Ripoti ya BOT mbona haitolewi!? Walioiandika wanawekewa shinikizo ili waibadilishe?

duhhh aliyesema husahau tuu kaniua kinyama comments kama hizo ningeweza ngekua nazipeleka kwenye jokes na udaku!!abt the ripoti...nadhani zitakuaj jumlishwa zoote then zitolewe mwisho wa kipindi chake then wa tz wapate ripoti kamili ya uongozi wake!!kwani ripoti za kawaida za wanafunzi si hutolewaga mwisho wa muhula?

ila lets be serious wajimini ni another wastage of resources hiyoo kamati zaundwa kwa mkwara mzitooo ila nothing is done after kamati hiyo wala even kuongelewa basi hiyo ripoti

Mtaalam,

Katika kipindi cha zaidi ya miaka 40 ya serikali yetu kumekuwa na tume nyingi sana zilizotoa mapendekezo mbalimbali lakini serikali ikayakalia na kuyatupilia mbali na wala watanzania hatukuhoji; mbaya zaidi tukaendelea kuiweka serikali hiyo hiyo madarakani miaka yote hiyo. Je kufanya hivyo ni nini kama siyo kusahau?
 
Mazingaombwe na usanii ni fani ya serikali ya awamu ya nne. Ukiona mpaka wafadhili wanakaa kimya kuhusu hii kadhia basi hapo inabidi upate hisia mbaya juu ya hawa tunaowaita nchi wahisani. Jana nimesoma gazeti la Mtanzania lilikuwa linasema JK alipokuwa US alikutana na MD wa IMF. MD wa IMF alimwomba JK awaambie wana zuoni wa nchini mwake waipime IMF juu ya utendaji wake. Kinachosikitisha ni kwamba huyu MD hakugusia chochote kuhusu ripoti ya BoT. Kabla ya uchunguzi kuanza kufanyika walipokutana mara ya mwisho JK aliulizwa juu ya uchunguzi na akatoa jibu kwamba utafanyika na watakaobainika kuhusika serikali itawashughulikia. IMF kwa upande wake walisema wanaisubiri kwa hamu hiyo report, je, hamu ya kusubiri hiyo report imeishia wapi? This was the right kumuuliza JK maana ma-auditor wameishamaliza kazi yao na wameishai-submit serikalini, kwanini serikali haiiweki hadharani? Hapa ndipo ninapoona unafiki wa IMF na hao tunao waita donors.

Kinachoendelea ni kwamba pamoja na mambo mengine report ile sina hakika kama itakuja kuwekwa hadharani bali itabaki huko huko serikalini na yaliyomo itakuwa ni siri ya IMF, WB, na serikali. Wananchi wa kawaida ndiyo tutakuwa tumeliwa na hao waliotafuna hizo watakuwa wamepona.

Mnadhani kwanini Ballali alikuwa na kiburi cha kugoma ku-resign wakati madudu yake yote yameanikwa hadharani? Kuna kila dalili zile check zilizokuwa zinalipwa kwenye yale makampuni fake fedha zake zilitumika kwenye kampeni ya uchaguzi ambao umemuweka JK madarakani, hapo unategemea nini? Hilo bomu la fedha za nje linamgusa Muungwana moja kwa moja na hivyo kupata ukweli ni kazi ngumu na hata uchunguzi wake umefanywa kwa shinikizo la wafadhili ambao nao wameanza kulainishwa na hivyo watawekwa sawa na huo ndiyo utakuwa mwisho wa maneno. MD wa IMF ni mmarekani, already kuna speculation kwamba Bush anataka kuweka base yake Bongo, hapo unategemea nini? Ndiyo tumeliwa hivyo na hakuna kitakachoendelea, tutabaki kuambiwa report iko kwa CAG mara imeenda Ikulu na ni Rais ndiyo ataitolea maelezo.

Labda tusubiri kama wabunge wataibana serikali kutaka iweke hadharani hiyo report. Hapo utamsikia Marmo na Dr. Burian wakisema hiyo ni siri na hivyo haiwezi kuwekwa kwenye public. Yale yale mambo ya Richmond, kwamba report ya PCB haiwezi kupelekwa bungeni kwa kuwa ni swala ambalo linahusu makosa ya jinai. Kwa kweli sheria za Bongo ni za ajabu sana!!!
 
