Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mwakyembe Mungu akubariki!

Nakubalina na wote waliosema ya kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania serikali imeanikwa wazi wazi . Nimesoma ripoti nadhani Mwakyembe amepiga msumari wa mwisho kwa Lowassa pale aliposema ...



Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.


Kwa maana nyingine Mwakyembe anasema ya kuwa Lowassa anatakiwa AFUKUZWE !

Yaani hapo Dr Mwakyembe ameongea na MSOMI, Mtu anayejua NINI maana ya BUNGE, MAJUKUMU ya KUWA KIONGOZI, MZEE MWENYE BUSARA na MPENDA MAENDELEO....

Safi Sana...kwa mara ya kwanza MB wa CCM anaona UOZO na anaupa jina hilo hilo UOZO.
 
Jamani eeh. Hili suala ni pana sana nimeisikia ripoti pale bungeni alipokuwa anisoma Mtetezi wa wanyonge Mh. Dk Mwakyembe nimepata na mshtuko na kilio baada ya kugundua kuwa hata TAKUKURU (TAKUKURUNDO taasisi ya kuzuia rushwa ndogondogo) nao wanahusika pamoja na ofisi ya mwanasheria mkuu. Sasa wataweza kweli kushughulikia suala la BoT na mheshimiwa ndiyo hivyo hilo suala ameliweka mikononi mwao
 
Jamaa wanasema wao ni wapambanaji watapigana hadi "Risasi" ya mwisho. Hawajiuzulu labda "maiti" yake. KWAHERINI
 
Good indeed Dr.Mwakyembe!Live long.Ripoti zote ziwe zinaanikwa,Bado tunasubiri BUZWAGI NA BOT nao waanike jamvini
 
Jamaa wanasema wao ni wapambanaji watapigana hadi "Risasi" ya mwisho. Hawajiuzulu labda "maiti" yake. KWAHERINI
 
Mie nadhani nimapema mno kuanza kutabiri kitakachotokea,tusubiri kitakachojiri leo kwenye kikao cha wabunge wa ccm,kikao cha baraza la mawaziri,na uelekeo wowte wa kisiasa,unaoweza kutokea muda wowote kuanzia leo mpka kesho saa tatu asubuhi
 
Jamaa wanasema wao ni wapambanaji watapigana hadi "Risasi" ya mwisho. Hawajiuzulu labda "maiti" yake. KWAHERINI

Mmmhhhh!!!! Kazi ipo kweli. Wakikataa si watakuwa fired? Labda kama wana ubia na JK.

Inabidi bunge lianze na Rostam. Nategemea upinzani wapigilie misumari kweli kweli kwa Lowassa, Msabaha, karamangi na Hosea. Lakini wasisahau kuomba Rostam achukuliwe hatua na bunge.
 
Mnyika, asante sana Mkuu kazi umeifanya na sisi ambao ilitupitia pembeni tumeweza kuipata na kuisoma......

WanaJambo wenzangu, sijui niseme ni mimi au kuna topic nyingi ambazo Dr Mwakyembe na Kamati Teule wameonyesha ambayo tuna kazi kubwa ya kuyatolea hoja..... Mungu atusaidie tufike tuendapo!!!!

Halisi, pia nakushukuru kwa kutuweka katika mkao wa kula. Kweli JF tuna waTanzania wenye moyo, endeleeni na moyo wa kutoa info ili tuendelee Kumkoma nyani....

Long live JF!!!
 
Kama kweli Mwakyembe amepiga dongo hilo, sasa asubiri moto wake. Anytime soon anaweza kushangaa kuwa his political career comes to an end, unajua tena mtandao hawana jema na wapenda mema.
Hata hivyo JK ameshatoa signal kuwa ameweka ngoma uwanjani it is up to wabunge to dance, wanatakiwa kuacha porojo na kufanya kazi tuliyowatuma. Inasikitisha sana madokta, maprofesa na watu wazima na akili zao wanawekwa mkononi na watu wa ajabu, waache porojo wafanye kazi tu! vote of confidence!
 
UWiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Uwiiiiiiiiiiiiii.
Jamani inatisha! inasikitisha! Cannot believe this! Mkataba usiokuwa na muhuri wa wakili? AMA KWELI BANANA REPUBLIC!
 
Mmmhhhh!!!! Kazi ipo kweli. Wakikataa si watakuwa fired? Labda kama wana ubia na JK.

