilisema kuwa wabunge wote wanatarajiwa kugawiwa ripoti hiyo ili waisome tayari kwa kuijadili. “

NA NI KWANINI WABUNGE WA CCM WAIJADILI HIYO RIPOTI YA RICHMOND KISIRI SIRI. KWANI TANZANIA KUNA BUBGE NGAPI?
KUNA BUNGE YA CCM NA BUNGE LA WAPINZANI?
Kesi hii ya Richmond naona rais J.Kikwete aipeleke kwa wananchi ili watowe mawazo yako kama vile alivyifanya kuhusu Federation ya East Africa. Viongozi hawakuwa na akili timamu wakati wa mkataba huu.
Kwa lugha ya kiarabu tunasema VIONGOZI WA SERIKALI WALIKUWA NI MAJUNUNI AU HAYAWANI.
 
Gembe JK akiwaacha hao waliotajwa live bila kuuma maneno nitaungana na wewe barabarani tuandamane kama wanatuua wacha watuue tu haina maana kuishi katika aibu kama hii ya kuwa na serikali ya kifisadi juu mpaka chini.

Katika kipindi chote cha miongo mitatu na ushee niliyoishi humu duniani sijawahi kusikia serikali ikivuliwa nguo kama inavyotokea sasa. JK HATA KAMA EL,KARAMAGI,ROSTAM NA WENGINE WALIKUPA MABILIONI YA KAMPENI LAKINI KUMBUKA HAWAKUKUPA 80% YA KURA NI WATANZANIA NDIO WALIOKUCHAGUWA. THE BALL IS ON HAND USIJEKUTULAUMU 2010 AMBAYO HAIKO MBALI SASA.
 
Hakika tumepata raisi wa pili Tanzania baada ya Nyerere wengine walikuwa wapitaji tu na kutupotezea muda, JK tangu umekuwa raisi umekuwa mtu wa ukweli siku zote na usiyefumbia macho maovu ya serikali, inasemekana wewe ndiwe uliyemrudisha spika asiende Marekani huko huko kwa kina Richmond alikuwa anafuata nini? hapa changa la macho.

Heko Baba kwa kumrudisha na leo hii tumejua nini kilichokua kinaendelea.

Nashangaa mbona wapinzani wanasema mambo na yanakua kweli, ukianza na Benki kuu, sasa serikali zilizopita madhambi si yalikua mengi sana maana wa kusema bungeni hawakuwepo wakati ule.

Yaani kama tungeweza kurudisha miaka nyuma haki ya Mungu wengi wangeumbuka. Mhhhh!!!!!
 
yes; afukuzwe sio kujiuzuru; hafail nilijua tu na kweli; ripoti zote zitakazopitiwa lazima kuna mkono wake; angalia siku ile pale londoni Karamagi akisaini jamaa pia alikuwa pale; so yaani huyu mtu hatufais kabisa hakuna asiyejua hilo-Mungu ambariki sana Mwakyembe kwa ujasiri huo; sasa wengine zaidi wajitokeze kama Slaa alivyokwisha kubali kufa kwa ajili ya TAIFA LAKE sio kuwa mnafiki
 
Hii ndiyo email address ya lamaa waliokur fedha zetu, mgire@rdevco.com Majina yao ni Mohamed A. Gire na Mohammed S. Huque, Ph. D, kama ni msomaji wa website za makampuni makubwa utangundua kuwa website hii ina mapungufu mengi, hakuna written Financial statement, cash flow etc, hakuna contact za makampuni au nchi mbalimbaliambazo wemewahi kufanya nao kazi, website hiihaina tofauti na kampuni yeyotr ya mjasilia mali anayeanza biashara ya bongo, hivi hawa ndugu zetu walikuwa wanafikiria nini? nadhaniinabii tuwapeleke Mirembe kabla ya kuwafungulia massshitaka yeyote. inabidi watanzania tuwe macho esp. vijana hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, vijana TUAMKENI SASA.
 
Back
Top Bottom