Baada ya siku chache tutaambiwa, "Ripoti ya BOT iliyokabidhiwa siri kali wiki chache zilizopita inagusa kitovu cha usalama wa Taifa. Kuitangaza hadharani ripoti hiyo ni kuhatarisha usalama wa Taifa letu, hivyo SIRI KALI imeamua kutoitangaza ripoti hiyo hadharani. SIRI KALI inawahakikishia Watanzania wote kwamba yaliyomo katika ripoti hiyo yatafanyiwa kazi mara moja kwa manufaa ya Tanzania na wale wanaohusika na upotevu wa pesa watashughulikiwa."
:confused:
 
Nasikitika sana kwani hakuna Mtanzania mwenye ujasiri wa kuulizia hiyo ripoti itatolewa line. Nasema Hakuna Mtanzania mwenye ujasiri wa kuulizia kwani hata hao watakaoulizia (Wanasiasa) tutasema wanatafuta umaarufu. Ni aibu tena kubwa kwa Tanzania.. Tume zimekuwa zikiundwa nyingi sana Matokea yeke hatujawahi kuyaona hata mara moja tunaambiwa ni siri... Siri ya nini kwa wananchi? kwa nini wakati wanaomba kura hawasemi kuwa kuna siri nyingi ambazo hawatatuambia? Where are we going? Utawala wa namna gani Huu? Watanzania tumekuwa mno Makondoo.. Kila kitu tukiambiwa tunakubali tuu. Hakuna mtu mwenye ujasiri wa kuuliza kwa nini tuenda kaskazini na sii kusini?

"Ee Mungu lini utatuletea Manabii kama Sokoine na Nyerere?" Hakuna mwingine.. wala sioni atayeweza kuja kukaribia.. Hata vijana wenzetu wameshakuwa zaidi ya wazee kama akin Kingunge.. Nasikitika sana Wenzangu.. Naona hata aibu kuimba Tanzania, Tanzania Nakupenda kwa moyo wote
 
msijali jamani the report will finally come out when the iron is cold. a period when the public will be less interested, we are all here to witness. ni kama ripoti ya MOI tu, this is our TZ. Political giants but economic dwarfs
 
msijali jamani the report will finally come out when the iron is cold. a period when the public will be less interested, we are all here to witness. ni kama ripoti ya MOI tu, this is our TZ. Political giants but economic dwarfs

Changa la macho. Kuunda kamati ni moja ya strategy ya ku-buy time.
 
Tayari mmeshalala...hiyo ripoti ya nini tena?.Tulishasema kila siku kuwa hizi huwa ni mbinu za serikali kupoza moto mpaka msahau halafu mambo ndiyo yanakuwa yamekwisha taratibu.
Halafu ndiyo tunasema kuwa hii ni serikali ya kuleta neema kwa kila mtanzania.Wewe uliona wapi nchi kuendelea bila ya kudhibiti rasilimali zake?..miujiza hiyo!

-Wembe
 
Ee Mungu lini utatuletea Manabii kama Sokoine na Nyerere?" Hakuna mwingine.. wala sioni atayeweza kuja kukaribia.. Hata vijana wenzetu wameshakuwa zaidi ya wazee kama akin Kingunge.. Nasikitika sana Wenzangu.. Naona hata aibu kuimba Tanzania, Tanzania Nakupenda kwa moyo wote


Msesewe tusililie manabii tu, JE sisi wananchi huwa tunachangia kuleta mabadiliko? leo yakiitwa maandamano ya kushinikiza serikali kubadili mikataba au kudai ripoti zas kamati, je ni wangapi wanauwezo wa kujitokeza walau kuonyesha kuwa kuna wananchi wengi wanapenda mabadiliko? Tusijikumbatie majumbani tu. We also have a role to play.
Leo kuna ripoti nyingi za mizengwe , ile ya muhimbili tumeambiwa inaundwa nyingine yenye wataalamu zaidi, sasa hapa wananchi tungemandamana na sisi tujue (kama sheria inaruhusu) yaliyomo kwenye hayo maripoti.
 