Inabidi bunge lianze na Rostam. Nategemea upinzani wapigilie misumari kweli kweli kwa Lowassa, Msabaha, karamangi na Hosea. Lakini wasisahau kuomba Rostam achukuliwe hatua na bunge.


Rostam ni mafia...haongeia sana na wala hajipeleki kimbelembele kwenye haya madudu; yeye anatuma wakina Lowassa, Karamagi pamoja na JK mwenyewe wamfanyie kazi zake chafu. Ameitwa na hii kamati teule amekataaa...inathibisha wazi kuwa RA hagusiki; JK anajua hilo, Lowassa anajua, na wabunge wote wanajua.
 
Kweli nimesikia mkakati ni mzito, Hakuna kuachia ngazi ndio kauli mbiu ya mkakati huo!
 
ripoti kali mno.

imoto inaunguza pande zote

mie liloniumiza ni jinsi gani watanzania tunavyokuwa wapenda majungu na wapenda domo nje ila tukiitwa tuthibitshe ukweli tunaanza kuuma uuma vidole.

ni aibu kutojiamini na kutokuwa jasiri wa kusema ukweli.

hii imeanza kunipa wasi wasi mkuu kuwa watanzania ni watu dhaifu na ni watu ambao tutachelewa sana kuendelea.

kumbe yanayosemwa amani yetu ni ya woga ni maneno ya kweli.

nnaamini kuna ukweli mwingi haujawekwa wazi kwa hofu.

nnaamini kuna mengi yatakuja juu mwaka huu.

hongera wenye kuitakia mema nchi yetu bila ya kujali itikadi zao iwe kisiasa au kidini cha msingi upuuzi wa kuinyonya tanzania na kuwakandamiza watanzania ukomeshwe

Mtu wa Pwani,

Nani anataka kufa? Watu hawakuwa na imani na hiyo kamati kwamba itawalinda. Kwasasa UKWELI wetu na MLINZI wetu ni JF.

Watu wakiwa na habari wazimwage tu hapa na zitafika zinakotakiwa.

Hiki ndio chombo chetu cha ukombozi na tujiandae mwaka 2010 kwa JF kuwa na role kubwa sana kwenye uchaguzi.
 
Wazee kwanza kabisa this was one of the reports za uchunguzi in Tanzania I have ever read. Very professional and to the point! Bravo Mwakyembe and your team.

Kwa wananchi wenzangu wote, the moment of truth has arrived, when we shall know if we have a president or otherwise. Honestly I cant give my verdict without giving JK a chance to act.

Talk of incompetence kuanzia kwa Ofisi ya mwanasheria Mkuu? no wonder JK alienda kuomba msaada wa wanasheria ulaya!!. This is slap in the face of tax payers. Talk of Hosea and his Ofisi, I mean if at all JK will do anything, he has a whole lot to do!

Lowassa? jamani yaani kweli with due respect you have done this to your fellow compatriots who are dying for lack of aspirin? and you pocket 152M everyday for two years?

Hivi waungwana as a nation kweli tunakwenda wapi? kama mtu aliyekabidhiwa treasury yote ya nchi ndo anakuwa mwizi hivi?

No way lets wait and see JK how he is going to act. But this is a moment of truth!!! Lowasa this is way too much for a country like Tanzania!!!! No way, Najua watanzania ni vilaza as you falsely assume, but trust me EL you wont go away with this matter!

Tanzania is bigger than LOWASSA!!!!
 
Jamaa wanasema wao ni wapambanaji watapigana hadi "Risasi" ya mwisho. Hawajiuzulu labda "maiti" yake. KWAHERINI

Mie nilitegeme maneno kama haya.I kno ROstam since 2004.Full Mafisoso.Na watalipiza kisasai.People will pay on this na tena hasa Dr. Mwakyembe na wenzakeTuwe Tayari Kumsaidia shujaa wetu na kamati nzima.

Lowa-saaaa you are damn unproffesional,BA Music And Dacing.?te teh Malimu alikuwa hakupendi na sijui kwanini Jk alikupenda?


CCM si Mama Yangu,Kikiacha Itikadi zinazofaa nakiacha
 
hapo maana yake nikwamba,watajwa wanasubiri pm,ajiuzulu,akikataa,na wao wanakataaa,ndio maana nikasajest tusubiri mpaka kesho asubuhi,maana kuna kitu kinategemewa kutokea usiku wa leo,tutege masikio
 
Back
Top Bottom