Msesewe tusililie manabii tu, JE sisi wananchi huwa tunachangia kuleta mabadiliko? leo yakiitwa maandamano ya kushinikiza serikali kubadili mikataba au kudai ripoti zas kamati, je ni wangapi wanauwezo wa kujitokeza walau kuonyesha kuwa kuna wananchi wengi wanapenda mabadiliko? Tusijikumbatie majumbani tu. We also have a role to play.
Leo kuna ripoti nyingi za mizengwe , ile ya muhimbili tumeambiwa inaundwa nyingine yenye wataalamu zaidi, sasa hapa wananchi tungemandamana na sisi tujue (kama sheria inaruhusu) yaliyomo kwenye hayo maripoti.

those tumes zawekwa for nothing jus kuchezea resources zetuu tu as nijuavyo mimi those members wanalipwa at hawakai bure bure or kufanya kazi ya kujitolea!
abt maandamano yani wategemea muwe na mawazo hayo na serikali iwe imelala tu?wakati kuna watu kama FFU hawana kazi za kudo wakingojea madili kama hayo wamalizie hasira zao kwenu nyie waandamanaji???
 
Ripoti ipo ndani ya "Surgery Room" ikifanyiwa upasuaji na kupakwa rangi ya kung'aa ili Watz wasiweze kuona kilichomo ndani.

Kuhusu maandamano, FFU hawawezi kuendelea kuwatumikia mabwana wakubwa kwani hata wao wamepigika na ugumu wa maisha. Who knows one day wata-support walalahoi.
 
Mtaalam,

Katika kipindi cha zaidi ya miaka 40 ya serikali yetu kumekuwa na tume nyingi sana zilizotoa mapendekezo mbalimbali lakini serikali ikayakalia na kuyatupilia mbali na wala watanzania hatukuhoji; mbaya zaidi tukaendelea kuiweka serikali hiyo hiyo madarakani miaka yote hiyo. Je kufanya hivyo ni nini kama siyo kusahau?


ndo maana nikauliza somewhere sijui tumelogwaaaa????maana sio bure
 
Ni zaidi ya wiki nne tangu tuambiwe kwamba ripoti ya BOT imekamilika. Je, kulikoni na ripoti hiyo, mbona haitolewi hadharani? :confused:

ngoja nipate popcorn mie

hivi yale majina ya wauza unga yalifikia wapi?
8aeg65y.gif
 
Mugo"The Great";112324 said:
Ripoti ipo ndani ya "Surgery Room" ikifanyiwa upasuaji na kupakwa rangi ya kung'aa ili Watz wasiweze kuona kilichomo ndani.

Kuhusu maandamano, FFU hawawezi kuendelea kuwatumikia mabwana wakubwa kwani hata wao wamepigika na ugumu wa maisha. Who knows one day wata-support walalahoi.

kip on dreaming abt ffu kuja kukusaidia wewe mlalahoi!hivi wajua pindi ffu ikishindikana jeshi uingizwa kudeal na tatizo??as wako wengi zaidi n if hujashtukia huyu muungwana katimua watu kibao wakubwa jeshini na kuweka masela zake ambayo ni mojawapo ya strategy kali kupita maelezo as huwezi tarajia siku jeshi nalo lije kupinga mabwana zao wakati la receive orders kutoka kwa mabest za huyoo mtaliii
 
Isipotolewa mpaka jan.2008 tutakuwa tumesahau.........teheeee sikujua kama Watanzania wanaongoza kwa kusahau..
 
kabisa mlikuwa mnasubiri report ya ufisadi wa tume iliyoundwa na mafisadi wenyewe? poleni sana ....next time dawa ni kuwapiga chini kwenye uchaguzi maana ndio dawa ya kumaliza ufisadi la sivyo itakuwa nyimbo tuu
 
Ripoti ya ukaguzi BoT isikaliwe-CHADEMA

2007-12-19 08:42:00
Na Godfrey Monyo


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitaka serikali kutoa ripoti ya uchunguzi juu ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Benki Kuu (BoT) kwa kuwa ipo tayari.

Aidha, kimesema kuwa kinashangazwa na ukimya unaoendelea kuhusu 'mafisadi' waliotajwa na kambi ya upinzani baada ya kuwatangaza kufanya ubadhirifu wa fedha za umma.

Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, alipokuwa akifungua mkutano wa kawaida wa Baraza Kuu la chama hicho.

Alisema ingekuwa busara kama taarifa hiyo ingetolewa na ijulikane kwa wananchi badala ya kuendelea kuwa siri na kuwafanya wananchi kukosa imani na serikali.

Aliongeza kuwa kitendo cha Mkaguzi Mkuu kutotoa ripoti hiyo wakati ipo tayari kinajenga mazingira ya kupotosha ukweli wa majibu ya uchunguzi.

Bw. Mbowe alisema habari walizonazo ni kwamba uchunguzi umeonyesha kiasi cha fedha `zilizochotwa` ni kikubwa kuliko kiasi kilichotajwa na kambi ya upinzani hapo awali.

``Serikali imepata kigugumizi baada ya kugundua kuwa kiasi cha fedha kilichochukuliwa BoT ni mara dufu ya kile tulichotangaza,`` alisema na kuongeza: "nakumbuka kuwa, awali tulielezwa taarifa hiyo itatolewa kwa wananchi haraka pindi wakaguzi hao watakapokamilisha kazi yao lakini cha ajabu wameendelea kukaa nayo.

Sisi tunadhani wana mpango wa kuibadilisha lakini lazima watambue kuwa fedha zilizofujwa ni jasho la Watanzania wanaolipa kodi na wanaohitaji taarifa za kweli kuhusu matumizi ya kodi zao.``

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa mbali ya serikali kupata kigugumizi cha kutoa ripoti hiyo, pia `mafisadi` wameshindwa kutekeleza azimio lao la kwenda mahakamani.

``Mafisadi wameshindwa kutushtaki. Tunataka kufahamu nini mstakabali wa taifa hili, wakati wa kuvumilia utapeli umepitwa,`` alisema.

Serikali ilifikia uamuzi wa kufanya ukaguzi BoT baada ya kutolewa malalamiko ya kuwepo kwa tuhuma za ubadhirifu.

Kwa mara ya kwanza tuhuma za ubadhirifu ziliibuliwa bungeni katika kikao cha bajeti cha Julai na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa, ambaye pia aliwatuhumu baadhi ya vigogo wa serikali kwa ubadhirifu wa mabilioni ya fedha.

Kampuni iliyokuwa ikifanya uchunguzi huo ni Ernst & Young ambayo ilipewa siku 60 kukamilisha kazi hiyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Novemba 24, mwaka huu ilieleza kuwa Ernst & Young ilikwishakamilisha kazi yake na kuikabidhi kwa CAG.

Taarifa hiyo ambayo pia iliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini ilieleza kuwa hivi sasa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anaifanyia kazi.

Aidha, Bw. Mbowe alisema amesikitishwa na kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Siasa na Uhusiano wa Jamii, Bw. Kingunge Ngombale Mwiru, aliyesema kuwa mjadala wa katiba umefungwa kwa sasa.

Kwa mujibu wa Mbowe, Bw. Kingunge aliitetea hoja yake kwa kusema kuwa suala la mabadiliko ya katiba haliwezi kujadiliwa hivi sasa kwa kuwa halipo katika ilani ya CCM.

Akizungumzia suala hilo alisema mjadala wa katiba hauwezi kufungwa na ilani za chama chochote na kwamba unawahusu Watanzania wote bila kujali itikadi au dini.

SOURCE: Nipashe
Wakuu, kama kuna mwenye full report tafadhali iwekeni mezani ...
 
hii ripoti haitolewi leo wala kesho, itatolewa muda muafaka wakati upepo ukiwa mzuri, ama labda wakuu wanatoa report in a summary form au pengine yatatolewa mapendekezo ya ripoti.

subira huvuta kheri lakini sometimes unaweza kusubiri milele.
 
Kuna dalili ya JK kudhalilila nini ? Kama watachelewa basi itavujishwa na tutaitoa hapa muda si murefu . We are working on it .
 
Back
Top Bottom